Wenza wa mabalozi ,marais wastaafu na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete(katikati) na Mke wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa ZAYEDESA mama Shadya Karume(wa nne kulia) wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka 2010 iliyofanyika leo jioni Ikulu jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa ZAYEDESA mama Shadya Karume akibadilishana mawazo na baadhi ya wake wa mabalozi wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka 2010 iliyofanyika leo jioni Ikulu jijini Dar es salaam.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na baadhi ya wake wa mabalozi wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka 2010 iliyofanyika leo jioni Ikulu jijini Dar es salaam.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kuwakaribisha wenza wa mabalozi, marais wastaafu na viongozi mbalimbali wa kitaifa kusherehekea kuukaribisha mwaka 2010. Pamoja na mambo mengine aligusia masuala mbalimbali ya kijamii yakiwemo kuwaendeleza watoto wa kike kielimu, kudhibiti maabukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa vijana na kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. mfano huo mzuri kabisa wanawake ... nguo sio lazima ziwe za ulaya nasie tujaribu ku PROMOTE vitu vyetu kama tunavyomuona mama kikwete anavaa tu vitenge au kanga hataki makuu. Na mama/bib yetu mpendwa mama maria nyerere, mfano bora sana.

    RIP Mwalim

    ReplyDelete
  2. Asante Dada Shadya umependeza na umetoka vizuri na kivazi ulicho kivaa ,kipo Tafauti na kivazi cha Ki Nigeria

    ReplyDelete
  3. safi sana kinamama wote hapo,jamani tanzania hatuna vazi rasmi la taifa so tutavaa vazi lolote tu,kama kinaijeria,kiganda,kihindi,kimasai nk

    ReplyDelete
  4. WIZI MPUTU.

    ReplyDelete
  5. RESPCTED TO ALL OUR MAMAS. WE THANK YOU FOR ALL INFINITELY.. YAANI PASIPO KIKOMO

    ReplyDelete
  6. Nimeangalia mara mbili mbili picha ya mwanzo na ya mwisho na nina hakika kuna wanaume (mzungu picha ya juu, mwafrika picha ya mwisho), jee hawa pia ni wake wa mabalozi? teh teh teh

    ReplyDelete
  7. Anon wa 02.41 alieandika title ameandika "wenza wa mabalozi" na sio wake wa mabalozi. Hivyo kama balozi ni mwanamke mwenza wake kwa kawaida ni mwanamume

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...