KARIBUNI SANA KATIKA
LIBENEKE LA MAPISHI NA CHAKULA
Ndugu zangu namshuku sana mwenyezi mungu kwakuniwezesha kumaliza masomo yangu salama Pia natoashukurani zangu za dhati kwa mke wangu kipenzi na mwanagu, wazazi na ndugu zangu kwa sapot yenu kubwa.
Mimi chef Issa nimeamua kuanzisha libeneke la fani ya chakula ambapo wale wote wenye taaluma hii na wapenda chakula cha aina yeyote watapata fursa ya kujifunza kutoa maoni na kufundisha pia mapishi ya aina mbali mbali
Tutakaribisha pia recipe mbalimbali toka kwa yeyote atakaye penda kuchangia mawazo lengo ikiwa ni kubadilishana ujuzi ili kila mmoja wetu afaidike na utaalamu husika. Mapishi ya ladha zote mchango wowote ule utaheshimiwa sana.
Tutakua na historia ya vyakula toka mataifa ya ulaya magharibi ambayo ni maarufu kwa vyakula vyao toka enzi hizo vikipikwa kwa mtindo wa zamani tuliouzoea na pia vikibadilishwa kwa mtindo mpya wa kisasa vikibaki na majina yaleyale hubadilika kwa kunakishiwa kwa mitindo mbalimbali.
Pia tutapata wasaa wa kujua historia ya vyakula na utambulisho kinatoka nchi gani na hasa tutagusa mataifa mama kwa nchi za magharibi katika sanaa hii ya chakula ikiwa ni Spain, England, France, German, Austria, Switzerland na Italy.
Tutaangalia pia utaalamu, sifa na aina za cheese, utundu wa kutengeneza na kunakshi chocolate na historia yote kwa ujumla. Pia tutapata nasaha ya kuona vifaa mbalimbali na kujifunza kuchonga matunda na mboga ktk maumbile tofauti mfano tunda kama apple unatengeneza bata mzinga inapendeza sana hakika ushirikiano wenu ndugu zangu utaifanya blog hii iwe chuo bora cha kubadilishana utaalamu wa fani hii ya chakula.
Kwa sasa nakaribisha maoni yenu na tuanze na nini baada ya maelezo yote hapo juu ili blog hii iboreshwe zaidi na kila mmoja wetu afaidi?
Pia nashughulikia uwezekano wa kufundisha kwa njia ya video hapa hapa katika blog yetu. wadu wote na ma chef wenzangu wazalendo karibuni sana sana sana katika Libeneke hili la chakula.
Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2010 cheers!! http://www.activechef.blogspot.com/
CHEF ISSA
MICHUZI BLOG TUMEIPITIA SAFI SANA HUU NDIO USOMI NA UZALENDO MAANA SIO SHULE YA MAPISHI TU NI TIBA PIA MWANZO MZURI SANA KIJANA AENDELEE NA SPEED HIYO HIYO ISIWE NGUVU ZA SODA INAPENDEZA SANA SANA
ReplyDeleteSasa kaka pananoga kwa mtaji huu mwanzo unatia hamasa kweli kaka masalad yale duh si mchezo ila hayo majani tunayo kweli hapa home maana sijayaonaga mimi Mdau Tegeta
ReplyDeleteJamani nimeshapata maujanja ya ya kumkaba mwanangu kweli chakula kizuri cha kupambwa sio mapaka mahotelini hata nyumbani tunaweza fanya mambo chef karibu sana Mama Winie
ReplyDeletemachef wazalendo toeni ushirikiano kwa vyakula vya nyumbani ili nasi tufaidi igeni mfano bora wa chef mwenzenu mzalendo mafunzo hayo watu wanalipia shule sisi tunapata sasa bure happy new year chef Issa
