Kitabu cha maombolezo ya Simba wa Vita, Mhe. Rashidi Mfaume Kawawa kilifunguliwa Ubalozini Stockholm kwa ajili ya kusainiwa tarehe 7-8 Januari 2010. Wadau wengi, wakiwamo mabalozi, wawakilishi wa balozi pamoja na watanzania na marafiki zao, walifika kuweka saini na kuhani msiba huu mzito kwa Tanzania
Bendera ya Taifa ikipepea nusu mlingoti Ubalozini Stockholm, Sweden, kuomboleza msiba wa Simba wa Vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa.
Balozi wa Rwanda Mhe. Jacqueline Mukangira akitia saini kitabu cha maombolezo
Balozi wa Malaysia Mhe. Dato' Kamarudin Mustafa akitia saini kitabu cha maombolezo
Balozi wa Croatia Mhe. Vladimir Matek akitia saini kitabu cha maombolezo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Sweden, Bw. Zam Khalifa, akitia saini kitabu cha maombolezo kwa niaba ya watanzania wa Sweden.
Mtoto wa Simba wa Vita, Bw. Amani Ally Mfaume Kawawa akitia saini kitabu cha maombolezo huku mjukuu wa Simba wa Vita, Kwesi Kawawa, akisubiri zamu yake.
Amani na Kwesi Kawawa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Ubalozini baada ya kusaini kitabu cha maombolezo






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Nje ya mada:
    Michu, hebu naomba uweke tetemeko lililotokea Haiti. Ni nchi maskini, na majengo yake mengi yalikuwa mabovu hata kabla ya tetemeko.
    Hadi Ikulu yao imeshuka.
    AP wanakadiria watu zaidi ya laki wanaweza kuwa wamekufa.
    Nia ni kuonyesha ambayo yanaweza kutokea Tanzania, ingawa hatuko kwenye eneo la majanga.
    1, Itusaidie kujiandaa na majanga (yoyote yale)
    2, Tuangalie uwezekano wa kuboresha/kujenga majengo imara
    3, nk

    Mdau aliyeguswa na mwenye hofu iwapo itatukuta

    ReplyDelete
  2. Ndugu Anon wa Jan 13, 10:06:pm. It is through what we think that we engage in creative process. If you think about earthquakes then you are sending out signals that invite events, circumstances and situations and people that resemble the environment that has to do with earthquakes. Never be fearful always fill your mind with good then danger wont approach you.Think positive and never negative things. If you are a christian read the book of Phillipians 4: 6-8. Utaelewa ninachosema.

    ReplyDelete
  3. Namwona mama Mwaiselage hapo kwenye picha ya chini.

    ReplyDelete
  4. Mlokole naona umepotea,..kumuamini Mungu na kusoma biblia hakuzuii watu kufanya mjadala wenye lengo la kujenga: kwa case hii, nini matokeao ya majanga kama haya ya tetemeko, na ingawa hatuwezi kuzuia, tujiandae vipi endapo janga kama hili likitokea?

    Unataka tusifikirie negatively, sawa.,na je tukiacha kufikiria na tetemeko hilo likatokea hapa kwetu wiki ijayo??...utasemaje

    Cha muhimu ni kuwa, pamoja na kujiimarisha katika imani zetu, kila mmoja na imani yake, mkristu, muislamu, budha, asiye na dini na mwenye kuabudu kwenye kichuguu,..

    wote kupokea mawazo hayo na watu binafsi kujifunza mbinu za kujiokoa endapo janga kama hilo linatokea,na mamlaka zijizatiti kwa kujenga uwezo wa kukabiliana na matatizo hayo,

    Mdau,
    Mkristu- Mkatoliki

    ReplyDelete
  5. nakuunga mkono mkatoliki wote watanzania tuna msiba na huzuni na maisha yanaendelea na mungu amlaze pema mzee wetu lakini hata haya ya haiti ni vizuri kuyaona na kuwaombea wenzetu kwa maafa kama haya na sisi kuwa tayari kujifunza jinsi tutakavyo saidiana ndugu yangu we anon usie elewa maafa kumbuka na tukae tukisali mungu atusamehe ni mwisho wa dunia na inatisha hata kama wee anon unakausha michuzi weka habari na haiti kwani siku zetu hatuzijui inasemekana tanzania hivi si muda ulipita mtetemeko wa ardhi mbogo je walipona watu hasa vijijini?

    ReplyDelete
  6. Nimefurahi sana kukuona mama yangu, pole na baridi - Seba kijitonyama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...