Bw.Michuzi naomba utuwekee risala nzuri tu ya marehemu umeme ambayo imekuta ikitandazwa katika simu za mkononi duniani kote.
RISALA FUPI YA MAREHEMU UMEME ZNZ
RISALA FUPI YA MAREHEMU UMEME ZNZ
Marehemu alizaliwa 1976 huko kidatu TZ BARA,Katika uhai wake aliwatumikia wazanzibar kadri ya uwezo wake,marehemu alisumbuliwa na maradhi mbali mbali kama vile kukatika mara kwa mara na mgao.
Wakati wa Salmin aliwahi kaufleti kwa kipindi cha ramadhani hadi siku kuu na serikali kuamua kuongeza sikukuu ya tano,mnamo mwaka 2008 Aliwahi kufleti kwa muda wa sk 28,na kufanikiwa kurudia hali yake ya kawaida kwa msaada wa madaktari kutoka NORWAY.
Mnamo tar 10/12/2009 Marehemu alikua katika matibabu na madaktari kutoka south afrika lakini hawakufanikiwa na kupoteza maisha Katika kijiji cha Fumba ZNZ.
Katika uhai wake marehemu alifanya mengi ikiwemo kumurika watu na mali zao pamoja na kukuza uchumi.marehemu ameacha watoto wawili,GIZA na JOTO,WAKE 2,TABU YA MAJI na HARAMA ZA NAULI KUPANDA,na HAWARA 2 Mapacha,DIESEL na PETROL.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.
AMIN
Mdau Nuramo'
Mdau Nuramo'
Greece.


Nuramo acha vituko vyako vya umangani bwana,utundu kama huu nani alikufundisha shauri yako Mh Karume akiona ujumbe wenye ukweli kama huo ujue zenji hutii mguu ndugu yangu,lakini ujumbe ulioutoa unapendeza sanaaa hongera kaka Nuramo
ReplyDeleteHivi viongozi wetu wanajifunza kweli kutokana na makosa? Maana hii si mara ya kwanza Zanzibar kukosa umeme kwa kipindi kirefu, than first time viongozii wa ngazi za juu wote waliondoka visiwani eti walikua ziarani nchi mbali mbali. Hii si hak, jamani tufanyeni kweli 2010.
ReplyDeleteUsijali, hajafa jumla, huenda akafufuka baada ya wk 3. Kwa taarifa tu, hata pacha wa marehemu aliyeko huko bara afya yake ni mbovu kwelikweli!
ReplyDeleteHapa muungano haujafa ukifa si ndio mtatafutana.
ReplyDeleteKumbe Zenji na nyie umeme unakatatika? Manake nilikuwa nasikia hakuna umeme kukatika Zenji..karibuni kwenye giza/joto sie machogo tumeshazoea
ReplyDeleteoh poleni sana kwa kuondokewa na kijana wenu mpendwa umeme ZNZ! Nimeshtushwa sana na kifo chake cha ghafla, kwani marehemu ni binamu yangu!
ReplyDeleteMimi naitwa kibatari bin Koroboi kama mnanikumbuka! tulipoteana kwa muda mrefu baada ya kutokuelewana na marehemu na kuniambia sihitajiki tena! lakini kama msemo usemao "when one door closes, another door open!" Hivo msijali sana mimi narudi nyumbani na tutapendana na nitakuwepo kwa miaka mingi sana sitokubali kuondoka tena!
Naomba mjiandae kunipokea kwa shangwe!
ila huku niliko jina ninaloitwa ni Fisadi, lakini hamna shida yote ni majina yangu!
Asanteni sana ndugu zangu, see u soon!
Fisadi CEO.
HA HA HA,Nyie kitu kidogo muungano sasa kama mnaona tutapata tabu,kwa nini msiuvunje basi tuone kama tutapata tabu,Mijitu mengine haina akili hata kidogo,Ubaguzi tu ndio mbele,na watu wanafikiri muungano ukivunjika kutakua na vita baina ya bara na visiwani,Na watu watatimuliwa pande zote,hizo ni akili finyu,muungano hata kama ukivunjika(Mungu aulinde)Kitakachobadilika ni system za ukaazi tu,mfano taxation,residency lakini sio watu watafukuzwa na kubaguliwa,Kwani EAC ilivunjika je hakuna raia wa Tz wanoishi kenya au Uganda na wao virce verca?Czech-Slovakia-Slovenia-Serb na montenegro-bOSNIA na Hesigovina-Senegal Gambia nk Je watu wanapigana wa pande mbili?toeni ujinga,hapa tunaongelea umeme sio muungano.Kwani kabla ya kuungana kulikua na umeme gani ZNZ?he !
ReplyDelete