Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Mwai Kibaki, wakati alipomtembelea Ofisini kwake Harambe House mjini Nairobi Nchini Kenya jana jioni. Makamu wa Rais yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu ya kiserikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed na Rais Mwai kibaki wa Kenya katikati, Makamu wa Rais wa Kenya Dk. Kalonzo Musyoka kulia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe. Mohamed Seif Hatib wa pili kushoto na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe.Seif Ali Iddi, wakiwa katika picha ya pamoja, wakati Makamu wa Rais na ujumbe wake alipomtembelea Rais Mwai Kibaki Ofisini Kwake Harambe House Mjini Nairobi Nchini Kenya jana.

Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema shein kushoto, akizungumza na Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Mama Paulina Kalonzo, walipokutana kwenye chakula cha jioni katika Hoteli ya Intercontinantal mjini Nairobi jana usiku, ambapo Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein yupo Nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Meli ya abiria yazimika ghafla baharini

    Meli ya Kampuni ya Sea- Gul iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, jana ilizimika baharini ikiwa na abiria zaidi ya 300.

    Kuzimika kwa meli hiyo kulisababisha taharuki kubwa miongoni mwa abiria hao, ambapo baadhi walikuwa wakilia huku wakiwasiliana na ndugu na jamaa zao.

    Meli hiyo ilitoka katika Bandari ya Dar es Salaam saa 6:00 mchana na ilitarajiwa kuwasili Zanzibar saa 11:00 jioni.

    Abiria waliokuwa katika meli hiyo, waliliambia gazeti hili kuwa walishuhudia meli hiyo ikipunguza mwendo na baada ya hapo kuzimika kabisa.

    Mmoja wa abiria hao alisema licha ya taharuki miongoni mwa abiria, nahodha wa meli hiyo hakuwa tayari kuwaeleza abiria hao nini kimetokea.

    Mkurugenzi wa Bandari Zanzibar (ZPC), Abdul Juma, alithibitisha kuzimika kwa meli hiyo na kwamba alipata taarifa hizo jana saa 7:00 mchana.

    Alisema aliwasiliana na manahodha wa meli hiyo ili kupeleka meli maalum ya kuvutia meli zilizokwama (Tag), lakini walikataa na kudai kuwa meli yao haina tatizo kubwa.

    “Tulijitahidi kuwashawishi tukawavute lakini walikataa wakasema tatizo ni dogo watarekebisha, “ alisema.

    Habari zilizopatikana jana zilisema kuwa baadaye meli hiyo ilivutwa na Tag iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Kenya na ilitarajiwa kuwasili Zanzibar saa 2:00 usiku.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...