Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni, IGP Said Mwema, akiongea na wanahabari mchana huu ofisini kwake jijini Dar. Shoto ni Afande Abdulrahman Kaniki.
IGP Mwema amesema kuwa suala la Jerry Muro kumiliki pingu linachunguzwa na Jeshi la Polisi na tayari timu ya uchunguzi imeshaundwa ili kubaini uhalali wa umiliki wake ili kuondoa utata uliojitokeza kuhusu raia kumiliki pingu.

IGP Mwema hakusema kama ni kosa ama la kumiliki pingu ila ameahidi kutegua kitendawili hicho baada ya uchunguzi huo.
IGP Mwema amesema ameunda kikosi cha askari polisi na kuwaagiza kusoma sheria na kuitafsiri vema ili kubaini ukweli wake katika umiliki wa pingu kwa raia.

"Si vibaya kukiri ujinga katika jambo usilolifahamu ndio maana nimeagiza vijana wangu kulifanyia uchunguzi suala hili kwa kupitia vifungu vya sheria na kutoa tafsiri yake kuhusu umiliki wa pingu kwa raia.

"Baada ya siku mbili nitawaita tena ili kuwapa ufafanuzi wa kina juu ya pingu hizi za Jerry Muro na pingu nyingine. Tutajua sheria inaeleza nini ili jamii ifahamu suala hilo na kuondoa utata uluiojitokeza kuhusiana na raia kumiliki kifaa hicho kinachotumiwa na majeshi kudhibiti uhalifu", alisema na kuacha wanahabari wakifurahi kwa uwezo wake wa kujieleza pasina kutumia jazba wala vitisho.

IGP Mwema ameongea na wanahabari chache baada ya watuhumiwa watatu ambao ni Mtangazaji wa Kituo cha luninga cha TBC1 Jerry Muro, Edmund Kapama na Deogratius Mugassa, kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kujibu tuhuma za kula njama, kushawishi kupokea rushwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 49 mpaka sasa

  1. Angalizo: Hii kesi imeshafika pahala pake na hatma ya washtakiwa iko mikononi mwa Mahakama na si vinginevyo. Hivyo mdau unapoleta maoni ambayo yanaweza kuingilia mwenendo wa kesi hii tafadhali nakusihi uwe makini tuheshimu Mahakama tafadhali. Samahani lakini kama nitakuwa nimewakwaza, si mnajua tena mambo ya kei vii oww ei.....

    - Michuzi
    -----------------------------------

    Sasa mbona unavunja angalizo lako?, si kesi ipo mahakamani, sasa mbona unatoa maelezo yaleyale uliyoyakataa. Ina maana siku tano zote hawajagundua kuwa there is LACUNA in our law kuhusu umiliki wa pingi?.

    Jibu analijua sana Afande mwema ndiyo maana hata kwenye charges mahakamani hakuna sehemu aliyoshitakiwa mtu kwa kumiliki Pingu. Hii nayo ni another comedy ila nafikiri kishagundua kuwa surbodinate wake alilipuka sasa yeye kama mkuu ni lazima azime

    ReplyDelete
  2. Dah, sasa jama hii imezidi, kiiila kona Jerriii Jerry, kukicha Jerry, mchana Jerry kukiwia Jerry, mie nshakinai yaani. Doh!
    Walete muvi mpya sasa maana zilizopita zote hatujajua kama stelingi aliuawa ama la wao wana-release CD mpya tu kila leo, tena si kila leo sasa, ni kila saa.

    Low A Sir na msururu wake?
    DOWANS?
    TANESCO (+ Kakobe sasa)?
    IPTL?
    Buzwagi?
    Makaa ya mawe Mchuchuma?
    Kagoda LtD?
    BOT na Balali?
    Mzee wa Vijisentie?
    Gavana na nyumba?
    Twin Tawazzz?

    Oi!

    CD mpya trela yake ipoje?

    ReplyDelete
  3. Na ikibainika kuwa si kinyume cha sheria kumiliki pingi.

    Kamanda Kova anatakiwa ajiuzulu mara moja.

    ReplyDelete
  4. Hapa kunaujinga kumiliki pingu ni halali kwa sababu kama watu wanamiliki Bunduki sioni ni kwanini wasimiliki pingu.Mfano umevamiwa na majambazi na umeweza kumzibiti huyo jambazi ni common sense unatakiwa kumfunga pingu ili uweze kummiliki na kuwajulisha polisi.

