NIMEOKOTA MILIONI 4.6 NIPELEKE WAPI?

Brother Michuzi,

Habari za kazi. Mimi ni mama Mkristu mlokole na nimempokea Yesu miaka minne iliyopita. Nimeajiriwa kama mwalimu wa English Medium School hapa mjini Arusha.

Wiki iliyopita nikitokea wilayani Monduli ambako nilienda kwa sherehe za Krismasi nilipanda basi na nikawa nimeketi na mzee mmoja wa kimasai. Alipofika maeneo ya Burka alishuka, na akawa amesahau mfuko wake wa rambo pale chini ya kiti alipokuwa amekaa. Sikuwa nimeuona mpaka nilipokuwa nateremka kwenye basi hapa Arusha mjini.

Ilinibidi kuangalia ndani ya ulie mfuko na nikaona kuna pesa za ajabu.

Sikumwambia mtu na nikazichukua nikashuka ndani ya basi na kungoja kama yule baba atakuja pale stendi ili nimpatie. Nilikaa pale stendi kwa masaa 7 (kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 12 jioni)na sikumwona kabisa yule bana japo kweli nilijitahidi kumtafuta.

Ilibidi niende nazo nyumbani. Kufungua nikaanza kuzihesabu. Zipo shilingi milioni 4 na laki sita taslim. Sasa yule baba simjui na tayari mimeshatoa matangazo kwenye redio nikisema aliyepotewa na pesa aje kwangu. So far sijamwona yule baba. Wanakuja matapeli tuu.

Nawaomba wadau wako wanishauri hizi fedha nifanyeje nazo? NIZITUMIE MIMI, NIPELEKE KWA MCHUNGAJI au NIPELEKE POLISI? Dhamiri yangu bado inanisuta.

Ni mimi
LAIZER M.J.D,
ARUSHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 62 mpaka sasa

  1. Ni bora ukasaidie yatima nazo.Kuna wazazi wengi hawana uwezo wa kuwalipia Ada ya shule watoto wao,wazazi hawana uwezo wa kulipia matibabu hospitalini,watu hawana uwezo wa kununua chakula.Chukua kiashi kama 2.3milion kawape hawa watu kama unawajua kweli wanahitaji msaada wako.Nyingine tumia wewe na familia yako
    Mdau Uk Edinburgh

    ReplyDelete
  2. teh teh teh... kaa nazo hadi ziki-expire..

    ReplyDelete
  3. DA KWELI WEWE MWAMINIFU NITUMIE MIMI NIKUONESHE PA KUPELEKA A/C NO 01J2477662800 CRDB MOROGORO

    ReplyDelete
  4. MOJA CHA KUFANYA KWA VILE WEWE NI MTU WA MUNGU NA UMESHATANGAZA HIVI NI KUWA WEKA KWENYE AKAUNTI YAKO. NENDA PALE ALIPOSHUKIA YULE MZEE UMUULIZIE NA UBANDIKE MATANGAZO YA KISWAHLI NA KIMASAI, NENDA KWA GARI ILILOPANDA ULIZIA MWENYE GARI KAMA UWA MNAKA TIKIKETI JARIBU KUKUMBUKA NAMBA YA SEAT ILI UWAULIZIE WENYE GARI KAMA WANA KOPI YA RISITI YA SIKU HIYO NA NAMBA YA KITI HICHO, NENDA MAKANISANI NA MISIKIINI UKATOWE MATANGAZO HAYO, NENDA KWENYE VYOMBO VYA HABARI VIKUBWA KAMA ITV, TBC, NA VINGINE KAMA HIVYO PAMOJA NA MAGAZATI MAKUBWA NA YA HAPO ARUSHA NA RADI ZA HAPO ARUSHA KOTE UKO TOA MATANGAZO NA UTOWE RIPOTI POLISI LAKINI USIPELEKE PESA POLISI WEKA NDANI YA AKAINTI YAKO MWENYE AKIJA UMPE, POLISI WASIKUTISHE KUKUAMBIA UPELEKE PESA POLISI HAMNA SHERIA KAMA HIYO UNACHOTAKIWA TU NI KUTOWA RIPORT POLISI NA KUACHA CONTACTS ZAKO MWENYEWE AKIPATIKANA AJE KWAKO KUZICHUKUWA. SI VIZURI KUTUMIA PESA YA MTU WAZEE WENGINE WANATISHA UTATUMIA UNAWEZA KUPATA MABALAA HATA KUFA PIA INAWEZEKANA. FANYA KILA KITU ILI UMPATE MWENYEWE NA WAKATI UNAMKABIDHI KUWE NA MAKABIDHIANO YA KISHERIA ILI KAMA NI TAPELI NA MWENYE NAZO HALALI AKITOKEA IWE RAHISI KUMPATA TAPELI, MUKABIDHIANE MBELE YA SHERI NA POLISI NA KILA MTU AACHE CONTACS ZAKE. UNAWEZA KUKAA NAZO HIZO PESA KWA MIAKA SITA BAADA YA HAPO KAMA MWENYWE HAJATOKEA NI ZAKO NA AKITOKEA BAADA YA MIAKA SITA UTAMTOLEA KUMBUKUMBU ZA JITIHADA ZAKO ZOTE ZA KUMPATA IKASHINDIKANA NA MIAKA SITA IMEPITA NIMEZITUMIA. KWA SASA FANYA KILA JITIHADA KUMPATA, LAKINI PESA ZIWE CHINI YA CUSTODY YAKO USIMPE MTU HATA POLISI USIMPE

