Mh. Zitto Kabwe ambaye kama waraka wake unavyosomeka hapo chini katangaza kujitoa kwenye mtandao huo mashuhuru kwa mijadala na hoja za haja wa:
www.wanabidii.net
Ndugu Wanabidii,
Wiki iliyopita kulikuwa na mjadala hapa Wanabidii kuhusu haja ya kutenganisha uchaguzi wa Rais na Wabunge. Mada ambayo ilichangiwa na watu wengi ikiwemo mimi binafsi. Ninaamini ni mada nzuri kabisa ambayo aliyeileta alikuwa na nia njema kwa nchi yetu na sisi wachangiaji tulichangia kwa nia njema kabisa.

Nilitahadharisha katika mada ile kuwa tatizo la mijadala kama ile ni kwamba ni rahisi watu kuhama kutoka katika hoja na kujadili watu. Hicho ndicho kilichotokea.

Gazeti la Tanzania Daima la Leo Jumatatu limeandika habari kuwa mimi ninataka JK aongezewe muda wa Urais. Chanzo cha habari hii ni mjadala wa humu katika wanabidii. Tanzania Daima ina waandishi na wahariri ambao tunafahamiana na wana mawasiliano nami. Hawakuthubutu kupata maoni yangu katika habari ile.Hii ni kinyume kabisa na maadili ya uandishi wa habari na kwa vyovyote vile, kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini hivi sasa, habari ile ina nia mbaya kwangu binafsi kama Zitto na kama Mbunge na Kiongozi wa CHADEMA.

Nimezungumza na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima Ndugu Kibanda ambaye naye ni MwanaBidii kumweleza masikitiko yangu. Naye pia amesikitishwa na habari iliyotolewa na gazeti lake yenye kichwa cha habari Zitto: JK aongezewe Muda

Nimemwomba waniombe radhi kwa habari hii. Mara yangu ya kwanza kutaka Tanzania Daima kufanya hivi hata kama huko nyuma wamewahi kuandika habari ambazo hazina ukweli wa kutosha. Kwa hili la leo nimeshindwa kuvumilia kwani habari ile itanijengea hisia mbaya mbele ya wananchi na wanachama wa chama changu.

Mimi napenda sana mijadala. Mijadala ni afya kwa Taifa. Licha ya mara kwa mara kunukuliwa ndivyo sivyo katika mijadala kadhaa bado sikusita kutoa maoni yangu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu nchi yetu. Nimekuwa nikikataa ushauri wa watu wengi sana kuwa nisichangie katika mijadala kama humu Wanabidii au hata JF. Hata hivyo, nikiwa muumini wa mijadala yenye afya na vile vile katika hali ya kusahihisha masuala fulani fulani au kuweka rekodi sawa nimejikuta nikiingia katika mijadala.

Sasa, naona ni vema nichukue ushauri wa watu na vile vile kufuata hisia zangu binafsi. Ninaomba niondolewe katika orodha ya Wanabidii na sitachangia tena katika Jukwaa hili. Nimechukua uamuzi huu kwa moyo mzito sana. Nitawakosa sana. Wenye nia mbaya kisiasa, ambao sasa naamini wamedhamiria kutekeleza nia zao hizo nao watanikosa naamini.

Kwa herini na kila la kheri.
Zitto,
Hamburg.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. mh zito kabwe kwanza nakupongeza sana kwa moyo na nia safi ulokuwa nayo,wewe ni mfano wa kuigwa kwa vijana wa tanzania,umekuwa ukisimamia ukweli siku zote hata kama inapobidi upishane kimawazo na viongozi wenzako wa chadema,wewe ni bado kijana mdogo,sema baadhi ya wazee kwenye nchi hii wanataka kukudidimiza,wanataka tuendelee na zile siasa za zamani,kama ni mpinzani basi always uwe adui wa chama tawala,au always uwe sawa kwenye chama chako,dunia inabadilika,siasa za majungu zitatupeleka pabaya watz,hili gazeti la tanzania daima ni kiini cha kuuwa democrasia ya tz,yani wao kila atalaopishana kimawazo na chadema ni adui wao,walianza kumuandama marehemu chacha wange sana,kisha cuf kuweka mgombea wao mbeya vijijini hili gazeti liligeuka kuwa adui wa cuf pia,ndugu yangu zito nakushauri usibadilishe msimamo wako wa kuwasaidia nccr mageuzi kuchukua kigoma vijijini,na wewe tafuta chama utakachoona utasimama bila fitna usimame kwa jimbo lako,vijana tuko nyuma yako,unaweza,lakini chadema watakupoteza,maana kama tanzania daima linakuchafua,its mean ni chadema wanakuchafua,maana hili gazeti kuna share ya mwenyekiti.