    Ni ujinga ulioje Mkuu wa Polisi hhajui kuhusu swala la pingu ni halali au sio halali na je ni kweli inachukua siku mbili kujua swala hilo?

    Come on huo ni ujinga na mjinga ni mjinga tu.Kuna vitu vingine vinatakiwa kutumia common sense na niaibu kuona mkuu wa polisi anashindwa kujua hilo ni afadhali angekaa kimya na kuja na jibu moja kwa moja.

    Mjusi

    ReplyDelete
  5. Sorry good street lawyers.
    Tusiague
    Mahakama itatenda haki
    Sifa zinaonesha jamaa alijijengea himaya ya jeshi lake na aliwahi kuomba rushwa kwa wengi na mdau juu amesema pia
    Tuthubiri pleaseeeeeeeeee

    ReplyDelete
  6. KUMBE HATA WENYEWE HAWAJUI KAMA NI KOSA! MBONA KOVA ALISHAKURUPUKA NA KUHUKUMU???? EH SALALEEE....

    mzozaji

    ReplyDelete
  7. HIVI HIZI POROJO ZITAISHA LINI? SIAMINI JESHI ZIMA LA POLISI TANZANIA LILIKUWA HALIJUI SHERIA ZA NCHI HII. ZIDHANI SWALA LA RAHIA KUMILIKI PINGU NI SWALA LA KUUNDIWA TUME!! NA HII INADHIHIRISHA WAZI JINSI NCHI HII ILIVYOJAA VIHIYO. SWALA LA PINGU NDAHANI LILIKUWA NI SWALA LA KUFUNGUA JARADA FULANI AU KITABU FULANI NA KUTOA JIBU. SASA HAPO TUME YA NINI?? MIMI SASA NISHACHOKA!!

    ReplyDelete
  8. Afande ingekuwa vizuri ukumbuke kwamba kuna Vibaka, wapiga dembe na wengi wanaonyanyasa, watoto, wakina mama na raia wema kwa wizi na matendo mabaya mchana na usiku lakini hatuoni juhudi zenu katka kuzima haya, lakini hili la Jerry limevaliwa njuga! kuna NINI ZAIDI. Kumbuka kuna watu wanamiliki pingu wengi tu1 tena zinauzwa kama heleni pembe nyingi za Dunia, pini za kufunga pingu hizo ndo utafautina. Pia kuna wanaotumia pingu katka kufanya mapenzi au tendo la Ndoa. Wakifungwa au kufunga ndo wanpata msisimuko tosha! Hivyo Pingu isingaliwe kwa mtizamo vinyu tu wa kufunga waarifu na nk. Panua uwanja wa upelelezi lakini kumbuka suala la "Invasion of personal privancy". KAZI YENU NI KULINDA USALAMA WA RAIA WALIPA KODI, YAANI WALIPA MISHAHARA NA MALUPULUP YENU NA SI KUZIMA SAUTI ZA WAPINGA UBADHILIFU!

    ReplyDelete
  9. Ushaidi wa kimazingira ni kama ifuatavyo:

    1. Kamera yake ilikuwa na nyumba za jamaa mhasibu anazojenga Morogoro so Jerry alikuwa anamchunguza

    2. Walionekana wote na CCTV hotelini ambako Jerry alikana kwenye maelezo yake kuwa hamjui jamaa

    3. Mhasibu alisema wazi kuwa ndani ya gari la Jerry kuna nini (pingu, bastola)

    4. Miwani ya mhasibu ilikutwa ndani ya gari la Jerry inaonyesha kimazingira walishakutana jambo ambalo jerry alikana.

    Jerry alikurupuka, laiti angesema alishamuona mahali au jana yake huyu mhasibu na wakakaa meza mmoja, maana unaweza hotelini kukaa meza moja na mtu usiemjua hasa kama CCTV kamera ikionyesha kulikuwa kumejaa..ANGEKUWA HANA KESI YA KUJIBU KABISA.

    Yeye Jerry ndo amekaribisha ushahidi wa kimazingira.

    Tatizo alishavimba sana bichwa....linaelekea kupasuka sasa.

    Maoni ya wenye akili timamu

    ReplyDelete
  10. Hawa watu wana matatizo; Polisi wamedai hadharani kuwa raia haruhusiwi kumiliki pingu; aliyedai hivyo ni mtu ambaye ameaminiwa kusimamia Kanda ya Jeshi la Polisi ya Dar na hivyo kuonesha kuwa ni mtu anayejua kile anachozungumzia.

