Ankal,
Heri ya mwaka mupya? Salaam kwa wadau wote wa globu ya jamii pia.
Naomba msaada kwenye tuta. Natafuta shule ya msingi ya English Medium
kwa ajili ya mwanangu. Ni mtoto wa kike, ana miaka 8, mwaka huu wa
2010 anaingia darasa la tatu.
Shule iwe Dar, Arusha, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Bagamoyo au Kilimanjaro.
Hivi sasa yuko kwenye shule moja ya English medium hapa Dar sema
kinachoniuzi ni kwamba kila baada ya miezi mitatu wana likizo hivyo
mtoto anarudi nyumbani (ambako huwa hasomi). Nataka shule ambayo mtoto
akienda kurudi ni baada ya miezi sita.
Wadau mnaojua shule za English medium katika maeneo yaliyotajwa hapo
juu naomba mnisaidie majina na namba za simu. Kama namba ya simu huna
basi jina tu sio mbaya.
Asanteni.
Wenu mdau.
Heri ya mwaka mupya? Salaam kwa wadau wote wa globu ya jamii pia.
Naomba msaada kwenye tuta. Natafuta shule ya msingi ya English Medium
kwa ajili ya mwanangu. Ni mtoto wa kike, ana miaka 8, mwaka huu wa
2010 anaingia darasa la tatu.
Shule iwe Dar, Arusha, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Bagamoyo au Kilimanjaro.
Hivi sasa yuko kwenye shule moja ya English medium hapa Dar sema
kinachoniuzi ni kwamba kila baada ya miezi mitatu wana likizo hivyo
mtoto anarudi nyumbani (ambako huwa hasomi). Nataka shule ambayo mtoto
akienda kurudi ni baada ya miezi sita.
Wadau mnaojua shule za English medium katika maeneo yaliyotajwa hapo
juu naomba mnisaidie majina na namba za simu. Kama namba ya simu huna
basi jina tu sio mbaya.
Asanteni.
Wenu mdau.
KUNA SHULE NZURI SANAAA INAITWA ST. PATRICK IPO ARUSHA NAMBA YAO KWA SASA SINA ILA NAWEZA KWENDA KUKUANGALIZIA NYUMBANI NI YA DAY AND BOARDING IPO ARUSHA.
ReplyDeleteThe following is a list of schools in Tanzania:Ingia website hii http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_schools_in_Tanzania utapata list kama hizi hapa chini na contact zao
ReplyDeleteAgape Lutheran Junior Seminary
Aga Khan Mzizima Secondary School, Dar es Salaam
Aga Khan Primary School, Dar es Salaam
Al Muntazir School Network, Dar es Salaam
Arusha School
Braeburn Schools, Arusha
Dar es Salaam Independent School, Dar es Salaam
Haven of Peace Academy, Dar-es-Salaam
International School Moshi, Moshi [1]
International School Moshi, Arusha Campus [2]
International School of Tanganyika, Dar es Salaam
Isamilo International School Mwanza, Mwanza [3]
Kwanza International School, Dar es salaam
Loyola School, Dar es Salaam
Montfort Agricultural Secondary School, Rujewa
Namfua Secondary School Kilimanjaro
East Coast Secondary School -Kibaha, www.kibaha.xaper.com
School of St Jude, Arusha, Tanzania
Shaaban Robert Secondary School, Dar es Salaam
Kisongo Academic College, Arusha
Ali Hassan Mwinyi Elite Schools, Dar es Salaam
kahororo seondary school Bukoba
Feza Nursery School-Dar'es-selam-Mikoceheni
Feza Nursery School-Dar'es-selam-Tegeta
Feza Nursery School-Zanzibar
Feza Primary School-Dar'es-selam-Mikoceheni
Feza Primary School-Zanzibar
Feza Boy's Secondary School-Dar'es-selam-Tegeta
Feza Boy's High School-Dar'es-selam-Tegeta
Feza Girl's Secondary School-Dar'es-selam
Kibosho Girls Secondari School- Moshi
Old Moshi Secondary School- Moshi
Mawenzi Secondary School- Moshi
Msaranga Secondary School- Moshi Rural
NA NYINGINE NYINGI
Ndugu, kama unaweza mtoto asome shule ya 'day' akiwa shule ya msingi. Kwani huu ni wakati wa kujenga tabia. Utashangaa mtoto kawa mkubwa ana tabia za walimu, au hata humjui vizuri mwanao. Samahani kwa kutokukupa jibu utakalo, nimeguswa tu.
