Natumaini kwa uwezo wa Mungu mko wazima,

Leo kwenye misa ya asubuhi kanisani Azania Front mchungaji aliyekuwa
anahubiri katufunulia siri nyingi sana za sheteni nakutupa shuhuda
mbalimbali jinsi shetani anavyofanya kazi.

Moja ya ushuhuda wake ni kisa kilichotokea hivi karibuni hapa Dar es
salaam. Napenda nikushirikishe ili uchukue hatua.

Pale salender Bridge ambapo anasimama trafiki akivuta magari, kuna mdada
alikuwa ndani ya gari lake kwenye foleni akisubiri zamu yake ya kuruhusiwa
na trafiki ifike apite. ndipo aliposogea kaka mmoja ombaomba, akasogea
kwenye gari la yule dada na kuomba msaada.

Dada huyo kwa kumhurumia akamsaidia. Alipompa pesa tu mkono wa yule dada ukaota manyoya ya paka, akachanganyikiwa alipokuwa anaendelea kushangaa trafiki akawa anaruhusu magari ya upande wake yule dada akawa hawezi kuendesha gari, ndipo trafiki akamsogelea na kuuliza kulikoni?!

Yule dada akatoa mkono wake na kumuonyesha trafiki na kumsimulia
kilichotokea na bahati nzuri yule kaka aliepewa pesa alikuwa mita chache
pembeni anamuangalia yule dada. Ikabidi trafiki aende kumuuliza yule
ombaomba kulikoni?

ndipo yule ombaomba akamwambia trafiki kuwa yule dada akimbusu tu atapona mkono utarudi kawaida.basi ikabidi yule dada atelemke aende kumbusu yule kaka, alivyombusu wakapotea wote palepale, gari ya yule dada ikabaki barabarani ndipo trafiki alipoita watu wakaanza kuisukuma ile gari na
kuiweka pembeni.

kuna dada mwingine alikuwepo leo kanisani baada ya ibada akawa
anatusimulia, yeye alikuwa nyuma ya gari ya huyo dada alishuhudia hilo
tukio anasema ni tukio la kweli kabisa ameshuhudia kwa macho yake.

Hivyo jamani nawatahadharisha ndugu zangu mlio na moyo wa huruma msipende kutoa pesa zenu hovyo sababu umekutana na maskini.
Biblia inasema maskini wapo na wataendelea kuwepo, mwombe Mungu kwanza kila unapotaka kutoa sadaka yako.
Mwenye Masikio na Asikie
Mdau Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. michuzi, upuuzi kama huu kuutundika hapa haiwezekani.

    ReplyDelete
  2. Mbona hii story kama ya Abunuasi, mimi naomba unisaidie kujua hili tukio lilitokea tarehe ngapi na saa ngapi? mana hawa wachungaji wetu siku hizi sio wakuwaamini sana. wanataka usisaide maskini ukawasaidie wao tu. hii ni dunia ya utandawazi na Ukweli. samahani kama nitakuwa nimekwaza mtu. habari ndio hiyo.

    ReplyDelete
  3. HII NI HABARI YA KWELI AU FIMBO TU, MBONA HATUKUPATA HABARI HIZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI, AU UNALETA HADITHI ZA BIBLIA/BIBLE, HADITHI ZA KALE, KWANZA MUNGU HAJAKATAZA KUSAIDIA SIKINI, NA BIBLIA/BIBLE PIA INAHIMIZA KUSAIDIA WASIO NACHO

    ReplyDelete
  4. edeleni kuwa matomaso..sijui na wewe mpaka uote kwato uson ndo utaamini...tomaso hakuamin km yesu alifufuka sasa nanyie jidai kama hamjui kwenye society kuna mambo ya ushirikina..thanks kaka kwa ushauri..matomaso endeleni kutoa hela mungu awaongezee..masikin hawapo barabarani tu..unaweza saidia kokote

