Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Tigo wamefanya ziara katika hospitali mkoani mbeya na kugawa (Meta)na kutoa msaada wa mablanketi mia mbili katika Hospital ya Rufaa kitengo cha kinamama, na kugawa mengine mia tatu kwenye hospitali zingine tegemezi mkoani Mbeya zikiwemo Makandana iliyoko Tukuyu, hospital Mbozi, Hospital kuu ya rufaa pamoja na hospitali ya ItendE ya JKT mkoani humo.
Katika ziara hiyo uongozi wa Tigo kwa kushirikiana na wafanyakazi wake wa huduma kwa mteja na timu ya mauzo (direct Sales Team) wametembelea wazazi na watoto waliozaliwa na kutandika baadhi ya mablanketi katika vitanda vilivyokuwa wazi katika wadi za hospitali hizo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Tigo Bw.Jackson Mbando ameueleza uongozi wa hospitali ya Rufaa Mbeya kitengo cha kinamama kuwa “lengo kuu la kampuni ya Tigo ni kutoa shukrani kwa wateja wake wote mkoani Mbeya na kudhihirisha kuwa tunawajali wateja kwa kuhakikisha wanakuwa na afya njema kwa njia ya kupambana na changamoto zinazokabili sekta ya afya.
Naye mkuu wa idara kitengo cha kinamama ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya kizazi na uzazi Profesa Joseph Mlay ametoa pongezi na shukrani kwa kampuni yaTigo kwa kuweza kutoa msaada huo na kueleza kuwa mablanketi hayo yatawasaidia wazazi wengi wanahudumiwa hospitalini hapo mara kwa mara.
“Kuna wakina mama wengi sana wanaojifungua hospitalini hapa META na tufahamu watoto wanahitaji sana joto la mama ili kuzuia magonjwa kama nimonia na kwa kuwa joto la mama peke yake halitoshi hasa kwa baridi kali mkoani Mbeya basi Tigo mmefanya vyema na niwapongeze kuwa mmelenga sehemu nzuri sana ya kuleta msaada huu.
Akiendelea kutoa shukrani kwa niaba ya mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa amesema kampuni ya Tigo iendelee kutoa misaada zaidi ili kila kitanda kimoja kiweze kuwa na mablanketi manne au matano kwakuwa idadi ya vitanda hailingani na idadi ya wagonjwa.
Aidha amesema katika msimu huu wa mvua na baridi mablanketi mengi zaidi yanahitajika kwakuwa wazazi kati ya ishirini na tano na hamsini huzalishwa kwa siku.
Pia amewasihi wadau wengine wajitokeze kwa wingi katika kutoa misaada na kuomba kipaumbele wapewe Rufaa wadi ya watoto Mbeya,Rujewa hospitali na Makandana na Mbozi.
Kampuni ya tigo inaendelea na ziara yake mkoani Lindi na Mtwara hivi karibuni. msaada huo uliotolewa mkoani Mbeya utagharimu jumla ya shilingi milioni sita na laki tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...