jamaa anapiga hatua kumi sinia...dah!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. ebwana kuna ustaadhi hapo mwenye barkhashia pembeni mwa jamaa mwenye shati la pundamilia ametoa tabasamu la uchu huku akimwangalia mbeba sinia
    ambaye pia amevaa uso wa mbuzi

    ReplyDelete
  2. huyo jamaa aliekaa mwenye shati la mistari,anaona kama anaeonewa shoti anatamani angemrukia huyo jamaa alieshika sinia la pilau.Lakini pila la shughulini tamu.

    ReplyDelete
  3. Msela mwenye fulana ya mistari kulia.. naona kainuka kidogo kutathmini idadi ya viazi mbatata na nyama, ili ajipange. Ukiona mikono inaning'inia hapo ujue wanaume washanawa. Ah..mpunga wa shughulini asikwambie mtu.. hata Muhidini Issa Michuzi analijua hili.

    Mdau Udachi.

    ReplyDelete
  4. hapo wakianzisha vagi watasema jamaa wagonvi kumbe wamechokozwa.

    ReplyDelete
  5. jamani maskhara acheni hapo kuna watu wanamakarama namaombi yao yanakubaliwa basi heshima inahitajika na dua kukubalika nyie endeleeni na mchezo.

    ReplyDelete
  6. Amini usiamini hiyo sahani ikitua tu kwenye ardhi.....basi ujue haina nyama wala kachumbari wababe wameshachukua na viko mikonoini mwao....na hiyo pilau kama haukuwa fasta basi unaweza ukaambulia tonge moja tu....Ilike our life back home.....full social

    ReplyDelete
  7. ebwanaeeeeeee!!!! hii kali kuna wana hapo wanautolea mpunga wa sahani macho ile mbaya bongo mterezoooooooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  8. Tatizo ni uwezo tu, lakini fadhila nyingi hapo. Kuhudhuria ni ruksa kwa yeyote, Kuchangia ni hiari/Uwezo. Kidogo tutagawana sote. Hakuna haja ya kujifungia ukumbini na kuwanyima, hususan wasiojiweza nao kujivinjari na wanajamii wengine kwa mapilau na minyama. Ankal ukikuta shughuli kama hii (Maulid, Ndoa, Msiba nk) katika pilika zako unachangia 200, ukienda kwenye mnuso kule plaza unachangia 450,000!!

    ReplyDelete
  9. Aww meen...LOL i was rolling on the floor laughing my ***off (ROTFLMAO). Imenikumbusha mambo ya waandazi....kisha sinia la mashee maarufu wale linakuwa na manyama kibaaao,Nazi hukuu naziii!!. Wengine wanaficha sinia duh LOL. Kisha TO GO ndani ya mfuko wa Rambo

    ReplyDelete
  10. kule nyumbani zanzibar hii inaitwa style ya magoli makubwa... teh teh teh

    ReplyDelete
  11. Ee Bwana, Shughuli kama hizi zinanikumbusha zama hizo za Mburahati, Kigogo, na Magomeni mwembechai! Sunia likiwekwa chini kwanza na mwendo wa kupiga reki matonge ya nyama na baadae ubwabwa! Kweli utajua bado kuna dhki ya mlo katika familia nyingi! Ingawa utafiti mwingi unaonyesha kuwa Binadamu wengi ushirikiana katika mlo/chakula na nadra ushirikiana katika mambo kujamiana, na wanyama wengi ushirikina katika mambo ya kujamiana na wanyama danra kushirikiana katika mlo: Lakni ninapokaa sasa na theory hizi mbali mbali za elimu ya saikologia naona wazi kuwa katika Hali ya Sinia hilo hapo juu ni wazi hakuna kushirikina katika mlo! Kama mto maoni anavyosema kuwa watu waemechokozwa! Kama msemaji mmoja Anic Kashasha alivyowahi kusema kuwa; "Adui wako mwombee njaa". Kweli njaa na dhiki ni rahisi sana kumrudisha binadamu katika kiwango cha mnyama.

    ReplyDelete
  12. Duh huyu jamaa mpangilio wa hatua 10 atakuwa anaumiza jamaa vibaya sana. Alitakiwa apige hatua kama 4 hivi halafu anaangusha sinia.
    Ankal hatua 10 haikubaliki kwanza imeshapitwa na wakati

    ReplyDelete
  13. Mimi nipo hapo pembeni ya jamaa mwenye Barakashia na nina ndizi mbivu kwenye mfuko wa shati. Mechi ilikuwa kali kiasi ndizi ilibidi niile baadaye. Maana sahani kuwekwa chini tu. Nyama zote hakuna. Mimi niliambulia Kachumbali na matonge manne. Nami nasifika kwa spidi.

    We acha, wali mchafu(Pilao) NOMA!!

    ReplyDelete
  14. hizo ndio zetu maeneo ya huku kwetu mwananyamala kisiwani kama maeneo ya madukamatatu,msikitini, zamaleki,kwasindano. hapo ukishakula ujue siku imepita ilakunawatu huwa tunawakwepa ukikaanao unaumia kwaniwanamatonge makubwa mfano huyo msela aliyevaa kofia kaegemea ukuta

    mdau
    mwananyamala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...