
Ligi hii itakutanisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali, lakini changamoto kubwa katika michezo hiyo ni mabondia wanawake Upendo Njau kutoka Kilimanjaro na Frola Machela kutoka Dodoma ambao nao watapambana katika michezo hiyo.
Michezo hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka ili kutafuta washindi ambao hapo baadae wataunda timu ya Taifa na kuingia kwenye mashindano ya kamataifa ili kuongeza ari na kukuza i mchezo huo hapa nchini. Msikilize Kaseba mwenyewe katika video hii hapa chini
Safi sana kaka. Ni vizuri kufanya mambo mwenyewe. Watu wengine wanawaibia tu. shikilia hapo hapo
ReplyDeletetatizo moja hapo kaka michuzi, hujamuuliza kaseba hao mabondia wanapigana katika uzito gani? maana hawezi kupiganisha watu wa uzito tofauti. hilo swali kwako ankal.
ReplyDeleteEeh bwana Mbesse si mchezo. Chakarika mjasirimali, watu ndio wenyewe. Mimi mdau tulikuwa wte pale Zanaki Dojo.
ReplyDeleteHongera Kaseba, you're one in a million lakini je, tukizungumzia usalama na mambo ya Insurance inakuwaje? Maana ninavyojua mimi kule Thailand kwenye huu mchezo wa Kickboxing watu waga wanavunjika mbavu, Mifupa ya kwenye mapaja, viuno na kadhalika...hebu tufafanulie na hilo boss Kaseba, senkyu!
ReplyDeletemdau,
Ashkmatit
Huyu Jamaa ni Kichwa!! Ukimsikiliza anavyoongea,mambo yote yanatoka moyoni kwakwe. Naomba contact ili tuweze kuchangia wenye uwezo.
ReplyDeleteAhsante
Mchezo huu ni maarufu sana yaani hata boxing sasa karibu inatupwa nje.
ReplyDeleteAnayeuliza uzito hakuna kitu kama hicho katika Kick boxing huwa kuna mijitu mizito inawekwa chali na vijamaa vyepesi tu ama kwa technique za vifuti au kwa mateke yaliyonyooka na jeb za kupoteza fahamu.
Siyo tu huko Japan au Thailand, Waholanzi ni moto wa kuotea mbali katika Kick Boxing.
Ni kweli, Japhet kitu cha msingi katika Wadhamini pata hata Hospitali moja itakayokuwa tayari kuchukuwa mzigo wa kuwahudumia majeruhi. Kwa kawaida wapiganaji huwa wanatakiwa kuwa na health insurance ambazo hucover michezo ya 'hatari' kama hii.
Bravo Japhet, ngoja nimalize kitabu changu mzee tuungane tulete vijana wa kiTz hapa Amsterdam naamini watawin; yaani kuna wa-Moroko, Wa- Tuturuki, wa- Surenam n.k wanaondoka na Euro 50,000 hivi hivi na bado nikifikiria kwa undani naona mguu wa Kaseba au hata sumbwi la Cheka ni bora kuliko hao.
Kinachotakiwa kwetu ni kufahamisha umma zaidi juu ya fani hii, mafunzo na lishe nzuri kwa wapiganaji na ufadhili kwa washiriki.