Picha na Habari na John Nditi, Kilosa
WILAYA ya Kilosa ya Mkoa wa Morogoro imeendelea kukabiliwa na janga kubwa la mafuriko kufuatia mito kadhaa ukiwemo wa Mkondoa na Magole kufurika maji ya mvua zinazonyesha katika Mkoa wa Dodoma pamoja na Wilaya ya Kiteto, Arusha na kusababisha maafa mapya kwenye vijiji vya Tarafa ya Magole kwa kubomoa nyumba kadhaa na nyingine kuzingira na maji.
Kutokana na mafuriko yanayoendelea kutokea Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya katika mkutano wake na wananchi wa kitongoji cha Mateteni cha Kijiji cha Mbingiri , Tarafa ya Magole , Wilayani Kilosa, amewataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo zaidi ya mafuriko kuyahama ili kujinusuru na maisha yao.
Mkuu huyo alitoa kauli hiyo jana ( Jan 12) baada ya kutembelea maeneo mapya yaliyokubwa na mafuriko ya Tarafa ya Magole baada ya kunyesha kwa mvua katika Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa, Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Kiteto , Arusha na kusababisha mito hiyo ukuwemo wa Magole kufurika maji na kuleta mafuriko yaliyozingira nyumba kadha na nyingine kubomoka katika kitongoji cha Mateteni.
Pamoja na mafuriko hayo kwaathiri wananchi wa Kijiji cha Mbigiri hususani kitongoji cha Mateteni, pia yameiathiri kambi ya wachina ya ujenzi iliyopo eneo la Magole Wilayani humo.
Kambi hiyo ya Kampuni ya Kichina ya ujenzi wa barabara ya Mikumi – Kilosa hadi Kilindi Mkoani Tanga , ambayo ujenzi wake imegawanywa kwa sehemu ikiwemo ya Magole hadi Turiani ,ambapo maji ya mafuriko hayo yameingia ndani ya makontena vifaa vya ujenzi pamoja na jengo la ofisi na kuharibu kompyta mbili ikiwemo ya mkononi ‘laptop’.
Meneja Mradi wa usimamizi wa ujenzi wa kambi ya Magole hadi Turiani, Robert Liu , alisema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati alipoitembelea Kambi hiyo kufuatia kukubwa na mafuriko hayo jana alfajili.
Kwa mujibu wa Meneja mradi huyo ambaye ni raia wa China, alisema maji hayo ialiingia kwa wingi ndani ya eneo la kambi hiyo na kupennya hadi kwenye makontena yaliyohifadhiwa eneo la Kambi huyo na kujaa ndani na kusababisha vifaa mbalimbali vya ujenzi kuharibiwa na maji hayo.
Hata hivyo alisema magari, makatapira na mitambo mingine ya ujenzi ipo salama licha ya kuingiliwa na maji hayo , licha ya ofisi yao kujaa maji ambapo kufuatia kuzingirwa na maji hayo waliamua kuchimba tuta kubwa kwa kutumia vifaa walivyonaavyo ili kuzuia maji yaziendelea kuingia kambini hapo.
“ maji yametuingilia alfajili leo ( jana) na yameingia kwenye makontena yaliyomo na vifaa vya ujenzi …naweza kusema vimeharibika , pia kompyuta mbili ikiwemo laptop zimejaa maji , isipokuwa mitambo na magari yapo salama …ofisi yetu pia imeingiliwa na maji na umetukuta tupo kwenye kikao cha kujadili hali halisi…lakini tumechimba tuta kuzunguka kambi yote ili maji mengine yasijekutuathiri zaidi “ alisema Liu
Kufuatia hali hiyo ya mafuriko, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi wote ambao nyumba zao zimeingiliwa na maji na ujenzi wake ni watope kuanzia msingi kutakiwa kuacha kuzutumia kwa wakati huu wa mafuriko ili kunusuru maisha yao.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi hayo hususani wa kitongoji cha Mateteni cha Kijiji cha Mbingiri, Tarafa ya Magole, kuchukua uamuzi wa kuhamia kwenye maeneo ya miinuko wakati wa mvua zinapoendelea kuwa nyingi ili kuepusha maafa zaidi.
