Violet Mzindakaya a.k.a Sister V
SWALI: Je utaweza kuwa mpiganaji katika siasa Kama baba yako manake baba yako ni mkongwe katika siasa toka enzi za hayati Mwl.Nyerere?

VIOLETH:Kwanza mpaka hapa ni mpiganaji kwa sababu nimejitahidi sana kumwangalia baba yangu nini anakifanya, mzee mzindakaya amefanya kazi na ana historia kubwa sana sina haja ya kuielezea kila mtu anatambua.
Ni mkongwe ndani ya chama na ni mkongwe katika uongozi wake kisiasa naendelea kusema kwamba sitaki kumwangusha yale yote aliyoyatenda mema mimi nitachukua kama yalivyo na kuyaendeleza kama binti yake ambaye naamini kabis kwamba katika muda wake wote huu aliokaa kwenye siasa bado nina kazi ya ziada ya kuendeleza kuweza kumfanya awepo na upiganaji unaanzia chini kwenda juu.
Nashukuru enzi za mwalimu nilikuwepo lakini nilikuwa bado mdogo Sana nilipata bahati ya kwenda butiama wakati huo mzee alikuwa ni mkuu wa mkoa wa kigoma nilipokuwa kwenye media pale sasa ndipo nilipoanza kumfahamu baba wa taifa vizuri. kadi yangu ya chama cha mapinduzi nimeipata mwaka 2000 nina miaka kumi sasa ndani ya CCM kuanzia vijana, na kadi zote za UWT na wazazi kwa hiyo upiganaji wangu mimi ndio umeanza rasmi na mzee mzindakaya kwenye halmashauri kuu ya mkoa akatangaza rasmi kwamba anastaafu kwa sasa akasema naoondoka.
Kwa hiyo hilo ni jukumu la sisi vijana wake kuendelea kuwemo kwenye siasa. mimi nitaendelea kulibeba jina lake na nitaendelea kuwa mwanasiasa ambaye kwa sasa hivi natumai ndio muda wangu muafaka kiumri na hata kwa nafasi ambayo nimeishika ni mdogo sana kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ni sio kitu kidogo ni kikao kikubwa sana cha chama chetu ambacho kinafanya maamuzi makubwa kabisa ya kitaifa kuchagua viongozi ambao ndio wanakuja kuwa wawakilishi wetu wabunge kwa hiyo si kazi ndogo kwa hiyo nitaendelea kwa kuyafanya yote aliyoyacha katika mustakabali ambao ni mzuri wa maadili na miiko ya viongozi wetu sisi hasa wa CCM.
kwa intavyuu yote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. It is interesting amesema role model wake ni Rais JK.Anaonekana amejizatiti kuongoza nchi yako. Ningependa tu kujua hivi baba yako amefanya maendeleo mangapi huko jimboni kwake ukizingatia ameongoza toka enzi za Mwalimu? Sisemi lawama za baba apewe mtoto maana itakua sio haki lakini tunapompa sifa Mzindakaya kuwa mwanasiasa mkongwe tusizungumzie tu kushika nyadhifa kwa muda mrefu cha muhimu ni mabadiliko aliyofanya kwa huo muda. Nawakilisha.

    ReplyDelete
  2. michuzi hongera kwa kubania maoni kuhusu lile swali kuhusu MO kurudiwa-rudiwa. nisamehe bure ingawa sijuwi tusi hapo liko wapi.

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani tumpe huyu dada nafasi..japokuwa kwa sasa ninachoona ni uzuri tu kwani simfahamu vizuri. Mzindakaya sitasema sana..ila kutumia vyeo na nafasi za wazazi wakati mwingine kunaweza kumuangusha mtu...kwavile mtu lazima awe tayari kukubali sifa...na lawama kama atamchukua mzazi kama role model. Kuwa mtoto wa mwanasiasa au Kiongozi hakumfanyi mtu kuwa kiongozi bora. Ila ni vizuri angalau kuna hiyo Nia..!! Yetu macho sisi wengine wazazi wetu hawakuwa na hizo nafasi..japokuwa lazima tukubali kuwa hatuwezi wote kuwa viongozi...Dada..tumia jeuri yako..kutumia jina la baba kutakuponza..huo ni uzoefu wa siasa tu...uko tayari kuwabeba wasioona kuwa baba yako alikuwa mtu mashuhuri hasa katika mabadiliko? In real sense ukionyesha watu kuwa you are two different people and you are a person of change, you have a better chance..nani anataka role models za miaka ya nyerere tarehe hizi?...you have a shot..but use your own charisma and intelligence usidandie cheo cha baba..goodluck..!! Mdau-USA

    ReplyDelete
  4. uongozi tanzania ni wa kuridhishana? umeanza visiwani (toka rais, mawaziri na hata wakuu wakurugenzi) na ushaanza kuingia na bara kidogo kidogo! watu wanapata kura kwa kuvaa makoti ya baba zao. Tanzania tambarare!!!!!

    ReplyDelete
  5. ...labda mi sijaelewa swali, lakini naona swali linamtaka "Sister V" kujielezea yeye kama yeye, na si historia na maadili ya Mzindakaya.

    Mpaka sasa ana sifa gani na amefanya nini kuendeleza mapigano juu ya Taifa letu? Na sio story za kwamba alienda Butiama, aliwahi kumfahamu baba wa Taifa nk.

    "Kwa hiyo hilo ni jukumu la sisi vijana wake kuendelea kuwemo kwenye siasa"....hii sentensi inaeleza wazi kwa nini "Sister V" yupo kwenye siasa.

    Naona uchaguzi mwaka huu utakua rahisi sana. Kaka Michu naomba tuletee wengine kama huyu tuwafanyie "interview".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...