Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt (kulia) akisalimiana na Mfanyabiashara wa biadhaa za Alovera Cecylia Mosha (kushoto) juzi jioni katika viwanja vya Bunge la Tanzania. Katikati ni Ofisa wa Bunge Neema Kiula. Balozi huyo yupo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kimaendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nawasalimu ndugu wote wa blog hii. Jamani ee ndugu zangu tuwache kasumba! Hii aloe vera ni dawa ya Kiswahili inaitwa SHUBIRI. Jamii nyingi za Kibantu, hususan Waswahili, wanaitumia tangu enzi za mababu. Kwa kuwa Ulaya hakuna shubiri ndiyo maana wameiita jina la "Kibiolojia" (Kilatini). Juzi juzi, dada mmoja ameniambia anataka kuniuzia vidonge vya "galik". Ninakamuuliza ni "galik" ni nini? Akaniambia ni kitunguu saumu!! Kitunguu saumu pia ni dawa ya kiasili Afrika na Asia. Tuna hazina kubwa ya madawa asilia, kama vile dawa za kutibu saratani (wilaya ya Same), dawa ya kutibu baadhi ya magonjwa ya ini (Iringa, Rufiji, Mwanza, etc.) Tujihadhari sana kesho na kesho kutwa tusije tukauziwa madawa yetu kwa majina ya Kizungu na kuendeleza dhana ya uongo na potofu ya kuwa eti sisi hatujagundua kitu, wakati intelllectual na cultural properties zetu zinaporwa na watu wengine halafu wanakuja kutuuzia hazina hiyo hiyo yetu kwa majina yao. J. Mushi (mtafiti)

    ReplyDelete
  2. ohh neema kiula tulisoma wote Iringa Girls jamani hata hujabadilika.....nimefurahi kukuona tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...