supa staa wa filamu za bongowood Steve Kanumba 'The Great' anaibuka na toleo jipya hivi karibuni liitwalo THIS IS IT.
Kwa habari kamili ya toleo hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. kwenye web yake nimeona ''this blog sponsored by'' mshkaji unakanumba hata kwenye blogging!!!! kweli we kiboko
    halafu mnatoa filamu kama njugu mawe hizo ni falam au comedy. hauko serious wewe kanumba.

    ReplyDelete
  2. Ankal!

    samahani kama nitakuwa si mfurahishaji kwa hili swali na mtizamo wangu,..Hivi hiki kinachofanywa na msanii huyu na mwenzake ray ni kukuza sanaa ya filamu au kuiua? Maana kwa mwaka msanii mmoja anaachia muvi 10 kweli ni sahihi? au ndiyo tamaa ya sisi binadamu ya kuangalia leo na kesho sina habari nayo?...mimi hii inaniuma sanaaaaaanaaaaaaaaa,kwani kwa kufanya hivi hakuna kitakachoendelea Tz kwa staili hii...plz michuzi kuwa mshauri wa kweli kwa kijana huyu kwa kumwambia atengeneze muvi nzuri na yenye vingi vipya na vya ajabu ,pia kuliandaa soko lake na promo iliyopangika kisha toa muvi moja ya kweli uza vizuri pata faida kubwa lisaidieeni soko na si kugeuka MURDER INC crew.....ili siku kweli aitwe Kamumba ze gret na si ya kujipa mwenyewe au na wewe Michuzi.

    Si Mimi.

    ReplyDelete
  3. This is it??....ur joking...buni jina lako mwenyewe bwana mnaiga iga tu why????

    ReplyDelete
  4. KANUMBA BABA JARIBU KUBUNI VYAKO THIS IS IT MUACHIE MAIKO JAKISONI, achana na mambo ya kukopi.

    ReplyDelete
  5. Movie mpya kila weekend! huo ni ulimbukeni wa ajabu.. Aisee jamani shule muhimu.Wazazi jitahidini kuwapeleka shule watoto wapate elimu nzuri manake hii mifano halisi ni changamoto.

    ReplyDelete
  6. Cover ya hiyo movie inavutia. Naomba kabla ya kumlaumu Kanumba kuwa kwa mwaka anatoa movies nyingi tukumbuke kuwa hii industry Tanzania bado inakuwa. Hivyo kama kuna mapungufu tuwape wasanii wetu ushauri na si kuwalaumu.

    ReplyDelete
  7. Anko, mimi naona Kanumba (the great fake) anapotoka na kwa kweli si tu kwamba anachemka bali ANATEKETEA KWA MOTO!! Hiwezekani ukatoa movies 5 ndani ya mwaka mmoja...hivi hizi ni movies au ni "short plays"?? Kama magwiji wa filamu wanatengeneza movie moja kwa miaka miwili hadi mitatau inakuwaje sisi tunatoa movies 10 kila mwaka?? Ndiyo maana mimi nashindwa kuona quality katika kazi zake na za wasanii wengine wa filamu hapa nyumbani!! Nashindwa kutofautisha maudhui na matukio katika picha zake...kwa kifupi ni ZERO!! Halafu kana kwamba hiyo haitoshi bado tunaiga majina...kwa nini hatuwezi kuwa wabunifu??...eti "THIS IS IT"!!! MJ alikuwa amedhamiria kurekodi kitu cha kuaga music industry na ndiyo maana aliandaa maonesho 50 ya kufunga kazi kabla mauti hayajamfika....that is why he called the tour "this is it"...nia yake ilikuwa ni kuwaambia wapenzi wake kuwa hii ni kazi niliyoiandaa maalum kwa ajili yenu na kuaga!! Sasa Kanumba hawezi hata kubuni jina lake mwenyewe?? Kwa kweli ni kero tupu....hana jipya ni michosho tu

    ReplyDelete
  8. Mnatania kazi za watu, kwanza cinema zote zinazotengezwa tanzania, wachezaji wote badaya ya kuogea kawaida kama watu wanaofanya wanaogea makazi ay mahali popote wao wanatumia namana watu wanaongea mashairi. pili kabla mtu ajatoa cinema lazimahafanye uchunguzi yaani reseach kuhusu hiyo cinema kama hii THIS IS IT, kanumba mwenye ni mnene kwenye cinema yenyewe actor ni mwembamba na pia background sound inakuwa inakuja na kupotea au mziki unasikika kwa sauti kubwa huku actors wanaogea .. je hawa mactors wote wamesomea wapi maana sio unakuwa mwamuziku au models na kuamua kua actor kwa sababu unajulikama an unajua kuogea ..jamaa hii ina vipaji na pia watu wanaonda kusomea fani hii. asante kwa kunbipa nafasi hii

