K-Mondo Sound wakiwa jukwaani

Bendi ya muziki wa dansi ya K-Mondo Sound imekamilisha video ya wimbo wake wa 'Magambo' na tayari imekwishaanza kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya TV nchini.

Kiongozi wa bendi hiyo, Richard Mangustino ameiambia Globu ya Jamii kwamba video hiyo imerekodiwa na kampuni ya NY Production iliyo chini ya King Dodoo la Bouche.

“Tunashukuru kwamba video yetu imekamilika na imeanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni na tunatarajia kuitambulisha rasmi kwa wapenzi wetu,” alisema.

Mangustino alisema baada ya kukamilisha video hiyo, wanatarajia kurekodi pia video ya wimbo wao mwingine uitwao Sharufa. Mangustino alisema baada hapo wanajipanga upya kwa ajili ya maonyesho yao ya kila wiki.

Alisema kwa sasa bendi yao inatumbuiza ijumaa pekee kwenye ukumbi wa Triz Motel, Mbezi Beach Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...