    ReplyDelete
  5. We Tafuna tu dada kwa jina la bwana wetu Yesu Kristu, anakupenda ndio maana amekupa wewe mwenyewe hujipendi!!

    ReplyDelete
  6. Naaah Mama WEWE HUKU OKOTA UMECHUKUA PESA ZA WATU!! Kuokota ni kama ungelizikuta njiani au sehmu yeyote na hakuna mtu yeyote maeneo hayo. Ulichofanya wewe ni kuchukua pesa za msafiri mwenzako aliyezisahau! Lile ni basi ulichotakiwa kufanya ni kuzikabidhi kwa wahusika ambao ni wamiliki wa basi hilo. Kwani naamini kitu cha kwanza atakachofanya mzee wa Kimasai ni kwenda kwenye ofisi za basi hilo kuulizia kama kuna mzigo wowote ulionekana. Sasa kwa wewe kuzichukua kumebadilisha utaratibu mzima wa ufuatiliaji wa mizigo ipoteayo katika vyombo vya usafiri na ulibidi USHITAKIWE. JE AKIJA AKASEMA ZILIKUWA MILIONI 20 utakataa. Je unakithibitisho chochote kuwa hazikuwa milioni 20?? Siku nyingine usifanye hivyo utaingia matatizoni. Ulichotakiwa kufanya ni hichi: kuzichukua moja moja na ukae kimya na labda ungetoa sadaka kidoogo kanisani au msikitini ili Mungu wako akusamehe AU Kuzikabidhi fedha zile kwa wahusika hapo ofisini kukiwa na mashahidi juu kama sio polisi pindi tu ulipofika safari yako. Haya mama mlokole mi nilikuwa nachangia tu! Bwana Asifiwe! Amin!

    ReplyDelete
  7. Finders keepers.... hizo ni zako polisi watagawana tu kula mwenyewe halafu mwombe mungu baadae, ni riski yako hiyo.

    Mdau North America

    ReplyDelete
  8. nakushauri weka benk kwa miezi mitatu kama hajatokea basi hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu kulingana na wema wako wa ukristo ulikuwa nao hivyo baada ya hapo tumia na timiza ahadi yoyote uliyoweka na Mungu kama ningepata... ningetoa sadaka fulani

    ReplyDelete
  9. Duh hongera sana kwa uaminifu wako watu kama nyie tungeliwapata katika serikali yetu tusingekuwa masikini, kwa ushauri wangu hizo pesa usizipeleke polisi endelea kusubiri akiwa hakutokea mwenyewe kwa kipindi kirefu itakuwa hiyo ni zawadi yako maana hutopata dhambi kwavile umeshatoa taarifa mpaka kwenye redio

    ReplyDelete
  10. Mama Ubarikiwe kwa moyo huo.

    Hizo pesa usizitumie, na wala usimpe mtu yeyote bali kaweke bank kwenye account yako ukisubiri mwenye pesa zake aje. Kama hatatokea kwa miezi kadhaa then iwe yako.

    Na kwa kuwa umetangaza wala huna shida tena, roho yako ni nzuri sana.

    Mzee aliyepoteza huenda hajui Kiswahili au hata kusoma.

    ReplyDelete
  11. maskini labda ilikuwa ndo school fees endelea kusubiri tu mzee wa watu labda hata kajinyonga masikini

    ReplyDelete
  12. UTAKUFA MASIKINI WEWE!!MDAU ANAYEKUONEA HURUMA....