    ReplyDelete
  5. Kuna uwalakini hapo! Polisi alikuwepo halafu taarifa zisifikie vyombo vya habari. Kama kuna mdau aliona ikitangaza kwenye Radio, TV ama kasoma kwenye magazeti (siyo) ya udaku atuambie ukweli wa jambo hili. Hata mimi, naunga mkono kwamba dunia hii imevamiwa sana na hata makanisani kuna watapeli. Hasa wachungaji! Sijawahi kuona siku hizi za karibuni mchungaji akasimama MIBARANI halafu asisisitize watu kutoa sadaka na zaka. Na katika kufanya hivyo, huwa wanajaribu kufunga mianya yeyote ile ambayo mtu anaweza kutumia kipato chake kama hiyo kutishia kutosaidia wahitaji. Lakini Biblia inasema kuweni macho maana kuna watu watahubiri na kuponya kwa jina la YESU kumbe ni mashetani. Mungu atupe nguvu ya kiroho kutuwezesha kupambanua haya katika wakati huu mgumu.

    ReplyDelete
  6. Michuzi hebu usituwekee habari ambazo watu wanatunga au wameota. Hii ni kutaka kuharibu dini, kwani mchungaji wa wkeli hawezi toa hadithi kama hii. Mtu ameenda kuangalia movie Princeses and the Frog ndio anakuja kutoa hadithi hapa

    ReplyDelete
  7. Ndugu yangu wa Feb 16, 09:58:00 PM. Suala siyo kutoamini, bali ni mazingira menyewe ya tukio. Inakuwaje tukio la kustaabisha namna hiyo tena watu waliona na polisi alikuwepo tusilisikie wala kusoma kwenye vyombo vya habari na badala yake iwe kanisani tu?

    ReplyDelete
  8. Watu wanaoamini hadithi kama hii, ni wale wale wanaoamini uwezo wa viungo vya albino. Upuuzi wa aina hii tafadhali wewe iliyetuma kwa anko, next time wasimulie watu wako wa karibu tu. Ogopa sana watu wanaosali kupitiliza au kuamini hadithi kama hizi hata kama zinasimuliwa na wachungaji - baadhi yao wanga vile vile

    ReplyDelete
  9. HIYO STORI NAMI PIA NIMEISIKIA HATA KABLA HAIJATINGA HUMU NDANI, KUNA MDAU ANAFANYAKAZI PALE NACP ALINISIMULIA JUMAPILI ILIYOPITA NA WAKATI ANASIMULIA ALISISITIZA KUWA NI TUKIO LA KWELI MAANA ALISHUHUDIA LIVE. KWA MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU, AWE NA DINI AMA ASIWE NAYO ANATAMBUA UWEPO WA MUNGU NA SHETANI HIVYO HAYA YANAYOSIMULIWA KUTOKEA SIO TATIZO KABISA HAIJALISHI UMEYAONA AU HUKUYAONA TAHADHARI NI BORA KULIKO UBISHI ETI KISA HUKUONA MAANA HAIWEZEKANI KILA KITU KITOKEE PALE ULIPO WEWE NDIPO UAMINI. KAMA HUAMINI HILI JIULIZE KWA NINI UNAENDA KANISANI AU MSIKITINI

    ReplyDelete
  10. Mmezidi kuangalia filamu za Naijeria!!!

    ReplyDelete
  11. Ni vigumu kuamini lakini haya mambo yapo, na siku hizi za mwisho mengi yatasikika na mengi yatatokea,ni shetani naye anajiinua kwa staili yake, silaha ni kumshikilia Mungu wako tu, damu ya Kristo inaondoa na kusafisha yote. Badala ya kuendelea kukataa kuwa haiwezekani jiulize hivi mashahidi wote hao waseme uongo? na watu waliogopa kwenda kwenye vyombo vya habari nani angeamini? si ni k.m wewe uavyokataa? Jamani tuendelee kuomba kwa bidii,Mungu yupo anatusikia na atatulinda kwa yote

    ReplyDelete
  12. Ni kweli haya mambo huwa yanatokea, nakumbuka wakati nasoma mkwawa kuna rafiki yangu alikuwa anatokea Znz. Siku hiyo tumefungua shule na yeye alikuwa anatokea Znz aliposhuka kwenye boti na kuelekea kituo cha daladala mkabala na bank ya NBC alitokea jamaa anaomba msaada ile jamaa kuingiza mkono mfukoni ili atoe hela na kumpa jamaa, fahamu zote zilimuishia mpk wasamalia wakaja kumsaidia ila ada yote ilikuwa imeeondoka.