    Sasa Polisi hao hao (hadi IGP) wanataka kuchunguza uhalali wa kauli yao.

    Sasa wao wenyewe waseme; wao wenyewe wajichunguze, na wao wenyewe waangalia sheria na kutoa tafsiri ya sheria hizo. Huu ni ulaghai wa kisiasa.

    Hakuna kosa la mwananchi kuwa pingu; period. Mnawapotezea muda wananchi kwa kutunga sheria zenu huku mnaendelea mbele ya safari.

    Ili mpate tafsiri ya hiyo sheria; mngemfungulia mashtaka Muro ya kukutwa na pingu, halafu Mahakama ndiyo itatoa tafsiri ya sheria hizo.

    ReplyDelete
  11. HIVI MKUU WA POLISI MZIMA HAJUI SHERIA.MPAKA AWEKE TUME KWA AJILI YA PINGU TU.SI UNAJUA TU MTU KUMILIKI PINGU SI SAHIHI.INASIKITISHA KUONA KWAMBA POLISI AJUI SHERIA YAKE.HIVI HUKO KWENYE CHUO CHA MOSHI MLIKUWA MNAKWENDA KUFANYA NINI?SASA WEWE SAID MWEMA MPAKA UUNDE UUNDE TUME KWA KITU UNACHOJUA.KWA NINI SISI WATANZANIA HATUPO WAZI KILA KITU KIPO KWENYE KATIBA.KWA NINI HAO WATU WACHACHE WANAOJIFANYA KUTOJUA KATIBA NA MMEWAPA MAMLAKA KAMA HAYO NA HAWAJUI HATA KAMA MTU AKIIBA KUKU NI KOSA.KWA HIYO TUNAWAKAMA WATU WENGI WASIO NA MAKOSA NA KUWAJAZA MAHABUSU NA KUWALISHA KWA KWA PESA YA WALIPA KODI.HILI LAZIMA TULIMALIZE SASA KWA KULISAFISHA JESHI LA POLISI.

    ReplyDelete
  12. ADILI NA NDUGUZEFebruary 05, 2010

    Safi sana afande Mwema kwa ufafanuzi mzuri juu ya suala hilo. Alimuradi Waziri Mkuu aliliongelea bungeni, nimefurahishwa kuona na wewe umekuwa mwepesi kutake charge na kutoa ufafanuzi. Hatukatai inawezekana Jerry amevunja sheria na polisi nao wakatekeleza wajibu wao. Mbona alipoibua suala la matrafiki wala rushwa afande ulichukua hatua. Wala waandishi wa habari hata pongezi hawakukupa. Lakini tangu Jerry kashtakiwa inashangaza kuona MCT wanatoa kauli ambazo zinaashiria kama vile polisi inanyanyasa. Na ofisi yako inalaumiwa. It goes to show jinsi gani media yetu ilivyo prejudiced and not balanced at all.

    Briefing yako ya leo was done proffessionally. Katika mazingira tuliomo kwa ujumla polisi inafanya kazi nzuri.

    Nina hakika kama angekuwa mwandishi mwingine wala lisingekuwa jambo kubwa. Hata kama Jerry hakuwa ameripoti yale ya trafiki suala lake lisingeleta minongono. Wala Waziri Mkuu au hata IGP wasingelazimika kuingilia. Kwa hiyo ieleweke concern ya watu ni zaidi ya Jerry kama Jerry bali concern ya watu wanafikiri polisi inalipiza kisasi.

    Afande well done and keep it up. Ukweli utajulikana tu mahakamani. Tunaomba kesi iamuliwe haraka

    ReplyDelete
  13. Mmmmh!!!!!!????Hata huyu hajui kama ni ruska au siruska kwa rai kumiliki pingu!!amakweli Tanzania we are done!!!Inamaana hajui kama zinauzwa na is up to mwenye cash kununua?Jamani hii nchi haina hata pa kumake comparison kwa jinsi mambo yanavyoenda kimbumbumbu!!mabosi wanaojidai kulinda nchi empty na rai wakaida atakuaje?bora tugawana hii nchi kila mtu achukue hamsini zake!!!!!!

