The Death toll is rising on this juction,
A week can not pass by without the occurance,
of an accident, Kids have died there, men and women have lost their
lives, and as I write this today there has just been an accident,
Rav4 and Toyota Surf, and it was a critical accident.

There is a wall, that i think has to come down by President's estate that
by Ursino Street, that wall is mabati that have protruded
off on the road that has to come down cause it acts as an obstruction to on coming trafic, apart from that we have to have speed bumps on those two streets
because cars travel at very high speed on these residencial places.

From
A Concerned Citizen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Inasikitisha sana, wadau hii junction ipo wapi?

    ReplyDelete
  2. Kwanini magari yaende kwa speed kwenye junction? Hili nalo mtailaumu serikali au JK? Hivi ukifika kwenye juction si inabidi usimame? ufike wakati sasa mtu akimuua mtu kwa ajali ya barabarani apewe adhabu kali hata ikibidi kufungwa maisha, ndio ajili za makusudi kama hizo zitapungua. Sidhani kama kuna mahala ukuta uko barabarani, hicho ni kisingizio tu kisicho na mantiki. Panapokutana barabara mbili lazima upunguze mwendo ikibidi usimame kama hauko kwenye barabara kuu unatokea kwenye feeder road. Tatizo watanzania wengi hawataki na hawapendi kufuata sheria yoyote ile hasa hizo za barabarani.

    Eti tena unadai kabisa muwekewe matuta kwani alama tu za kuonyesha speed limit hazitoshi? Na tena speed limit kwenye makazi ya watu zinajulikana wazi kwanini uendeshe zaidi ya limit?

    Barabara ya Chole karibu na kona mbaya yenye kimlima ilikuwa inaangusha magari kila siku, na mara nyingine magari yanaingia mpaka ndani kwa watu, wakawekewa kibao kinachoonyesha limit ni 50kph. Basi badala ya kufuata hayo wakaamua kuchukua rangi na kufuta hicho kibao. Hao nddio watanzania wepesi wa kulalama lakini si wa kuwajibika!

    Mswahili

    ReplyDelete
  3. No love loss, hakuna haja ya speed bumps huko

    ReplyDelete
  4. Kiswahili je??

    ReplyDelete
  5. Hii junction ipo Mikocheni A, karibu na Shoppers Plaza. Zamani palikuwa na nyumba mbili za serikali maeneo yale, moja alikuwa anaishi
    Rupia nyingine Rais Kikwete. Hizo nyumba hata kama zimeuzwa bado zitakuwa na watu wa serikali. Nina hakika kilio cha mdau kiko kwenye mchakato wa kushughulikiwa maana serikali ipo hapo hapo.

    ReplyDelete
  6. Dar (TZ) has become the city where the speed bumps are at! :(

    Matuta hayawezi yakawa ndiyo dawa ya matatizo. Wenzetu walionza kujenga barabara zamani na ambao wana magari mengi sana kuliko sisi hawatumii matuta kama sie.

    Na wala hauwezi ukadai eti Waswahili ni watu wa ajabu sana kiasi kwamba njia pekee ni kuwajengea mituta.

    Nionavyo mimi, matatizo yetu yanatokana na yafuatayo;

    1. Miundo mbinu haitoshi. Barabara ni chache mno kiasi kwamba watu inawalazimu kufanya lolote kufika point B.

    2. Bado TANROADS wana mawazo mgando ya kufikiria in 2 Dimensions. Misongamano mingi inatokea pale barabara mbili kubwa zinapokatizana. Nawashauri TANROADS wafikirie sana kujenga flyovers. Mkishajaribu ya kwanza na kuona inawezekana, mtashangaa mlikuwa wapi siku zote msifikirie hivyo.

    3. Hamna maitenance. Kashimo kadogo kanaweza kakasababisha foleni ya kilomita tano kwani kila gari linapofika hapo hupunguza mwendo. Hii inatokea pale Kawe kwenye junction ya kwenda Golf Club ya JWTZ (Avocado).

    4. Matuta mengine yamewekwa mahali pabaya kabisa, kwa mfano yale matuta mawili mbele ya madaraja ya pale makao makuu ya JKT Mikocheni. Nadhani yamewekwa pale kwa sababu punguani mmoja aliamka nakufikiri kuwa yanahitajika ili watu wasigonge daraja! Kitu kama hichi hakijawahi tokea kwa hiyo wangeyatoa tu. Kama ni kugonga, hata pamoja na hizo bumps, dereva mbovu atayagonga tu.