    Kwa wadau wanaolalamika kuwa tukio hilo hawakulisikia kwenye vyombo vya basi ni wakati wao kusikia kupitia katika blog hii kwani nacho ni chombo cha habari,na pia huwezi kusikia kila kitu mambo mengi tu yanatokea katika jamii yetu na yote hayatangazwi.
    Asante ankal kwa kutuwekea hii.
    Ni juu ya mtu kusuka au kunyoa!

    Ankal ile maada yangu mathematics niliyokutumia umeipiga chini!

    Mdau Kichali

    ReplyDelete
  13. hivi wewe uliandika habari hii sijui kama akili imo kichwani inakuwaje unaamini mambo kama haya,je kwa mujibu wa mchungaji kwa watu masikini wasipewe je nchi masikini nazo hivyohivyo je huyu mchungaji kila cku kuomba misaada kwa ajili ya ujenzi wa hapa na pale kuwa na wao wasipewe je huyo taarifa imetokea lini mbona hatukusikia na huyu trafiki si angetoa ushaidi, cku hizi watu wanabuni njia za kukusanya pesa sasa baadala ya maskini bora utoe kanisani ili naye apate gawiwo lake lakutosha.habari hizi mchu.unatoa kanisani sio kwa watu anatufundisha tabia ya aliyenacho asimwone masikini sidhani kama ni kauli njema kwa waumini

    ReplyDelete
  14. jamani tusibishe bure haya mambo ni ya kishirikina na yapo kabisa. Tunachotakiwa ni kumuomba Mungu wetu wa Mbinguni atulinde na atupe ufahamu, hatukatazwi kusaidia masikini ila kabla hujamsaidia sema na Mungu wako hata kwa maneno machache tu naye hatakuacha uangamie kamwe kwani Mungu wetu ni mwaminifu na hakuna kinachomshinda.
    Mbona kuna wadada flani walimsaidia albino aliwatembelea hostel kuomba msaada wakajikuta wanampa pesa na wanamfuata mpaka anapoenda (bila wao kujijua) matokeo yake wakafika kwenye chumba kilichojaa maalbino wa kiume wengi, kilichoendelea humo ndani mimi na wewe hatujui ila walikaa humo ndani siku mbili na siku ya tatu akawa anawapeleka sehemu nyingine ndo njiani wakakutana na mtu anayewafahamu ile kuwaita tu fahamu zikarudi albino akakimbia!! hiyo ni true story!

    ReplyDelete
  15. Huyu mdau hajashauri watu wasitoe sadaka au kusaidia maskini, amesema "mwombe Mungu kwanza kila unapotaka kutoa sadaka yako". Ni vema sana kuzingatia hio sentensi na sio kukosoa tu. Kama huamini unasoma then unayaacha hapa si kila kitu huwa tunakuwa tumeona.. vingi tunasimuliwa tu. Nadhani watu mmeamua tu kumkosoa huyu mdau.

    ReplyDelete
  16. jamani habari ndio hiyo sio lazima wote muikubali yeye katoa tahadhari mpaka muwe tomaso? tunashukuru sana kwa taarifa me niliipata pia, serikali yetu haihusiki na mambo ya kichawi kwanini mnataka kupata tamko? kamtafuteni yule traffic, clouds fm kwenye power breakfast mbona wameisoma? au sio chombo cha habari?

