Bosi wa kampuni ya Tan Academy of Mix Fight & Thai Boxing, ambaye pia ni bingwa wa Kick Boxing, Japhet Kaseba, akionyesha picha kwa wanahabari wakati akizungumza nao leo kuhusu Ligi ya Bingwa wa Mabingwa wa mchezo wa Kick Boxing Tanzania itakayofanyika kwenye ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa jijini Dar kuanza tarehe 27 mwezi wa pili na kuisha tarehe Machi 27 mwaka huu.

Ligi hii itakutanisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali, lakini changamoto kubwa katika michezo hiyo ni mabondia wanawake Upendo Njau kutoka Kilimanjaro na Frola Machela kutoka Dodoma ambao nao watapambana katika michezo hiyo.

Michezo hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka ili kutafuta washindi ambao hapo baadae wataunda timu ya Taifa na kuingia kwenye mashindano ya kamataifa ili kuongeza ari na kukuza i mchezo huo hapa nchini. Msikilize Kaseba mwenyewe katika video hii hapa chini





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Safi sana kaka. Ni vizuri kufanya mambo mwenyewe. Watu wengine wanawaibia tu. shikilia hapo hapo

    ReplyDelete
  2. tatizo moja hapo kaka michuzi, hujamuuliza kaseba hao mabondia wanapigana katika uzito gani? maana hawezi kupiganisha watu wa uzito tofauti. hilo swali kwako ankal.

    ReplyDelete
  3. Eeh bwana Mbesse si mchezo. Chakarika mjasirimali, watu ndio wenyewe. Mimi mdau tulikuwa wte pale Zanaki Dojo.

    ReplyDelete
  4. Hongera Kaseba, you're one in a million lakini je, tukizungumzia usalama na mambo ya Insurance inakuwaje? Maana ninavyojua mimi kule Thailand kwenye huu mchezo wa Kickboxing watu waga wanavunjika mbavu, Mifupa ya kwenye mapaja, viuno na kadhalika...hebu tufafanulie na hilo boss Kaseba, senkyu!

    mdau,
    Ashkmatit

    ReplyDelete
  5. Huyu Jamaa ni Kichwa!! Ukimsikiliza anavyoongea,mambo yote yanatoka moyoni kwakwe. Naomba contact ili tuweze kuchangia wenye uwezo.
    Ahsante

    ReplyDelete
  6. Mwanafunzi mwenza wa `Sele- Kumcha'February 10, 2010

    Mchezo huu ni maarufu sana yaani hata boxing sasa karibu inatupwa nje.
    Anayeuliza uzito hakuna kitu kama hicho katika Kick boxing huwa kuna mijitu mizito inawekwa chali na vijamaa vyepesi tu ama kwa technique za vifuti au kwa mateke yaliyonyooka na jeb za kupoteza fahamu.
    Siyo tu huko Japan au Thailand, Waholanzi ni moto wa kuotea mbali katika Kick Boxing.

    Ni kweli, Japhet kitu cha msingi katika Wadhamini pata hata Hospitali moja itakayokuwa tayari kuchukuwa mzigo wa kuwahudumia majeruhi. Kwa kawaida wapiganaji huwa wanatakiwa kuwa na health insurance ambazo hucover michezo ya 'hatari' kama hii.

    Bravo Japhet, ngoja nimalize kitabu changu mzee tuungane tulete vijana wa kiTz hapa Amsterdam naamini watawin; yaani kuna wa-Moroko, Wa- Tuturuki, wa- Surenam n.k wanaondoka na Euro 50,000 hivi hivi na bado nikifikiria kwa undani naona mguu wa Kaseba au hata sumbwi la Cheka ni bora kuliko hao.

    Kinachotakiwa kwetu ni kufahamisha umma zaidi juu ya fani hii, mafunzo na lishe nzuri kwa wapiganaji na ufadhili kwa washiriki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...