“ nimezungukia maeneo yenu …nimeona bado kuhahatari kubwa sana ya nyumba zetu kutuangukia ..bado maji ni mengi na mvua zinaendelea kunyesha, hazinyeshi hapa kwetu bali ni maeneo mengine …maji haliyoingia kwenye nyumba zenu si mvua za Morogoro , maji yanatoka Dodoma , yanatoka Kiteto na yanapita kwenye mto huu “ alisema Mkuu wa Mkoa huyo
Hata hivyo alisema ni wajibu wa Serikali ya Wilaya na Mkoa kuendelea kuwasisitizia wananchi wa Wilaya hiyo na meneo mengine yenye tabia ya kukubwa na mafuriko , kuchukua tahadhari kubwa pindi mvua kubwa zinaponyesha kwa kuyahama makazi yao na kwenda kuishi kwa ngudu na jamaa wakati serikali inapofanya jitihada za kuwasitiri kwenye makambi.
“ sasa hivi wananchi ni waelewa wa majanga kama haya na hasa baada ya athari zilizotokea Mjini Kilosa ambao mafuriko yamepoteza watu wawili na wengi kuhathiriwa …hivyo ninaimani wataondoka maeneo yote yenye mafuriko na kwenda kuishi kwa ndugu na jamaa , wakati Serikari ikijipanga” alisema Mkuu wa Mkoa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendegu, alisema Wilaya hiyo imekubwa na janga kubwa la mafuriko ambayo yametapakaa kila sehemu na kuwaomba wananchi kujihadhari na kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi ya vijiji, Kata , Wilaya na Mkoa pindi wanapoingiriwa na mafuriko hayo ili wawezekusaidiwa kuokolewa kwa haraka.
Hata hivyo aliwaomba wananchi wenye makazi sehemu za miinuki kuwasaidia waathirika ambao nyumbazao zimebomoka na kuzungira na maji kuwahifadhi kwa muda wakati hatua nyingine zikiendelea kuchukuliwa na Serikali ya Wilaya na Mkoa.
Mbali na kuwaomba wananchi hao, pia aliwataka akina mama kuhakikisha wanawangalia vyema watoto wao kipindi hiki cha mafuriko ya mvua kutokana na maeneo mengi yaliyochimbwa mashimo kujaa maji na kutaharisha maisha ya watoto kuweza kutumbukia.
Awali Mwenyekiti wa Kitogoji cha Mateteni ambacho chenye wakazi wengi katika Kijiji cha Mbigiri, Tarafa ya Magole, Iddi Mwingilia, alisema hatua zilizochukuliwa ni kufanyika kwa tathimini ya kujua ukubwa wa madhara hayo pamoja na idadi ya nyumba zilizobomoka , kuzungirwa na idadi halisi ya wahanga.
Hata hivyo alisema inakadiriwa nyumba zaidi ya tisa imebomoka kutokana na mafuruki hayo na nyingine kadhaa kuingiriwa na maji kutokana na mafuriko ya mto magole kujaa maji hayo.
Naye Mustapher Chopeka, mkazi wa kitogoji hicho, alisema ni zaidi ya siku tatu mafuriko hayo mejitokeza na kwamba yaliongezeka zaidi siku ya Januari 12, mwaka huu ambapo maji yaliwazingira kuanzia majira ya saa nane usiku na kauendela hadi alfajiri ya siku hiyo.
“ haya maji ya alfajiri ndiyo yalikuwa ni mengi na yamesababisha madhara makubwa na tunashukuru mungu wakati huo watu walikuwa macho baada ya kuigiliwa saa nane usiku …hatujasikia mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha” alisema Mkazi huyo
Mafuriko katika Wilaya ya Kilosa hususani katika Kata nane ukiwemo na Mji Ndogo wa Kimamba yalianza kuanzia Desemba 26, mwaka jana ambapo yaliwaathiri zaidi ya watu 23, 980 sawa na kaya 5,605 na kuwafanya watu 9,970 kukosa makazi na kuishi kwenye kambi za muda 16 na nyumba 4,699 kuzingirwa na maji na nyingine 1,143 kubomoka hadi Januari 5, mwaka huu.
Si watu wote wenye ndugu na jamaa ambao wanaweza kukimbilia kwao
ReplyDeleteJitihada na misaada viendelee lakini pia Tumuombe Mungu atuepushie madhara na atupe mvua za kiasi.
ReplyDeleteMafuriko haya yanatokana na ukataji miti hovyo ambao umesababisha kina cha mto kupungua hivyo maji kusambaa hovyo, haya ndiyo malipo ya uharibifu wa mazingira. Lazima tujiulize ni vipi mvua kidogo ya siku moja mto unafurika na kwa wale wanaolijua daraja hilo la Magole watakuwa wamejionea wenyewe kwa miaka mingi changa ulivyokuwa umekaribia kuliziba kabisa hilo daraja. Ukataji miti kwenye milima usipodhibitiwa hali itakuwa hii hii kila mwaka na hivi sasa mji wa Morogoro na uko hatarini kuangukiwa na mlima wa Uruguru.
ReplyDelete