Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. James Msekela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo Jumatatu kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza kesho Jumanne. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kweli nchi yetu inaharibu vipaji. Dk Msekela ni mtaalam mzuri sana wa "High Voltage", kanifundisha pale FOE ila ndiyo hivyo wanasiasa hawawajali kabisa wataalam matokeo yake inakuwa kubanana hukohuko. Je tutafika?

    ReplyDelete
  2. Nadhani hata kufundisha alifundisha kwa mwaka 1 au miwili tu?! Na kwa sasa sidhani kama umeme anaukumbuka tena!!!??? Na nina hakika hawezi kurudi tena kushika chaki!?
    Tutafika lakini kila mtu kivyake.

    ReplyDelete
  3. Prof. Mwandosya, Prof. Mgombelo, huyo Dr. Nsekela wote vichwa vya umeme viliondoka FoE. Sasa vichwa siasa!

    ReplyDelete
  4. Du, kweli kalcha ni tofauti kila mahali. Huku majuu kushikana mikono hivyo inaweza kuwa nongwa kweli na kutafsiriwa vingine. Kusalimiana sawa..ila kutembea mmeshikana mikono hivyo? Mhh...kazi kweli.

    ReplyDelete
  5. Hivi hapo Waziri Mkuu na Mkuu wa mkoa wameshikana mikono??? Aha hiyo sooo!!

    ReplyDelete
  6. Watanzania kwa kujifaragua na kuiga mambo hatuwezekani,nani hajui kwamba Tanzania ni poa tuu wanaume kushikana mkono?nani hajawahi kushikwa mkono wakati anaishi Tanzania ?Soma habari ufurahi ,tuache kasumba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...