    ReplyDelete
  17. Nami mke wangu kanisimulia nikamkanya sana, juu ya kuamini haya mambo. Huu ni uzushi vinginevyo watoe taarifa zilizokamilika. Watupe namba ya gari iliyoko salender bridge, pia watuambie kama kuna mtu kaenda ulizia gari lile.
    NIONAVYO YAWEZEKANA MCHUINGAJI KASIMULIWA NAYE KAINGIA KICHWA KICHWA. Nafanyakazi karibu na pale na kama ingekuwa kweli basi ningejua tu. Iweje mtu ana mkono wa paka halafu mimi nimsogelee, sijipendi?? ikitokea hivyo kila mtu anachukua vector yake.

    Tatizo ni kuwa mtu akisimuliwa habari anataka kui"own" aonekane alikuwepo kumbe ni hadithi tu.

    Kuna jamaa wakati wa ujambazi NBC Ubungo alisimulia kuanzia majambazi yanafika, yanapora, yanakimbilia shekilango, yanapinda kuelekea tandale, Kwa mtogole yanaelekea Manzese, yanashika Moro Road, yanaelekea Mburahati n.k na yote hayo anasema alishuhudia mwenyewe!!!!!! na wakati wote risasi zinarushwa!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. tupo ofisini jamaa anatusimulia alikuwa kwenye foleni pamoja na huyo dada ni kweli ameshuhudia yakitokea trafiki mwenyewe alichanganikiwa.sijui tutawezaje kupambana na matendo haya nguvu za gizani kama si mungu atuwezeshe

    ReplyDelete
  19. Jamani acheni kutukana watu. Haya mambo yapo, na pale ni karibu na baharini mapepo wabaya wengi wanakaa humo.Mimi nilisika tu nilipofika ofisi

    ReplyDelete
  20. ni maswali machache yakijibiwa ntaamini asilimia mia moja hili tukio:
    1. huyo dada aliyopotea hana ndugu? maana hadi sasa hamna taarifa ya mtu kupotea!
    2. Gari lake lilifanywa nini baada ya hapo, maana kulisukuma na kuliacha pembeni vibaka si wanalifanyia? afu pale kuna kituo, kama lilisumumwa hadi kituoni, siku ya leo haiishi mi ntavunja ratiba zangu zote na kuwaletea picha!
    3. Kila siku saa saba mchana, polisi wanakusanya waandishi wa habari na wanatangaza matukio ya jijini, hata kama dogo kama mtu kukamatwa na bangi kisokoto kimoja, sasa mi shaongea na ripota wetu wa polisi, anasema hili hadi leo halijatangazwa, ina maana huyo traffic polisi hakuripoti hilo tukio?
    4. waliokuwepo na kushuhudia wanajua vizuri siku hizi matomaso tulivyo wengi kutokana na watu kuwa waongo sana, basi watuambie namba za gari, rangi na aina ya gari, maana si lilibaki hapo, au ndio walirogwa wote?
    5. Mwisho naungana na mdau hapo juu, hivi ilitokea lini? saa ngapi?

    Tanzania bila imani potofu inawezekana! na inaanzia kwa maswali madogo madogo tu kama haya!

    ReplyDelete
  21. Mambo haya yapo ni mambo ya giza (shetani) la msingi ni kumwomba Mungu ili kuepukana nayo. Amini usiamini ndio maana watu tunakwenda makanisani na misikitini ili kujiepusha na mambo kama haya.

    ReplyDelete
  22. Jamani hebu fikirieni... hao wote wanaosema walishuhidia LIVE, mbona wanaandika kama ANONYMOUS. Watoe Majina zao na contact zao ili wanahabari wapate hizo LIVE walizoshuhudia.

    ReplyDelete
  23. enyi matomaso endeleeni kutokuamini hivyo hivyo mpaka yawakute mimi nimesimuliwa na huyo trafiki hili tukio na si omba omba to jihadhari hata na majirani hata ndugu anaweza kukuomba hela na kuifanyia uchawi kuna chuma ulete na vitu kibao kazi kwenu cc wakristo tunaojua haya hatutoi hela mpaka tuiombee kwanza unapotoa hela mwambie Mungu naomba hii hela ikatumike kwa mema na si kinyume na Mungu atakulinda au ni bora usisaidie barabarani saidia yatima kwenye vituo maalum

    ReplyDelete
  24. WE ULIYEANDIKA UNAMIAKA MINGAPI??