    ReplyDelete
  14. Poa mkuu lakini kuna wanasheria kibao Tanzania kwahiyo sizani kama inabidi ichukue kalne nzima kujua uhalali wa pingu.Ulitakiwa kujua hiki kitu kabla ujaongea na waandishi wa habari.Credibility zenu zinatutisha wananchi
    Pia nafikiri pingu hazitumiwi kudhibiti uhalifu bali kuwadhibiti wahalifu wanapokamatwa.

    ReplyDelete
  15. Sasa mzee, hata kama wewe kama kumiliki pingu ni kosa au laah ina maana kama si kosa basi Kova atapona kuwajibishwa?Na kama atawajibishwa kwa kupotosha umma na wewe itakujwaje kwa kutojua?

    ReplyDelete
  16. I just want to give my props to IGP for the way he stepped up to solve this issue, he has demostrated the character of a good leader and that is to accept that he doesnot know everything, and promise to research the whole issue and comeback with an answer. good job.

    ReplyDelete
  17. Sasa hii Polisi imekuwa Mahakama inaanza kutafsiri sheria?...kama hawana nia mbaya na Jerry Muro na hakuna sheria inayozuia kuwa na pingu, ya nini mpaka IGP aunde timu ya kuanza kutafsiri sheria badala ya kuiachia Mahakama kazi hiyo? Hivi ni kweli Polisi wanaweza kujihukumu vibaya katika kesi yao wenyewe?...

    Wameacha kazi ya kufuatilia uhalifu wenye madhara makubwa kama ujambazai na ajali za barabarani wanashughulikia vitu vidogo kama hivi??..MWEMA NAE NIMEANZA KUMTILIA MASHAKA KAMA KOVA!

    ReplyDelete
  18. This police officer is a joke.
    He should know the Law.
    If he does not know such a simple thing then how did he get to be in that cheo?


    Bongo can be a JOKE

    This is ludacris

    ReplyDelete
  19. Michuzi hii haiwezi kubaniwa kabisa!!!!!!!!
    swali je kweli pingu amekuwa nazo sasa kwa muda wa miaka minne kabla ya kupata stakabadhi?.

    Rejeeni video yake mwenyewe ya awali!!

    ReplyDelete
  20. Zungu Wa MbiziFebruary 06, 2010

    Hapa ninatatizwa kiaina....hivi IGP Mwema kama kiongozi wa ngazi ya juu kabisa katika jeshi la polisi na msomi wa kiwango cha kutosha inakuwaje yeye mwenyewe hashindwe kutoa tamko kuhusiana na umiliki wa Pingu kwa raia?? ina maana havielewi vipengele vya kisheria kuhusiana na raia kumiliki pingu???.....hii yote kuhusiana na kuweka "timu ya vijana" kuchunguza umiliki wa pingu kwa raia ni upotezaji wa muda na usumbufu usio na kichwa wala miguu....Kweli Bongo Tambarare!!!!

    ReplyDelete
  21. duh madesa hadi kwa kina saidi mwema...mi nilijua sikuzote hizo wangekuwa washadesa...na sm tym huwa nikiona mapolisi huwa nadhani misheria yote kwa kikwa kumbe lol!!! ni full madessa...kwikwikwikwi!!

    ReplyDelete
  22. kwahio na yeye IGP pia hajui sheria inasemaje kuhusu raia kumiliki pingu? kwanini asingesubiri hawe na huakika ndio aje kutegeua kitendawili? manake sio kama kategua kitu.

    na kama haturuhusiwi kumiliki pingu yale maduka ya silaha yanauza pingu watachukuliwa hatua gani kuvunja sheria za nchi? au watasamehewa kwani hata jeshi la polisi halikuwa linajua sheria inasemaje?

    ReplyDelete
  23. Jino kwa JinoFebruary 06, 2010

    Jerry alimwaga MBOGA za Traffic.. Nao wamwagia UGALI wa rushwa.
    Mpaka sasa ni ngoma draw 1-1.
    Tunasubiri penati za Mahakama kumjua mshindi atakuwa nani.
    Stay tuned!!

    ReplyDelete
  24. Jeshi la polisi halina wanasheria ?

    ReplyDelete
  25. Kwanza ingawa mimi si mwanasheria, lakini nadhani ni kazi ya wanasheria wa serikali kuitafuta sheria yoyote inayohusiana na umiliki wa pingu na kuitafsiri kwa vyombo vya dola.

