Salaamu zetu za mwaka mpya kwa Sweden ni kwamba mkae mkao wa kula,Stars United haiji kutembea,mjiandae vyema,sasa hivi tupo kwenye mazoezi ya kufa mtu,tunajua Sweden wana timu nzuri,tunajua tutapata upinzani mkali,lakini vijana wangu wamenihakikishia ushindi wa Sweden kwao itakua suluhu,wanaongea sana,wanapenda kucheza mpira na mdomo,
pamoja na kuwa na wachezaji wazuri,msisahau Stars United ni mkusanyiko wa wachezaji wa Marekani nzima sio kucheza mpira tu pia huzingatia kipaji cha mchezaji kwa maana nyingine kuanzia kipa mpaka wachezaji wa kusubiri ni MA-PELE. Yaani kontroli kuanzia ukucha mpaka unywele. Sasa sijui aanze nani asubiri nani. Nawaoneeni huruma sana. Sweden punguzeni mdomo na kuwatisha wachezaji wa Stars united. Msione wamekaa kimya, kumbe wanakuangalieni kihindi,mwezi wa saba sio mbali. Mmsije lia na kusaga meno.
Meneja
Stars United FC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...