Hi ankal,
Leo asubuhi pale barabara ya kilwa road hapa Dar! Kwenye kipita shoto cha JKT Mgulani, jamaa aliona anachelewa kuzunguka! Akakunja hapo hapo kwenye tuta na kuaruka chwaaaap! Akawa kafika. Bongo Tambarare kama wanavyosema FFU wa Ughaibuni chini ya afande mkuu Ras Makunja. Na hapo hafanywi kitu...
Wape wadu hyo!

Mdau
Ekonjo
Sent from my BlackBerry® smartphone

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Huyo jamaa mwendawazimu bila shaka atakuwa ameamka na konyagi kichwani.maana chui chui haiwezi kumpagawisha kiasi hiki....dah kwa style hii lazima tuendelee kufa kama mbu.

    ReplyDelete
  2. mdau Ekonjo, jinsi ulivyoelezea tukio hili, mie mbavu kushneh kazi yake. Kweli wachekeshaji mpo wa kutosha! LOH ha ha haha!

    ReplyDelete
  3. Agano la kaleJanuary 20, 2010

    Kwanini uogope kuvunja sheria wakati waharifu hawaadhibiwi? Alichofanya huyu driver ni kitu cha kipumbavu sana, na wadau wengi humu hawataipenda hii.

    Kwa akili ya kukurupuka, ningesema kwamba huyu dereva asiruhusiwe tena kuendesha gari, afungwe jela na apigwe viboko, na pia agharamie matengenezo yote ya uharibifu aliousababisha.

    Lakini pia akili yangu inanisuta kwamba; kumpa huyu dereva adhabu kali wakati kosa lake ni dogo sana ukifananisha na makosa ya watendaji wakuu wa serikali yetu; raisi mstaafu, waziri mkuu aliyelazimika kujiuzulu, mawaziri walionunua rada kanjanja, viongozi wa EPA na RICHMOND na kadhalika. Kama wote hawa hawaadhibiwi, jee kumuadhibu dereva huyu itatosha kuleta "law and order" katika nchi yetu?

    Jibu ni kwamba hapana.

    Ingawa ukweli ni kwamba huyu dereva atapewa adhabu kali sana kwa sababu yeye siyo mtendaji wa serikali na wala siyo mteule wa rais kikwete.

    Kwa mwenendo huu hatutafika kamwe

    ReplyDelete
  4. kwa kweli inavyo onekana ni kuwa hili lori lilikuwa linapita kwa kukimbia mizani halafu pili linaharibu njia mpya ambayo kwa kweli watanzania tutalipa mpaka vitukuuu vyetu haya madeni ya kujengewa barabara uhalali wa hapa ni kuwa gari litaifishwe na pili Tanroads wanatakiwa wachukue Insuarance ya gari hilo kwa malipo ya ukarabati wa hiyo njia maana baada ya lori kutolewa lazima pafanyike matengezo.

    ReplyDelete
  5. mvunja nchi ni mwananchi,halafu kesho watu wanalalamika brbr zetu hazidumu,namna hii hatufiki popote

    ReplyDelete
  6. Hizo "shoti-kati" zinatokea kila barabara bongo na nikila siku. Wenyewe (wabongo) wamezoea "kufaulisha"

    ReplyDelete
  7. hahahaaa mi nilihisi tu lazima ukipita utai-snap hili lori. Nilipita late sana pale JKT nikalikuta, dah kweli pombe ya mnazi sio chai jamani..


    Eddymak

    ReplyDelete
  8. ADILI NA NDUGUZEJanuary 20, 2010

    Aaaaii!!Imeniuma jamani. Dududu!!Hata kuthamini uzuri wa barabara? Natamani kutukana. Kudadadeki?**^""xx##

    ReplyDelete
  9. Bongo kweli tambarare ukiwa na shs10,000 tu mfukoni unaweza kuingia na gari lako mpaka kizimbani mahakamani na polisi na hakimu watakuwa wanachekelea ulaji tu.

    ReplyDelete
  10. NIMEPITA MARA KADHAA SEHEMU HII NA HII BARABARA NI KATI YA BARABARA MBOVU KABISA KUJENGWA KATIKA MIAKA YA KARIBUNI JIJINI DAR ES SALAAM.
    TAZAMA VIZURI NA UTAKUTA MZUNGUKO HUO NI MDOGO KWA LORI LA AINA HAPO JUU.VILE VILE VIZINGITI VYA MATOFALI(KERSTONES) NINDOGO SANA NA FUPI.
    ZAIDI YA HAPO USIKU KWA VILE HAKUNA TAA, HAKUNA MABANGO YOYOTE YA KUONYESHA MBELE KUNA MZUNGUKO.
    WIZARA YA MUINDO MBINU/TANROADS WAMEKABIDIWA BARABARA BOMU AMBAYO HAIKUPATA USIMAMIZI WA KITAALAM TOKA KWA WAHANDISI WETU.
    LINGANISHA NA BARABARA ZILIZOJENGWA NA KONOIKE MIAKA 15 ILIYOPITA BARABARA ZILE BADO ZINADUNDA.

    ReplyDelete
  11. ebwana eeh Bongo noma December nilikuwa likizo Bongo madereva wote wanaendesha style hii hii manake nilishindwa kudirve mdogo wangu akawa yeye ndo ananidrive alivokuwa anafanya anajua mwenyewe manake nilikuwa najisikia aibu nafumba macho nifumbua sioni drive mwengine anayeshangaa kumbe nivitu vakawaida kudrive in icoming lane kucomeka u turn nk drive bila kuvunja sheria haoni raha

    ReplyDelete
  12. Mchapa KaziJanuary 21, 2010

    Wadau kabla ya kulaumu inafaa kuuliza hilo tukio lilitokea saa ngapi.

    Kama ilikuwa usiku na kama mnavyoona hiyo round about haina reflectors (viakisi) dereva anaweza asione kwamba kuna round about hapo.

    Na hilo ni lori, barabara swaafi imenyooka, ina lami, na usiku huwa hakuna magari mengi kwa hiyo dizaini dereva alikuwa amechochea mwendo hivyo akashindwa kusimama ghafla, ndio akaparamia tuta.

    ReplyDelete
  13. Hii! kamanda wa ffu wa Ngoma africa,haya tazama sasa kazi ya bongo tambarale yako? kweli bongo tambarale

    ReplyDelete
  14. Ama kweli!! Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Kwenye ITV leo 21/1/2010 saa 12 jioni dereva wa lorry amehojiwa akasema; yeye alitoka Tanga na mgeni wa hiyo njia mpya, kulikuwa na daladala linakuja akakwepa na kujikuta amepack kwa lazima hapo. Nampongeza kwa hilo hakuwa na jinsi kwani ameokoa maisha ya walikokuwa kwenye daladala. Tafakari,,,,, kama asingefanya hivyo ingekuwaje? Hiyo barabara itatengenezwa kwa kodi zetu.

    ReplyDelete
  15. Natumai TANROADS watakuwa wameona hii na watarekebisha kabla hayajatokea maafa makubwa.

    Ni kweli ile roundabout imebanwa sana na hili pia wanatakiwa kulirekebisha.

    ReplyDelete
  16. Dereva hana kosa. Hamna kiashiria chochote cha kuonyesha kuna Round about. Ukiangalia kwenye picha alijaribu kufunga breki akaachia (alama za tairi barabarani). Angekomaa na kukata kona basi angeangusha lori. Nampa big up dereva kwa uamuzi wake wa kupanda kizunguko.

    TANROADS, Alama ziko wapi?!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...