    Pili, tangu sakata la jerry muro lianze, zoezi hili lilitakiwa liwe limekwishafanya kikamilifu.

    Tatu, mizengwe iliyopo inaashiria kwamba serikali haina sheria inayomkataza jerry muro kumiliki pingu isipokuwa inamtafutia hatia kwa lazima.

    Nne, watanzania inabidi tuachane na huu upumbavu wa kusema "mungu atatulipia"; kina mandela, castro, george washington, kemal ataturk na wengineo wangeng'ang'ana na hii dhana ya udhaifu, dunia hii mpaka leo ingekuwa ya ma-aristocracy.

    Tano, jee... jerry muro akifa/akiuawa huu ndiyo utakuwa mwisho wa mapambano? maisha yake yatakuwa yamekwenda na maji kwa bei rahisi au itakuwa changamoto ya mapinduzi kwetu vijana?

    ReplyDelete
  26. Nina kila heshima kwa IGP afande Mwema ila cha kusikitisha ni kwamba polisi hawawezi kuruhusiwa kutafsiri sheria ila mahakama ina uwezo wa kutafsiri sheria na mwanasheria yeyote aliyeidhinishwa na mahakama kufanya hivo. Pia paralegals wanaweza kufanya utafsiri huo chini ya mahakama.

    Afande tutakuwa na uhakika upi kwamba utafsiri huo utakuwa bayana bila ya kutanguliza makusudio yalioonyeshwa na maafande wako kuhusiana na suala la Jerry Muro?

    Pili kama kulikuwa na uwezekano huo kwa nini huyu mwandishi apandishwe kizimbani kwa makosa ambayo inawezekana kutokuwa sahihi kama kulihitajika kuwa na utafsiri wa sheria?

    Nafikiri ni wakati sasa kuna umuhimu wa kutafsiri sheria nyingi na kusambazwa kwa wananchi ili Watanzania wajue sheria nyingi na waweze kuepuka kufanya makosa yatayoweza kuwaletea matatizo kwenye maisha yao.

    Sisi ni wananchi ambao tutapenda kuona tunaishi kwenye mazingira ya kufuata sheria pasipo kuzivunja na kuzifanya jamii zetu kuwa salama na adilifu zaidi.

    Nashukuru kuchangia mawazo yangu na Kaka Michuzi naomba kama maoini yangu yanaweza kusikilizwa na viongozi wetu wa jeshi la polisi, itakuwa vema.

    ReplyDelete
  27. ITACHUKUA ZAIDI YA MIAKA 25 HADI 50 KWA TANZANIA KUKOMAA KIDEMOKRASIA! BADO DEMOCRASIA NI CHANGA UBABE UNAENDELEA KATIKA NGAZI ZOTE ZA UONGOZI NA MAMLAKA MBALIMBALI. MAKAZINI, SERIKALINI, KATIKA VYAMA HAKUNA DEMOCRASIA, WANANCHI WANASHUHUDIA MAMBO MACHAFU YANAYOENDELEA LAKINI UKINYANYUA MDOMO UNAZIMWA MARA MOJA KWA NJIA TOFAUTI. SISHANGAI KWA HAYO YALIYOMPATA JERRY MURO NI KWA VILE AMEGUSA ANGA ZA WATU KUWAFICHUA WASIO TENDA HAKI(WALARUSHWA NA WABADHILIFU WA MALI YA UMMA) HIYO NDO ADHABU ANAYOIPATA NA LENGO NI KUTAKA KUMZIMA ASIENDELEE KUGUSA ANGA ZA ULAJI WA WATU. HUO NDO UBABE UNAOENDELEA NA INAONYESHA KWAMBA HAKUNA DEMOCRASIA BADO NI CHANGA TUNAITAJA TU MIDOMONI LAKINI KIZAZI KILICHOPO KWENYE NYAZIFA MBALIMBALI KITAKAPOPITA NDIPO KIZAZI KIPYA KITAKUWA KINAELEWA NINI MAANA YA DEMOCRASIA HALISI.
    WANANCHI BADO TUNA SAFARI NDEFU KUELEKEA KWENYE DEMOCRASIA YA KWELI!
    MDAU WA DAMU USA

    ReplyDelete
  28. Mimi naona hili jambo linaonyesha dhahiri ya kuwa jeshi la polisi kwa sasa linaongozwa na watu wasiojua nini wanachokifanya. Kwa hiyo wanaquestion Muro kuwa na pingu, sasa kama ni kinyume cha sheria kwa nini aliuziwa? Na jee watalifungua lile duka kesi pia ?