ReplyDeleteInaonyesha mzazi hupendi kumuona mwanao nyumbani, unapenda kuelelewa hata wakati wa likizo, du! hiyo ni tabu sana kwani ulezi ni kati ya wazazi na waalimu. Mwache mtoto shule hiyo hiyo, na acha uvivu wa ulezi.
ReplyDeletekuna shule moja iko kilimanjaro ya masista toka kenya and tanzania) nzuri sana iko maeneo ya holili nikipata contact zao nitakujulisha.
ReplyDeleteNi kitu gani kinachokufanya usitake mtoto awe anarudi nyumbani kwa likizo muda mfupi mfupi? Ni usumbufu anaokupa au? na inakuwaje unasema mtoto akirudi likizo huwa hasomi? Huna muda nae? Jitahidi ujifunze kuinvest time kwa mtoto wako. Kurudi kwake kwa likizo nadhani ni nafasi nzuri kwako kama mzazi ya kukufanya uwe karibu na mtoto na kuweza kujua udhaifu wake katika masomo mbali mbali,, na hivyo kupeleka feedback huko shule... unless wewe sio mzazi wake au sio responsible parent ndo maana unacomplain hii issue.
ReplyDeleteMdau unaye tafufa shule ya namna hiyo jaribu kuulizia shule ya msingi ya kisabato iliyopo Kongowe. Ninauhakika mtoto akienda shule mwezi wa kwanza anarudi likizo mwezi wa sita. Pia wanapata mapumziko ya wiki moja hapo katika na hata kwa muhula wa pili.
ReplyDeleteKha! we mama humpendi mwanao kiasi hicho? hivi unajua madhara ya mtoto kuishi bording? tena ni mtoto wa kike? unataka shule ambayo mtoto awe unakutana nae mara 2 kwa mwaka? unalako jambo.
ReplyDeleteMimi mwenye ni mama na nina watoto 3,na mimi mwenyewe nilisoma bording,kwa uzowefu wangu binafsi sipendi mwanagu awe mbali na mimi kiasi hicho,saa ngapi utakuwa karibu na mwanao kumuelewa tabia zake?saa ngapi atapata mapenzi ya wazazi? tena mbaya zaidi na nyinyi wazazi kama wote ni wafanya kazi ni mateso makubwa kwa watoto, labda kwa kukusaidia fanya utafiti kwanza kwa mtoto ambae amesoma bording kuanzia darasa la kwanza mpaka form four na mtoto aliesoma bording kuanzia form one mpaka four inaweza kukusaidia kidogo.
Usharu wangu kwako kama hiyo shule anayosoma ni nzuri muache aendelee akiwa likizo nyumbani mtafutie tuition awe anasoma,jamani tuwe na huruma hawa watoto tunawatesa sana kukulia bording school sio kuzuri kabisa.
Ni ushauri tu,take it or ignow.
Pole kwa matatizo ya shule;; Nipo hapa Kilimanjaro kuna shule nzuri sana ya mapadre na masista wa shirika la Holy Spirit ipo Soweto Moshi inaitwa Moshi Airport Academy School; Box 6402 MOSHI AU TELEPHONE NUMBER 2750228 2754495.
ReplyDeleteNImekusaidia kwa vile nachukia sana shule ya likizo ya miezi mitatu mitatu nachukia sana sana
Nguzo english medium ni school safi sana na ipo morogoro ukitaka more info wasiliana na leylaomar17@yahoo.com.
