Baadhi ya washiriki wa kongamano la watanzania Tamil Nadu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi nje ya ukumbi wa mkutano wa Holy Cross brothers, Chennai.Kama ilivyo ada watanzania wanaoishi katika miji mbalimbali ya jimbo la Tamil Nadu, India walikutana kuanzia tarehe 26 mpaka 27 disemba 2009 katika mji mkuu wa jimbo hili, Chennai. Watanzania hao walipata nafasi ya kufanya kongamano la siku moja kujadili mustakabali wa jumuiya na hasa zaidi kujadili mikakati ya kuiimarisha jumuiya hii. Moja ya mafanikio makubwa ya kongamano hili ilikuwa kupatikana kwa fedha kiasi cha USD 200 kuchangia gharama za hosting za website ya jumuiya inayotarajiwa kuwa hewani kufikia tarehe 30 januari.
Konagamano hilo la siku moja lilizinduliwa rasmi na Mh.Col. Saleh Farah (Mb – Rahaleo). Katika hotuba yake ya ufunguzi Mh. Farrah alisisitiza umuhimu wa malengo yanayotuweka pamoja na kujifunza kuitumia jumuiya kama chombo cha kusaidia wakati wa shida. Aliwahimiza wajumbe kutokatishwa tamaa na uchache wao bali kujenga misingi imara ya jumuiya ili watakaokuja kuirithi waelewe malengo ya waasisi wa jumuiya.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Ndg. Deus Valentine alimshukuru Mh. Farrah kwa moyo wake wa utayari kushirikiana na wanajumuiya hata pale alipopata taarifa ndani ya muda mfupi. Mwenyekiti alimshukuru zaidi Mheshimiwa kwa utayari wake na ukarimu kwa kujitolea kugharamia gharama zote za kuanzishwa kwa tovuti ya jumuiynzia inayotarajiwa kurushwa hewani kuanzia mwezi wa Januari, 2010. Hatahivo alimuomba mgeni rasmi ashirikiane na wanajumuiya kutangaza mema mengi aliyojionea katika jimbo la Tamil Nadu hasa zaidi nafasi za kimasomo ambazo gharama zimethibitika kuwa ndogo kuliko kusoma nyumbani.
Kongamano la siku moja lilifuatiwa na mkuatano mkuu wa mwaka ambao ulihusisha pamoja na mambo mengine mjadala juu ya mabadiliko ya katiba na uchaguzi wa viongozi wapya. Mabadiliko ya katiba yameidhinisha kuundwa kwa mfumo mpya wa uongozi ambapo kamati tendaji itabadilishwa na kuwekwa sekretariati itakayoongoza utendaji wa jumuiya. Utendaji wa jumuiya utaongozwa na mtendaji mkuu ambaye ni katibu mkuu atakeyeshirikiana na mweka hazina kuunda sekretariati. Nafasi ya mwenyekiti itakuwa ya muda itakayokuwa ikishikiliwa na Mwakilishi wa mji ambapo vikao rasmi vya jumuiya vitafanyika. Mabadiliko haya yanalenga kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji wa jumuiya.
Jumuiya ya watanzania Tamil Nadu inawashukuru wote waliochangia kufanikisha kongamano na mkutano mkuu. Kwa namna ya pekee inamshukuru Mh. Saleh Farrah kwa mchango wake. Inawakaribisha wazazi na wanafunzi ambao wangependa kusoma katika jimbo la Tamil Nadu kwa elimu ya juu kuwasiliana na uongozi wa jumuiya ili kupata habari za uhakika kuhusu vyuo bora. Nafasi zilizopo ni nyingi na elimu ni ya hali ya juu kwa gharama nafuu kabisa.
Mungu ibariki Tanzania.
Imetolewa na Sekretariati ya Jumuiya ya Watanzania Tamil Nadu
Watanzania.tamilnadu@yahoo.com
+919840543985

Nice work..except one thing. Wanamume wa Kibongo lazima wajifunze kuwajali wanawake. Hupigi picha na kuwaweka wanawake pembeni hivyo...walitakiwa wawape wanawake wao kipaumbele na kuwaweka mbele tena katikati..huo ndo ustaarabu jamani...!Mdau-USA
ReplyDeleteduh wadau wa India choka mbaya, hakuna box huko mwanangu ni pilipili tu !!
ReplyDeleteHongera kwa Mshikamano huo; Endeleza kitabu hapo Chenai. Nimefurahi kuona na Sista Borgia (kasisi) akiwa hapo, bila shaka huopo shuleni tena . Hongera sana sista. Mungu abriki yote
ReplyDeletemdau - USA. Tungependa kufuata ustaarabu unaouzungumzia ila kuna suala la itifaki (protocol) lazima lizingatiwe hata kwenye kupiga picha.
ReplyDeleteIndia sio choka mbaya ubebe boksi ya nini kama hela ya kula ipo? Labda utueleze mdau huko ulaya mnakochimba makaburi.