    ReplyDelete
  13. kumpata mwenye pesa halisi itakuwa ngumu zikienda polisi hazitamfikia mwenye nazo na ukipeleka kanisani watafaidi wachache ushauri wangu ni kuwa kwakuwa wewe umesema ni mcha mungu basi nakushauri kiasi cha pesa saidia wasiojiweza na kiasi kingine tumia mwenyewe kwa faida ya na pia katoe sadaka kiasi kingine kanisanikumbuka pengine hiyo ni thawabu yako toka kwa Mungu na pia ni mtego toka kwa huyohuyo Mungu anatakakuona uaminifu wako ,kwa kifupi hiyo ni sawa na bahati kwako

    ReplyDelete
  14. HUJAOKOKA.

    PESA SIO ZAKO UNAHESABU ZA NINI. CHUKUA MFUKO KAMA ULIVYO AND DO THREE THINGS.

    PELEKA POLISI UTOE TAARIFA. KUHAKIKISHA ALIYEPOTELEWA ANAPATA HAKI YAKE MAKE SURE PESA ZINAPOKELEWA NA KUHESABIWA IN YOUR PRESENCE AND THEN WAKUPE DEPOSIT SLIP STAMPED AND PROPERLY SIGNED.

    KATOE TAARIFA KWA MCHUNGAJI ASAIDIE KUTANGAZA ILI HABARI IWEZE KUWAFIKIA WATU WENGI.

    KATOE TAARIFA KWENYE VITUO VYA REDIO NA TV. KUTOA TAARIFA NI BURE.

    KAZI BADO UNAYO NDUGU YANGU, POLE.

    ReplyDelete
  15. mpe ankal

    ReplyDelete
  16. kwa sasa kapande mbegu, muombe mungu ama kwa hakika utamwona mzee na utampa fedha zake taslimu na mbegu za ziada

    ReplyDelete
  17. Wewe unajitakia matatizo bure ndugu yangu. Kama bado unazo hizo pesa watu watakukaba bure wazichukue, kama huna nawe unachokoza nyuki unajitakia makubwa.

    Utazidi kukutana na matapeli ......
    Hizo pesa zikabithi kwenye usalama sasa hivi halafu endelea kutangaza.

    ReplyDelete
  18. Hizo ni za kwako... Mungu huwa anatoa kwa njia zake mwenyewe. Usikute ulikuwa unamlilia Mungu ukihitaji msaada wa pesa. Sasa amekupatia kwa njia yake. Zitumie tu dada kwa roho nyeupe! Hujaiba.

    ReplyDelete
  19. dada hongera sana kwa uaminifu wako. natumaini ulishazipeleka benki kwenye akaunti yako wakati unasubiri mwenye nazo kujitokeza, manake majambazi wasije wakakuvamia nyumba kwa kuzani ziko humo ndani, na pia unapopeleka hayo matangazo ni vema ukataja pia kwamba pesa hizo ziko benki kwa sasa. Ni kwa usalama wako tu. Mungu akulinde dada, na kama walivosema wengine ukipita muda tosha hajatokea basi ni zako, wala usije ukajisikia vibaya ungekua na nia mbaya ungekaa kimya tangu mwanzo.

    ReplyDelete
  20. Kama kweli wewe umeokoka na umejazwa nguvu za roho mtakatifu, mwombe Mungu akufunulie maana yake nini kuokota hizo pesa, kama kuna kikundi cha maombi uwashirikishe swala hili kisha roho mtakatifu akikufunulia nini maana yake, toa fungu la kumi kanisani na salio ni zawadi yako ya mwaka mpya. Na tumia kwa lolote utabarikiwa wala usiwe na wasiwasi. Kumbuka ulimwomba Mungu nini na wakati mwingine majibu ndo yanakuja kwa njia hiyo. Na inawezekana alionekana kama mzee wa kimasai kumbe alikuwa ni malaika wa Bwana!
    Wakati mwingine wakristo wanajaribiwa kwa njia hii ili kupimwa imani yao. Na inaelekea Mungu ana mambo mengine mengi mazuri juu ya maisha yako endelea kumtegemea wa suimwache kwani atakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua.
    Ubarikiwe dada kwa kuwa mwaminifu.
    Ndimi mtumishi wa Bwana!

    ReplyDelete
  21. MUNGU huwa anazidosha kama majani nyie hamaamini
    umedondoshewa wangu.........kama unashida sana zitumie au kasaidie yatima wasijiweza

    ReplyDelete
  22. DADA!

    HAKIKA WEWE NI MCHA MUNGU, NAMUOMBA ALLAH AKUPE YALIYO MEMA ZAIDI.

