Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji akila kiapo cha Urais Mbele ya Rais wa Mahakama ya Katiba ya Msumbiji Jaji Luis Mondlane katika viwanja vya Uhuru jijini Maputo Msumbiji leo.
Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji akinyoosha juu katiba ya Msumbiji muda mfupi baada ya kula kiapo kuendelea kuingoza nchi hiyo kwa muhula wa pili wa Urais katika sherehe zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Maputo.Kushoto ni Rais wa Mahakama ya katiba wa Msumbiji Luis Mondlane aliyemwapisha Rais Guebuza.
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akiteta jambo na JK wakati wa sherere za kuapishwa kwa Rais Armando Emilio Guebuza kendelea kuingoza Msumbiji katika muhula wa pili wa Urais jijini Maputo.Katikati ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na shoto kabisa ni Rais Joseph Kabila wa DRC Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.



Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akisisitiza jambo wakati akizungumza na JK wakiwa na mwenyeji wao Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji katika ikulu ya Mjini Maputo muda mfupi baada ya Rais Guebuza kuapishwa kuendelea kuingoza nchi hiyo katika muhula wa pili wa urais.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mgosi wa kayaJanuary 15, 2010

    "HEY MR.KIKWETE YOU KNOW JIKO HALIKAMILIKI WITHOUT MAFIGA MANNE,I GOT 5 SO U CAN DO IT" Hapo Zuma akimpa Kikwte nasaha za kuwa na wake watano

    ReplyDelete
  2. HAHAHA MGOSI WA KAYA UMENIVUNJA MBAVU, MAANA NA MIMI NILIKUWA NA WAZO KAMA LAKO! HAHAHAHA

    ReplyDelete
  3. Hapo ni kweli Mzee Zuma anawaambia jamani, "Mwenzenu nimeamua kuweka mambo wazi, mambo hadharani, nyie vipi hizi nyumba ndogo ndogo zenu si mhalalishe tu kieleweke??!!"

    Mshini wami....Give me my machine Gun!!
    Mdau

    ReplyDelete
  4. hala hala Zuma jamani maana yeye kwa mimama kama huyo first lady wetu ni mgonjwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...