ReplyDeleteYah ni culinary chember tumeiona na inatufaa tupo pamoja kijana wetu
ReplyDeleteSasa pale kwenye faida za matunda mbona kiinglish tena sisi tusiojua tufanyeje jamani hapa ingekua kiswahili tungefahamu zaidi jamani embu chekicheki kautaratibu ka kubadilisha kua kaluga ketu tulikozoea wajameni NGOSHA ORIGINAL
ReplyDeleteKARIBU SANA KIJANA NA LIBENEKE LAKO LA CHAKULA SALAMA KWELI INAPENDEZA SANA KAZI NZURI NA SHULE IMETULIA HAPA NDIO UNATUTHIBITISHIA UWEZO NA UTAALAMU WAKO LETE MAMBO MAZURI NA MAKUBWA ZAIDI TUNAKUUNGA MKONO KAMA ALIVYOANZA ANKAL
ReplyDeleteHii naona sio shule ya upishi tu ila ni shule ya chakula bora maana naona mambo mengi mazuri ikiwa kuhamasisha watoto wale matunda na mboga tutafaidi sana kama mambo yataendelea hivyo Mama Mbezi
ReplyDeleteHii ndio faida ya libeneke sasa misosi na misupu yakufa mtu kwakwenda mbele Mpenda kula
ReplyDeletekweli mwaka huu mpya na ishu mpya kwa wale tusojua kupika lazima kieleweke tuuu asante kwa kutuletea maujuzi raha sana manake tunakupata vyema full kimatumbi nayasubiri mapishi ya chapati manake mh acha tu nikipika utadhani mnatafuna ngozi lol issa chef adumu mkuu wa nanihii adumu milele. AMEN
ReplyDeletedogo anaonekana kuiva katika fani kwani watu wengi ni wachoyo wa elimu kama yeye kajitolea kushirikiana na machef wazawa inapendeza sana nimependa ufafanuzi na maelezo anayotumia kweli kijana kafudhu tuantegemea mengi na mazuri zaidi hongera chef issa
ReplyDeleteMichuzi yupo katika libeneke toka mwaka 2006 leo 2010 sio kazi ndogo kuliendeleza libeneke inahitaji moyo kwli na kujituma mwanzo mzuri sana chef issa mungu akujalie ufikie malengo yako watu wengi watakukatisha tamaa vumilia wengi tunathamini mafunzo yako na tunakuunga mkono kaza buti utafika Mdau Mikocheni
ReplyDeleteKaka michuzi hiyo blog umeidesgn wewe nini? naona rangi za yanga hahahahahahaaaaa ukweli imetulia sasa kazi kuiendeleza maana wakaanga sumu watakurudisha nyuma tu we komaa kwa kwenda mbele usife moyo uwezo unao mungu kakujalia chef wetu tupe makulaji Mdau NBC
ReplyDeleteukijiita profesional chef uwe kweli profesional nimekubali maana nyota njema huoneka mapema utambulisho tu unaonyesha mtu huyu ni msomi na anaijua fani yake ufafanuzi wa maelezo umetulia najivunia kua mtanzania ktk ulimwengu wa utandawazi nasi tupo juu katika fani mbali mbali Mdau Sweden
ReplyDeleteMAHOTEL YA KARIAKOO NA MIGAHAWA MINGINE TOENI USHIKIANO WAPISHI WENU WAJIFUNZE KUNAKSHI CHAKULA KATIKA SAHANI KWA UTAALAMU ZAIDI KWANI NI KIVUTIO PIAKWAMLAJI
ReplyDeleteChef issa umeongelea sana swala la ushirikiano ni kitu adimu sana watu wengi wakifanikiwa wanapenda kujibagua ila wewe unajaribu kuwavuta karibu ma chef wenzako na wapenda chakula wote ilimbadilishane mawazo safi sana
ReplyDeletePia nimependa maelezo unayoyatoa yanaeleweka kabisana kazi kwetu sasa kufatilia.
