Nominees and winners of the awards
Frontline Management Team with Comittee
members join thw Woman of the year Anna Lukona For a Picture

Winners,Rita Paulsen and Susan Mashibe

Emelda Mwamanga-Young Achiever Award

Nancy Sumari Shaking hands with daughter of
Bibi Titi Mohammed after presenting Lifetime achievement award
Names of winners and
categories of the awards, from the final
event that took place over the weekend
at the Mlimani City Conference Centre in Dar es salaam

1. Arts and Culture Award(sanaa na utamaduni)- Rita Paulsen,

2.Health Award(Afya)- Prof. Esther Mwaikambo.

3.Science and Technology Award(Sayansi na Teknologia)- Susan Mashibe

4. Social Welfare Award(ustawi wa jamii)-Theresia Aloyce.

5.Education Award(Elimu)-Anna Lukona

6.Public Sector Award(Umma)- Mercy Sila

7.Agriculture Award(Kilimo)- Janeth Mlowe

8.Information and Communication Award(Habari na Mawasiliano)- Betty Mkwasa

9.Sports Award(Michezo)- Anna Filbert Bayi

10.Business Entrepreneur Award(Mjasiriamali)- Odilia Martin

11.Lifetime Achievement Award- Bibi Titi Mohammed

12.Woman Of The Year- Anna Lukona

13.Young Achiever Award- Emelda Mwamanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Michuzi, naomba tujenge utaratibu wa kutoa taarifa kamili. Kwa mfano ni vigezo gani vimetumiwa kuchagua washindi hao? wakina nani walipendekeza majina yao? walitumia vigezo gani? washindi wengine wanatia shaka!!

    ReplyDelete
  2. Mnapeana tu hizo tuzo eh?

    Mbona hamtaji hizo achievement zao ni zipi?

    Baadhi tunawajua kama Imelda Mwamanga; Rita Paulsen; Betty Mkwasa na hayati Bibi Titi Moh'd, ila hao wengine hmmm...

    Kwenye ujasiriamali mwanamke namba moja ni Dk. Mch. Mhe. Getrude Rwakatare. Je ni kwa nini mmembania?

    ReplyDelete
  3. Inaonekana walioshinda wote kwenye hizi awards ni kimamama wa Kikristo pekee, Kwa hiyo hakuna muislamu yeyote aliestahili kushinda au aliefanya jambo linalostahili kushinda hizi awards? au hizi ni awards zinazotolewa ki-waraka waraka. Hatuzungumzii award ya Bibi Titi hapa.

    ReplyDelete
  4. Hapo ndiyo kinamama wanaponimaliza: Utamaduni na Sanaa Rita Paulsen. Ingekuwa bora wangeita hiyo category wangeiita Burudani za Kisasa badala ya Utamaduni na Sanaa. Kama sanaa angepewa Prof Penina Mlama, Dk Amandina Lihamba, Bi Kidude, Mama Thecla Mjata, Mama Mary Cidossa, Carola Kinasha, Bi Shakila, au msanii mwanamke mwingine yoyote.

    ReplyDelete
  5. MAMA NTILIE MMEWASAHAU NA MCHANGO WAO MKUBWA HAPO MJINI WA KUSHIBISHA MATUMBO YA WATU WAKIWA MAKAZINI, PIA HATA AKINA MAMA WA NYUMBANI WANAOWAPIKIWA WAUME ZAO PIA WANASTAHILI AWARDS CHA KUFANYA NI JINSI GANI YA KUWAPATA WASHINDI KARIKA NYANJA HIZO - NAWAKILISHA HOJA KWA MAJADILIANO.

    ReplyDelete
  6. 8.Information and Communication Award(Habari na Mawasiliano)- Betty Mkwasa. Vipi Joyce Mhaville hakufiti hapa? Au Sakina Datoo?

    ReplyDelete
  7. sina hakika na kigezo walichotumia waandaaji but kuna watu kama kina Maria Sarungi i think they deserve some recognition in what they do jamani, hasa kwa mchango wao ktk sanaa (ref; ART N STYLE program) pia hata katika upande wa sanaa ya mitindo hapo Tz.It jus sad actually.But here we go ni bongo tambarare ISN'T???????
    DIDI

    ReplyDelete
  8. NI WANAWAKE WANGAPI WALIOSHIRIKISHWA, NIKIANGALIA PICHA INAONEKANA KUWA WENGI WA WASHINDI NI WALE WANAOJULIKANA NA WAANDAAJI NA PIA NI WAKAZI WA DAR.

    ReplyDelete
  9. HUYO NI MTOTO WA BIBITITI AU NI MJUKUU WAKE?

    ReplyDelete
  10. nahisi hii kitu ilikuwa si fair ama hamkuipa muda sana , acheni usanii, ritha paulsen amefanya culture gani, mtu kama betty mkwasa information na communicatiion how tangi amepelejkwa sijui ukuu wa mkoa lini mmemsikia mbona kuna watu they desrve that recognation, hapa tanzania kuna wanawake wanafanya mechanial jobs na nini,......kwanini amadvocate changes, watu ni haohao tu jamani, acheni usanii warembo, or you should have given a time, and more research the show was totaly unfair

    ReplyDelete
  11. hahahahhhaaaahahahahahaa kwi kwi

    nicheke mie lol...kazi ipo!!!

