mbunifu wa mavazi ali rhemtullah
mamodo katika viwalo vya ali rhemtullah
wakati wa Swahili Fashion Week

SWALI: Ni changamoto gani unakutana nazo katika swala zima la ubunifu wa mavazi?

ALI: Changamoto ni nyingi sana kwa hapa Tanzania unajua hatuna kiwanda chochote wanachotengeneza vitambaa unakuta ukienda kariakoo kununua vitambaa vya mteja na ukienda kushona na baada ya week 3 unakuta kitambaa kimeisha ukirudi kariakoo tena unakuta stock ya vitambaa havipo tena unaambiwa urudi baada ya week mbili unakuta unasimamisha kazi zako kusubiri vitambaa viagizwe toka nje.

SWALI: Ni mtu au watu gani ambao huwezi kuwasahau kwa namna moja ama nyingine waliofanikisha wewe kuwa hapo ulipo?
ALI: Ni watu wengi sana kwa ujumla kwanza ni wazazi wangu wamenipa support sana unajua wazazi wengine wakiona watoto wao wa kiume wanajiingiza kwenye mambo ya Fashions wanakuwa hawakubali watasema sio kitu cha maana hakitokulipa lakini wao waliniruhusu nifanye ninachokipenda kwa hiyo nimekubalika Tanzania, wa pili ni mama yetu wa mitindo ASIA IDAROUS yeye ndio alinipa nafasi ya kuonyesha nguo zangu mara ya kwanza katika show yake, mtu wa tatu yeye ni Techinical Adviser wangu bila yeye pia nisingeweza kufikia hapa yeye alikuwa kwenye Industry ya Fashion miaka mingi sana mwanzoni alikuwa anafanya kazi na Mustafa Hassanali pia amekaa sana Tanzania anajua game la ubunifu linakwendaje amekuwa akinikosoa hapa na pale ili niweze kuwa na Style yangu ya kipekee.

SWALI: Designs zako za nguo zinapatikana madukani?
ALI: Bado hazipatikani
SWALI: Kwa nini?
ALI: Unajua kwa Tanzania hatuna Kiwanda cha kutengeneza nguo kama kungekuwa na kiwanda sawa ungeziona lakini mpaka nisafiri India au China unakuta ni made in huko lakini Designer ni jina langu.
soma intavyuu yote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...