    ReplyDelete
  29. michuzi asante sana kwa kutoweka comment yangu iliouliza mambo ya maaana.

    mungu akubariki uendelee kuwa muandishi wa habari mzuri mwenye kuchuja habari zaidi na zaidi,milele na milele amen.

    ReplyDelete
  30. christabellaFebruary 06, 2010

    michuzi mi nina swali naomba unisaidie kujibu pamoja na wadau wengine,hivi hizo pingu je watu wa usalama nao wanaruhusiwa? maana kuna vijana wengi wanajiita wapo usalama wa taifa wanatembea na pingu na hapa nimeambiwa hairuhusiwi inakuwaje waungwana

    ReplyDelete
  31. Ankal kama wewe ndiye ulieandika hicho kichwa cha habari kwamba huyu side mwovu ametegua kitendawili cha pingu utakuwa unatuchanganya,hatuna tatizo kwa wewe kuwa CCM au mtu wa sirikali,but where was side mwovu before all this thing go to court,pili kama anataka kuchunguza uhalali wa raia kuuziwa pingu,anatakiwa akachunguze hilo duka la sirikali au lililo kabidhiwa dhamana na sirikali kumuuzia pingu raia,na siyo mteja .H Town

    ReplyDelete
  32. Tanzania kila mtu anataka kuwa mwanasiasa. Saidi Mwema sikutegemea angetoa jibu la kisiasa kidizaini hiyo. Aibu.

    Bongo kuanzia baba lao, watoto mpaka wajukuu wooooote vichwa maji. Ndio maana nchi yetu maskini aisee miaka karibia 50 baada ya uhuru. Ukiwa unaongozwa na viongozi wenye kung'amua mambo kidizaini hii unazani utapiga hatua yoyote mbele? Haiwezekani ng'oooo

    ReplyDelete
  33. ...... and i am told the guy (igp) is a lawyer.

    ReplyDelete
  34. Wewe uliyeuliza kuwa jeshi la polisi halina mwanasheria? Ni kwamba kwa kwa level ya polisi kama kovu au side anatakiwa kuwa law school graduate lakini wakina Haruni Mahundi wamestaafu,wabakia vilaza. H Town

    ReplyDelete
  35. Mtaka MazuriFebruary 06, 2010

    Ankal, huwa unabania sana maoni yangu, ila hili neno naomba ulirushe Ankal,

    jamani huyu IGP, ni mwanasheria , yaani alishindwa kutafuta sheria husika inasemaje na kutueleza mpaka aunde tume, pingu tu Tume je ingekuwa bomu si tungeunda Bunge? au Bongo Tambarare ???? Eti tume ya kusoma na kuitafsiri, Mwema huoni hata aibu??

    Halafu huyu IGP kwanini aliita waandishi wa habari wakati hana majibu ya hilo suala? Kwanini aingetafuta jibu kwanza ndio akaita waandishi wa habari?
    au ndio allowance za kutosha ?!!

    Jamni hata hili suala tunafanya siasa, Jerry ametoa Stakabadhi ya manunuzi ya pingu yake ambayo aliinunua kwa 25 elfu, habari ya msingi ni "whether is it legal for a person to possess a handcuff or not? hapa illegality ya kumiliki pingu na so tume wala vinginevyo....!!

    Nimesikitika sana !! Hii ni ajabu....

    ReplyDelete
  36. oh tanzania nchi ya amani, wajinga ndio waliwao
    WATANZANIA AMKENI, TUNATAKIWA KWENDA MSITUNI, HAWA WAZEE WALIOPITWA NA WAKATI WATAZIDI KUNGANGANIA MADARAKA

    Michuzi najua hii haitaona mwanga wa jua, kweli safari yetu bado ni ndefu.

    ReplyDelete
  37. Afande Saidi Ali Mwema hukuhitaji kuunda tume kujua kama ni kosa ama si kosa kumiliki pingu. Ungemshitaki tu huyo Jerry kwa kukutwa na kifaa kisichoruhusiwa, na huko mahakamani wataalamu wa sheria wangetutafsiria sheria kama raia kumiliki pingu inakubalika kisheria ama la.

