WADAU KIBAO WALIHUDHURIA KISOMO CHA HITIMA YA BABA YETU SIMBA WA VITA , HAYATI RASHID MFAUME KAWAWA, JUMAMOSI HII KATIKA ST ANNE'S MOSQUE-ST ANNES ROAD,TOTTENHAM , LONDON N15 5QG WIKIENDI HII NA KUDHIHIRISHA KWAMBA MSIBA HUU MZITO WA TAIFA UMEGUSA WENGI. JUU NI WAKATI WA MAWAIDHA. PICHA ZOTE NA AYOUB MZEE
SHEKHE AKISOMA WASIFU WA MAREHEMU
WADAU KIBAO WALIHUDHURIA
NYUSO ZA HUZUNI ZILITAWALA
BALOZI WETU UK MH. MWANAIDI MAAJAR (PILI KULIA)
AKIWA NA BAADHI YA WADAU KWENYE HITMA
WADAU WAKISIKILIZA MAWAIDHA
JUU NA CHINI NI WADAU WAKIPATA MLO BAADA YA HITMA









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Nakuona Sheikh Ayubu na Professor Kangusu hapo!!Si mchezo..Mimi niko kwa mbaali

    ReplyDelete
  2. Mtani wa Simba wa vita, NchumbijiJanuary 11, 2010

    Hizo chupa za rangi ya kijani ni kinywaji gani jamani? Macho yangu hayapendi kuona HEINEKEIN kwenye khitma, mate yamenijaa mdomoni. Mnisamehe!!!

    ReplyDelete
  3. Jamani hebu nisaidieni ST ANNE'S MOSQUE kweli imekaa sawa?

    ReplyDelete
  4. watu wengine bwana yaani wanajifanya kujuwa sana na kuwana dhana mbaya kwa wenzao kupita kiasi. nakusema wewe mdau wa pili na dhana zako za HEINEKEIN! umeona wapi HEINEKEIN hapo? chupa za kijana ni drink either ya seven up au sprite na kila mtu anajuwa hilo ila mwenye akili finyu kama wewe. samahani michuzi lakini sometimes its too much!!!!!

    ReplyDelete
  5. mdau wa tatu ulichouliza ni kizuri. kusema kweli huo msikiti ninavyojuwa mimi ulikuwa ukiitwa Sultan Selim Mosque (zama hizo nilipokuwa nasoma mitaa ya seven sisters road). Watu wengi wanauita st anne's mosque kwa kutumia jina la barabara ulipo huu msikiti yaani st anne's road. kusema kweli mimi naona ni kosa lakini watu wanaurefer hivyo bila hata ya kufikiri matumizi ya neno st na mosque pamoja.

    mdau portsmouth

    ReplyDelete
  6. Ulaya kweli hakuna mana.....MBONA HAKUNA DALILI YA MSOSI JAMANI!

    ReplyDelete
  7. Nimemwona mtu kam Baraka kam sikosei u bin wake Mbilinyi looh Baraka kumbe uko Uk waz ma Tuition Mate pale kwa Mwl.the late Nyooka shule ya uhuru mchanganyiko enzi za 80'z looh jion tunakutana wengine haya kaka rudi bongo bana maana ulikuwa kichwa njoo uukwae U GM

    ReplyDelete
  8. profesa Kangusu ndio mgombea ubunge mwaka huu huko KIGOMA.

    ReplyDelete
  9. MDAU wa Mon Jan 11, 12:56:00 PM, Acha hasira juu ya mdau wa pili. Kwanza yeye amejitambulisha kama mmakonde mtani wa Simba wa Vita, sasa hasira za nini, pili si kila chupa ya kijani ni Sprite na 7up, kwa taarifa yako kuna vinywaji vingi vya rangi hiyo...Sio kila anayevaa kanzu ni sheikh...natumaini umenipata.

    Wabillah tawfiq.


    Msuluhishi.

    ReplyDelete
  10. Mambo vp Mdau Anonymous wa 03:34:00PM.Nikumbuishe Mzazi jina lako nani.

    Ni mimi Baraka Nginilla na wala si Baraka Nginilla.Najua utakuwa na habari kuwa Mwalimu Njooka alifariki kitambo kidogo.


    Nilikuwepo bongo mwaka jana na Mungu akijalia huenda nikaja tena mwaka huu.Sema ndiyo nilikuwa sijui watu wako wapi,naishia kuonekana mi ndiyo mgeni jiji la Lukuvi.

    Ushakuwa GM nini Mzazi? Mzazi ikitokea kazi nitakayoiona poa na nikiwa nimeamua kupiga kazi Bongo au Afrika popote pale nitarusha CV kusikilizia.

    Nikitextie au nipigie 0044 751909 7330.

    Baadaye Mzazi wasalimie ex Njooka classmates unaokutana nao.

    ReplyDelete
  11. Unashangaa St Anne's Mosque? hilo ni jina la mtaa kama mtaa wa kisutu basi Kanisa au Msikiti uitwe Kanisa la Kisutu(mtaa) au Msikiti wa Kisutu(mtaa).

    Haya 'sinza kwa remmy' nayo unashangaa?

    Tunashukuru kwa blogu ya jamii kutufungua macho, maana zamani unaambiwa tembea uone, sasa tunaambiwa 'click' uone.

    Mdau
    Mtaa wa St Anne

    ReplyDelete
  12. Mdau Ex Njooka student/pupil.Nilimaanisha mimi ni Baraka Nginilla na sio Baraka Mbilinyi.

    Later

    Shukran Misupu,kwa kuniwezesha kuacha simu yangu hapa nimeweza kuongea na rafiki yangu tuliyesoma naye Azania toka 1989 - 1992.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...