
Fresh Jumbe: Wakongo wanatawala soko la dansi Bongo
Gwiji wa muziki wa dansi Bongo anayeishi Japan, Fresh Jumbe Mkuu, yupo nchini huku leo ikiwa ndiyo kwanza anafunga wiki tangu alipowasili kwenye ardhi ya JK.
Yupo hapa kwa ajili ya kutoa shoo kali za muziki wake. Ijumaa hii yupo kwenye Ukumbi wa Landmark Hotel, Ubungo, Dar es Salaam hapo atashirikiana vema na Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.
Fresh pia anajiandaa kwa ajili ya Tamasha la Sauti za Busara ambalo amealikwa, litakalofanyika pande za visiwa vya marashi ya karafuu, Zanzibar kama kawa.
Katika ‘intavyuu’ na mwandishi wa Global Publishers, Hemed Kisanda, Fresh anasema kuwa muziki wa dansi wenye asili ya Kitanzania umefunikwa kwa kiwango kikubwa na ule wenye ladha ya Kongo.
Kutokana na hilo, Fresh akasema kuwa havutiwi na hali iliyopo kwamba soko la muziki wa dansi linakuwa mikononi mwa Wakongo, wakati ‘enzi za mwalimu’, Wabongo walijidai sokoni na kwenye maonesho yao kumbi zilijaa.
“Enzi hizo tulifanikisha muziki wetu kuwa juu tofauti na ilivyo sasa,” anasema Fresh ambaye anafanya maisha yake ya muziki nchini Japan.
Fresh ambaye amewahi kuzitumikia bendi mbalimbali nchini wakati huo kama DDC Mlimani Park, Juwata Jazz, Bicco Stars, Safari Sound na Dar International, anasema kuwa dhamira yake ni kufika mbali kisanii.
Anawataja mastaa wa Afrika ambao wanampa ‘mzuka’ wa kuumiza kichwa ili afikie rekodi zao kuwa ni Angelique Kidjo, Yossou N'dour, Yvonne Chakachaka na Hugh Masekela.
Ni kweli wakongo wanatawala muziki wa dansi Tanzania. Na yeye kama mwanamuziki anatakiwa ajue ni sababu gani hali inakuwa hivyo kimuziki na sio kuwabagua. Kwani hata yeye huko anakopigia mziki Japan sio Mjapan. Na kama dhambi ya ubaguzi inatafuna itaanza kwake. Kama tumekubali soko huria tukubali na ushindani. Ngoja na jumuiya ya Afrika Mashariki iote mizizi tutakaa vijiweni tu tukilalamika ooh wenzetu wamechukua kazi zetu na blah blah!
ReplyDeleteHana lolote huyo Fresh Jumbe na aache mapozi. Kama anaona kuna umuhimu wa kukuza mziki wa nyumbani na sio ule wa kikongo angetueleza mzizi wa mziki wa kongo kupendwa. Baya zaidi miziki ya kikongo na kinaijeria inapigwa hadi ulaya.
Uchawi unajulikana ni kuacha kuiga na kufuata utamaduni wetu. Sio wewe unakuja na bandana kichwani huku unabana pua na kusema "Miziki ya kikongo inatawala bongo"
SO WHAT?
good mr baraka aache ubaguzi huyu jamaa kashaishiwa eti ndoto zake kujiendeleza zaidi wapi wewe ushachoooka,miaka 20 na zaidi unapiga muziki bado unahitaji kujiendeleza tu badala ya kuitwa gwiji?angalia mifano akina vumbi wenzio wanakomaa na fani,we geuza ubao tu upige box basi,wakongo wanatawala muziki bongo kwasababu wabongo wenyewe wanaiga muziki wa kongo vilevile ndo mana mtu unaamua uwafuate wakongo basi ujue moja.