ReplyDeleteMimi nitakusaidia mwanangu nimempeleka uko Bagamoyo kuna shule inaitwa Mwasama na ni maarufu sana pia ina waalimu wazuri
ReplyDeleteHAYA KAZI KWAKO,FOTOBINBARAZA
Mtoto wa miaka 8 kwenda kusoma shule ya bweni, mbali na wazazi wake? mhh, kila la kheri katika msako wa shule. Morogoro kuna shule moja inaendeshwa na masista wa katoliki, unaweza kujaribu, nimesau jina.
ReplyDeleteLAZY!! UNAOGOPA KULEA NDUGU YANGU. WHY DOING THAT??
ReplyDeleteKWA MTOTO WA MIAKA 8 SHULE YA LIKIZO YA MIEZI 3 NI MUHIMU SANA KWA MZAZI KUWEZA KU-MONITOR MAENDELEO YA MTOTO KIELIMU NA KITABIA.
FIKIRIA TENA.
We mzazi vipi? hutaki mwanao mdogo ivo arudi nyumbani? unataka shule ndio ikulelee mtoto?
ReplyDeleteKama kwa bahati mbaya English haipandi au huezi msaidia mtoto wako kusoma wakati wa likizo kwa sababu yoyote ile basi mtafutie hata kijana wa form six awe animpa assignment za hapa na pale na kumsomea vitabu pia.
Nadhani kwa umri huo mdogo ni vizuri watoto kupumzishwa kila inapowezekana na vizuri kwa mtoto na vizuri kwa mwanafunzi wa kiwango chochote kile.
watu wengine bangi kweli!!!
ReplyDeletesasa english medium maana yake si mambo huko ni kizungu uzungu tu, wewe kama unataka shule za kusoma kwa miezi 6 mfululizo si umpeleke kiparang'anda.
OTHERWISE, NAMNA GANI VIPI LIKIZO AJE KWETU.
uamuzi ni wako
hovyoooooooooo..sasa kama akirudi nyumbani si umtafutie masomo ya ziada tu?sidhani kama mtoto wa miaka 8 ni vyema awe mbali hivyo na mzazi,tena kwa muda kama huo unaoutaka wewe.au umeshastukia kama mtoto si wako?u sounds little strange!!??
ReplyDeletekuna shule ya baording iko kilimanjaro nzuri tu ya masista. wasiliana na head teacher wao. shule inaitwa ST.RITALISA OF MT CARMEL. IKO NJE KIDOGO YA MOSHI. HOLILI AREA. VERY NICE SCHOOL. TEL.0782337976.ALL THE BEST
ReplyDeleteWEWE VIPI? HUYU MTOTO WA KWAKO? BABA NA MAMA YAKO WAPO? KAMA MAJIBU YAKO NI NDIYO MIMI NAKUSHAURI AENDELEE KUSOMA SHULE HIYO HIYO AMBAO KILA MIEZI MITATU ANARUDI NYUMBANI.
ReplyDeleteHALAFU KWA TAARIFA YAKO TU HAKUNA SHULE AMBAYO WATOTO WANASOMA KWA MIEZI SITA MFULULIZO BILA KWENDA LIKIZO.
MTOTO MDOGO WA MIAKA 8 KWA NINI ASOME SANA?
MTOTO MDOGO KAMA HUYU ANATAKIWA AISHI NA WAZAZI WAKE KARIBU. KAMA UNATAKA AENDA SHULE NA KUKAA HUKU KWA MUDA MIEZI SITA BASI HATAKUWA NA TOFAUTI NA WATOTO YATIMA WANAISHI KWENYE VITUO.
