Ankal, naomba wadau watathmini utajiri wa nchi yetu na watoe tamko kama kweli tunashindwa kujenga daraja kama hili hapo ferry kuelekea Kigamboni. Hili ni daraja lililopo nchini Mali.
Kweli inauma.
Mdau Mali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. sasa meli zitapita wapi tukijenga daraja kama hili kigamboni? underwater tunnel ndio solution

    ReplyDelete
  2. tutaweza kulijenga kama mafisadi wote watakuwa hawapo kwenye system.

    ReplyDelete
  3. Mi naamini hatuwezi ikiwa ujenzi wa nyumba ya Gavana tu ni mabillion ya pesa!itishindikana kujenga daraja?

    ReplyDelete
  4. Uwezo wa kujenga kama hili tunao kabisa. lakini Ferry halitakiwa kama hili linatakiwa kubwa mara tano ya hili ili meri ziweze pita kuelekea bandarini.

    ReplyDelete
  5. Mafisadi watakula wapi? Kitu kingine ni serikali kutokuwa na priorities ktk mambo muhimu.

    ReplyDelete
  6. Huezi jenga daraja kama hilo kwenda Kigamboni wewe kwani litazuia meli!

    ReplyDelete
  7. mdau anatoa wazo nasi tujenge daraja. suala la meli zitapita wapi au ukubwa daraja si hoja.
    Hoja ni nia,uwezo tunao.

    ReplyDelete
  8. Tutengeneze kwanza ile 'kip left' ambayo Ankal amekuwa akiibandika hapa. Sijaiona siku nyingi, sijui ameshapigwa marufuku kuifotoa?

    ReplyDelete
  9. Mitazamo tofauti, nafikiri kwanza bandari kuu ihamishwe kubaki bandari kwa ajili ya meli ndogo za abiria na mashua nk ambazo zinaweza kupenya chini ya daraja, itaongeza nafasi kwa makazi ya watu, ofisi kupunguza foleni kuzunguka maeneo yalipo bandari sasa

    ReplyDelete
  10. Itabidi kwanza wawe na plan ya kuihamisha port then ndio watajua wafanye nini kuhusiana na ujenzi wa daraja la kuelekea kigamboni.
    Ndio maana wanawaomba wawekezaji ili waje wajenge mji na daraja na wala wananchi msiwe na shaka atakaetaka kuhama atalipwa na atakae amua kubaki anaweza aka sign contract ya kujengewa na kulipana na hao ma invester.
    Sijui kwa nini mnashindwa kuwa na uvumilivu kabisa watanzania wenzangu.Mambo mazuri hayataki haraka.
    CCM from Chimwaga.

    ReplyDelete
  11. Ninavyojua mimi daraja ambalo linategemewa kujengwa (NSSF wakifanya mchakato wa uwezekanaji) litajengwa baada ya bandari, kama sijakosea huko Kurasini na si pale 'ferry' ya samaki. Sina hakika kama panaitwa Kurasini upande ule :)

    ReplyDelete
  12. Kazi ambayo imetukabili sasa hivi sio kesho.Ni kuitoa CCM chama cha wacache walafi,tawala ya kifalme madarakani.UHAMUZI TUTAKAO UFANYA SASA WATOTO WETU WATATUSIFU HAPO BAADAYE.KAMA TUTAKAA KIMYA WATOTO WETU WATASEMA WAZAZI WENGI HAWAKUWA MAKINI .NDIO MAANA TUNA MATATIZO HAYA SASA.FUTURE NZURI INATAKIWA KUTOA NA KUTEKELEZA SASA HIVI.ASANTE MWALIMU NYERERE MUNGU AKUWEKE PAHALA PEMA.TUMEONA KAZI NZURI ULIYOIFANYA.LAKINI BAADA YA WEWE KUTOKA TU WAKAINGIA WATU AMBAO BALAA LAO LINAONEKANA SASA HIVI.TUMECHOKA SASA TUSIMAME NA KUIONDOA CCM.NA TUANGALIE CHAMA KINGINE NA KULEKEBISHA KATIBA ILI MTU YEYOTE ATAKAE INGIA ATAOGOPA KAZTIBA.NA WATU KUKIMBILIA MADARAKA

    ReplyDelete
  13. KUNA WATU HAWATUMII AKILI HUMU SASA DARAJA KAMA HILO MELI KUBWA ZITAPITA WAPI? DARAJA LABDA LIJENGWE UBAVU WA KURASINI KULE. ILA KAMA PALE FERYY LABDA IWE KAMA DARAJA LA LONDON ENGLAND LA KUFUNGUKA NA HILO HAIWEZEKANI NA UMEME WETU WA KU BAHATISHA. PAZI.

    ReplyDelete
  14. Wakijenga daraja kama hili wawe tayari kuwa na kampuni ya uokoaji watu toka majini.Nijuavyo wabongo wanavyoendesha magari kwa pupa kila siku patakuwa na magari si chini ya matatu chini ya bahari.
    NB kuhusu bandari kuna Two options.
    wajenge daraja lenye urefu(kwenda juu) utaorahisisha meli kupita bila bughudha na pili daraja linaloweza kufunguliwa kuruhusu meli zipite, najua hii option itakuwa ghali kwa sirikali yetu

    ReplyDelete
  15. aliyeanzisha mada lengo lake ni kuchochea watu tufanye tafakari, maana yake siyo lazima tu-copy hilo kama lilivyo.

    alichojaribu hapo ni kusema, hatuna vision ya kujikwamua daraja likajengwa.

