Wanenguaji wa bendi ya FM Academia wakionyesha umahili wao wakati bendi hyo ilipotumbuiza kwenye mkesha wa mwaka mpya katika ukumi wa Kijii cha Makumbusho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ama kweli. Binadamu? Wengine wameenda kumshukuru Mungu na kuiombea nchi. Wakati huo huo wengine wako kwenye ibada ya sanamu ya Ngwasuma. Du. Tunapaswa lumuomba toba Mungu

    ReplyDelete
  2. Michuzi,

    Hivi ratiba ya FM Academia wikiendi hii ikoje??

    ReplyDelete
  3. Mdau 1 hapo, nami naongeza jambo moja hapo. Wengine wanaomboleza kifo cha Mzee Kawawa, ''Simba wa vita''.

    ReplyDelete
  4. Nyerere alipokufa, redio hazikupiga muziki wowote zaidi ya nyimbo za injili takriban mwezi mzima. Hata sherehe kama za harusi zilizuiwa kupigwa matarumbeta. Ona sasa kwa mzee Kawawa, watu wanakula ngwasuma na mambo mengine utafikiri hakuna kilichotokea hapa bongo.

    ReplyDelete
  5. Kila mtu na nafasi yake na hayo ndio maisha yalivyo. Binafsi sioni tatizo lipo wapi kama wengine walikuwa kwenye ngwasuma na wengine kwenye maombi au kwa kuwa wengine wanalia na wengine wanacheka.
    Kitu ambacho sijaelewa au sitaki kuelewa nikuhusu wale walioenda kuliombea Taifa kama wanavyosema wenyewe, wanaliombea Taifa ili liweje kwani Taifa letu lina matatizo gani?
    Hapa watanzania tuache porojo na tufanye kazi, makosa yetu au matatizo tuliyonayo ni ya viongozi wetu ambao kwa mtazamo wa kawaida maombi wala hayawasaidii na wao kila Ijumaa na Jumapili unawaona misikitini na makanisani na michango ya pesa nyingi ambazo wamezipata kwa kuuza nchi yetu.

    Sasa engine tuakusanyana tuliombee Taifa ili iweje? Kwa miaka mingapi sasa tunavyozidi kuliombea Taifa kwa madai yetu na matatizo ya makusudi yanaletwa na viongozi wetu?
    Watanzania tuufanye mwaka huu wa 2010 uwe wa mabadiliko, vitendo vizidi maneno hata tukiwaombea kila kukicha hawa wanaotuuza kila siku haitusaidii. Imefika wakati watanzania tujione kuwa tnahusika na kupunguza maneno ya kiswahili kuwa watajijua wenyewe. Tugomee yote yasiyo na faida kama kweli tunataka maendeleo.

    Nawakilisha mtz niliyekatishwa tamaa.

    ReplyDelete
  6. Matumbo hayo jamani. Pigeni Situps basi au ingieni Gym basi

    ReplyDelete
  7. wewe ulisema matumbo hayo,kwanimatumbo yana nini cha ajabu ala?matumbo ya beer na mchemsho hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...