FIKIRI VIZURI
Mtoto asome mbali na mzamzi wake, mda gani utakuwa nae, ucheze nae, akuzoeee, umulize leo umesona nini shuleni? Umulize leo umefanya nini? Hata ukiletewa malalamiko shuleni usubiri mpaka miezi 6 ndio umkanye. Mtoto wako atakuwa na mapenzi gani na wewe? Tabia yake ya ukubwani utaijuwa vp? Kama huko anasoma la ashaanza uhuni, maana watoto wengine tabia mbaya uhanza wakiwa wadogo? Brazza mi sikushauri mtoto mdogo uwe nae mbali nahisi ili litakuwa somo tosha kwa Watz wote. Mtoto wa miaka 8 anahitaji mapenzi ya baba na mama
ReplyDeleteMaofisini kuna mambo ya kudanganyana haswa mambo ya shule za watt, usilogwe kuuliza kuhusu shule utaambiwa mengi mazuri tu mabaya hawasemi!
ReplyDeleteniliingia mkenge nikapeleka kibint changu 10yrs boarding jamani naweza kulia hapa bure yaliyomkuta siwezi kusimulia maana ni ya aibu na mpka leo NAJILAUMU sana
bora wewe ulipata wazo la kuja kuuliza hapa na mimi naungana na hao wanaokwambia KAA NA MTT WAKO
na mara nyingi wazazi wanapeleka watt wao brdng bila sababu za msingi eti mwingine anakwambia mtt hapendi kula hivyo akienda huko atajifunza, eti miezi 3 yupo home eehhhy!!
kuna siku utataka kukaa/kuongea na mwanao na hasiwe na time na wewe TRUST ME
8 yrs ni mdogo sana
Hivi wazazi wengine huwa mnalazimishwa kuzaa watoto au vp? inakuwaje mtoto wa miaka 8 umpeleke bording yaani kwa akili zako kama wewe umeshindwa kulea (kwanngu mimi mzazi anayepeleka mtoto mdogo hivyo bording ni mvivu wa kulea hakuna sababu nyingine) mwanao itakuwaje kwa sister au mwalimu kukulelea mwanao, tena kumbuka hyu sister haangali mtoto wako tu kuna watoto kama 20 hivi ambao anapaswa kuangalia (kuwalea) ooh god kwanini mnazaa sasa? "arme kind"
ReplyDeleteNapenda kuwashukuru wote waliotoa majibu kwa ufasaha.Hao wengine ni waosha vinywa tu hakuna mtu hata mmoja ambaye ambaye hampendi mwanaye mwanaye mngeuliza huyu mtu anayetafuta shule yuko kwenye hali gani kwanza.Nikiwa na mimi ni muasilika wa hali kama hiyo hizi medium english zimekuwa kama mradi na mtoto anaporudi anarudi na ada mpya na hapo nyumbani kwenu wanafanya kama mradi mtoto aliwa shule haumwi wala simu za ajabu ajabu haupokei ila anaporudi tu mambo yanaanza leo kuna ili kesho kuna lingine. hii yote ni sisi wazazi tuliopo ughaibuni kwa ajili ya kutafuta maisha kwa hiyo jamani msituelewe vibaya hata za sekondari tutumieni majina
ReplyDeleteWaafrika, kusoma siyo kitu kinachoweza kufanywa na kila mwanadamu. Kama mwanao ana uwezo mzuri wa kusoma, lazima utakuwa umeshalijua hilo kama ana miaka minane. Kama bado hujalijua hilo, baasi endelea kumuangalia anaweza kufanya kitu gani. Ingawa hii haina maana kwamba asisome shule.
ReplyDeleteUsije ukampeleka kampala au nairobi, watoto wote "with no exception" waliokwenda kampala au nairobi walikuwa "sexually abused" na wanafunzi wenzao au watu wengine, ingawa hawasemi.
Nimewahi kufundisha kampala na nairobi na najua ninachokizungumza.