    ReplyDelete
  2. kamanda zito kabwe,wewe ni zaidi ya mwana siasa,na umeonesha wazi uko wazi kuacha uongozi kukwepa siasa za majungu,wewe ndio kiongozi bora na sio bora kiongozi.

    ReplyDelete
  3. mheshimiwa nakushauri ukihame hicho kama mara moja,other wise watakudhalilisha mbele ya safari,jiuzulu cheo kwa heshima,yasije yakakukuta ya kusimamishwa uongozi.vyama viko vingi vyenye kukuhitaji.nenda nccr mageuzi ama cuf.

    ReplyDelete
  4. Hiyo ni hatua ya kwanza, ya pili kujiondoa Chadema kwani Dr. Amani W. Kaburu yuko wapi?
    Hizo ndo siasa kaka ambazo unasema si chaguo lako.
    Sitisha uamuzi wako tuendeleze mapambano si umeshakanushaa, waswahili tunasema ukiamua kuwa bondia basi usiogope ngumi za uso.

    ReplyDelete
  5. MatunyagantumbiliJanuary 11, 2010

    Zitto, nakupomgeza kwa kujitoa kwenye mtandao wa majungu. Tatizo la waandishi wa bongo ni wavivu sana. Wanafanyakazi kivivu wewe huwezi kupata habari ya mtu kwenye mtandao halafu unaitafsiri unavyojua wewe na kuandika ili mradi uuze gazeti.

    Inabidi gazeti la Tanzania Daima wamuombe radhi zito kwa kuweka wazi kuwa walikuwa wamemkopi vibaya kutoka kwenye mtandao.

    Kwa nini hawakumpigia simu au hata kumuandikia email kama yupo nje yanchi na wanaogopa gharama ili kumsikia yeye anamaanisha nini katika post zake?

    Halafu je hao Tanzania Daima wana uhakika gani jina la Zitto wa kwenye mtandao ni Zitto halisi?. Huu ni ukanjanja kabisa ndiyo maana mimi siku hizi haya magazeti ya bongo sinunui ni wavivu wa kufanyia kazi habari zao na matokeo yake wanatupotosha tu.

    ReplyDelete
  6. That's being a coward!

    ReplyDelete
  7. hii taarifa ameitoa kule wanabidii pia. akawapiga kopi watu kibao ha ha ha ha . CC freeman Mbowe, CC Wilbroad Slaa, CC Jenerali ulimwengu, CC Kibanda, CC Axaveli Lwaitama nk teh teh teh teh. sawa muheshimiwa sana wamekupata, wamekufikia.
    naona unakula nondozzz jermany hapo!! na hujaoa bado, big up sana mwanangumwenyewe Zitto kamua kamua baba, taifa hili linakungoja sana, kama sio wewe basi john mashaka, au Mimi mwenyewe Kamanda.

    ReplyDelete
  8. Mie kapuku, sina hali wala mali, sina cheo wala dhamana, sina chama wala nini, basi mwanawane nikajikuta mtu kaniumbukiza kwenye hilo limtandawo la Bidii forum bila hata kujijua wala kusubscribe. Nikawaambia haya mnitoe kama mlivyoniingiza,maana hamujui hata maana ya privacy ya mtu? Wakanitoa.

    Sasa bwana Shemeji wewe unampigia simu huyo muhariri wa gazeti wa nini? Au na wewe ulitaka wakuandike? Wakati unajua kabisa huyo muhariri lazima aedit gazeti, na katika kuedit anajua hiyo habari yako haikuandikwa kisahihi kama ulivyosema ni mojawapo wa moderator wa Bidii forum sio? kwa hiyo ulichokuwa unampigia simu afanye nini? Wakati yeye ndiye mwenye makosa?

    Kama ni kweli wamekuchafua nenda kweny vyombo vinavyohusika na masuala ya ethics katika habari huko watatiwa adabu.

    Shemeji kuja kutwambia sisi kwenye blogu ya jamii haikusai kupata haki yako, unakuwa mwoga kama sio mtoto wa UJIJI? Wacha kututia aibu watu wa UJIJI, hata mkoloni alituogopa unaacha watu wachache wakuchezee kama hutoki Ujiji! unanitia aibu. Wapeleke kwenye baraza la habari hao. alaa!!