    ReplyDelete
  38. Jamani mbona tanzania utani umezidi? itakuwaje kuundwe tume kuchunguza suali hili? Polisi ni chombo cha sheria na ni jambo la kuangalia vitabu vya sheria za nchi tu na kusema lipo suali hili au halipo. kama halipo basi hakuna kosa. sasa nini haja ya kuwa na tume? jee ndio itakuwa mtindo wa sasa kila mtu akikamatwa na kitu au kufanya kosa tutaunda tume? Tuamkeni watanzania!!!! hawa jamaa wengine wanatuchezea shere sasa!!!!

    ReplyDelete
  39. WANAJUWA KAMA NI KOSA AU SI KOSA ILA HAWATAKI KUKURUPUKA TU NA KUTOWA JIBU AMBALO SI SAHIHI, HUYO HAPO PEMBENI PA AFANDE SAID MWEMA NI MY MATE AT JKT BULOMBORA (ADDULAHAM KANIKI=MGOSI WA GAYA) ALIKWENDA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA ALIFANYA DEGREE YA LAW NA ALIAJIRIWA NA POLISI MAKAO MAKUU HAPO CENTRAL NA ANAFAHAMU SHERIA FIKA, KWA WALE WENYE KUMBUKUMBU ALIKUWA NA PAGE YAKE YA MASWALA YA SHERIA KATIKA DAILY NEWS ALIKUWA ANACHAMBUA SHERIA KILA SIKU NA SHERIA MPYA KATIKA HILO GAZETI SIJUWI KAMA BADO ANAENDELA. HIVYO NI FIKA WANAJUWA SHERIA JUU YA PINGU. HONGERA AFANDE KANIKI NAONA UMEFIKA MBALI SANA MZEE. NI MIMI MATE WAKO JKT (1985/86 OPERATION OKOA) BULOMBORA (EDWARD A.)

    ReplyDelete
  40. ...IGP ni mwanasheria na vilevile wanasheria ni wengi katika jeshi la polisi,lakini tatizo la polisi elimu haitumiki kinachahotumika ni mazoea ambayo wameyakuta, na kutokana na mazoea hayo basi wale wenye digrii za sheria hupoteza walichosoma katika vyuo vya sheria.Kwahiyo,wanabaki kumilikiwa na mazoea na nini afande alichosema.Mwisho wanakuwa masalia ya vyeti lakini mukichwa unakuta hakuna kitu tena.

    Hivi hakujawahi kutokea kosa la namna hiyo huko nyuma katika historia ya jeshi?

    wamejaa tunnel vision,hawawezi kuona mbali ?

    Mwisho tusubiri tafsiri sahihi ya mahakama na sio tume ya IGP

    ReplyDelete
  41. Hivi in January ? au ON January ?
    Polisi wetu bwana.Angalia charge sheet.

    ReplyDelete
  42. Bongo nako uzushi, swala la kumiliki pingu linaleta utata? itakuwaje kw wale wapenzi wanaopenda kufungana pingu kwenye tendo la ndoa? :-)

    ReplyDelete
  43. huyojamaa naye anaonekana mjanja mjanja, we pingu za nini kwenye gari kama sio msanii?

    ReplyDelete
  44. sheria wangetutafsiria sheria kama raia kumiliki pingu inakubalika kisheria ama la.


    •Tarehe Sat Feb 06, 05:37:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Jamani mbona tanzania utani umezidi? itakuwaje kuundwe tume kuchunguza suali hili? Polisi ni chombo cha sheria na ni jambo la kuangalia vitabu vya sheria za nchi tu na kusema lipo suali hili au halipo. kama halipo basi hakuna kosa. sasa nini haja ya kuwa na tume? jee ndio itakuwa mtindo wa sasa kila mtu akikamatwa na kitu au kufanya kosa tutaunda tume? Tuamkeni watanzania!!!! hawa jamaa wengine wanatuchezea shere sasa!!!!


