Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Amani abeid Karume akiangalia waya maalum wa kusambazia Umeme utaopita chini ya bahari kutoka Tanga hadi Pemba, kazi inayofanywa na meli ya Nexans Skagerrak kutoka Norway pichani chini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. tuwape nchi yao jamani.. si wanaitaka? tutawauzi umeme, vyakula na watatusaidia kulipa kodi kama forena

    ReplyDelete
  2. Mliona Pemba imetulia,hakuna mgao wa umeme ijapokua si wote wenye umeme,sasa mnataka kuwaweka katika mgao na deni,Huo umeme wenu wa masharti leo kuna maji kesho hakuna hautaki mtu,SASA Kama mnataka kuuza umeme kwa nini msiitoe hiyo nchi yetu?KWA SABABU MNANUFAIKA NYUMA YA MIGONGO YETU,HATUNA THAMANI KABISA SASA TANZANIA KWA SABABU YENU.HATUJIVUNII CHOCHOTE NA TUMEFUNIKWA,HAO VIONGOZI WA ZANZIBAR HAWANA MPANGO WOWOTE NGOJA CUF IINGIE MADARAKANI MTACHUKUA HUO UMEME WENU SIO,MAENDELEO YALIFIKA ZANZIBAR KWANZA MKAYABANA SASA MNASEMA NINI?TV YENYEWE NA INTERNET MMEPATA JUZI SIO.

    ReplyDelete
  3. Viongozi wa CCM wote hawana mpango,ya nini kukiweka kisiwa cha Pemba mashakani tena?SHIDA YA UMEME IPO LAKINI SIO MGAO,SSA MNAWAPELEKEA MGAO WA BURE,HAWA CCM WAMEROGWA?Au ndio wanatafuta sababu kuwa umeme unatoka bara? wizi tu huko bara mara dowans mara upuuzi gani hawana mpango wowote,

    ReplyDelete
  4. Kwani sisi tunahitaji msaada wenu,nyinyi sio munajipendekeza kwetu.Mumeuwa nchi yetu kwa kutaka mututawale.Kabla ya nyinyi wakoloni weusi nchi yetu ilikuwa nzuri sana,hata viatu mulikuwa munakuja kununua Zanzibar.Hiyo nchi yenu mpaka bajeti yenu haitimii mpak a kwa wahisani.Nyinyi ni ombaomba tu.

    ReplyDelete
  5. nje kidogo ya mada - kwa hakika huwa ninaburudika ninaposoma habari juu ya vigogo wetu jinsi tunavyotaja. katika maelezo ya picha ninafikiri mwandishi amesahau neno moja mheshimiwa. ubainifu kamili ulipaswa kuwa "Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Daktari Amani Abeid Karume" ... haki ya Mungu raha tupu!!!!

    ReplyDelete
  6. Mimi ni mtanganyika na napenda sana umoja, ila hizi comment za hawa waunguja zinanifanya niwaze tofauti kabisa. Hawa jamaa wana mawazo mabovu kabisa ,kwamba tunawanyonya, nafikiri imefika wakati sasa tuwaachie visiwa vyao alafu waanze kukatana mapanga wenyewe wazanzibari na wapemba ili wajifunze.

    ReplyDelete
  7. Hizi ni habari njema kwa kisiwa cha Pemba, haswa wale wamiliki wa ardhi pembezoni mwa bahari.

    Tukizingatia kama Unguja mashamba yote ya pembezoni mwa bahari yameshajaa, utalii utakimbilia Pemba.

    Ningeliwashauri wale wenye jamaa zao na mashamba yao wakawa makini na kuchukua makosa yote yaliyofanyika Unguja kama ni funzo.Unguja ilifanya kosa kubwa kuuza ardhi, hili kosa lisirudiwe Pemba...ARDHI INAKODISHWA SIO KUUZWA!!!!

    Kila la kheri!

    ReplyDelete
  8. Umeme Upi? Huo ambao unakatika mpaka J.K. Nyerere Airport? Lol..!! Mdau, New York, USA

    ReplyDelete
  9. tunaomba hiyo tenda wapewe WACHINA

    ReplyDelete
  10. haki ya nani vile,,,tena???

    naskia dar bado kuna mgao?kwanini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...