    Mie ndio maana niliacha zamani kusoma sijui JF sijui Bidii forums sijui nini? ntafanya kazi zangu saa ngapi, ntasoma hizo news za udaku saa ngapi? Hivi kwanza kumbe hili gazeti la Tanzania daima bado lipoo eeh!!

    Mswahili

    ReplyDelete
  9. MH Zito Kabwe, wewe ndio dira ya vijana, chachu ya siasa ya upinzani Tanzania, mhimili wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla, tegemeo la wanamageuzi ndani na nje ya CCM na future ya uongozi wa nchi hii. Nimekuwa nikifuatilia hali ya kisiasa na kauli zinazotoka kwako na zinazokuhusu wewe na I am smelling a rat. Siku zote nimekuwa nikihofu sana kwamba ipo siku tutaamka na kuambiwa yaleyale ya Dr Masumbuko Lamwai, Dr Kabourou,Thomas Ngawaiya, Jidulamabambasi etc kuhusu Zito. Chonde chonde Zito usiondoke CHADEMA. Ndicho chama pekee chenye muelekeo wa kuleta upinzani bara. Usimwache Dr Slaa peke yake. Ninyi wawili ndio manabii wa siasa za upinzani Tanzania. Imarisheni upinzani kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Najua CCM watakuwa wamekushawishi sana na hata kujaribu kuku-kolimba several times lakini kaza buti.

    ReplyDelete
  10. Mheshiwa Zitto hiyo ni makala ya sita kwenye gazeti hilo la MBOWE kukuchafua jina lako.

    pia usisahau makala yaliyoandikwa na Mwanakijiji kwenye Gazeti la Kulikoni kuwa wewe unampigia debe DR.Idrissa Rashid awe Mkurugenzi wa Tanesco kwa vile wewe umenunuliwa na Mafisadi.

    nadhani una haki zote kuyashitaki magazeti hayo.

    pia kule Jamii Forum kwa vile ni Forums ya Chadema/Wachagga hivi sasa kila ukiandika unatukanwa na kukashifiwa.

    kama umegundua kule JF Mwanakijiji au Mawazo kama alivyosema Mtanzania amekuwa akitumia majina ya Mwafrika,David Solomon au AbdulHalim kukuchafua wewe kwa vile tu yeye ni muajiriwa wa Mbowe kwenye Jf.

    kuhusu Chadema wewe usitoke kwani umetumia nguvu zako nyingi sana.huwezi kuwasusia Nguruwe Shamba la Mihogo.Cha muhimu ni kubanana huko huko.

    una haki ya kumsaidia Kafulila na wengine kama ilivyo kwa Mengi ambaye ana kadi ya CCM lakini anaisapoti Chadema kwa pesa na hali zote.
    Mdau Kanda2 wa JF.

    ReplyDelete
  11. Zitto,

    Politics has always been and will continue to be a contact sport, in other words if you can stand the heat stay out of the kitchen.My advice to you is stop whining about the bad call, play the game the way it is supposed to be played.

    ReplyDelete
  12. chadema hawana mpya,na mwisho wa mwaka watakiona cha moto,hakuna jimbo wataweza kurudisha.watz wameshashutuka kuwa chadema ni ngos ya ukoo,asante sana marehemu chacha wangwe,david kafulila,dandu na mhe zito kwa kutufungua macho kuhusu hiki chama.

    ReplyDelete
  13. narudi cuf,kweli sitanii,yani hiki chama kila anayegombana na mwenyekiti ni adui na anatumiwa na mafisadi.tumeshtuka.hadanganywi mtu hapa.

    ReplyDelete
  14. mara mia uwape mafisadi wa ccm kura kuliko chama chenye ukabila.ni hatari kwa taifa.kabwe shtuka dogo.

    ReplyDelete
  15. Sababu hasa ya kujitoa ni nini? mara nyingi wewe mwenyewe ndio unajichanganya sana kwenye maoni yako kwenye mijadala. Suala la msingi ni kuwa makini unapochangia na kuondoa utata. lakini hata kama umeamua kutochangia tena si ungeacha tu kuchangia kwani hadi uage? Au ulialikwa rasmi? Zitto tatizo lako unataka tu mijadala watu waanze kujadili kujitoa kwako? Mi ninavyojua mtu ka hutaki kuchangia unaacha tu huna haja ya kumake an issue. Ok kwa heri si tunaendelea kujadili

    ReplyDelete
  16. Wewe Zito Kabwe embu cha kutubabaisha sisi, kwani ukijitoa mijadala itakuwa na hasara gani? Wewe ni mdau tu kama wadau wengine kwenye mambo ya mijadala.

