Mtaa wa Goliondoi Arusha, Mlima Meru ukionekana kwa nyuma

Mkuu nataraji mwaka mpya umefika salama salmini huko nyumbani na ktk pita pita yangu nimekutana na habari hii ya kuwa Arusha ni mji wa nane ktk majiji mabaya duniani ni kweli Arusha mbaya kiasi hiki?


na nani aliyesababisha mji au jiji letu kuwa ktk hiyo list isije ikawa watu wenye mtimanyongo tu na kutaka kuchafua hali ya utalii nchini naomba wajulishe wahusika ili waweza kuwajibu na kuwakaribisha na kutembelea Arusha kama viongozi wa wolverhamptohn walivyofanya na kuweza kulitangaza jiji letu kwa maana zaidi na sio kwa ubaya.


Chini ni sehemu ya habari ya wahusika wa mji wa tano kwa ubaya walivyo wajibu na sisi tunatakiwa kuiga na chini kabisa ni list ya miji mibaya duniani.
-----------------------------------

Civic leaders in Wolverhampton rejected the findings of a Lonely Planet survey which ranked the city as the fifth worst place on earth.
The list, topped by the US city of Detroit and based on traveller feedback, saw the West Midlands city deemed to be less attractive than the capital of El Salvador, as well as other "hated" cities in India, Tanzania and Mexico.
Wolverhampton was placed fifth on a revised Lonely Planet list of nine most hated cities following "swift and fierce" reaction to an initial request for travellers' least favourite destinations.
On its website, Lonely Planet gave reasons for the selection of the cities other than Wolverhampton, describing Seoul in South Korea as having no heart or spirit.
But Wolverhampton, which can trace its history back to 985 AD, was described as being "so bad that we don't even have it on this site!"
In a statement, the leader of Wolverhampton City Council, Neville Patten, said it was "quite obvious" that representatives of the respected travel guide publisher had failed to visit the city.
Mr Patten said: "The picture they paint of Wolverhampton is not an accurate one.
"If they had come here, they would have seen that Wolverhampton is one of the most progressive cities in Britain. Wolverhampton is such a friendly, open place which is why so many people want to come and live and work here.
"We have first class facilities for residents and visitors and this is certainly not a downtrodden or Third World city.
"I would like to invite Lonely Planet to actually come here and take a tour so they can see for themselves what a vibrant place it is."

AND LONELY PLANET'S NINE MOST HATED CITIES ARE....
Detroit, Michigan
Accra, Ghana
Seoul, South Korea
Los Angeles, USA
Wolverhampton, England
San Salvador, El Salvador
Chennai, India
Arusha, Tanzania
Chetumal, Mexico

http://letempya.blogspot.com

nakutakia siku njema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mi nadhani hiyo list sio ya miji mibaya, ila ni ya miji inayochukiwa. Unajua mtu anaweza akachukia kitu, hata kama kizuri, kutokana na sababu zake binafsi, ushanifahamu?

    Hivyo labda hao waliofanya hiyo tathmini walibase kwenye experience zao binafsi kwenye hiyo miji. Mathalan, wakazi wa miji hiyo hawana time na wageni/ watalii, au labda walipata shida ya kupata usafiri kiurahisi, au vitu walivyovizoea huko kwao havipo katika hiyo miji.

    Sidhani kama Seoul ni mji unaochukiwa. Sidhani pia kama Arusha ni mji unaochukiwa, ila hao waliofanya tathmini ndio hawakuipenda au kuifurahia hiyo miji tajwa (kimpango wao!), hivyo wasigeneralize.

    Mi nadhani watumiwe hii ripoti yangu kwa kuanzia.

    ReplyDelete
  2. Mie ni mtu wa Dar-es-salaam ila Arusha naipenda sana ni nzuri kitu kinachoiangusha ni Ujambazi na Arusha ni sehemu ya utalii inaonesha watu wa nje wanalalamika sana pengine ndomana wameiweka hivyo kwa manufaa yao ila yetu Arusha pazuri. Pazi.