    ReplyDelete
  16. Wewe mdau wa Jan, 17 16:00 PM itakuwa umezaliwa baada ya 1985. Huyo mwalimu unayemsifia hakuona kigambo kunahitajika daraja? Alikuwa madarakani miaka 24 na daraja hakujenga. Na si kigamboni mambo mengi yalimshinda. Watu wa kusini wanajua adha ya usafiri. Kaja mkapa kamaliza mambo yote, daraja la mkapa liko fresh watu wanapiga gia za magari yao. Lakini Mwalimu wenu kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha watu wanapanga foleni kwenye maduka ya kaya masaa 12 kusubiri kilo moja ya sukari. Aaaaah, sitaki hata kukubuka taabu tuliyopata.

    ReplyDelete
  17. kwa sababu watu wa mali akili zao fupi ndio maana wamejenga kitu kama hicho,sasa meli zinapita wapi...

    ReplyDelete
  18. Kinachotakiwa sasa ni kusafisha nchi tu. CCM na vitakataka vyake wote waondoke. Bila hivyo mtaishia kuleta madaraja ya wenzenu tu. Uchaguzi unakaribia watabaki kutoa hoja na hope za uongo. Mara oo nikipita nitaweka vijana!! mara ya kwanza ilikuwa nikipita nitaweka wakinamama. leteni hoja za ukweli kuliko kudanganya watu. mtatupeleka pabaya CCM. Na hao wapinzani sion wowote.

    ReplyDelete
  19. US BLOGGERSJanuary 14, 2010

    INGEKUWA RAHISI SANA KUJENGA HILO DARAJA KAMA WATU 3 AMA 4 WANGEKUWEPO KWENYE CABINET YA PRESIDENTI 2010 BAADA YA UCHAGUZI
    1. WAZIRI WA FEDHA AWE PROF. NDULU
    2. WAZIRI WA WANAWAKE NA WATOTO LIUMBA
    3. WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA JOHN MASHAKA
    4.WAZIRI WA MICHEZO JACK PEMBA
    5. WAZIRI WA HABARI NA BLOGS MICHUZI
    6. MICHEZO NA UTAMADUNI KANUMBA
    7. ELIMU YA JUU MTIKILA N.K

    ReplyDelete
  20. Niliwahi kuwa na majadilianao marefu na mmoja kati ya mainjinia toka wizara ya ujenze walipotembelea Washington DC miaka miwili iliyopita.Yeye alisisitiza kuwa ujenzi wa daraja unawezekana lakini lazima tuta lianzie mbali ili likifika feli pawe na muinuko wa kutosha kupitisha daraja juu na meli ziweze kupita chini.Baada ya majadiliano marefu nilimpeleka kuona interchange ya I-495 na I-395pale Springfield,VA.Aliangali kama dakika nne bila kusema kitu.baada ya muda alisema kuwa inawezekana kujenga daraja la feli/Kigamboni magari juu na meli chini bila tuta kuanzia mbali.Nilimpeleka kuona Bay bridge na Baltimore tunnel,MD.Baada ya hapo alisema uwezo tunao lakini utaalamu hatuna.Wadau hii imekaaje

    ReplyDelete
  21. Uwezo tunao tena kwa sana. Vipaumbele ni hayo madudu tunayoshuhudia kila kukicha. Waungwana wetu wana nia na uwezo wa kukimbilia ikulu, lakini sababu hawana!!! ukimuuliza mtu kwa nini unataka kuwa rais anakutumbulia mimacho!!!tumegota tena kwa sana!!

    ReplyDelete
  22. ukiwa na akili finyu utaona daraja lijengwa pale pantoni inapovusha watu....hahahahaha...daraja haliwezi kujengwa sehemu kama hiyooo..kama mdau mmoja amedokeza ipo sehemu baada ya bandari ndipo wanapokusudia kujenga daraja....wao end up kuja na plan kama hizi si wajinga ila wanakuwa wamsha analyse mambo mengi kwenye project kubwa kama hizi. mimi nimeshafanya project kubwa lakini kitu kinachorudisha tanzania nyuma ni usaniii mwingi na raia kutokuwa na uwoga wa kuwa wabadhilifu..."TUTAFIKA VIPI NA NAFASI NYINGI WAMEPEWA WATOTO WA VIGOGO VYENI VYENYEWE FAKE!

    ReplyDelete
  23. Uwezo wa kujenga daraja tunao.Na wataalamu wakae waone ni kipande ipi inafaa kujengwa hilo daraja.Zile pesa zitakazobakia zoteeee kwenye wizara zote za Tanzania na taasisi mbalimbali za serikali ifikapo May - June wakati wa bajeti ya mwaka mpya, wasizivuge vuruge kama walivyozea kila mwaka zotee zirudi serikalini na zianze kujenga na kufanya mambo ya maana. Serikalini kabla ya mwaka wa fedha kuisha ni pesa nyingiiiii mnooooo huwa zinabakia na mwishoni mawaziri na makundi yao huzivuja kwa kujinunulia makochi, magari, masimu ya gharama, masafari, walsha na semina bila mpango. Hizo pesa zirudi na zipangiwe kazi kama hizi za kujenga na kufanya mambo mengine.
    Mafisadi wanyongwe period.
    Tufanye mambo ya maendeleo kwa ajili ya nchi yetu na kwa ajili ya watu wote wa Tanzania.

    ReplyDelete
  24. eee Jehova t=ingilia kati,,,naamini siku tutafika tu

    ReplyDelete
  25. nyie vp kwani meri haziwezi kuzunguka nyuma ya kigamboni au kigamboni inaungana na zanzibar ndiyo point yenu.au vipi mie siwaelewi.mdau.

    ReplyDelete
  26. sasa wewe mdau ulieleta topic hii unataka tanzania tutowe pesa za kuwajengena magavana alias zake majumba ya faragha ili kuondosha bughudha ya mlala hoi? Ni lazima utafutwe haraka na kupewa adhabu kali kwani ni msaliti wa taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...