    USHAURI WANGU NI KUIWEKA HIPO PESA BANK WAKATI UNASUBIRI BABU WA KIMASAI ARUDI.

    NA IKITOKEA HAJARUDI BASI NAFIKIRI NJIA NZURI NI KUITUMIA HIYO PESA KATIKA NJIA AMBAZO MUNGU ANGEPENDA.

    UNAWEZA SAIDIA WATOTO MAYATIMA, AU WAZEE KWA NAMNA ENDELEVU. SIO KUWANUNULIA SODA AU KUWAPA CHAKULA. LAKINI UNGEWEZA CHANGIA KATIKA UJENZI KAMA WA KISIMA CHA MAJI.

    ALTERNATIVELY, IINGIZE HIYO PESA KWENYE BIASHARA AMBAYO UNAJUA INAWEZA KUTOA FAIDA KUBWA, HALAFU UKAENDELEA KUSAIDIA MASIKINI AU WATU WENYE UHITAJI KATIKA JAMII MPAKA IFIKIE HIYO 4.6M

    BAADA HAPO KILICHOBAKIA NI CHAKO. ILA NAKUSHAURI USIFANYE PUPA KWANZA, VUTA SUBIRA HUENDA BABU WA KIMASAI ANA UDHURU HIVYO HAPATIKANIKI. MPE HATA MIEZI 6

    UBARIKIWE SANA

    ReplyDelete
  23. Hujaokoka, una matatizo ya akili. Kila siku si unaomba Mungu akupe mkate. Kakupa unakataa, wewe ni taahira.

    ReplyDelete
  24. Hizo pesa feki, huyo mzee kakuingiza kingi, anasubiri uzipeleke Bank, halafu anakuja. Ukitoa Bank, zinakuwa halali. Huraa.
    Natania mwayego, ni kutokana na kuangalia sinema sana. Tehe tehe

    ReplyDelete
  25. Mkata IssueJanuary 06, 2010

    Ule ule mtindo wa utunzi wa habari za kusisimua.

    Nisipotoa ushauri nao ni ushauri tosha.

    ReplyDelete
  26. Hizo hela ni zangu. Zilinidondoka wakati nipo safarini kwenye migodi yangu ya Tanzanite.

    Kaa nazo mpaka nitakapokuja kuzichukua na nitakupa sehemu yako kwa ajili ya uaminifu wako.

    Anti natania tu lakini nakupongeza na kukusifu kwa uaminifu wako. Mungu akubariki.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  27. Tafuta admission ya shule kiwanja uje kubeba box na kushika nyaa, hiyo nauli tosha!

    Ukishindwa kiwanja nenda ata kwa Zuma.

    Dah!

    ReplyDelete
  28. wapewe YATIMA NA WAJANE

    ReplyDelete
  29. asante sana hizo pesa ni zangu. Nipe namba yako ya simu tuwasiliane.

    ReplyDelete
  30. mi anaunga wazo la kumpa ankal mithupu, ili usafishe nafsi yako kwa sababu ankal atazitumia kuboresha blog ya jamii ambayo wakati mwingine hutumika katangaza mikutano ya kiroho na mapambio kwa wingi......
    ...i`m just playin wich y`all....

    ReplyDelete
  31. Hongera sana dada kwa uaaminifu wako. Tungekuwa na viongozi wa nchi kama wewe aisee tungekuwa mbali, sijasikia watu waaminifu kama wewe miaka mingi sana.
    Ubarikiwe usipeleke pesa polisi watazila zoteee, kaa nazo endelea kutangaza akija mwenyewe mpe pesa zake.
    Au Mungu kakushushia nini?? endelea kuomba Mungu akuonyeshe inaweza ikawa umepewa zawadi na Mungu haluuuuuuuuu!!!!!!!

    ReplyDelete
  32. mhangaikajiJanuary 06, 2010

    MIMI NILIWAHI KUPOTELEWA NA HELA KIASI HICHO HICHO 4.6 MILLION WAKATI NASAFIRI KWENYE BASI MWAKA 2006 NILIWEKA KWENYE RAMBO, HIVYO NITUMIE MIMI KWANI NAONA KAMA "DEJAVU" VILE! A/C YANGU NMB 01J111800458996

    ReplyDelete
  33. dear kaka,

    Kwa ushauri wangu, naomba uzipeleke kwa watoto yatima..kwani hujui sababu za kuweza kuzipata wewe hizo pesa, na kama ni riski yako basi ndio imekuwa huwezi badili mipango ya Mwenyezi Mungu.
    Tena nashukuru kusikia kuwa nawe ni mtu wa Mungu. Sikushauri kabisa uzipeleke polisi wala kanisani, kwani wengi wao matumbo yameshiba na sioni kama wataweza kuzitumia kwa kusaidia jamii.