    ReplyDelete
  25. Wanao "pretend" hawajaamini tukio limetokea tuone kama leo wakipita hilo eneo akaja mtu tuone kama hata watafungua japo kioo licha ya kunyoosha huo mkono..kutoa msaada.

    Cha msingi tuwe imara katika maombi na tumshike sana Mungu atuepushe na hila za mwovu shetani.

    ReplyDelete
  26. Kikubwa ni kujikabidhi katika mikono ya Mungu kila inapoitwa leo.Tatizo letu tumemsahau Mungu ,hatusali jamani,tunaishi ishi tu.

    Tuwe na subira,kama yametokea tutasikia tu!

    ReplyDelete
  27. Jamani, naomba hii habari ili watu iweze kuwa ya kuaminika, inatakiwa watu at least waweke picha ya hilo gari likiwa limetelekezwa kama ilivyodaiwa (Au ndo hivyo, kila mmoja aliogopa na kuchukua vector yake, au kila aliyepiga picha alipotea au camera zao kutokufanya kazi?). Mimi naamini kuwa mazingara yapo na ndio maana neno hilo 'mazingara' likawepo. Ila hili jambo linahitaji information zaidi ili liaminike kwa jamii... Maana miaka ya nyuma ITV walishawahi kuonyesha watu ambao inasadikika ni wanaanga wa kienyeji ambao waligongana angani.. na wengi tulishuhudia kupitia ITV mmoja akiwa juu ya paa la nyumba na mwingine akiwa juu ya mti wakiwa wamevalia mitambara na vibuyu huku wakiwa wamepauka mwili mzima..(story cut short)..
    Sasa tunaomba habari zaidi kuhusu hili.. Tunajua serikali haina imani za kishirikina, kwa hiyo polisi pia hawawezi kutoa habari za kishirikina.. ila ikitokea huyo dada akija kupatikana hapo ndipo polisi wataweza kuelezea kuwa kuna mtu kapatikana (lakini sio kichawi, polisi haiusiki na mambo hayo). AU NDIO SERA MPYA YA KUTOKOMEZA OMBAOMBA? MAANA KILA MTU AKIOGOPA KUMSAIDIA OMBAOMBA, ITABIDI WAHAMIE SEHEMU AMBAZO WATAPATA MISAADA.. SERIKALI ILIJITAHIDI KUWAONDOA OMBAOMBA KIPINDI CHA NYUMA, LAKINI WALIPORUDI SISI KAMA WANANCHI TUKAENDELEA KUWASITIRI NA WAKAENDELEA KUSHAMIRI.. SERIKALI ILITAKIWA KUWAOMBA WANANCHI KUFANIKISHA ZOEZI HILO KWA KUTOWAUNGA MKONO OMBAOMBA.. Ila naona hii sera mpya ikiwaingia wananchi kichwani basi serikali itafanikiwa..otherwise, watu wakistukia chezo, ngoma inabaki pale paleeeee....!!

    ReplyDelete
  28. WADAU TUKIO HILI KUTOTOKEA KTK VYOMBO VYA HABARI SIYO KIGEZO MAANA MIDIA ILIKUWA BIZE NA RUFAA YA BABU SEYA NA NEC DODOMA.

    ReplyDelete
  29. Jamani,

    Hii habari na mimi niliisikia,
    watu wengine walipigiwa simu mda ule ele tukio linatokea pale surrender, kila mtu alipigiwa na mtu tofauti, na waliokua wanapiga simu walikuwepo neo la tukio. yaweekana ni kweli limetokea sema tu wahusika hawataki kuliweka hadharani sana kwa sababu wanazozijua wao.

    jambo hili kua uzushi inawezekana ilakwa asilimia chache sana. Nadhani Kaka Michuzi atusaidie kufanya utafiti. Kwa wakati huo huo tusipuuzie tuchukue hatua na kua makini..
    Yesu alififuka wapotshaji walikuwepo ili mradi ukweli usijulikane katika hili tuwe makini pia.

    Asante.