JAMANI MSIMLAUMU SANA YAELEKEA HUYO NI MTOTO WAKE WA KAMBO SO KUMUONA ONA HOME INAMSUMBUA SANA WAKATI MAMAYAKE NA HUYO MTOTO JAMAA ANA MPENDA KWA SANA SO DAWAANAONA NI BORA DOGO AWEANAKUWA SHULE 4 LONG TERM
ReplyDeleteKweli Bongo tambarare!! yaani mzazi hata uzazi wa Part-time umemshinda. Haya ndio mambo unakuja kukuta mtoto anaaccent ya Kikenya kumbe Mkwere.. Hivi wazazi design hii hata diaper walibadili kweli? Unadhani uzazi ni kulipa skuli fizi? hiyo si hata Madonna anaweza kumlipia. So, Mjomba, punguza kwenda kwenye kikontena na nyumba ndogo ulee mitoto yako!! Nyamafu we!!
ReplyDeleteMdau, Boston, US.
upumbavu tu,nani alikwambia kukaa sana shule ndio kufaulu?
ReplyDeleteshule niliyosoma mimi,tunaanza muhula mwezi wa tisa,mwezi wa kumi mwishoni tunafunga kwa wiki moja,mwezi wa 12 tunafunga kwa wiki mbili kwa ajili ya x-mass,mwezi wa pili ile wiki ya valentine day tunafunga kwa wiki moja,mwezi wa 3 tunafunga kwa wiki moja kwa ajili ya st.pad,mwezi wa nne tunafunga kwa ajili ya pasaka,mwezi wa tano tarehe 30 shule zinafungwa kwa ajili ya form six na form 3 wafanye mitihani.
hao si wengine ni wazungu ambao ndio mnaowaiga kwa kila kitu.
punguani wewe,kaa na mwanao ujue ana kipaji gani na nini anapenda.
Mpe mtoto makala za Mashaka.
ReplyDelete(US Blogger)
Nakuomba saaana saana usikilize watu wanayokuambia ndugu mzazi maana Haujui kabisa mambo mengine yanayotendeka in Boarding school and it's even worse because your daughter is Just 8 for heaven's sake, Have some mercy and please try to be a parent figure.
ReplyDeleteI don't really know what situation you're in but believe me, when that girl is a teenager, you'll regret having done this. I thank my parents for having made a choice of letting me go to a very good English medium primary DAY school and an English Medium boarding secondary school, it worked very well and I can be nothing than thankful to them. If she's such a nuisance then just look for a part time teacher or tuition since then she'll study at home, if her not studying really bothers you.
Trust me, six months is a very long time, I just turned 17 but I need some kind of support system which is my parents,...
I have no Idea what kind of parent you are, I've been to a strict Christian boarding school and I know what goes on,... she's just too young to handle such kind of separation from her parents. IF YOU REALLY CARE ABOUT YOUR DAUGHTER THEN PLEASE CUT THE CRAP AND THINK TWICE!
Kama shule anayosoma ni nzuri then all you have to do ni kumtafutia activity nyingine akiwa likizo. Unaweza kumtafutia swimming classes, language course, piano etc. Kusoma sio darasani tu.
ReplyDeleteJamani uwongo si kazi, mimi nimeshare nyumba na watoto waliosoma boarding Tanzania kuanzia wadongo na wangine kuanzia form 4 na siye wengine tulikua daycare toka vidudu mpaka form six.
ReplyDeleteBwana ukweli ni kuwa tabia zinakua tofauti sana kati ya mtoto aliyesoma boarding toka vidudu au toka form 4.
Yaani wote nilioishi nao waliosoma boarding toka watoto tabia zo ni very awkward...kwanza ni wachafu, wavivu, very selfish na wahuni sana tu.
Mimi as a mama nimesema sitampeleka mtoto wangu boarding school hata iweje mpaka high school au hata akiwa college...
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...jitahidi kuweka stamp yako akiwa bado mdogo na ni kwa faida yake akiwa mkubwa...
KELAND NURSERY & PRIMARY SCHOOL IS THE BEST IN DAR.
ReplyDeleteIpo Kunduchi salasala RTD.