    •Tarehe Sat Feb 06, 06:00:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    WANAJUWA KAMA NI KOSA AU SI KOSA ILA HAWATAKI KUKURUPUKA TU NA KUTOWA JIBU AMBALO SI SAHIHI, HUYO HAPO PEMBENI PA AFANDE SAID MWEMA NI MY MATE AT JKT BULOMBORA (ADDULAHAM KANIKI=MGOSI WA GAYA) ALIKWENDA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA ALIFANYA DEGREE YA LAW NA ALIAJIRIWA NA POLISI MAKAO MAKUU HAPO CENTRAL NA ANAFAHAMU SHERIA FIKA, KWA WALE WENYE KUMBUKUMBU ALIKUWA NA PAGE YAKE YA MASWALA YA SHERIA KATIKA DAILY NEWS ALIKUWA ANACHAMBUA SHERIA KILA SIKU NA SHERIA MPYA KATIKA HILO GAZETI SIJUWI KAMA BADO ANAENDELA. HIVYO NI FIKA WANAJUWA SHERIA JUU YA PINGU. HONGERA AFANDE KANIKI NAONA UMEFIKA MBALI SANA MZEE. NI MIMI MATE WAKO JKT (1985/86 OPERATION OKOA) BULOMBORA (EDWARD A.)


    •Tarehe Sat Feb 06, 06:06:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    ...IGP ni mwanasheria na vilevile wanasheria ni wengi katika jeshi la polisi,lakini tatizo la polisi elimu haitumiki kinachahotumika ni mazoea ambayo wameyakuta, na kutokana na mazoea hayo basi wale wenye digrii za sheria hupoteza walichosoma katika vyuo vya sheria.Kwahiyo,wanabaki kumilikiwa na mazoea na nini afande alichosema.Mwisho wanakuwa masalia ya vyeti lakini mukichwa unakuta hakuna kitu tena.

    Hivi hakujawahi kutokea kosa la namna hiyo huko nyuma katika historia ya jeshi?

    wamejaa tunnel vision,hawawezi kuona mbali ?

    Mwisho tusubiri tafsiri sahihi ya mahakama na sio tume ya IGP


    •Tarehe Sat Feb 06, 06:13:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Hivi in January ? au ON January ?
    Polisi wetu bwana.Angalia charge sheet.


    Post a Comment ~ Rudi Mwanzo ~ mtumie Rafiki YakoCopyright 2006 - 2009 © ISSA MICHUZI. All Rights Reserved.

    Sasa hivi ni saa:
    2:40:40 PMDecember 7, 2009



    Idadi ya watu

    ReplyDelete
  45. Bunch of Dumbs , what a daamn shame.. In 2010 we should stop these kind of intimidation politics.what is next ? to spill Acid on his face?

    ReplyDelete
  46. KUMILIKI PINGU SIO KOSA! HUKU UK PINGU ZINAUZWA KWENYE MADUKA KIBAO! WATU WANAZITUMIA KUFANYA MAPENZI! BONGO MAMBO HAYO BADO? UKITAKA KUMFUNGA MTU SIO LAZIMA UTUMIE PINGU HATA KAMBA SI ZIPO? HII INAONYESHA JINSI GANI POLISI WETU ZERO!! NDIO MAANA HAWANA HATA NJIA ZA KUDHIBITI AJALI BARABARANI...OVYOOOOOOO!

    ReplyDelete
  47. "IN JANUARY" NI SAHIHI LAKINI KAMA UNATAJA DATE/TAREHE NDO UTASEMA "ON" SAY ON 6TH OF DECEMBER 2008 HAPO WAKO SAWA NI "IN JANUARY"

    ReplyDelete
  48. Tume ya kuchunguza uhalai wa raia kumiliki pingu iliyo undwa na IGP MWEMA, taaarifa kutoka kwa mdau zinasema mpaka tume hiyo kumaliza uchunguzi bajeti yake imetengwa ni shs 100,000,000(milioni mia moja) kutokana na ugumu wa kazi hiyo.

    Imekaaje hiyo wadau?

    michuzi hachelewi kuibana hii,kwani michuzi yenyewe sisi wadau tumeengezea maji tu michuzi ilisha pikwa huko huko mambo ya ndani hapa uyu anatuzuga tu sasa.

    ReplyDelete
  49. KAMANDA KOVA NA IGP MWEMA MNASTAHILI KUJIUZULU MAANA DHAHIRI MMEONYESHA KUWA HAMJUI KAZI WALA LOLOTE KATIKA USALAMA WA RAIA. NI AJABU KWENU KUTOJUA KUWA KUMILIKI PINGU NI KOSA AU SI KOSA!! YAANI MNAUNDA TUME KUCHUNGUZA AU KUFATILIA KUJUA KUWA KUMILIKI PINGU NI KOSA AU SI KOSA!!! MKO HAPO KUFANYA NINI MIAKA YOTE HII?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...