ReplyDeleteTUWE WAKWELI WATANZANIA,TOKEA MIAKA YA 60 BENDI ZA TANZA NIA ZIMEKUWA ZIKIIGA NYIMBO NA STALI ZA KONGO,ILI NYIMBO AU BENDI IWIKE ILIKUWA LAZIMA IGEUZE NYIMBO ILIO WIKA KILINGALA KUWA YA KISWAHILI,ZIKO NYINGI MOJA WAPO(NAPENDA NIPATE LAU NAFASI NIPATE KUSEMA NAWE KIDOGO)#MOKOLO NAKOKUFA# NA WAKATI HUO TULIKUWA NA BENDI MAHILI,KILWA JAZZ,DAR JAZZ,WESTERN,CUBANO MARIMBA,NK.MWISHONI MWA MIAKA YA 60,BENDI ZA KONGO ZIKALIONA HILO NDIO ZIKAANZA KUJA,FORVERTE YA KASHEBA,KIKI,BAZINO,BABA GASTON ALIKUWA ANAPIGA KINONDONI MKWAJUNI NYUMA YA MASAI INN,TP SANTA FEE MNAZI MMOJA GETAWAYS KISHA WAFUATA MARQUIS DU ZAIRE 1971 NQKUTEKA SOKO LOTE LA MUZIKI,BENDI ILIO KUWA INASHINDANA NA WAKONGO NI CHAKACHUA,MSONDO WA NUTA NA BENDI NDOGO ZA AFRO 70 NA SOKOMOKO(PRINCENSS BAR)WANAMUZIKI WA KWETU SI WABUNIFU NA HUSANI WANAMUZIKI WA SASA WENGI WAO WAMEINGIA KATIKA MUZIKI ILI WATOKE KIMAISHA KIBONGOBONGO.MAWAZO YAKO MAZURI KILA PENYE NIA PANA NJIA NA KWENU JAPAN KUNA VICHWA KAMA LISTER KEYBORD,ABOU NAWENGINE KANINI MSIUNGANISHE NGUVU MKA FUATA NYAYO ZA TATU NANE,FANYENI TAFITI MTUPIGIE SINDIMBA,KIODA LIZOMBE,TOKOMILE VANGA NK, KAMA KINA KOFFI WANAVYO GEUZA NGOMA ZA KWAO WHY NOT NYIE,MIMI NI MBONGO NA MPENZI WA MUZIKI UKWELI WAKONGO WAKO JUU TUTAKE MSITAKE,DAR INTERNATIONAL ILIPO GAWANYIKA NA KUZALIWA SIKINDE NDIO BENDI PEKEE ILIOTIKISA ANGA YA KAMANYOLA LAKINI PIA HAIKUWA BENDI YA WABONGO TU KULIKUWA NA WAKALI WALIO LOWEA NCHINI NAO WALIKUJA NA WAKONGO,MICHAEL ENOCK(MZAMBIA)JOSEPH MULENGA(MZAMBIA)ALIKUJA NA TP SANTAFEE KAMA MPIGA BESI NA GEORGE KESI MKENYA.TUSIPOTOSHE HISTORIA TUKUBALI UKWELI ALAFU TUANZIE HAPO, HONGERA SANA NJENJE NAWAPA 5,MDAU MAC-DONALD KWA MSOMALI CARDIFF!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMr. Fresh, sikuhizi biashara zote ni za soko huria (free market) mteja anafuata anachopenda. Labda wanamuziki wazawa inabidi waongeze ubora wa muziki wao kama ilivyokuwa zamani, lakini si vizuri kuwashambulia wakongo au kufikiri kuwa wapenzi wa muziki hajui kizuri na kibaya. Nafagilia wana taarab kwani wao wamejitahidi sana kiasi cha kufanya muziki wao kupendwa sana na watu wengi.
ReplyDeleteFresh Jumbe,uliyoyasema ni ukweli mtupu,na kuna watoa maoni hapo juu wamekurupuka tu,kwa kuanza zogo,kuwa fresh ache ubaguzi!sasa katika maelezo ya hapo juu ni neno gani? la kibaguzi.