0713 236938
dahh
ReplyDeleteNdo wazazi wa kisasa hao. mtoto akizaliwa analelewa na House Girl
kutwa mama kiguu na njia ukimuuliza yupo buzy na kazi.akirudi hata ajaribu kuonyesha upendo kwa mtoto hakuna kwa muda mfupi hamna mtoto akimsogelea anamwita house girl amtoe kisa ana dai amechoka. akifikia umri wa kwenda shule mnampeleka boarding akalelewa na waalimu. Ole wenu matokeo yake mtakuja kuyaona mkizeeka. Mnafikiri na wao watataka kukaa na vizee vinavyojinyea nyea na kijikojolea. Matokeo yake kipindi hicho kutakua na nyumba za wazee kama ilivyo ulaya na wao watawapeleka huko kwa sababu hawana upendo na wazazi wao sababu hawakulelewa nao na wajibu wao ni uwalipia kwa mwezi tuu kwenye hizo nyumba mchezo umeisha. Kwa kwa hali ya bongo hizo nyumba zitakua ovyo ile mbaya. Kazi kwenu mnao wakimbia watoto wenu.
Mdau Bongo Forever(I love my kids i will never send them to bording school when they are young)
There is a little school called Southern Highlands School in Mafinga town. Excerpts follow bellow:
ReplyDelete"The Southern Highlands School has maintained outstanding academic performances in Standard VII National Examinations, with all candidates who sat for examinations passing and being selected for progression in government secondary schools. The school has consistently been ranked among the best primary schools in the country.
* Southern Highlands School boasts 9 straight years of 100% passes for all Standard VII candidates.
* In the National Standard VII examinations for the year ended 2008, the National Examination Council of Tanzania, NECTA, ranked the school 4th (out of 147) in Mufindi District; 7th (out of 823) in Iringa region; 68th in the nation (out of 13,948) primary schools.
* In the National Standard VII examinations for the year ended 2009, the National Examination Council of Tanzania, NECTA, ranked the school Number 1 in Mufindi district (out of 149) and Iringa Region (out of 830) respectively; 14th in the nation (out of 14,376 primary schools.)
Southern Highlands School
P. O. Box 34
Mafinga, Tanzania
Phone: +255 26 2772661
Fax: +255 26 277254
e-mail : southernhighlands97@yahoo.com
Contact them for more info.
Wala usihangaike kulipa mamilioni kumpeleka boarding ambayo atakaa huko baada ya miezi sita unamuona. Wee mpeleke Msimbazi kwa masista kabisa, huko wewe unapeleka pesa kidogo ya kusaidia matumizi basi imetoka hiyo, atalelewa pamoja na watoto yatima. Maana nakumbuka zamani tulipokuwa wadogo ulianza kulia mama!! Basi tulikuwa tunaambiwa na cousins wetu, mama, mama, mama yuko Msimbazi. Nilipopata akili ndio nilielewa nini maana ya mama yuko Msimbazi.
ReplyDeleteHuko Msimbazi masista watamlea, watampa chakula, nguo, na elimu, na atacheza na yatima wenziwe, kisha utakuwaga unamuona kwenye luninga watu wakipeleka msaada.
Sasa unataka nikwambie nini? ikiwa hutaki kumuona huyo mtoto hapo nyumbani, anakunyima raha za kuselebuka na Ngwasuma si bora umpeleke mahala utakapomuona akishamaliza shule? Kuna single parents ambao maybe wake zao walikufa wanapeleka watoto kulelewa huko tangu wako wachanga!