    ReplyDelete
  30. YAANI WEWE NDIO SHETANI UNAKATAZA WATU WASISAIDIE MASIKINI WAKATI DINI ZOTE ZINASEMA TUSAIDIE MASIKINI.

    MCHUNGAJI NA AKILI ZAKE KABISA ANASAMBAZA HOFU KWA WAUMINI KANISANI. LABDA MICHANGO KANISANI IMEPUNGUA SANA ANAONA LABDA WATU WANAWAPA MASIKINI BARABARANI HAWATOI KANISANI.

    HIYO STORY INAWAFAA SANA WANAO AMINI USHIRIKINA NDIO WAOGOPE KUSAIDIA BARABARANI.

    MASHETANI WAPO KILA KONA. JE HUYO DADA ANGEENDA KUNUNUA KITU WAKATI ANALIPA MKONO UKAOTA MANYOYA....JE AACHE KUNUNUA VITU MADIKANI??!!!

    MWAMBIE MCHUNGAJI WAKO AHUBIRI MAMBO YA MAANA.

    ReplyDelete
  31. wewe ulio tuletea habari hii kama ni mtu mzima basi wewe ni unaimani za kichawi au umechanganyikiwa huwezi kuandika ujinga kama huu kwenye blog ya jamii hadisi za kitotoo au ndo kwanza umefika mjini?umetoka huko vijijini mlikuwa mnatishana kwa sababu hakuna umeme basi unataka kutuletea story za kijinga wapumbavu wote mnaesapoti ujingaa kama huuu.

    ReplyDelete
  32. NYIE WATU MNAOBISHA. KWA TAARIFA YENU TU NI KWAMBA HAPO SALENDER BRIDGE NJIA INAYOELEKEA MASAKI MBELE KIDOGO KUNA MBUYU MKUBWA SANA. MKITAKA NENDENI MKAUTAZAME MUONE UNA VITU GANI NDIO MTAAMINI. WAGANGA WA KIENYEJI ENEO HILO NDIO ENEO LAO LA KAZI LA KUTIBIA WAGONJWA WAO NA KUTOA WATU MASHETANI. NAAMINI STORI YAWEZA KUWA YA KWELI KWA SABABU ENEO HILO NDIO KIOTA CHA WITCH DOCTORS.

    ReplyDelete
  33. Upuuzi mtupu.Michuzi usituwekee habari ambazo hazina maana.Dunia ya leo mtu unaamini miujiza,uchawi?Fanyeni kazi kwa bidii,someni, maendeleo si uchawi ni Juhudi binafsi.achaneni na imani potofu.

    ReplyDelete
  34. hivi kuna mtu apa amelazimisha WATU KUAMINI?utajiju unayejidai hujui km kuna uchawi..tunamwamini mungu tuendelee kuasali..mchungaji alititoa mfano km umeelewa habari..acheni kukashifu watumishi wa mungu..POLENI MATOMASO WOTE ILA MNANIFURAHISHA SANA KUJADAI HAMJUI UCHAWI...huamini nenda pale salender police ukaulize..ppl are bize..hamna wa kuja kukuhakikishia

    ReplyDelete
  35. Jamani huyo ombaomba awe anasimama Tegeta, Tabata, Ukonga etc. halafu awe anawagusa watu, watu wambusu ili waweze potoweka huko walipo halafu kutokea tena pale posta mpya, ITASAIDIA SANA TRAFIK. Yamani Waziri wa Miundombinu amtafute huyo jamaa labda ndio solution yetu ya huu msongamano wa magari.