    ReplyDelete
  3. KUPITIA NA HAMASA ZA SERIKALI NIKIMAANISHA VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI WENYE NGUVU KIKATIBA ZA KUHAMASISHA WANANCHI KUFANYA JAMBO FULANI LA MSINGI KWA JAMII BASI NDUGU ZANGU KWA PAMOJA TUWE NA NEW YEAR RESOLUTION YA 2010, MIJI YOTE PAMOJA NA VIJIJI VYOTE, YAANI MAHALA POPOTE ANAPOISHI BINADAMU TANZANIA TUWE TUNAFANYA USAFI KILA JUMAMOSI KWA KUJITOLEA/HARAMBEE. TUSAFISHE MAENEO YA NYUMBA ZETU, MIFEREJI, BARABARA NA TUPANDE MITI KWA WINGI SANA MITI JAMANI NA USAFI WA HALI YA JUU KATIKA MIJI YOTE, SERIKALI ZA MITAA/SERIKALI NDOGO/ COUNCILS/ HALIMASHAURI TUHIMIZANE USAFI JAMANI. RAIS WA NCHI PIA AWE ANASHIRIKI KATIKA HILI KUHAMASISHA WATU. USAFI NI MUHIMU PIA UNAVUTIA WATALII NA KUUINGIZA PESA. MASHIRIKA YA UMMA NA WATU BINAFSI WANAWEZA KUFADHILI MAMBO HAYA, HATA MICHEZO, MUSIC VINAWEZA KUTUMIKA KATIKA HILI

    ReplyDelete
  4. badala ya kutafuta mchawi tujiulize arusha in infrastructure gani kuitwa a City? Kuna barabara za lami urefu gani? upatikanaji wa maji? shopping facilities? recreation facilities(within the city)?
    na tuache kelele nyingi! Arusha ni hyphe na haistaili kuitwa jiji ni town kwanza! Serikali inapaswa kuangalia hilo! Kabla ya kupiga kelele nyingi!

    ReplyDelete
  5. NAMZIMIA BUSH.

    ReplyDelete
  6. If you'd like to stay in the city center, Arusha Backpackers Hotel is the best place to stay. Its a budget hotel/hostel which has got single rooms @ $10, Double Rooms and Double sharing or Twin Rooms @ $16, Dormitories that can accomodate up to 4 persons at a time @ $7 per person per night, and Triple Rooms @ $8 per person per night. The food is great, the view from the restuarant and bar unique and excellent. The music is fantastic...

    The prices mentioned above are the latest.

    You can make a booking via hostelworld.com or directly with the Reservation Manager using the following email address: info@arushabackpackers.co.tz or reservations@arushabackpackers.co.tz

    Its also a good meeting point for most expatriates, volunteers and tourists in Arusha. Its located within a 5min. walk from the central bus station and the Shoprite Shopping Center.

    The security there is perfect and the service outstandingly impressive.
    source: lonelyplanet

    ReplyDelete
  7. Like Jamani said, you need to know your city. I was mugged in NYC and it was in a "safe " neighbourhood near hotels and tourist areas. I have lived in Dar for 25 years and I think I was mugged less than 3 times.

    Yuu just have to use common sense. What you pay is what you get. Just follow where locals go to have a good time, if you ask they will be happy to show you around. Dar is not Nairobi. Dar is one of the safest cities in Africa and like most big cities including London (towel stolen in the youth hostel), Munich (i was chased by Skin Heads ("Turkish GO Home"), Amsterdam ( sandles stolen) you just have to be careful. Will it stop me from going there again? NO! However when i travel now, I don't get as stingy as before when it comes to accomodation and food. And I always try to hang around in a group.
    Source:lonelyplanet.com

    ReplyDelete
  8. Tusiwe tunaangalia neno 'hated', 'worst' pia tuangalie 'buzzing', 'cozzy' city.

    Arusha kupigiwa kura maana yake nzuri ni:
    1. mjini maarufu kwa utalii
    2. unapatikana kwa urahisi ktk intaneti.
    3. kuna vivutio watu kuutembelea
    4. mji maarufu Afrika mashariki.

    Changamoto:
    1. mkoa, serikali kuu, wizara ya utalii, bodi ya utalii na wadau kutumia umaarufu huu kujiongezea kipato.
    2. kuimarisha miundo mbinu kama maji safi, barabara, umeme, teknohama, huduma kwa wateja(watalii wa kutoka nje/wandani)
    3. kuimarisha ulinzi maradufu ya sasa.
    4. tour operators kujiwekea viwango vya juu vya huduma kwa wateja.

    Kwa ujumla hii sio habari mbaya, ila ni nzuri kwa maana tumepata feedback inayotupatia changamoto ya kuboresha mambo mbalimbali yaliyobainishwa hapo juu.