kiukweli mzazi akae na mwanae muda mrefu iwezekanavyo. huyo mtoto wa miaka 8 laiti ungejua jinsi anavyokuhitaji psychologically... umeulizwa unataka mwanao afanane na walimu wake kitabia? hebu ngoja kwanza, ni kweli huyo mtoto wa 8yrs unayetaka aende boarding arudi after 6 months ni wako? i know it is very bad question but u deserve to be asked that way! au kama ni wa kwako, unaplan ya kusafiri mwaka mzima na huna ndugu unayemwamini kukaa na mwanao? if that's the case it makes a bit of sense, la sivyo pls kaa na mwanao, ujue ana hali gani kiafya, kielimu na ujue anasocialize namna gani! kumbuka muda wa kumuacha akae mbali na wewe utafika na hutopata tena nafasi ya kuwa naye karibu, kwanini usitumie muda huu kukaa naye karibuni jamani? nina kijana wa 11 yrs, sifikirii hata kwa mabomu kumpeleka boarding school for now, angalau akienda f5 nitaona cha kufanya, na pia nikipata day school bado he will be day sccholer! ana haki ya kukaa na mimi, nijue ni nini kinamfurahisha, what triggrers his anger (ili niweze kumsaidia), i need him to have enough access with me atakapo balehe ili kama akiwa na swali lolote akijiskia kuniuliza aniulize mimi mzazi wake... heee jamani kaeni na watoto wenu, mtajilaumu sana ikiwa bahati mbaya mtoto ata end up kuwa na tabia mbaya, akiwa na mzazi hata akiwa na tabia mbaya mzazi hutajilaumu coz at least u tried! hey, kwaheri...MTOE HATA HIYO BOARDING YA 3 MONTHS AND LET THE CHILD BE DAY SCHOLAR, AKITOKA SHULE JIONI MPATIE MWL WA KUMSAIDIA HADI SAA MOJA THEN MTOTO ANASOCIALIZE FOR AT LEAST 1 HR ANAENDA KUPUMZIKA MAHALI PASAFI AMBAPO UNAHAKIKA KUWA NI PASAFI NA PIA UNAHAKIKA KABISA KUWA KALA WHAT HIS/HER BODY NEEDS! PARENTS SHOULD TAKE OWNERSHIP AND BE RESPONSIBLE FOR THEIR KIDS GROWTH AND WHATSOEVER!
ReplyDeletehivi kiingereza mtoto si anaweza kufundishwa nyumbani tuu? au wewe mzazi pia maimuna?
ReplyDeleteNingekushauri uwe makini sana na hizo mshule za bording especialy hizo za mapadri maana wanatumia dini ili watu waamini kuwa watoto wao wako salama lkn utashangaa watoto wana lawitiwa kila siku na hao mapadre.Jitahidi uwe na mwanao muda mwingi ujue ana tabia gani na pia anapata upendo kutoka kwenu wazazi huko mabording ndiko watoto wanajifunza wizi, ulezbian, ugay,umalaya na pia wanakua abused na kuwa bullied bila kujua wapi waelekee kupata msaada au nani wa kumwambia maana wewe mzazi huko karibu nae na pengine abuser ndie mtu aliepewa uangalizi wa huyo mtoto.wito kwa wazazi muwe makini sana na watoto hata nyumbani muwe makini na ndugu mnao ishi nao na pia kuwa karibu na kujenga urafiki na mwanao ili iwe rahisa kuelewa mapema nini kinachoendelea kuhusiana na mwanao.
ReplyDeleteVictim of abuse
St, si sijui nanni vile, Mt, mapadre sijui masister schools, sawa lakini mpleleke pia Daaru l arkam, chamazi au Morogoro, pia Mudio islamic na hata kirinjiko, mbona nyingi tu hata za upande wa shilingi??? au ndo mnaogopa??? tehetehe