    Mitandao ya mijadala itaendelea tu hata kama Zito atakuwepo au hatakuwepo.

    ReplyDelete
  17. USHAURI WA BURE KWA ZITO NI KWAMBA HASIJIONE YUKO SANA TOFAUTI NA WADAU WENGINE KWENYE HARAKATI ZA MAPAMBANO.

    WATANZANIA WAPO MILIONI ZAIDI YA 40 SASA HIVI NA WENGI TU WANA UWEZO MKUBWA WA KUJENGA NA KUTETEA HOJA DHABITI KWA AJILI YA MAENDELEO YA TAIFA LAO.

    KWA HIYO BWANA ZITO NADHANI WEWE NDIYE UNAWAHITAJI ZAIDI WATANZANIA WENZAKO KULIKO WAO WANAVYOKUHITAJI WEWE.

    ReplyDelete
  18. Mambo ya wanabidii kwa nini uyalete huku Zito? Sometimes I think unahitaji kushauriwa before coming up with issues. Tafuta washauri ndugu yangu.

    ReplyDelete
  19. Vyama vya siasa na wanasiasa wa sasa Tanzania wanakosa kujielewa kuwa ukifikia ngazi fulani ktk chama mambo au mijadala mizito inatakiwa itolewe kwa kufuata taratibu za kichama.

    Mfano CCM na magari ya uchaguzi 2010 makatibu wa vitengo kila mtu anasema lake, kwa nini wasikae halafu katibu mkuu kutoa tamko la kichama?

    Tukija kwa CUF, kuna vigogo wanatamka kutaka kutengua katiba ya muda wa mihula mingapi Rais wa Zanzibar aongoze, bila ya Vigogo wa CUF kuzungumza na katibu mkuu au wmenyekiti wa CUF kutoa tamko la kichama.

    Kwa CHADEMA mara tunasikia kiongozi mwandamizi wa CHADEMA kuunga mkono mwajiriwa aliyefukuzwa, bila ya kwanza vigogo wa CHADEMa kukutana halafu Katibu Mkuu atoe tamko.

    Mijadala ktk maglobu si mizuri kwa mtu mkubwa ndani ya chama chama chochote, hasahasa kama inakinzana na sera na ilani za chama chake au kama ni masuala mazito yanayoweza kutumiwa vibaya kukiyumbisha chama.

    Mwisho kosa ni kurudia kosa na ukubwa ni jiwe.

    Mdau
    Makini

    ReplyDelete
  20. Wewe dogohuku ni kutapatapata tu. Kunahaja gani ya kutaarifu umma kuwa unajitoa? Wewe anza mbele kimya kimya kama ulivyoingia. Ebo!

    ReplyDelete
  21. i dont knw but i feel lyk Zitto umeanza kubore kiaina,,

    ReplyDelete
  22. wewe zitto ni mtu wa makuu,sijui taarifa hii umeileta ili iweje, mimi hata hiyo site ya wanabii nilikuwa siijui na wala sijawahi kuisikia ndio nimekuja kujua leo hii kutoka kwako

    ReplyDelete
  23. Ihave been reading about Zito for a while now and i have came out with the opinion that, either the guy is lacking political maturity or he doesnot even know what he did put himself into.I`m saying this because the fight he started with CCM through parliament and his speeches is not over yet and he now want to fight his own shade. My advice to you is get out of the game and try to figure out what you want to accomplish and how to it.If you don`t understand what i`m trying to tell you look at Dr.Lamwai or your former leader Dr. Kabourou,

    ReplyDelete
  24. jamani mimi kama mimi,nilianza kuona upinzani unaleta mabadiliko fulani katika nchi sababu ya zitto kabwe nikawa na matumaini ya kuwa na tanzania isiyo na rushwa.

    lakini sasa baada ya kuona kua ameingizwa kwenye kamati ya madini na muheshimiwa rais,nikaona sasa huku ni kumfunga mdomo,then akawa yuko tofauti na viongozi wenzie wa chadema ,nikajua ohoo tiari hapo hamna kitu.tena mara anaachana na siasa mara anaandika barua ya kujiuzulu vyeo vyote chadema ikiwa ni pamoja na ubunge,nikaona sasa hapa nchi hii upinzani una ubabaishaji kwani wakiimarika tu wanavurugika mara malumbano ya chinichini ilihali hali inakua si shwari katika chama.

    chadema mkicheza ndio basi tena mtapotea kama nccr-mageuzi
    au na wewe zitto ni kama mrema fulani unatumiwa kuvuruga vyama na ccm nini?

    ni bora waungane waunde chama kimoja kikubwa cha upinzani

    otherwise let me vote for ccm forever .

