Home
Unlabelled
dk. shein ziarani kenya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Meli ya abiria yazimika ghafla baharini
ReplyDeleteMeli ya Kampuni ya Sea- Gul iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, jana ilizimika baharini ikiwa na abiria zaidi ya 300.
Kuzimika kwa meli hiyo kulisababisha taharuki kubwa miongoni mwa abiria hao, ambapo baadhi walikuwa wakilia huku wakiwasiliana na ndugu na jamaa zao.
Meli hiyo ilitoka katika Bandari ya Dar es Salaam saa 6:00 mchana na ilitarajiwa kuwasili Zanzibar saa 11:00 jioni.
Abiria waliokuwa katika meli hiyo, waliliambia gazeti hili kuwa walishuhudia meli hiyo ikipunguza mwendo na baada ya hapo kuzimika kabisa.
Mmoja wa abiria hao alisema licha ya taharuki miongoni mwa abiria, nahodha wa meli hiyo hakuwa tayari kuwaeleza abiria hao nini kimetokea.
Mkurugenzi wa Bandari Zanzibar (ZPC), Abdul Juma, alithibitisha kuzimika kwa meli hiyo na kwamba alipata taarifa hizo jana saa 7:00 mchana.
Alisema aliwasiliana na manahodha wa meli hiyo ili kupeleka meli maalum ya kuvutia meli zilizokwama (Tag), lakini walikataa na kudai kuwa meli yao haina tatizo kubwa.
“Tulijitahidi kuwashawishi tukawavute lakini walikataa wakasema tatizo ni dogo watarekebisha, “ alisema.
Habari zilizopatikana jana zilisema kuwa baadaye meli hiyo ilivutwa na Tag iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Kenya na ilitarajiwa kuwasili Zanzibar saa 2:00 usiku.