    ReplyDelete
  36. In fact mimi naishi Urusi ni mtanzania niko masomoni. Nimepata hii habari kwa email kutoka kwa ndugu yangu TZ. nikampigia kumwuliza hii habari ni yakweli? akasema hata kwenye vyombo vya habari vimetngazwa. Yaani TV, radio na Magazeti. Kwa hiyo kama watoa maoni wezangu, mimi siwezi kuoment lolote kuwa hilo tokeo limetokea au halijatokea. Cha mhimu ni kwamba Mchungaji hajakataza watu wasitoe sadaka kwa masikini na watoe kwao wachungaji au makanisani tu hapana, alichoshauri, ikiwa hilo tukio nilakweli, inabidi watu tujihami na kutoa toa msaada kwa kila anayeonekana ombaomba mitaani, kwani shetani akitaka kuvuna anachotaka ana uwezo wa kujibadirisha kwa kila aina ya sura ili apate kile alichonuia kukifanya. Kwa hiyo wa Tanzania wezangu tunapopata habari kama hizi jaribuni kuzitafakari kwanza kabla hamjatoa maoni yenu.Picha ninayoipata hapa inaonyesha kuwa watu mmekurupuka kutoa maoni bila kutafakari kwanza.Mchungaji ni kazi yake ya kutoa mawaidha, maonyo,mashauri na tahadhari kwa waumini wake na kwa watu wote watakao kuwa tayari kupokea hayo maoni kwani anafanya wajibu wake. kwa hiyo iwe ni tukio la kweli au si kweli limetokea, mimi naona maoni ya Mchungaji bado yanapaswa kuheshimiwa na kupokelewa kwa moyo wa dhati bila masihala yoyote.kuona kuwa mawaidha ya hii habari ni ya mhimu kwetu sisi, sidhani kama mtu yeyote aliyesoma hii habari,siku akipita Hapo salender bridge akasimama kwenye foleni ndeefu halafu akatokea ombaomba akaja dirishani kuomba kitu je kuna mtu atatoa? hata kufungua dirisha tu mimi siwezi kufungua na ninajuwa wote ni hivyohivyo.Mchungaji ametoa tahadhari kwa matukio yaliyotokea na ambayo bado hayajatokea bado ili yasije yakakukuta.
    Ndimi mtoa maoni mwezenu.

    ReplyDelete
  37. Hii Habari hata mimi nimeisikia.Pia siwezi kusema ni habari ya ukweli ama la,ila tuchukue hii habari kama tahadhari na halazimishwi mtu kutoa/kutokutoa misaada kwa ombaomba.Cha muhimu Habari umeipata,ukiendelea kuwapa misaada bila tahadhani litakalo kupata ni juu yako wewe mwenyewe.
    Mama S,Dar.

    ReplyDelete
  38. Huu ni uthibitisho wa kwamba wabongo wengi ni watu wanaopenda kushabikia habari za kipuuzi,itawezekanaje mambo kama hayo yatokee halafu pasiwepo na taarifa rasmi ya kutoka kwenye mamlaka husika( polisi) ilihali mambo hayo yametokea tena mbele ya mamlaka (trafiki)hizo? kama wabongo wengi mtakuwa na kumbukumbu mwaka 1993 watu walijazana kwenye kituo cha polisi Buguruni kwa uvumi kwamba kulikuwa na mtu amegeuka nyoka baada ya kupewa dawa na mganga, sasa nikikumbuka hayo ya Buguruni nikilinganisha na haya ya sasa napata jibu la mara moja,nyie tuiteni majina yote mnayotaka kutuita lakini ukweli unabaki palepale wabongo wanaoelekea kuwa wengi sasa wamekuwa ni watu wa kusikia na kuamini mambo bila kufanya tathmini so sioni ajabu sana watu kushabikia upuuzi kama huu.Amkeni sasa.