    Shauri langu ni uzitumie kwa ajili ya kuwasaidia wale wenye shida haswa, Mwenyezi Mungu atakulipa kwa njia nyingi na tofauti.

    Kila la kheri.

    Hs

    ReplyDelete
  34. Na mimi naunga mkono, apewe Ankal Michuzi ili aboreshe globu ya jamii. Fanya hivyo mpendwa utapata thwawab.

    ReplyDelete
  35. Na mimi naunga mkono, apewe Ankal Michuzi ili aboreshe globu ya jamii. Fanya hivyo mpendwa utapata thwawab.

    ReplyDelete
  36. Ninamuunga sana mkono anon wa Tue Jan 05, 11;31:00 PM kwa kusisitiza kumbuka ulimwomba nini Mungu; pia usimpe mtu hizo pesa ziweke bank ukisubiria mwenye zake kwa kipindi cha miezi mitatu hajatokea toa fungu la kumi endelea kuzitumia.

    ReplyDelete
  37. Zipeleke DECI upande mbegu ili baadaye uvune

    ReplyDelete
  38. Hongera sana mtumishi wa bwana. Hapo umeonyesha uaminifu wako kwa mungu. Kumbuka mwaka uliopita ulikuwa wa mambo magumu na huu ni mwaka wa marejesho. Mungu atakurejeshea kila ulichopoteza mwaka uliopita na pia amekupa haja ya moyo wako.
    Kumbuka kutoa sadaka na nyingine tumia kuendeleza biashara zako au kujiendeleza.

    Ubarikiwe katika bwana

    ReplyDelete
  39. Dada, wachungaji pia wana mahitajiyao ya kijamii na hela hizo watazitumia tuu kwa mahitaji hayo. Chukua hizo hela nunua Bibilia na uzipe mashirika ambayo yasiyo ya kiserikali ambayo yatazisambaza kwa wakristu humu Tanzania na hata Uganda. Michael

    ReplyDelete
  40. mpe anko michuziiiiii.......kama jina lake...hzo kwake ni madafu 2

    ReplyDelete
  41. Duh, ila wewe ni mwizi kwa kuwa haukuwa ni mwisho wa safari kwa nini ulichukua na kufungua mzigo ambao sio wako?

    Na kama uliokota na kuona mwenyewe amesahau kwa nini usiuwakilishe kwenye uongozi wa basi bila kufungua?

    na tutajuaje sasa kama kweli ulikuta kiasi hicho na sio zaidi?? ila sheria haiko upande wako mpaka sasa.

    kila la heri!!!!!!!

    ReplyDelete
  42. Katika dunia ya leo ni watu wachache sana wenye moyo kama wako. Ulivyotangaza ni sawa subiri miezi 3 basi amua kama kutoa sadaka au zitoe kwenye kituo cha kusaidia watoto yatima nk, Lakini kwa nini umetaja kiasi kamili? Maana watakuja matapeli aina nyingi, ilikuwa utaje siku,gari sehemu aliyoshukia na pia kama unamfahamu kwa sura ili isiwe rahisi kujileta asiyehusika kuja kutapeli.HONGERA

    ReplyDelete
  43. zipeleke CCM, uchaguzi umekaribia. au niletee mimi nikuwekee.

    ReplyDelete
  44. Dada Mungu akubariki sana kwa uaminifu .
    1. Huenda huyo MZEE alikuwa ni malaika wa Mungu aliyetumwa kukuletea pesa hizo. Je, hujawahi kuwa na uhitaji wa pesa hivi karibuni? Kumbuka maombi yako ya nyuma. Lakini kabla ya kuamini kuwa ni malaika Mwombe Mungu adhiririshe hilo, kama sio malaika mwenye pesa hizo atatokea tu.
    2. Tangaza kwenye vyombo vya habari kuwa kuna mzigo ulisahaulika kwenye basi hilo, elezea aina ya mzigo na rangi yake. Usitajeklikuwa na nini ndani yake. Atakayejitokeza na mhoji kwa undani a prove kweli ni mzigo wake.mahojiano hayo yafanyike kisheria isije ikatokea utapeli. Vilevile acha kutangaz kiasi cha pesa kilichopo usije ukavamiwa na wezi.Asipotokea kwa muda ambao Roho mtakatifu atakushuhudia kuwa umetosha,tumia hizo pesa, usisahau kutoa fungu la kumi. kabla ya kuzitumia mwombe Mungu na kukemea mapepo ambayo yanaweza kuwa yalitumwa kukumaliza kwa njia ya pesa.
    Otherwise Mungu akubariki kwa uaminifu huo.