    ReplyDelete
  25. Tunaomba uendelee kuchangia katika style ya anonymous.

    Asante.

    ReplyDelete
  26. Zitto,

    Wewe bado ni kijana kula maisha rafiki yangu.

    Hii kujitafutia uheshimiwa unaanza kujiona wa maana sana ndio maana wadau wanakushangaa.

    Vijana wa rika lako sasa hivi wanakula maisha, wanatanua na mademu, n.k.

    Sasa ukikomaa na uheshimiwa utakuwa kila saa unajistukia unashindwa kufanya mambo ya kawaida kama ya vijana wengine.

    Ukikandiwa kidogo tu unacharuuuka, mpaka nasikia wakati fulani ulitaka Bunge likuombe radhi.

    Mfano siku ile ulipokuwa out na Wema Sepetu kwa nini ulimwachia? Angekuwa msela mwingine angeshaua saa nyingi.

    Ni hayo tu. Don't take life too seriously you'll never get out alive anyways.

    Nyerere tu mwenyewe ameshasahaulika, sembuse wewe!

    ReplyDelete
  27. Nakubaliana na mdau anayesema Zitto ana lack political maturity ! Hii ni michezo ya kitoto tulikuwa tunafanya zamani,KUSUSA ! Stupid..mtu mzima aliyekomaa hafanyi hicho kitu, either angejibu hoja au angekaa kimya..sio kuandika barua ya kujitoa!! Umebore Zitto, jiangalie tena. Tunajua wewe ni binadamu na unaweza kuteleza, hauko perfect

    ReplyDelete
  28. Halafu watu mnaomuomba omba ooh sijui endelea kuchangia mnaniboaaaaaaaaaaaa. Sijui wewe ni kijanna tunakutegemea sijui nini.. mwenzenu analamba pesa huko nyie mnabaki ooh tunakutegemea.Si mliona kwenye JF alivyokuwa akitamba kuwa ana uwezo kwa sababu alikuwa analipwa sijui 400,000 kwa siku kwenye tume ya Bomani, ooh mshahara wangu , ooh nina hammer, sijui nina shangingi utumbo mtupu. Na hatujui aliramba ngapi Dowans hatat kutetea kununuliwa sasa nyie mnasema ooh tunakutegemea.. jamani watanzania mmerogwa?

    ReplyDelete
  29. Njia rahisi ya kujiongoa katika makundi pepe bila ya kusumbuana na moderator au mmiliki wa kundi. Soma maelekezo katika wavuti.com linki hii hapa http://bit.ly/7LTY9B posti ina kichwa cha habari: How to stop direct group invitation and add-ups in a Yahoo! or Google groups.

    ReplyDelete
  30. Unajitoa ???? So what ????

    Wasalimieeeeee !!!!!!

    Anza mbele tu !!!!!

    ReplyDelete
  31. Mh.Zitto Kabwe, kumbuka maneno ya hekima "Uongozi ni Jaa' na kama gwiji mwandishi wa vitabu alivyosema kuhusu raia wa nchi ya kusadikika 'Kukumbuka fimbo baada ya kuumwa na nyoka'.

    Hivyo Mh. Zitto Kabwe kwa vile 'Uongozi ni Jaa' usishangae watu wakajaza takataka zao katika Jaa lako, na watu kutafsiri kuwa zote taka ni zako.

    Jiepushe na hoja nzito ktk ma-globu, radio-show n.k bila kwanza kufanya 'brain storming' na vingunge wenzio ktk chama (maamuzi ya pamoja, maana chama ni watu na watu ndo shughuli hasahasa kwa viongozi wa juu kama wewe.

    Mdau
    Che-Guevara.

    ReplyDelete
  32. Moderator nadhani humtendei haki Zitto maana umeiweka hii mail amabyo aliwatumia wanabidii na watu wake wa karibu na sio katika mitandao mengine kama blogu hii.Ni wazi aliyeituma hii hakuwa na ruhusa wa haki ya kuisambaza kama alivyofanya. Matokeo yake watu wengi wanatafsiri kama vile yeye ameileta hapa kulalama wakati sio hivyo.