    Mdau
    Majani ya Chai

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Letempya ukisoma maelezo yako uliyonukuu :

    'The list, topped by the US city of Detroit and based on traveller feedback, saw the West Midlands city deemed to be less attractive than the capital of El Salvador, as well as other "hated" cities in India, Tanzania and Mexico'.

    Nukuu ya paragraph hiyo hapo juu ina maana Arusha, Tanzania ni bora zaidi ya baadhi ya miji ya huko USA, UK, South Korea,Mexico n.k

    Hivyo naunga mkono maelezo ya mdau wa Majani Ya Chai kuwa tutazame habari hii ktk mtazamo chanya wa kupambana na changamoto za kuvutia watalii wajisikie raha ktk roho wajapo Tanzania.

    Mdau
    Kakakuona

    ReplyDelete
  10. Wadau check this out;
    The only reason given for Wolverhampton's inclusion on the list is a link to a reader anecdote where the city is tastelessly compared to Ground Zero in New York immediately after the September 11 terror attacks.
    The message, written by an online user called 'Myanmarbound', reads: 'Those photos remind me of the story about the man from nearby Wolverhampton who happened to be in New York on 9/11.
    'Next day he went down to Ground Zero when George Bush was doing his tour of the devastation and glad handling the crowd.
    'Bush comes up to shake his hand asks him where he's from. The man replies 'Wolverhampton'.
    'I don't know that place,' says Bush. 'What state is it in?' 'The man from Wolverhampton looks around him and and replies, 'It's pretty much like this really.'

    I do not the main reason for Arusha ranks.

    Read more: http://www.dailymail.co.uk/news/article-1239478/Wolverhampton-named-fifth-WORST-city-planet.html?ITO=1490#ixzz0bNaGKiAF



    Read more: http://www.dailymail.co.uk/news/article-1239478/Wolverhampton-named-fifth-WORST-city-planet.html?ITO=1490#ixzz0bNZLuSTN

    ReplyDelete
  11. Ninakubaliana na uchunguzi huo kuhusu Arusha. Arusha ni mji ambao eneo kubwa limejengwa bila mpangilio(plan) na inaendelea kwa kasi kujengwa hivyo na serikali ina liona hilo na ipo kimya. Miundo mbinu ni zero, ujambazi, ukabaji, na ulevi wa gongo na bhangi upo juu kiasi cha kutisha.
    Wakazi wengi vijana, hasa wenyeji(waarusha, wameru, na wamasai) si wastaarabu hata kidogo.
    polisi hawawajibiki ipasavyo kwani wamezidiwa nguvu, hawana morali wala mafunzo ya kutosha na ya mara kwa mara ili kwenda sambamba na kasi ya uhalifu wa ndani na wa kimataifa.

    ReplyDelete
  12. Mimi nawashangaa watanzania kama Mr. Haruni kukubali kila kinachosemwa na wazungu kuwa ni sahihi.

    Ustaaarabu sio kuanzisha klabu za kuchangamsha wageni kwa mila na utamaduni wa kizungu- mfano 'Strip Clubs', baa za bangi kama Uholanzi, 'casino za kamari', gay/ lesbian clubs n.k

    Hawa watalii wanasema wanajisikia 'upweke' na kuwa 'bored' kwa kelele za mabati ktk guest house mvua ikinyesha, hawapati nafasi ya kulewa mpapka wakatapika, watembee na vichupi tu wapate sun-tan n.k

    Ila kuna changamoto za teknohama, usafiri wa ndege, menu za chakula vya kigeni,barabara na kuboresha usalama.

    Mgau
    Abunuasi Msomali
    Arusha.

    ReplyDelete
  13. MIJI MINGI YA KITALII DUNIANI HUFAIDIKA KWA KUENDELEZWA KUTOKANA NA MAPATO YA UTALII, SASA ARUSHA MBONA HAIFAIDIKI NA MAPATO HAYO? PESA ZINAKWENDA WAPI? WATANZANIA TUJIFUNZE KUHOJI NA IKIBIDI KUDAI MPAKA KIELEWEKE KITU. MBONA CCM CHINI YA MFUMO WA CHAMA KIMOJA ILIKUWA IKIFAIDIKA NA MAPATO YA MASHIRIKA NA MAKAMPUNI.

    ReplyDelete
  14. Stay and rest in hostel do more exciting that you never expect to happen.

    Rio Pousadas

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...