ReplyDeleteWabongo tuache ulimbukeni wa kubabaikia mziki wa kigeni,badala yake tuwape moyo wanamziki wetu hili tujivunie chetu,na wito huu sio ubaguzi bali na uzalendo,kwa mtu yoyote yule mwenye hakili timamu na anayejua nini?maana ya sanaa katika nchi,lazima atapata jibu kuwa sanaa za maonyesho na utamaduni katika nchi yoyote hile ndio ROHO au Moyo Mzizi wa jamii katika nchi,sasa leo hii kama watanzania watakuwa wapambe nuksi wa kushabikia mziki wa Kongo hata kinachoimbwa hawakijui,si tunaonekana kama vile wendazimu tunaochekerea jalala? na hatimaye kuondoka na ugonjwa au? hivi mshawai kusikia bendi za Tanzania zinaenda kupiga tour kongo au? sasa kwa nini? hapa bongo ndio pawe kambi ya visi? kila mfupa urushiwe hapa?maporomota hapa kwetu wanatumia mamilioni ya fedha kuziahalika bendi za kikongo ,si wangetumia fedha hizo?kuimalisha bendi za hapa na kuzisafirisha nje?
Sasa leo mnakurupuka kwa maoni ya kuwa FRESH JUMBE aache ubaguzi,amjioni kuwa nyie ni vipofu wa mawazo msiona mbele? na Fresh Jumbe darubini yake kaona mbali na kuona kuwa wakongo watawala soko la mziki bongo,huu ni ukweli,na hii inatokana na sisi wabongo weneyewe kuwa wababaikaji.
Fresh Jumbe Hongera sana sana kwa mtazamo wako,watanzania tulio wengi tupo pamoja na wewe
tunalipa zaidi katika taarab,mduara,mchiriku,na ile nini sijui inafananana mchiriku,,,
ReplyDeletesasa tuanze ingiza nyimbo za kabila zetu mbalimbali!!
Wee anonn wa 09:32 nadhani ungekuwa muungwana kwa kuwasifia wanamuziki kaka akina Dr. Hukwe Zawose, Tatu Nane na wengineo. Yeye anaishi na kufanya kazi zake Japan wewe unadhani ni kwanini? Hakuna aliyekurupuka hapa sisi tunachotaka kusema huyo Fresh Jumbe inamwasha pilipili asiyoila wala asiyojua ladha wala aina yake. Uache ushabiki na kurukia hoja. Hii hoja imekaa kimaslahi zaidi. Hili ni soko huria hakuna mtu aliyewekewa mipaka isipokuwa ni ubunifu tuu. Ukiiga cha mwenzio unajulikana. Haya hebu tueleze huyo FRESH anapiga mziki wa aina gani huko Japan? Angekuwa anapiga mdumange,sindimba basi. Umeshasikiliza mziki wake?
ReplyDeleteMimi kwa upande wangu sioni lolote jipya zaidi ya yeye kuja kuwasanifu watu wa bongo. Changamoto iliyopo huku kwetu katika kila kitu tunakosa ubunifu. Mathalan mtu anaweza kumwona jirani yake kafungua duka kesho yake na yeye kafungua matokeo yake ni msururu wa mafremu. Ukienda Sinza huwezi kupita nyumba tatu bila kukutana na baa ama gesti sasa huo ni ubunifu.
Uache ushabiki na kuropoka kwa hisia kuwa makini. Nani amekwambia sisi ni vipofu tusioona mbele.Una ushahidi.
Mwambie huyo Fresh wako aende BASATA akaongee na kama unamuona mzuri sana kanywe naye chai.
Mimi nawaona wanamuziki mfano hapa Tanzania wako wengi kwenye game na sijasikia kelele wala nini na wanafanya vizuri na ni watanzania. Ishu ya Kongo imeanzia wapi.
Walikuwapo wakina Remmy, Makassy,Marquis, Ndala Kasheba na wamepiga na watanzania je hao hawakuwa wakongo?
NENDA ZAKO BWANA HUNA LOLOTE WEWE.
aah wapi fresh jumbe mwenyewe miziki yake haibambi kabsaa siyo kihivyo ungekuwa unatoa vitu kama kina mbaraka mwishehe hapo tungekuona upo juu lakini wa kawaida sana bora wazee wetu wa ngwasuma kuliko wewe usituletee za kuleta peleka hukohuko kwa kina suzuki yamamoto nanihii moto!!
