President Jakaya Mrisho Kikwete with Barrick's Gold Corporation top management team at Mwanza state Lodge Monday evening. From left they are Barrick Tanzania Executive General Manager Mr.Deo Mwanyika, Aaron Regent Barrick's Chief Executive Officer and President of Barrick Gold Corporation(Second left), President Jakaya Kikwete, Kelvin Dushnisky Barrick Executive Vice President(fourth left) and Greg Hawkins Barrick's Chief Financial Officer.
Photo by Freddy Maro


HAO VIONGOZI WA BARICK SIJUI WANAMCHUKULIAJE JK HASA WAKIFANANISHA MIKATABA WANAYOSAINI BONGO NA ILE WANAYO SAINI BOTSWANA. ALAFU USIKU KUCHA AKINA PINDA WANAFIKIRIA AKOMESHE VIPI VISEMINA VYA WATUMISHI WA UMMA, BADALA YA KUTUMIA MDA MWINGI KUTAFAKARI KWANINI SERIKALI INAPOTEZA MABILIONI YATOKANAYO NA RASILIMALI ZETU. NYERERE HAKUSHINDWA KUITA WAWEKEZAJI WA NAMNA HII LAKINI ALIONA NI HERI MADINI YAKAE ARDHINI HAYATAOZA MPAKA TUTAKAPOKUWA NA UWEZO WA KUYACHIMABA WENYEWE. KUTOKANA NA UBINAFSI WA VIONGOZI WA SASA WAKAONA YACHIMBWE TU HATA TUKIAMBULIA ASILIMIA TATU KULIKO YACHIMBWE WAKIWA HAWAPO MADARAKANI HIVYO WASIYAFAIDI. BINAFSI NAWACHUKIA SANA VIONGOZI WETU KWA KUSAINI MIKATABA YA NAMNA HII MAANA NIMEBAHATISHA KUSOMA MMOJA.
ReplyDeleteMichuzi nibanie kama vp nimechoka kubembeleza
Du! JKeiiiiiiiiiiiiiiii
ReplyDeleteUmeona wanachelewa ukaamua kuwafuata? wewe ni kiongozi nambari wani bwana kwanini wasije kwako magogoniiiiii? Nomaaaaaaaa
Naona mjomba kenda chukua comisheni yake mwenyewe hamna kuaminiana mwaka wa uchaguzi huu hahaha!
ReplyDeleteHAWA JAMAA WA BARRICK WANAFANYA LOBBYING KWA RAIS KIKWETE. NA HII SI MARA YA KWANZA KWANI KIKWETE AMESHAONANA NA HAWA JAMAA MARA NYINGI TU TANGU AINGIE MADARAKANI. SASA KWA SABABU KIKWETE KAZI YA URAIS ALIPEWA NA WANANCHI INABIDI AWAELEZE WANANCHI HUWA ANAZUNGUMZA NINI NA HAWA JAMAA MARA KWA MARA. JE MAZUNGUMZO HAYO YANA FAIDA KWA WATANZANIA WOTE HAWA NI KWA HAO BARRICK NA VIONGOZI WACHACHE WA SERIKALI?
ReplyDeleteKWA UJUMLA SERIKALI INABIDI IWE MACHO SANA NA MAKAMPUNI YA NJE KWA SABABU MAKAMPUNI YA NJE YANAIBIA SANA NCHI HII. KWANZA- KWA KULIPA KODI KIDOGO HAPA NCHINI (KAMA ILIVYO KWENYE DHAHABU KWA SASA 3%), PILI- KWA KUFANYA MANUNUZI MENGI KWA BEI YA JUU KWA KUTUMIA MAKAMPUNI MAMA, TATU, KWA KUUZA BIDHAA NJE KWA BEI YA CHINI SANA KWA KUPITIA MAKAPUNI MAMA, HIVYO FAIDA BADALA YA KUONYESHWA NA MAKAMPUNI YA HAPA NCHINI INAONYESHWA NA MAKAMPUNI MAMA KWENYE NCHI ZAO-HII INA MAANA KODI YA FAIDI INALIPWA KWAO SIO HAPA KWANI HAPA KAMPUNI INAONYESHA HASARA KILA MWAKA.