    Mwisho, uongozi wa sasa wa TANROADS unamapungufu makubwa sana kwani wamekalia strategy ya kujenga matuta tu kila mahali - mpaka Highways!! Badala ya kujenga barabara, wanakaa vikao kujadili tujenge wapi matuta zaidi. Wabadilishwe.

    ReplyDelete
  7. Ndugu yangu mbona mi sielewi hii junction ipo nchi gani, naamini madereva wengi wanatembelea michuzi blog ila English yao sio mzuri hivyo. Wewe mwanachi mguswa naomba uangalie audience yako ili ujumbe wako ufike kwa walengwa. Anyway thanks for ya concern we will all be careful. Be blessed

    ReplyDelete
  8. and that, that you write in that kiswahili that we understand that good, and that next time you remeber.

    ReplyDelete
  9. Nakualina na mchangiaji wa pili.

    Umefika wakati tukaacha kulalamika/kulaumiana na kuchukua HATUA wenyewe.

    Naijua hiyo KONA/JUNCTION, ni watu wanaotoka URISINO ndo wanatakiwa kusimama, kabla ya kuvuka hiyo MIGOMBANI.

    Cha MUHIMU hapa, Urisino road ipakwe rangi (zebra) na kuwekewa ALAMA. Kama tuta, basi viwekwe vile viDOGO, tena huku huku URISINO.

    Matuta tutaweka kila barabara? Angalia Bagamoyo road (kipande cha Mwenge mpaka njia panda Kawe), foleni ya asubuhi/jioni inachangiwa sana na MATUTA. wamejapunguza, lakini bado foleni haijaisha

    ReplyDelete
  10. andika nchi wewee!!

    pili,nendeni ivory coast mkajifunze miundo-mbinu ya barabara inatakiwa iweje kwa mafano tu (TANROADS)

    ivi why matuta jamani?hii system ya wapi?

    ReplyDelete
  11. watanzania unafiki mwingi tu. Nyie mnaosema jamaa aandike kiswahili, si muanzie na kubadili sheria kuwa lugha ya serikali ni kiingereza? gazeti la seriklai, daily news, mahakama zetu, sheri zetu ni kiingereza. sasa mtu anaweza kutumia lugha ya taifa ua ya serikali. acheni upuuzi.

    ReplyDelete
  12. Habari za leo wadau.

    Kwanza natoa pole kwa watu wote waliopata ajali katika kiunganisho hicho na barabara za TZ kwa ujumla.

    Kwa kifupi WATANZANIA WENGI HATUFUATI SHERIA. Ukiangalia za barabarani ndio kabisaaa. Kuweka matuta, zebra nk haitasaidia kama madereva hawatakuwa makini na kufuta sheria za barabarani. Mfano mzuri ni zebra za Victoria, Makumbusho, Millenium towers na nyingine nyingi. Mtu anadiriki kumpigia honi mpita kwa miguu kwenye zebra?!!!

    Nadhani tukiongelea jinsi gani ya kuwafanya madereva wazingatie sheria za barabarani, pamoja na ufinyu wa njia ambalo pia ni tatizo lakini italeta tofauti kubwa sana kabla ya kuanza kujenga fly overs ambazo madereva nadhani watapaa kwa speed.

    Ni hayo tu.

    K.O.R.

    ReplyDelete
  13. Hilo eneo nimeshapita mara kadhaa na kukuta ajali zaidi ya mara 2. Tatizo linatokana na barabara ndogo inayopita mbele ya nyumba ya JK, yaani barabara ya Ursino, kufanywa barabara kuu badala ya barabara kubwa inayokutana nayo, yaani barabara ya Migombani. Hivyo magari yanayotoka kwa kasi kwenye barabara ya Migombani yanagongwa na magari yanayotoka barabara ya Ursiono yakidhani yao ndiyo yanapewa kipaumbele kwa kuwa yanapita kuna alama inayoonesha hivyo.

    Suluhisho:

    Aidha barabara ya Ursino ifanywe barabara ndogo kama ilivyokuwa zamani

    au

    Waweke Mataaa

    au

    Waweke Trafiki

    au

    Waweke Matuta

    au

    Familia ya JK ihame!

    ReplyDelete
  14. Hakuna cha barabara kubwa wala nini pale ipo STOP sign katika barabara ya Ursino (ile inayopita kwa JK) sasa kwa nini wewe dereva husimami na kumpisha yule anayetokea Migombani Street? Hiyo haraka ya sekunde chache ya nini?

    Ni kutokufuata sheria ndio kunafanya ziwepo accidents nyingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...