ReplyDeleteAnon# Baraka mfunguo,
ReplyDeleteunaonekana umekasarika sana na maoni ya mchangiaji Anon:9:32,na umedandia hoja bila ya kutafiti,inaelekea jina lako Baraka halilingani na hoja zako na Mfunguo nalo pia alilingani kabisa na hoja zako,si bora ungeitwa Yohana Mbumbu?.hivi unapomalizia kwa kutaja baadhi ya wanamziki kama vile Remmy,Makassy,Marquis,Ndala Kasheba kuwa walipiga kazi na watanzania? katikaa bendi ulizozitaja aslimia 99 ya wanamziki wake walikuwa ni wa kutoka kwao kongo,ilibidi wawachukue baadhi ya watanzania kutoka na amri iliyotolewa miaka ya 70s kuwa bendi zote za kigeni zifunge virago,upo hapo?ikawa hakuna jinsi lazima wajichanganye kwa kuingiza watanzania ktk bendi zao.ndio maana ukaawaona wanamziki
wa bongo kama Gojero Choyo akifanya kazi na Orch.Makassy,Hamza kalala,Hassan Ayas,Zagalo,Fredy Mwalasha na wengine, wakaingia Matimila bendi ambayo ilimilikiwa na mtanzania marehem Mvula(RIP)lakini uongozi walipopewa wakongo basi bendi hiliwachukua wakongo 99%,upo hapo?
Aliyekuwa mimliki wa Orch.Safari Sound Bw.Hugo Kisima aliwapa aliwapa ajira wanamziki wengi wa kikongo na watanzania wachache akiwemo mpiga drum Ramadhani Mtono,Bw.Kisima siku alipohamua kuichanganya bendi hiyo kwa kuwaingiza akina Hassan Rehan Bichuka na Muhidin Maalim Gurumo,wakaanzisha mtindo wa NDEKULE bendi ikawa na mvurugano,Bichuka na Gurumo wakatoka,kilichosabisha ni wanamziki wa kikongo hawakutaka kuwa chini ya Muhidin Gurumo, sasa nani? hapo mbaguzi?
ktk historia ya mziki wa dansi wa tanzania na kongo ni mwanamziki mmoja tu aliyekubali kuunga mkono juhudi za watanzania si mwingine ni bali Cosmas papa micky na bendi ya Orch.Nova Sucess,Papa micky alikubali kuwapa zawadi Msondo,kwa kuwapa mwanamziki marehemu Joseph Lusungu,akajiunga na Nuta jazz sasa msondo ngoma,upo hapo?
Lakini ktk magwiji wote wa mziki wa kikongo wanaoishi hapa kwetu,sio KIKI,wala marehem Kasheba,sio marehem Chinyama Chianza, na wala si Ramadhani Ongara,hakuna aliyekubali kujiunga na bendi za wabongo na akapiga chini ya uongozi wa watanzania.
Sasa Fresh Jumbe anayo haki ya kila njia kuwashawishi wanamziki wenzie watanzania kuwa wajitahidi katika kilaa hali kufunika soko lao la mziki bongo.
Bw.Baraka Mfunguo,inaelekea wewe ni mlokole wa mziki,lakini hujui siri ya maana ya kuwa mwanamziki?na wala ujui kuwa mziki na wanamziki ktk jamii kuwa ni tahasisi ya hatari? kama ungeelewa nini?maana ya wanamziki na tahasisi zao,basi usingekurupuka kwa kutoa mawazo pumba.
fresh jumbe anayo haki ya kusema mdomo mpana kuwa soko la mziki hapa kwetu linatawaliwa na wakongo,na wanamziki wa bongo na sisi wabongo wenyewe tuhamke sio wazo baya,pia sio ubaguzi,bali ni wito.sasa wewe kwanini? ukose usingizi kwa wito wa Fresh Jumbe.
