naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. joel bendera akiwapoza wanahabari waliotaka kususia kukava ujio wa drogba na ivory coast usiku kuamkia leo uwanja wa ndege wa julius nyerere jijini dar baada ya askari kuwajia juu wanahabari na kuwazuia wasifanye kazi zao kwa sababu wanazozijua wenyewe.
huko nje ya fensi mashabiki walikuwa wanamsubiri drogba na wengie kwa hamu. waliambulia kumuona kiduuuuchu tena kwa mbali
wanahabari wakiwa wamesusia kukava ujio wa ivory coast baada ya kunyanyaswa na askari uwanja wa ndege
wanahabari wakiweka msimamo wa kususia baada ya askari kuwanyanyasa katika kukava ujio wa ivory coast. hakuna mpiga picha aliyepiga picha ujio huo.
katibu mkuu wa chama cha wapiga picha nchini, bw. selemani mpochi, alieleza masikitiko yake ka vitendo vya askari kunyanyasa wanahabari wawapo kazini kwenye ujio wa aina hiyo, na kuhoji kwa nini inakuwa hivyo wakati Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ujio wa timu hiyo unapewa uzito unaostahili ili kuitangaza Tanzania vyema.
habari kamili





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sidhani kama kususia kupiga picha ilikuwa ndo suluhisho au njia ya kueleza kukasirishwa na kunyanyaswa kwa waandishi/wapigapicha. Wangetumia njia zozote kupata picha hizo halafu wangewaumbua hao askari. Waandishi wa TZ bwana! hawaishi vituko, wanasahau ule msemo usemao, wanasusa, sisi twala!! wajifunze kutoka kwa waandishi wenzao ulaya, katika hali kama hiyo wanafanaje? usalama kwa timu kama hiyo ni muhimu, na naamini si bure, huenda waandishi waliwatolea lugha za matusi askari, nao wakakomaa. kuheshimiana ni jambo la msingi.

    ReplyDelete
  2. kiukweli wasingesusa ila kweli ile miaskari ya pale eapoti huwa ina gundu sana yani ni mimbumbumbu ya hali ya juu kila kitu yao imezoea mabavu sijui yakoje na sailimia kubwa yananuka midomo yani wanaboa sana kutaka misifa yao kijingaa ovyo sana mtaishia kufuga mabata!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...