ReplyDeleteI DONT REALY KNOW KWANINI WATU WAKO SO AGAINST BOARDING SCHOOLS,MIMI NAONA THE TYPE OF BOARDING SCHOOL UNAYOMPELEKA MWANAO MATTERS ALOT.KUNA MDAU ALIDAI ETI SHULE ZOTE ZA BWENI ZA NAIROBI NA KAMPALA ZINAABUSE WATOTO,TENA AKADAI KUONGEZEA, WITH NO EXCEPTION..INAONEKANA YEYE NDIO THE ABUSER WA WATOTO HAO MANAKE ANAONEKANA YUKO SOOOOO DAMN SURE.NIMESOMA BOARDING SCHOOL NAIROBI NA SIKUFANYWA LOLOTE BAYA.LIKIZO NILIKUA NARUDI MARA 6 KWA MWAKA.NILIJIFUNZA KUJITEGEMEA MAPEMA SANA AND I TURNED OUT TO BE A VERY CONFIDENT INDIVIDUAL.KILA SIKU NAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA SUCH AN OPPORTUNITY.SHULE NILIMALIZA ZAMANI NA NIKO BONGO NA WAZAZI WANGU TUKISHIRIKIANA KULIJENGA TAIFA
ReplyDeleteJAMANI ACHENI KUJUMULISHA MAMBO OVYO ETI WANAFUNZI WOTE WANAOSOMEA U WALIOSOMEA KAMAPALA/NAIROBI/NJE WANAKUWA/WALIKUWA SEXUALLY ABUSED!!!! HAYA MAMBO KAMA YAPO BASI YANATOKEA MAHALA POTE DUNIANI KAMA YANAWEZEKANA BOARDING ZA NJE BASI HATA BOARDING ZA TANZANIA, SI BOARDING TO HADI DAY SCHOOLS, KWANI KUNA WATOTO WANGAPI WANALAWITIWA MITAANI MWETU HUMU NI WENGI TU SO THAT IS POINT LESS TO BRING UP HERE, JUST OFF POINT. KUHUSU UMRI MIMI SIONI KAMA KUNA TOFAUTI KATI YA MTOTO WA MIAKA MINANE NA YULE ANAYEANZA FORM ONE AMBAYE ANAENDA BORADING HAWA WOTE NI WATOTO SASA IWEJE TUSIWE NA WASI WASI NA HUYU NA TUWE NA WASI WASI NA HUYU, ALL JUST RUBBISH POINTS. KAMA YEYE ANAONA NI VYEMA MWANAE AENDE BOARDING SCHOOL MWECHENI AMPELEKE, ATAJUWA MWENYEWE NAMNA YA KUMUELEKEZA NAMNA YA KUISHI HUKU SHULE. KUNA WATU WAZIMA NA AKILI ZAO WAKO BOARDING, VYUONI NA UNIVERSITY WANAFANYA VITU VYA KIJINGA SO GONNA BE NOT ALIEN THING TO HER. CHA MSINGI NI KUWA NAE KARIBU NA KUMUELEKEZA NAMNA YA KUISHI NA WATU MTOTO ALELEWI KAMA YAI, THEY NEED TO BE TOUGHNED NDO MAANA TUKO NYUMA KI-ELIMU KWA KUOGOPA KULAWITIWA, UKIENDA KWENYE INTERVIEW NA DEGREE YAKO UNATOLEWA KAPA NA MTOTO ALIYEMALIZA FORM KENYA/UGANDA.
ReplyDeleteDuh! hii kali; sijawahi kusoma Nairobi wala Kampala na sijawahi kushindwa kiingereza na mwafrika wa kutoka nchi yoyote ya afrika.
ReplyDeleteUkipeleka mtoto Nairobi machizi lazima watamfyonza utamu tuu.
Huku maofisini kuna mambo sana; utasikia Beti anasema "Mwanangu freddy anaondoka jumamosi, anakwenda shuleni nairobi..., amenimalizia pesa yote jamani...";
Asha naye utamsikia "Amani amenipigia simu kutoka shuleni kwao Kampala anataka pesa tena..."
Basi hapo Ester naye lazima akamshike koo mumewe; kwanini mtoto wao, Sean anasoma Njombe na hasomi Nairobi au Kampala.
Kero zinaanza ndani, ugomvi bila sababu ya msingi; matokeo yake Dume likitoka kazini linaona likakae baa lipige tembo lake kwanza kukimbia fujo za ester nyumbani.
Nyinyi hayo mambo ya kuiga iga hayo...! Tangu lini Nairobi au Kampala kukawa Uingereza? Kwa mlioishi ughaibuni, baadhi yenu mmewahi kuishi na wakenya ughaibuni. Ni kweli Kenya au Uganda kuna kiingereza cha kukufanya umpeleke mtoto wako akanyonywe utamu?