KUNA TETEZI KWAMBA KAMPUNI MOJA IMEINGIA MKATABA NA SERIKALI UNASEMA KUWA ITALIPA MRAHABA WA ASIMILIA 10 TU. KAMA NI KWELI HII NI KICHEKESHO KWANI TAYARI TUNA MFANO WA ASILIMIA 3 KWENYE DHAHABU SASA BADO SERIKALI INAKUBALI ASILIMIA 10 KWENYE MAFUTA.
michuzi usibane hii comment, kwani itasaidia hata wajukuu wako baadaye. Nia hapa ni kujenga Tanzania sio kufurahisha wala kuchukiza watu.
Anon wa kwanza kabisa hapo juu hebu tuskanie hiyo mikataba uliyoiona halafu itundike kwenye internet wananchi wengine tujue kinachoendelea.
ReplyDeleteSasa hivi inakuwa ngumu kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika sakata la madini maana mikataba iliyosainiwa hatujui inasemaje.
Sasa watu wenye busara hatuwezi kuongea bila kujua mkataba unasemaje.
michuzi , mdau hapo juu amesema kweli kabisa. siku hizi hamna kuaminiana kabisa , mzee mzima kaamua kufuata mgao wake mwenyewe mwanza..
ReplyDeletehabari kaka michuzi nina hoja ntuonyataka kuongelea lakini iko nje ya mada
ReplyDeletejana kwenye usiku wa habari mwandishi shupavu tanzania jery muro alituonyesha jinsi askari wanavyochukua rushwa naomba ufutilie zile picha then uweke kwenye globu yako ili wadau wengine wapate kuona
Nchi yetu Tanzania itachelewa sana kupiga hatua za maendeleo. Sababu kubwa ni majungu. Watoa maoni karibu wote hapo juu ni majungu. Naamini watoa maoni hawa watakuwa wafanya kazi ktk ofisi mbalix2. Kwa maana hiyo wanalipwa mshahara bila kufanya kazi. Maana muda wa kazi wao wanaandika majungu hapa mtandaoni. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteNi kweli kabisa kuwa wengi waliotoa maoni hapa wanajaribu kutokotesha majungu. Ni vizuri kufanya utafiti wa jambo husika kisha utoe maoni yako na si kukurupuka kama wengi wetu tunavyofanya. Kumtuhumu JK ki hivyo ni utovu wa nidhamu kwa viongizi hasa wanaojitahidi angalau watanzania tupate kidogo kilichobaki baada ya wajanja wachache kuchua.
ReplyDeleteJamani tuweni wastaarabu katika kufikiri na kuandika.
anon wa kwanza umenena, wananchi tunapewa abstract ya mkataba contents private ni kwaajili ya usalama wa taifa
ReplyDeleteHii picha inanikumbusha picha ya Rais Obama na wakuu wa kampuni ya wawekezaji (kama ipo).
ReplyDeleteHIVI WATANZANIA TUNA NINI? MBONA TUNA WIVU WA KIJINGA? WATU WANAKAMATA CHAO MAPEEEMA HATA UNGEKUWA WEWE PENGINE UNGEFANYA HIVYOHIVYO NI HELI KEKI IKILIWA NA WATU WACHACHE WAKASHIBA KULIKO WAKALA WATU KIBAO ALAFU WOTE MKABAKIWA NA NJAA.
ReplyDeleteWAZUNGU NI KIFUPI CHA WAZUNGUKENI KWA HIYO WATANZANIA INABIDI KUWA MAKINI WANAPOFANYA NAO DILI
ReplyDelete