Mdau OYSTERBAY
Blog imetulia sana sana tupo sambamba
ReplyDeleteGood start fabalous,fantastic, malvalous, wonderfull chef tuane big up
ReplyDeleteNaona standard na speed kama ya misupu hahahahaaaaaa teheteheeeee kila lakhelikatika kulisongsha libeneke la misosi mkuu
ReplyDeleteMi nasubiri kwenye kuchongachonga mamboga hapo ndio patamu mzee tupe maujanja na mautaalamu chef wetu
ReplyDeleteBwana Chef nitakupata vipi?
ReplyDeleteNataka nikupe offer ya kazi kwenye hoteli yangu moja pale Serengeti.
(US Blogger)
Safi sana chef Issa. Kila la heri na libeneke, nitakuwa nazuru libeneke mara kwa mara.
ReplyDeleteSASA UMESOMEA WAPI? NA ELIMU KIWANGO GANI? NASI TUNATAKA KUSOMEA PIA. EBU TUPE CONTACTS/ADDRESS/ANUANI JINA LA CHUO, PIA BLOG YAKO YA CHAKULA JARIBU KUANDIKA SENTENSI FUPI FUPI. NIMEANGALIA BLOG YAKO, NI SENTENSI MOJA BLOG MZIMA, WENGINE INATUWIA VIGUMU KUSOMA KWA VILE INAPOTEZA MTIRIRKO WA KILA UNATAKA KUKIELEZA. UNAWEZA KUFANYA SHORT COURSE YA WRITING SKILLS ILI KUNOGESHA MAANDIKO YAKO.
ReplyDeleteKumbe umeoa? Basi tena na ma-culinary yako.
ReplyDeletekwani kuoa tatizo jamani si anaweza tu akakutaiga woods hahahahahahahahah bado unanafasi tu jimwage
ReplyDeleteWe unataka kumpa kazi si utembelee blog yake maana inahabari zake zooote then wasiliana nae
ReplyDeleteukitaka kujua chuo alichosomea ikusaidie nini we mzushi???? vyuo vya hotel kibao na ngazi za elimu wanazotoa ingia www.hotel-school-finder.com chagua nchi angalia kozi unayoiweza na gharama nenda kasome kama unaqualify maana kuiga kwa tembo hupasuka msamba sio mangi au mpemba akifungua duka nawe unataka kufungua litadoda ushangae jipange fanya unachoweza acheni kuchimba yasiyowahusu.
ReplyDeleteAtakua kasoma tu ulaya si unaona snow hiyo katika picha jamani! huyu dogo nilimuonaga UK naona atakua kasoma Manchester metropolitan halafu swiss alikwenda kwenye lile litamasha la nguvu ingia katika google utapata adress za vyo vyote hivo mdau.
ReplyDeleteS.J.L UK
hahahahahahaaaa duh wajameni mnatakaga mautaalamu au mnakata kachef ketu wajameni hiiiiii msikatege wajameni tuachieni katufundishe mamisosi wajameni sasa kuoa sikameamuaga mnataka kumtaiga wood hiii acheni wajameni NGOSHA ORIGINAL
ReplyDeleteHuyo ndio Chef Issa Kapande, taalam la mahanjumati.
ReplyDeleteNani kasema wanaume hawajua kupika? Ila wanaume wanapika kwa maslahi, nyumbani hawataki maana hakuna maslahi.
safi sana hii itasaidia na wanaume wajue kupika misosi sio mngoje mpikiwe tuuu hadi chai safari hii ni zamu kwa zamu mjifunze kupika mmesikia??? ukipenda kula ujue na kupika
ReplyDeletemdau canada
Chief Issa,
ReplyDeletekaribu sana ktk libeneke, idea yako ni nzuri kwa kuwa unajikita ktk kitu ambacho wengi wanahitaji kukielewa kwa undani - mapishi. Kaza buti mdau tusonge mbele. Endelea kutuhabarisha ili tuboreshe milo na afya zetu.
Pongezi kwako na bila kuwa mchoyo wa fadhila pongezi kwa michuzi kwa kutuletea habari hii njema ili wengi tunufaike.
tembeatz.blogspot.com