    ReplyDelete
  9. Kwenye filamu za kibongo wanaongea kiswahili lakini jina la movie ni la kiingereza. KWANINI? MI SIELEWI KABISAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Kaka misoup mimi kama kama m-tz ninayependa movie za hapa sasa december katoa movie mbili kwa mpigo baada ya mwezi mmoja anatoa ya pili, kwa bongo industry movie ni mwezi mmoja tu ndoo maana ubora sio kabisa.

    ReplyDelete
  11. Kanumba endelea na kutafuta maisha kwa jasho lako. Hao wanaokusakama wamefanya nini katika jamii kikaonekana? Tena chondechonde 'kwenye riziki hapakosi fitina' Kaza buti songambele. Maendeleo yanakuja kwa kukopiana. Ila mwisho nakushauri pia ujiendeleze na masomo ya juu maana ulimwengu wa sasa elimu ni kitu kinachothaminiwa sasa. Huko tunakokwenda jamii itaanza kuwa inachagua filamu kutokana na upeo wa aliyeitengeneza. Zaidi ya hayo everthing is great. Keep it up

    ReplyDelete
  12. Mtaka MazuriFebruary 26, 2010

    ankal na wadau wengine habari zenu?
    kwa kweli mi siongei sana but namshauri kanumba before afanye huo ufilm wake aconsult lawyers, hiyo jina ni ya Wacko Jacko, na hiyo kitu ina amount to copyright infringement, au ndo mambo ya bongo tambararez??

    ReplyDelete
  13. YAANI KWELI MMEKOSA JINA NA KUITA THIS IS IT???????????????????REAL ACHENI MAMBO YA KUIGA YAANI INATIA KICHEFUCHEFU.

    ReplyDelete
  14. kanumba kama umeshindwa kuenzi ubora wa fani za watu ni bora urudi kwenu kijijini. ndani ya miezi 2 movie 3?? what's that!!! that's crazy man u r not serious. tatizo ni nini??? ni tamaa ya pesa au??? hebu kuweni serious bwana acheni tamaa za kijingajinga. halafu kutafutia umaarufu hapa michuzi blog uache uwe unatokea kwenye blog yako sisi si vichaa wa kuja kututangazia uzinduzi wa movie ya tatu ndani ya miezi mitatu hapa michuzi. tupo nje huku wenzio wanakaa miaka mitano wanaandaa movie moja na likitoka linakuwa hit. unaona movie za tangu miaka ya themanini hadi leo bado unaziangalia na kuzipenda zinavutia sababu wenzio walifanya kazi. mimi nimeanza kuangalia coming to america ya eddie murphy nikiwa mdogo lakini leo nakwenda dukani nainunua bado, vile vile za wacheza movie wengine, sasa wewe ukiniuliza jina la movie yako uliyoicheza mwezi wa tatu mwaka jana hata jina tumeshalisahau sababu hazina ubora wowote hazivutii kuendelea kuangalia na kuangalia na kuangalia sababu ya ubora kisa tamaa zenu za pesa mnashindwa kuandaa vitu vyenye ubora. halafu mnajiita ma superstar wa bongo huo ni usupastaa gani kama movie yako inasahaulika ndani ya miezi 2?? au kama unaweza towa movie 3 ndani ya 4 months??? hamna usupastaa wowote superstaa hapo ni michuzi tu anajulikana dunia nzima na blog yake watu hawaichoki kila siku miaka nenda miaka rudi sasa nyie movie zenu unaangalia leo kesho unamuachia mtoto achezee sababu hazina ishu.
    nadhani umenielewa kama hujanielewa shauri yako kaeni hivyohivyo na mkumbuke ukimwi manake nyie wasanii wa nyumbani huko mnavimba mabichwa yenu mnabaki kusasambuana kila kukicha.
    michuzi nawe usinibanie apate ujumbe wa huyo.

    ReplyDelete
  15. yaani wadau ni kweli mnavyosema kwa mwaka mmoja huwezi kutoa movies zaidi ya 10,lakini huu wakati tuliokua nao ni biashara tu na si jengine mdau nchi za nje.