    ReplyDelete
  45. jaman, kwanza hongera sana kwa kuwa mwaminifu sana na kuto kukaa kimya na hela za watu.
    mm nakusahuri sana usizitumie mpaka hapo utakapopata ufumbuzi wake. watakuwepo watu wa kukushauri vitu vya ajabu sana bt stay focused to be faithful not only to man bt to GOD he hu knows all things.
    nakushauri ukaziweke benki hizo hela kwa usalama zaidi. watajitokeza maraafiki wengi sana sasa hivi, bt be careful, wanaweza kuwa wengi kwa ajili ya uharibifu wako.
    God is faithful, he will fight on ur side.
    KUMBUKA: ukiwa mwaminifu kwa MUNGU na yeye atakuwa mwaminifu kwako.
    HE NEVER FAILS. HE IS SO FAITHFUL. SO LOVING. SO CARING . IF ONLY U STICK TO HIS RULES, PRINCIPLES AND REGULATIONS.
    BE BLESSED.

    ReplyDelete
  46. dah wewe mama unatania ama unasema ukweli watu hatuna hela alafu unasema hizo habari watakuvamia humo ndani kwako hiyo ni fungu lako la kumi mungu kakupa mshukuru na usiache kumuomba....

    ReplyDelete
  47. mama HelenasraJanuary 06, 2010

    duuh watu kama nyie bado mpo zama hizi?
    tuwasiliane ili tufanye mpango wakukupeleka makumbusho maana mmebaki wachache sana nahisi mtatoweka kabisaaa..
    Natania tu...
    mungu anajibu maombi kwa njia nyingi mama,,,ndo maana hata mwizi huomba apate mtu wa kumkaba na kweli wewe na hela za mkopo unajikuta unapita anga zake,baadae unasema ile njia mi huwa hata sipiti sijui imekuaje leo ningejua ningepanda taxi..hayo yote mungu anakuwa alikufunga ili ukampe huyo mwizi kwa kuwa kamuomba.
    sasa wewe ni mcha mungu nina uhakika lzma ulimuomba hakuna mtu asiye na matatizo yanayohitaji pesa,ndio kakuletea hvyo ingawa ni tofauti na alivyomletea mwizi..
    TUMIA TU KWA RAHA ZAKO

    ReplyDelete
  48. Mali na vyote viujazavyo ulimwengu ni mali ya Bwana, Pereka Kanisani uone kama Mapadri/Wachungaji hawajazitumia,hahaha, we Masai kweli ungekuwa unatoka kwa akina Masawe wala usingetwambia

    ReplyDelete
  49. Hiyo ni Mungu amekupa na wewe hakikisha unaitumia vizuri.

    ReplyDelete
  50. hongera mamangu kwa moyo wa uaminifu uliopewa. ushauiri wangu ni kwanza uache kuwapa watu anuani yako eti waje kwako, watakuua bure mametu na wanao wabaki yatima. ushauri ziweke kwanza bank, pili katoe matangazo kwa hilo bus ulilopanda, hapo mzee aliposhukia. useme tu mtu aliyesahau mzigo wake, husiseme kiasi cha pesa wala km nipesa. aliyezitupa akipata tangazo hilo akaja , vizuri unamuuliza baadhi ya maswali, km uliufungaje mzigo, nini kilichomo ndani nk. kisha unaongozana naye bank kuchukua mzigo wake. wakati unatangaza mwambie tuwasiliane kwa namba fulani ikiwezekana ubadiri namba kabisa, akikupigia umuhoji kwenye simu kabisa, baadhi ya maswali niliyokupa hapo juu na mengine unayoyajua wewe, akishajibu vizuri, unamwambia tukutane mjini kwani pesa zipo bank tayari, na ukifika mjini unajibanza sehemu uhakikishe unamchunguza kama ni yeye. akikosekana basi kasaidie yatima na wajane. Mungu atazidi kukubariki. amen

    ReplyDelete
  51. kwa kweli kumpata huyo baba ni huko burka ukiweka tangazo kule anaweza akapatikana na hakika atakuwa kawaeleza jamaa zake wa huko burka na kingine hawa njeree asiliamia kubwa hawajui kusoma na redio wanapenda kusikiliza RTD hapo kuna kazi kanisani polisi usipeleke hata kanisani kuna mafisadi polisi ni wanafiki asipopatikana toa fungu la kumi saidia yatima na wajane nyingine tumia usimalizie zote kwenye msaada hata maandiko yanasema ipende nafsi yako kwanza

