Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia huduma za utafiti wa mazao kwa kutumia teknologia ya kisasa walipotembelea katika kituo cha utafiti wa Kilimo Gigiri Nairobi Kenya. Dk. Shein yuko katika ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini Kenya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein katikati, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na watendaji wa kituo cha huduma za mawasiliano cha Safaricom, wakati walipotembelea kituo hicho Mlolongo Nairobi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Myyngano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, akipanda mti kama kumbukumbu alipotembelea Taasisi ya utafiti wa madawa KEMRI mjini Nairibi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Serikali ya Kenya ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Dk. Kalonzo Musyoka katika ukumbi wa Serena Hotel mjini Nairobi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kushoto, akitembelea shamba la kilimo cha mbogamboga katika kijiji cha Kari Nairobi Kenya.
Mkuu wa mpango wa mafunzo katika Kituo cha Utafiti wa mimea ya aina mbalimbali Kari mjini Nairobi Dk. Simon Gichuki, akimuonesha Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein mpango wa Elimu kwa jamii juu ya uaandaaji wa mimea wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika kituo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Kenya Dk. Kalonzo Musyoka wakiangalia ng’ombe wa kisasa wa maziwa, wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Shamba la kilimo na mifugo la Dk. Musyoka katika kijiji cha Yatta Nairobi Kenya. Picha na mdau Amour Nassor wa Ofisi ya Makamu wa Rais.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...