    ReplyDelete
  39. Mtoa maoni wa 18:02:23:00pm.Umesema kitu ambacho hata mimi nakumbuka hiyo ya mtu aliyegeuka Nyoka.Infact bwana usiwe tomaso jamani, Hiyo habari ya nyoka ni kweli ilivuma sana, lakini si wote ambao kweli walishughudia hilo tukio.Wengi waliamini kuwa limetokea na hata hawakuona.Nikiwa mimi ni mmojawapo pia sikuona na tena nilikuwa naishi upanga wakati huo jirani kabisa na Mhimbili.Walisema hilo joka lilipelekwa Mhimbili watu walikwenda kuona.Iliaminika masikioni mwa watu japo wengine hawakuona. Hivyo hata hili swala itakuwa ni ujinga ukikongomalia kuwa ni la uwongo eti kwasababu tu hukuwepo au hukuona au hupati evidence ya kuonyesha kuwa ni lakweli.Unajuwa bwana jambo hata kama nilakweli lakini ukalijengea hoja ya kulipinga litaonekana si la kweli hata kama ni kweli limetokea.Sasa unachobisha ninini? wewe mwenyewe umesema ullikubaliana na mtu aliyesemekana aligeuka nyoka, sijuwi uliona au ulisikia tu ukaamini sijuwi. Sasa mtu kugeuka nyoka ni miujiza au mazingaombwe ya kishetani, hiyo unaamini ilitokea, okay lakini mtu kugeuka mkono wake kuwa na manyoa ya paka na halafu kupotea kimaajabu ambayo pia ni miujiza au mazingaombwe ya kishateni hiyo hutaki kuamini au kukubali kuwa imetokea mbona unashangaza bwana?
    Anyway, kuna events nyingi sana za aina hiyo zimetokea si lazima tuziamini lakini zikitokea ni kuwa na tahadhari sana kama alivyotoa tahadhari mchungaji wa Azania front.Sio uishi kwakutegemea hayao hapana, Jikabidhi kwa mungu kikwelikweli ili hata inapotokea unatoa msaada kwa masikini Mungu aweze kukuepushia balaa ambalo limesemekana limetokea hapo Salender brige au lile lililombadirisha mtu kuwa Nyoka.Siyo kila jambo jema huzawadiwa kwa mema, hata jambo jema mwanadamu ufanyalo huzawadiwa kwa mashida kama hayo yaliyo mtokea huyo msichana.mimi niliposoma hiyo habari nilishituka nikasisimka mwili mzima.Pengine tusubiri labda tutasikia zaidi kwenye vyombo vya habari.Hatujuwi.
    Lakini tuwe makini kwani hili limetokea kwa huyo msichana, je vipi ingetokea kwako bado watu wangekuwa na mijadala hii hii tunayofanya hapa.
    Tusiwe na vichwa ngumu jamani.
    mtoa maoni.

    ReplyDelete
  40. unajuwa jamani kila jambo lina mafundisho fulani, hata kama hilo jambo halikutokea au limetokea kweli, lakini jambo mhimu mchungaji alilolitoa, kwangu mimi nimejifunza kwamba anamaana kwamba, si kila mtu anayekujia kukuomba msaada anakuwa anania nzuri, hata kama kweli anashida anataka umsaidie na wewe unaona kabisa kuwa kweli anashida, inabidi uangalie maramia mia kwa usalama wako wewe.Kwani mwiungine anaweza kukusogelea nakusema anashida ile unamsaidia tu anageuza msaada wako kuwa mateso. Ni kweli alihitaji msaada lakini pia alikuwa anania yake ingine ambayo wewe hukuijuwa.Unakuja kujuwa baadaye baada ya kuumia. Hiyo inakuwa bahati ikiwa bado uko hai, lakini ukipotezwa kama huyu dada wa watu masikini ndiyo hivyo tena. Wewe utapotea lakini ndugu zangu wamebaki na Pengo.
    Ndiyo maisha ya binadamu hapa jamani silazima liwe ni hilo tukio tu, Hata jinsi tunavyoishi. Mtu anakuomba msaada, anaishia kukupeleka pabaya. Be careful ndugu zanguni si kila waombao kusaidiwa wanahitaji msaada, wengine wanazaoi jambo.Roho za kishetani tunaishi nazo humu humu jamani.Utazigunduaje? kwa matendo yake, utazikwepaje? sikiliza Mchungaji Azania Front.
    Kuna watu wanasura za kibinadamu lakini roho zao ni za kishetani, ni maagent wa au mawakala wa kishetani kabisa.Utawajuwaje? matendo na maneno yao.
    Utawakwepaje? Shika wosia wa Mchungaji AZANIA.
    Ahsanteni sana ndugu zangu. Mimi ni mbongo mwezenu niko ITALY.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...