huyu ni mmoja wa wanaosadikiwa kuendesha genge la utapeli linaloingia mtu kwa gia ya kutaka usaidie kupata tenda WFP ya kuuza dawa ya kuhifadhi chakula huko Kigoma, ambapo wadau wengi wameshalizwa.
huyu hapo alipo ni kituo cha polisi ambapo alinaswa baada ya mwanamama aliyemlia milioni 3 awali kumwita ammalizie milioni 2 alizodai zimebaki kabla ya kutoa sample ya hiyo dawa apelekewe supplier ambaye ni mzungu. mtego ukawekwa na alipopokea pesa na kutoa hiyo sampo ambayo ni juisi ya nini sijui akanaswa.
utapeli kama huu wamefanyiwa watu wengi na tayari habari zimezagaa kila mahali lakini inaonesha bado watu wanazidi kulizwa, na wengi zaidi wamepigiwa simu na hao jamaa na kuchomoa kwa kujua wao ni matapeli.
Majuzi mdada mmoja alifanikiwa kuwanasisha polisi matapeli watatu ambao walifikishwa kituo cha oysterbay wakiwa na gari ambalo likaja kugundulika ni la wizi. habari ambazo Globu ya Jamii imezipata ni kwamba hao jamaa watatu wameshaachiwa kwa kile kinachosemekana kukosekana ushahidi. yaani jamaa walidakwa kabla hawajapokea pesa na kutoa hiyo sampo.
wadau wengi wameilalamikia Globu ya Jamii kudai kwamba jeshi la polisi, pamoja na kujua kamchezo hako, lakini linachukulia kama ni masikhara kwani ni takriban miezi sita sasa toka jamaa waanze kucheza kamchezo hako lakini hawajanaswa na genge lao kuvunjwa. wadau wanahoji kulikoni???

mdau uliye mgeni ya utapeli huu

BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Keland Primary SchoolDecember 05, 2009

    Hata kama wameachiliwa huru lakini watanzania msichoke kuwafikisha katika vyombo vya dola na kutoa picha zao hadhani ili iwe fundisho kwa wengine

    ReplyDelete
  2. hivi bado tu mnapeleka kesi mahakamani?? hili ni kama zengwe la kesi ya babu seya ushahidi kwani walishindwa kupata calls walizokuwa wanampigia dada na kuanalyse sauti? sayansi jeshi la polisi bado ni kitendawili..

    mimi nilishatoa ushauri kwamba mpk tuwahukumu wawili halafu tuone kama wataendelea na huo ushenzi

    maskini dada wa watu sijui yatayomkuta

    ReplyDelete
  3. kwa mtindo huu wa kukamata watu na kuwaachia ndio unasababisha wananchi kujichukulia sheria mkonon

    ReplyDelete
  4. sasa huu ni uzembe au tuseme jeshi la polisi nalo linahusika? ok hakuna ushahidi katika hilo la utapeli, je vipi kuhusu hilo gari la wizi? Maana katika nchi zingine kitendo cha kukututwa na mali ya wizi na hususani km mali hiyo is repoted stolen, basi wewe uliokutwa nayo ndio utakaefikishwa kortini km mwizi. Jamani sawa kuna rushwa lakini bongo imeoza wanaostahili kufungwa hawafungwi tutafika kweli?

    ReplyDelete
  5. Hata babu nanihii wanaweza kumuachia, bila aibu!

    ReplyDelete
  6. HAPA NAONA KUNA UMUHIMU WA KUCHUKUA SHERIA MKONONI. KAMA MTU ANAFIKISHWA POLISI ANAACHIWA ILI HALI FIKA INAFAHAMIKA NI TAPEL, NASEMA KUNA UMUHIMU WA KUCHUKUA SHERIA MKONONI,YAANI TUNATAKIWA KUWA RAIA WENYE HASIRA!!!

    ReplyDelete
  7. ex Michuzi girl frendyDecember 07, 2009

    oh dear! waliachiwa kwa kukosa ushahidi!!! sasa huyo dada aliyewakamatisha si ina maana maisha yake yako hatarini? akidhurika na hawa matapeli nani atakuwa responsible? Huyo dada namshauri aende ubalozi wa nchi mojawapo za magharibi akaombe visa atimue sababu maisha yake yako hatarini!
    Angekua huku angepewa witness protection program angekuwa ana uhakika na usalama wake lakini huko ndo hivo tena. Dada nakuombea Mungu akulinde ur own government has just put ur safety in jeopardy!

    ReplyDelete
  8. heeeeeeee sijaielewa hii "ex Michuzi girl frendy"

    michu vp tena apa...

    wenye hela ndo wanasihi,na habari ndo iyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...