KIPA wa zamani wa Yanga, Juma Mpongo ni miongoni mwa wachezaji wanne walioongezwa na Moro United katika dirisha dogo la usajili wa timu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Mpongo aliyewahi kuidakia Twiga SC iliyowahi kucheza Ligi Kuu mwanzoni mwa miaka ya 2000, ametua Moro akitokea Rwanda alikokuwa anaichezea soka ya kulipwa katika klabu ya Electrogaz inayomilikiwa na kampuni ya umeme ya Rwanda.
Mbali ya Mpongo, wengine wapya ambao pia ni wachezaji huru ni mabeki Abdulrahman Matanda aliyeichezea Prisons ya Mbeya msimu uliopita na mshambuliaji Said Ally.
“Said aliichezea Moro United msimu uliopita, lakini hakusajiliwa mapema kutokana na kutingwa na shughuli binafsi na hivyo kuchelewa usajili, hivyo anarudi nyumbani.
“Na mchezaji wa nne ni beki, anaitwa Amani, lakini kuna taratibu ndogo ndogo zinakamilishwa na habari zake zitaanikwa rasmi ndani ya muda mfupi.”
Awali, Moro United ilipanga kusajili washambuliaji wawili, lakini kutokana na ubora wa vijana wa timu ya U-20, benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Juma Mwambusi limeona ni vyema iwatumie zaidi vijana hao kwani uwezo wao hauna tofauti na ule wa wachezaji wengine wazoefu waliokuwa wanawindwa kusajiliwa.
“Kwa mfano, katika under 20 tuna nyota kama Thomas Ulimwengu ambaye pia yupo katika kikosi cha Marcio Maximo, yuko Lambele Jerome, Michael Victor na wengine, mahiri kwelikweli. Hawa wakiungana na akina Ndabila (Yona), Hussein (Swedi) na wengine, hatutakuwa na presha katika mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.”
Kutokana na kukamilika kwa usajili, timu inatarajiwa kuingia kambini mara baada ya kukamilika kwa michuano ya vijana ya U-20 kwa timu za Ligi Kuu.
IMETOLEWA NA:
ERIC ANTHONY
-MSEMAJI WA MORO UNITED
0755 755 551/ 0717 092 020
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...