    ReplyDelete
  52. ASANTE SANA NDUGU KWA UAMINIFU WAKO...PESA HIZO NI ZANGU MIMI NILIMTUMA MMASAI AKANINUNULIE MIFUGO MNADANI AKADAI ZIMEPOTEA ! !KWA KWELI NILILIA SANA NA KILIO CHANGU KIMESIKILIZWA KABISA! ! SASA FANYA TUONANE PALE BILLICANAS KWA NYUMA WANAPOPAKI MAGARI NYUMA SIKU YA JUMAMOSI SAA 5 USIKU ILI UNIKABIDHI HIZO PESA NA UTABALIKIWA SANA! UTANITAMBUA HIVI: NITAVAA KANZU NYEUPE NA KOFIA YA BLUU KICHWANI... ASANTE SANA KWA WEMA WAKO HUO ! !

    ReplyDelete
  53. KUNA WATU HAPO WANASEMA HAKUOKOTAAMEIBA/AMECHUKUWA. MIMI NAPINGA NA HAO, NI WAZI AMEOKOTA HATA MWENYE BASI HAWEZI KUWEKA PESA CHINI YA KITI, PIA HAMNA GROUND YOYOTE YA MWENYE NAZO KUJA NA KUSEMA ZILIKUWA MILIONI 100, KWANI HAKUKUWA NA MAKABDHIANO YOYOTE RASMI YA KUHALALISHA HOWM MUCH THE MONEY WAS!!! WALA USITISHIKE HUWEZI HATA KIDOGO UKAMBIWA ZILIKUWA BILLIONI 100, KWA KUFANYA HIVYO SHERIA ITABIDI IFUATE MKONDO WAKE NA HATA MWENYE NAZO PIA ANAWEZA KUZIKOSA KWANI HAKUNA HATA ALAMA MOJA INAYOWEZA KUDHIBITISHA KUWA PESA NI ZAKE. NA WALA USIPELEKE POLISI HAKUNA HATA SHERIA MOJA YA NCHI INAYOONYESHA UKIOTA KITU PELEKA POLISI UNACHOTAKIWA NA KUTOWA RIPOTI TU NA UNAENDELEA KUWA CUSTODIAN WA HICHO KITU HADI MWENYE NACHO ATAKAPOTOKEA NA KUNA TIME LIMIT YA KUKAA NACHO ASIPOTOKEA KWA MUDA HUO NI CHAKO NA SHERIA ITAKULINDA STATUTORY OF LIMITATION, SIX YEARS ARE ENOUGH AFTER THAT THE MONEY IS YOURS

    ReplyDelete
  54. HII NI HADITHI YA KUSIMULIA. HAKUNA UKWELI WOWOTE

    ReplyDelete
  55. Rafiki hiyo pesa ni ya kwangu ati....nashukruru sana rafiki kwa kunitunzia hiyo pesa...hebu fanya nitafute kwa number hii hapa mama (0777777777) maana utakuwa umeniokoa na mama yoyo maana alitaka kunichinja! We ni mutu aminifu sana rafiki...Mungu akubariki...nitakupa sawadi ya mbusi moja rafiki.

    ReplyDelete
  56. DADA, KUWA NA FIKRA JADIDU PIA..
    BIBILIA INASEMA -MGONJWA NDIYE ANAYEMFUATA DAKTARI..

    WEWE UNATANGAZA YA NINI?? WAKATI MWENYE FEDHA HAJATANGAZA KUPOTEZA MWENYEWE KWENYE HIVI VYOMBO VYA HABARI???

    MILLION 4.6? AFU ARUSHA? TENA APANDE HIECE? KWENYE MFUKO WA MALBORO?..

    COME ON!!
    THINK LOUDER..

    ReplyDelete
  57. HII SIO YA KWELI. WALA SIAMINI JAMBO HILO !....HUMU DUNIANI HAKUNA MTU MWEMA WA NAMNA HIYO USIDANGANYE WATU ! HAKIKA AKITOKEA MTU MMOJA TU MWEMA WA NAMNA HIYO DUNIANI ATAWEZA KUUAMBIA MLIMA KILIMANJARO UNG'OKE KUTOKA HAPO ULIPO UKAOTE MAENEO YA MWANZA AU UTAWANYIKE NA HAKIKA UTATAWANYIKA AU KUYEYUKA KABISA. JAMANI KWA KWELI 1+1=11 HABARI NDIYO HIYO ! !