    ReplyDelete
  16. kuhusu kutoa movie kama njugu hilo hata mimi si liafi hii inaonyesha kwamba hawafanyi uchunguzi ama marejeo na utafiti wa kina wa stori wanayotaka kutueleza na hii ndio sababu unapoangalia film zakibongo lazima utaboreka,lakini kuhusu jina this is it je mna laumu kwani stori ina husu music ama.......kama aihusu music basi sio isue ya kulaumu

    ReplyDelete
  17. Kwa mara ya kwanza naona poster ya Movie ya Kibongo ni nzuri, ila imenibore Jina la movie, , anyway huwa siangalii hizi movie sababu zina makosa na uigaji mwingi kiasi baada ya kuburudika una shikwa na hasira , hakuna ubunifu . Ila na dhani zina walengwa wake ambao zina waburudisha ndio maan una weza ona mtu anatoa movies 3 kwa mwezi sababu ya soko lipo kwa watu fulani.

    ReplyDelete
  18. Tangu zianze filamu za James Bond mwaka 1962 hadi kufikia 2008 zimetoka filamu 22 tu(miaka 46!)zikiwa na thamani ya dola Bilioni 4.81. Kanumba kisha toa filamu ngapi tangu aanze mambo ya filamu?Je kama uigizaji filamu unalipa hivyo huku wakiwa na backup ya Teknolojia watoa filamu za James Bond siwangeshafyatua hata filamu 100 hadi sasa? Mi nadhani Tanzania bado hatujaaanza kutoa filamu nadhani hizi tuziite Michezo ya kuigiza tu kama kidedea au Tausi n.k kwani humu muvi nzima waweza angalia bila hata kuona glasi inavunjika! Yaanihata mtu kuchaniwa shati hamna! Watu wana igiza kama watu wa enzi ya utumwa kichwani nywele zina dawa? Kweli watu wa zamani walikua hivyo?Mtu ana igiza katoka jela kichwani ana wave au rasta ? Hizi ndio Bongo fleva zetu jamani,ila wakumbuke kwamba vumbi likitimka hutua chini mvua ikishanyesha hakuna vumbi tena

    ReplyDelete
  19. this is it ushuzz kuiga tuu tafuteni vya kwenu na mkiiga mvilipie ebo na ungeweka upuuzi huu kwenye blog yako vile haina wateja kutuletea shobo huku kwa michuzi manake unajua hii blogu ni dunia nzima ndo mana mnaletaga matangazo yenu ya biashara si mna blogu zenu?? michu blogu inabamba sana kuna watu ati na wao wana viblogu basi hakunaga comment zimelala doro jamani sio kila mtu lazima awe na blogu wengine tuwe tunachangia mada viblogu vingine vimenyambaaaa hadi basi iga ufe!!

    ReplyDelete
  20. kaiga hadi staili ya maiko j kushika watoto kofia uvaaji hupendezi msanii kuwa mbunifu na hayo maigizo yenu mnayoyaita movie nendeni hata kwenye school of arts mkaongezeongeze ujuzi manake bado saaana ati kuna siku mcheza maizo mwenzenu akadai ati nyie ni kama kina van dame nilicheka nusu nizimie kuonekana kwenye movies uchwara ujifananishe na van dame denzel washington ni upuuzi wa hatari!!!

    ReplyDelete
  21. hivi na nyie hizo mnazieta movie??? mtakuwa mnachekesha .mi sema kweli siweZi na sijawahi kuangalia hizo mnazo hita movie.lastly wewe kanumba kujiita the great hinaonesha jinsi gani ujakwenda shule.acha kutuletea unumba numba hapa.wewe ni mchezo comedy si films kaka wewe ni wakutengeneza short comedy tv films is MOVIES kama unavyo jitapa.

    ReplyDelete
  22. Kaka Michuzi mimi ninasikitika sana na watunzi nawacheza filamu za bongo nimejaribu kuangalia filamu zao kweli inatuabisha sana Watanzania na kutoonyesha kanakwamba hatuna ujuzi au tumevamia fani ambayo sio yetu.
    Mimi ni najua kuna watu wengi wenye ujuzi wa filamu, ila kwamtindo huu "THIS IS IT" sio ishu kabisa.
    Mi ningewaomba Watanzania wote tuungane pamoja kuzigomea kwa kutokununuwa hizi filamu za Kitanzania ambazo hazina ujuzi wowote ndio wataelimika.
    Inaniuma sana tena sana. Asante

    ReplyDelete
  23. kanumba na swahiba wako nabii yohana mbona haujamuweka kwenye kamuvi kako?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...