Jina lako zuri sana Baraka Mfunguo lakini alifanani na mawazo yako,kwani hauna ufunguo wowote wa baraka badilisha jina
Fresh Jumbe hoyeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteukisikia mwanamziki ana uchungu wa kuupandisha chati mziki na wanamziki wa bongo wenzie ndiye huyu,fresh jumbe big up kwa mtazamo wako,wa kuwapa moyo na kuwahamsha usingizini wanamziki wa hapa nyumabani,kwa kweli wanajitahidi sana,lakini wanavunjwa moyo na sisi watanzania wenyewe,ambao baadhi yetu tunapewa ongo ya chupa ya bia kwa kuwafagilia wakongo.si unaona mjamaa Baraka mfunguo anon w 02:42, alivyojawa na jazba iliyochanganyika na chuki binafsi,heti yeye anataka uyafumbie macho unayoyaona,yaani sisi wabongo ndio tunawafunja nguvu wasanii wetu,ilifikia wakati hata wanenguaji walienda kuchukuliwa kongo,wakati tunao mabinti zetu wanajua kunengua kuliko wakongo.si mwenyewe umejionea wanenguaji wa Twanga jinsi wanavyosugua kisigino.
mwenzetu Baraka Mfunguo hayaoni haya anatetea ni sehemu yake anayopewaga offer ya bia,hatumshangai kwa ili maana upambe ukizidi za sana matokeo yake mtu anageuzwa kuwadi.
Fresh Jumbe hongera sanaaaaa kwa wito wako.Mungu ibariki Tanzania na watanzania .
mdau wa Mbagala kibonde maji
wewe Anon: Baraka inabidi usamehewe tu,kwani unaonekana ni mtu mwenye chuki na Fresh Jumbe,nisingependa nikujadili sana kwani nitakuwa nakupa umaarufu usio stahili kuwa nao.
ReplyDeleteBaraka Mfunguo,una matatizo ya ulokole wa mziki wa kikongo,jaribu kutafakari wito wa Fresh Jumbe,arafu chambua hoja,vinginevyo utatoa hoja utumbo,fresh jumbe kawaimiza wanamziki wenzie wa bongo kuwa wajitahidi waweze kutawala soko la mziki la nyumbani,sio kuwachia wakongo,kwa mtazamo huo wa fresh jumbe sio wito mbaya au wa kibaguzi.lakini Baraka unaonekana jinsi ulivyo mnafiki na chuki,kuwa Fresh Jumbe kafanikiwa kimziki nchini Japan ,wewe upendi mswahili mwenzio afanikiwe
ReplyDeleteWadau nashukuru kwa maoni mazuri. Mimi sio mnafiki na ndio maana jina langu linaonekana katika maoni. Na sina chuki dhidi ya Fresh Jumbe. Isipokuwa ni tofauti ya utetezi wa hoja na mtazamo. Mimi ni mpenzi wa nyimbo za kitanzania na watanzania wenyewe isipokuwa sipendi ubaguzi ama kubaguliwa.
ReplyDeleteSasa Baraka Mfunguo,
ReplyDeleteUmeshindwa kutetea shutuma unazozitoa "Ubaguzi" katika wito wa fresh Jumbe tuelezee wapi ?kasema wakongo wabaguliwe?.
Fresh Jumbe katoa wito kwa kuwahamsha wanamziki wenzio kuwa soko la mziki limetawalia na wakongo,kwa hiyo wajitahidi sana sana kuwa na mbinu za kibiashara na kuahakikisha kuwa soko lipo mikononi mwa wanamziki wa nyumbani.
na huu sio wito mbaya kibiashara.
hakuna ubaguzi au neno la kibaguzi lilitumika.
bali wewe uliingia kwa jazba katika hoja na kuona mtazamo wa jumbe ni wa kiubaguzi!tazama juu ktk hoja yako umemaliza "So what!
yaani ni moja kwa moja unataka pasiwepo mabadiliko ktk soko la mziki.
Acha yaishe tujaribu kuwa wangalifu katika hoja na wito maoni yetu haya yanasomwa na mamilioni ya wadau unaposema "Ubaguzi" unaweza kuleta vurugu mahala penye amani.