Vodacom Tanzania inapenda kuwakumbusha wateja wake wote kuwa zoezi la uandikishaji wa namba za simu lililoanza Julai Mosi mwaka huu bado linanaendelea na litakwisha tarehe 31 Disemba 2009. Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia.

1. Swali: Ni kwa nini nisajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Ni ili niweze kujilinda na kuilinda namba yangu kutoka kwa wale wanaotumia vibaya huduma za mawasiliano.
2. Swali: Ni wapi ninapoweza kuisajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Fika kwenye Vodashop au wakala wa M-PESA yoyote yule aliye karibu na wewe ukiwa na kopi (kivuli) ya moja ya vitambulisho vifuatavyo;

I. Kitambulisho cha kupigia kura
II. Pasi ya Kusafiria
III. Kitambulisho cha Pensheni (NSSF, PPF, LAPF, PSPF)
IV. Leseni ya Udereva
V. Kitambulisho cha kazi pamoja na barua ya Mwajiri
VI. Kitambulisho cha Shule au Chuo
VII. Barua iliyopigwa muhuri kutoka kwa Mtendaji Kata pamoja na picha ndogo

3. Swali: Je kuna gharama yoyote ya kusajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Hapana, usajili ni BURE
4. Swali: Je zoezi hili la kusajili namba za mitandao ya simu limeanza lini na litakwisha lini?
Jibu: Zoezi hili lilianza Julai mosi mwaka huu na litakwisha Disemba 31 mwaka huu.
5. Swali: Je ni nini kitatokea iwapo nitakuwa sijasajili namba yangu ya Vodacom baada ya Disemba 31 mwaka huu?
Jibu: Kulingana na maelezo kutoka Tume ya Mawasiliano, mteja husika atajulishwa na kisha namba yake itafutwa kutoka kwenye orodha ya namba za simu.
6. Swali: Je ninaweza nikasajili namba ya mteja mwingine?
Jibu: Ndiyo, unaweza kusajili namba ya mteja mwingine iwapo tu unayo maelezo yote yanayotakiwa na Tume ya Mawasiliano.
7. Swali: Je ninatakiwa niisajili tena namba yangu ya Vodacom hata kama nimeshajisajili na huduma ya M-PESA?
Jibu: Hapana, huhitaji kuisajili tena namba yako iwapo umeshajisajili na huduma ya M-PESA na umeacha nakala ya kitambulisho chako. Iwapo haukuacha nakala ya kitambulisho basi itakubidi uache nakala ya kitambulisho chako chenye picha.
8. Swali: Je ni idadi ya namba ngapi za Vodacom ninazoweza kuzisajili?
Jibu: Hakuna idadi ya namba unazotakiwa kuzisajili. Unaweza kusajili namba nyingi kadri uwezevyo.
9. Swali: Je kuna usiri wa kiasi gani kwa habari nitakazozitoa wakati wa kusajili namba yangu?
Jibu: Makapuni yote ya simu yanatakiwa kwa mujibu wa sheria kutunza kwa usiri mkubwa habari zote zitakazotolewa na wateja wake.


Pamoja daima.
Vodacom Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. nasikitika sana,nilienda kujisajili kwa namba yangu, fun enough nikaambiwa imeshasajiliwa na mtu mwingine,na hapo kumbuka nilishatoa information zangu zote pamoja na kopi ya kitambulisho changu, nasubiri muda ukifika kama nitafutiwa, naendelea na namba zangu za competitors maana sina jinsi

    ReplyDelete
  2. Je unaweza kusajili simu zaidi ya moja? je namba zinazotumika kwenye internet nazo zisajiliwe?

    ReplyDelete
  3. We mbwiga anony wa Fri Dec 04, 01:40:00 PM, hawasajili simu, wanasajili line!

    ReplyDelete
  4. Bro Michu tafadhali nijulishe. Mi niko ughaibuni ,likizo nilikuja mara ya mwisho april, sasa nitasajili vipi maana line nikonayo huku? Na bado nahitaji kuendelea na line yangu pindi nikija vekesheni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...