    Nimewasiliana na Zitto na amenihakikishia kuwa hana taarifa ya mail yake hiyo kuletwa hapa na ni muda mrefu sana umepita tangu apite katika blogu hii.

    Na wale ambao wanapenda kufikia conclusion bila ya kujua ukweli na mantiki ya Zitto kuamua kuwataarifu wenzie kuwa ameamua kujitoa ni muhimu wakafuatilia kile alichokiaandika Zitto katika mtandano wa wanabidii na jinsi gani gazeti la Tanzania Daima lenye kumilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA lilivyopotisha habari kwa makusudi kabisa.

    Pia wale wanaomshauri Zitto kutumia annonymous - majina ya kivuli nanyi nawashauri kuepuka haya mazoea ya kushabikia siasa za kinafiki. Ni wajibu wetu kuwashauri, kuwajali na kuwalinda wanasiasa wenye uthubutu kama wa Zitto wa kuwa wawazi na wakweli katika kutoa maoni yao kwani hiyo ni faida yetu sote kuelemika kuhusu siasa za nchi yetu.

    Tukumbuke kuwa bila ya kupambana na ama wanasiasa ama waandishi wa habari wanaoamini katika usemaji ama uandishi wa kiujanjaujanja wa kupindisha maneno ya watu kwa manufaa yao ama ya wafadhli na waajiri wao, tutaendelea kuwa siasa chafu zinazoendeshwa kwa kutumia vyanzo vya udaku na longolongo.

    Moja ya vitu ambavyo nimekuwa nikijaribu kufanya ni kuwaleta viongozi wetu karibu na wananchi katika hali ambayo inaruhusu sisi kujua, kutambua na kuelemika zaidi kuhusiana na mambo ya kiuongozi, kiutawala na kisiasa ili kuweza kuwa katika nafasi ya kufanya maamuzi sahihi.

    Hata hivyo nimeshuhudia mara nyingi viongozi hao ambao wengi wao ni wale wenye heshima kubwa na upeo mkubwa wa mambo nchini kuamua kukaa mbali na kuficha maoni yao kuhsu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini kuhofia na uhuni kama huu aliofanyiwa Zitto na Tanzania daima.

    Ni jukumu letu kulinda haki yetu ya kupata habari sahihi kutoka kwa wadau na uongozi kama Zitto. Badala ya kumgeuza mbuzi wa kafara ni muhimu kukemea, kupinga na hata kuchukua hatua dhidi ya wabakaji wa demokrasia na utamaduni wa uwazi na ukweli.

    Bila ya kufanya hivyo tutaendelea kuweka rehani utanzania wetu mikononi mwa wanasiasa wajanjawajanja wenye kutegemea siasa longolongo ambazo huzifanya kwa kificho ama kutumia vyombo vya habari wanavyomiliki ama kufadhili.

    Omarilyas

    ReplyDelete
  33. Tatizo la huyu dogo anajidai mno anaona kama yeye anabusara sana kuliko watanzania wote jaman tujue kabisa hizi hoja zote ambazo zinawapatia umaarufu hawa jamaa sio zao binafsi nikuwa zimeandaliwa na chama chao wao wakatumwa tu kama waakilishi wa kuzitoa sasa wakifanikiwa kuzitoa vizur na kuzaa matunda sis tunaanza kuona kama huyo mtoa hoja anaakil sana ni shujaa No,No,Nooo hiyo ni hoja ambayo zimetayarishwa na chama chake zito akapewa akazitoe bungen zikazaa matunda kwa hiyo tusimwone zito kama ni malaika sifa zinatakiwa ziende kwenye chama CHADEMA ndio shujaa na sio zito,Zito yuko pale kufuata maelekezo ya chama.Hata Dr.Slaa yote anayotoa ni maagizo ya chama chake.Wewe angalia zito akijitoa CHADEMA nafasi yake itachukuliwa na kijana mwingine na huyo kijana atapewa hojaa na chama atazitoa na atapata umaarufu vilevile.Kwani kama sio CHADEMA ni nan angemjua zito?na ni nan angesikiliza hoja zake? si watu wangemwona wa kawaida tu?kwa hiyo asijisikie sana la kufanya akishukuru CHADEMA kwa kumwinua akaonekana akatambulika na jamii na ajaribu kujishusha kidogo ajue kuna watazania ambao hawajapata nafasi ya kujulikana wanaakili na busara kuliko yeye.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...