    ReplyDelete
  58. Mchangiaji 'anonymous' hapo juu ni kweli wapo watu waaminifu wa namna hiyo, na tena wengi tu, labda wewe na wachache wengine mnaoamini haiwezekani kufanikiwa mpaka udhulumu. Kama ungekuwa umeokoka kama huyo dada alivyosema, ndiyo ungeelewa ana maana gani, tofauti na hivyo utadhani kila mtanzania ni fisadi.
    Mimi kwa upande wangu ningeungana na wengine waliomsihi huyo dada avute subira, asifanye pupa. Kutangaza kwa watu ni kiasi gani alichonacho naona amefanya haraka. Ningemshauri yafuatayo:
    1. Angerudi kwenye ofisi ya lile basi akawauliza kama kuna mtu amekuja kuwauliza kwamba amesahau fedha kwenye basi. Namshauri asiwe anatembea na hizo fedha kwenye viroba, bali aziweke mahali salama.
    2. Kama kuna matangazo yametolewa kwenye radio, asitaje kwamba aliyepoteza ni mmasai au asitoe taarifa nyingi sana juu ya hilo suala ili iwe rahisi kwake kuchuja mchele na chuya kwa watakaojitokeza. Aseme tu kwamba kuna mtu aliyesahau kitu kwenye hilo basi tarehe fulani awasiliane na ofisi ya hilo basi. Ofisi hiyo uwe umeiachia no. yako ya simu ili huyo mtu akiwasiliana nao wakisharidhika naye wampe no. yako uwasiliane naye.
    Ni vyema taarifa za kuwa alishuka wapi, saa ngapi, alikuwa amevaa nini, na alikuwa anakiasi gani aziseme yule mwenyewe anayedai kuwa fedha ni zake. Na nina amini kwamba hata sura yake utaikumbuka ukionana naye. Ila pia mimi naona matatizo mawili hapo:
    1. Kama alivyoshauri mwingine hapo juu, nashindwa kuelewa kilichokufanya ukapekua mzigo wa mtu mwingine ni nini? Hiyo inakuhusu vipi wewe? Kwa nini usingeshuka ukaendelea na safari yako? Au kama safari ingekuwa ni mwisho, kwa nini usimwambie dereva kwamba unaona kuna mzigo kama umebaki kwenye basi na hauna mwenyewe? Kama utingo au dereva wa basi wangezichukua hizo fedha wewe inakuhusu nini? Una uhakika gani kama wasingempa? Haya ndiyo matatizo ninayoyaona ya watu kujiingiza kwenye kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu! Kama ungekuwa unamfahamu huyo mtu ni kitu kingine, lakini hatua uliyoichukua ya kuchungulia ndani ya begi la mtu na kuambaa nalo nashindwa kuielewa kabisa! Ungekuta ndani ya begi kuna uchafu je, ungelichukua bado?
    2. Kama ni mmasai, wengi hawasikilizi redio wala hawasomi magazeti, kwa hiyo chaguo alizonazo ni ama kwenda kwenye ofisi ya hilo basi au kuingia mitini akihofu kuulizwa hizo fedha kazipata wapi. Kwa hiyo ni naona kwa hali ilivyofikia sasa, uendelee kuvuta subira ukishirikiana na ofisi ya lile basi au ikishapita miezi mitatu uzipeleke hizo fedha kwenye ofisi ya hilo basi na kuzikabidhi ukiwa na mashahidi siyo chini ya watatu, watu waaminifu siyo wasanii. Wenye hilo basi watajua nini la kufanya.

    Ahsante.

    ReplyDelete
  59. mimi ni mlokole pia ila nakushauri ki2 kimoja ukimpata huyo baba usitake hela yake hata shing 10 hiyo ni corruption...unachotaka n hapo sasa?kama kumtafuta kamtafute hukooo aliposhuka sio kwenye net coz yeye anaweza kuwa mkulima hana hata radio nenda mtafute ukimkosa sikiliza akili yako!!!!
    inavyoonesha huitak hiyo ela nenda kwa wajane na yatima kadiposit huko ili ubarikiwe!!!

    ReplyDelete
  60. ao waliokujia si matapeli, na wao walipoteza pesa(kiasi hichohicho) ila kwenye basi jengine, tatizo hawakumbuki basi walilopanda

    ReplyDelete
  61. michuzi huwachi na we kwa story zako

    ReplyDelete
  62. Kama hujui matumizi Njoo tukutane sakina Nikuonyeshe mimi na vijana wangu tunavyoichana PESA kama maji.nusu saa kwisha yote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...