    ReplyDelete
  12. Kwa jinsi waandaaji walivyo na mtindo uliotumika hao walioshinda ni sawa, mimi naona waandaji wa kitu kama hiki walipaswa kuwa watu wazima kidogo na wenye uzoefu mkubwa wa maisha ya kina mama na sio wasichana wadogo halafu uchaguzi ungekuwa ni waandaji kuchunguza nani anafaa na sio kama ilivyo sasa hivi hawa wameshindanishwa ni kama vile waliingia kwenye ligi kwa hiyo aliyeshinda amaeshinda

    ReplyDelete
  13. Wewe anon wa Dec 07, 08:36 acha udini. Kila kitu udini udini tu hata huwazi vitu vingine vya maendeleo, usipoangalia akili yako itadumaa. Mimi ni Mwislamu mbona sioni tatizo lolote la zawadi hizo. Ninakusihi utoke huko kwenye udumavu wa kimawazo. Mwishowe utauliza mbona hakuna mwanamke wa kabila lako.

    ReplyDelete
  14. Age ya waandaaji haihusiani, ila inaonesha ni jinsi gani wanahitaji kushikwa mkono na watu wenye busara, ukiangalia ni wale watu wanaowafahamu wao tu ndio waliowapata tuzo, Prof Amandina Lihamba ndio haswaa mwenye TUZO YA SANAA NA UTAMADUNI.. au angalau basi hata Shani Kitogo.. au labda niwe sijaelewa, labda mlikuwa mnaangalia utamaduni na sanaa za kigeni. Otherwise, chukulieni hizi comments zote positively ili mueweze kufika mbali, kweli watu wote wametoa maoni yenye points za kweli.. msione tabu kukosolewa you have a waay to go ladies.

    ReplyDelete
  15. Jamani, watanzania kwa ulalamishi ndio wenyewe, mimi kwa uelewa wangu wa mashindano kama haya ni kunakuwa na categories zinawekwa na watu wanatakiwa watume kazi zao kulingana na categories na ni hiari ya mtu kushiriki kama hukushiriki hutakuwepo katika kinyanganyiro, na hawa watu pamoja na kwamba mimi niko nje ya Tanzania niliona matangazo yao kwenye mitandao, nyinyi walalamikaji kama mlikuwa na mapenzi mema na mama ntilie mngewaelimisha watume kazi zao kwenye ushindani, mtindo huu huu unatumika kwa Awards za CNN hata Kili music awards cha kushangaza wakishinda watu, ambao hawakujigusa kushiriki ni wa kwanza kulalamika, ila wanatakiwa kuongeza categories kama ilivyoshauriwa na wengine lakini msilalamike, watu wengine hawapendi kushindana wala hawataki umaarufu

    ReplyDelete
  16. tatizo wadau lipo ni kuwa huu utaratibu wa kutupigisha kura bila limit ndio unaochangia kupata washindi wasiofaa kwenye matukio mbalimbali, mf Bongo Star, tuzo za Kili nk. iweje mtu mmoja apige kura bila kikomo? that's why tunapata washindi wasiostahili mara kwa mara. halafu tatizo jingine ni kuwa hao watu wanaochagua, (mostly sisi wapiga kura na waandaaji), ni vijana wa siku hizi, ambao hatuna hobbies za kujua historia ya nchi hii, nani kafanya kipi muhimu, nk. Ndo maana kwenye hiyo list unawakosa watu walioachivu kikwelikweli kama Prof Tibaijuka, Mama Kairuki, Dr Migiro, Mama Kate Kamba, Dr Rwakatare, akina Siti binti Saad, etc. Haya tuendelee kupotezana, ulaji wa watu huu

    ReplyDelete
  17. Mbona siwaoni wakinamama wa mikoani na uswahili hapa katika hizo tuzo?

    Hapo naona ni watu wanaojuana na kukutana kwenye mitaa yao ya MASAKI, OSTERBAY, MIKOCHENI na UPANGA. Ni wale wale masocialites wa mjini kama sikosei.

    Hivi hawa wamemsaidiaje mwanamke wa kawaida kweli, ukimuondoa Marehemu Bibi Titi na wachache ambao mchango wao unapitia kwenye ajira zao kama huyo mama wa Tanzania Education Fund, otherwise yeye kama yeye amefanya nini hasa kwa juhudi zake binafsi?

    Kuna kinamama wanachakarika huko Moshi, Arusha, na hata hapo Dar kulea watoto yatima tena kwa tabu!

    Kuna kinamama wajasiriamali wameanzia chini kabisa kwenye mtaji wa shs elfu ishirini na sasa wana biashara kubwa kubwa tu, hawa ndio changamoto na wangepaswa kuwa recognized. Lakini kumpa tuzo mtu ambaye maisha yake ameyapata kwenye silve plate ni kitu cha kuchekesha. Lakini ndio BOngo yetu hiyo ya matabaka na kujuana.

    ReplyDelete
  18. JAMANI HATA MKE WANGU AMEFANYA MENGI...ANAHANGAIKA NA WATOTO WATATU MIMI NIKIWA KAZINI..AWAPIKIE AWALISHE AWAVALISHE AFANYE NAO HOMEWORK KISHA AHAKIKISHA WANAJIFUNZA MILA NA DESTURI NA UTAMADUNI UTAKAOWAFANYA WAWE ACCEPTABLE MEMBERS WA SOCIETY MBONA YEYE HAKUPATA AWARD? KUNA MKONO WA MTU HAPA...!! MDAU-NY, USA

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 03, 2013

    kipofu na hadithi ya punda....nipite zangu mie!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...