kwa mbele
katikati
ufukweni

Broo Michuzi
Sijuwi njia gani nitumie ili niweze kutangaza kwenye glob hii ya jamii kwa hiyo nimeamua kutuma email hii na natumai dhumuni langu litafanikiwa. Tafadhali naomba uniwekee tangazo hili kwenye glob ya jamii.

Tunauza kiwanja maeeneo ya bwejuu Zanzibar Kiwanja chenyewe ni beach plot kipo beside Palm beach hotel Bwejuu Zanzibar.

Muuzaji ndie mmiliki mwenyewe hakuna mtu wa kati (dalali ) kina hati miliki na kimelipiwa ada zote. Kwa yoyote anaehitaji tafadhali wasiliana na number 0777414185 or 0715414186

Pia nimeweka picha kidogo
hapo juu za kiwanja chenyewe
Ahsante sana
Mdau Bwejuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. sasa mbona tunataka kuziana ufukwe wa bahari? vipi tena ?

    ReplyDelete
  2. na milioni mbili na nusu naweza pata .hichi kiwanja nimekipenda sana/

    ReplyDelete
  3. mdau hakuna dhumuni.Neno madhumuni halina umoja.....ni kama maji.wanipata?

    ReplyDelete
  4. kiwanja kina ukubwa gani ??? usijibu kama ?? taja kipimo kwa mita au futi .sheria ya mipango miji ni kuanzia baharini hadi mwanzo wa kiwanja lazima kuwe na mita 60 , je hii sehemu ya uwazi ipo ??

    ReplyDelete
  5. MBONA TUNAUZIANA MCHANGA WA PWANI, THAT IS NOT A PUBLIC PROPERTY?

    ReplyDelete
  6. Tue 02, 02:03:00AM, SHOULD HAVE WRITTEN (IS THAT NOT A PUBLIC PROPERTY?) angalau na wewe unainukia lakini ni vizuri ungetumia kiswahili tu kwani nacho kina njia ya kuuliza swali. Mimi ninashauri uuziwe wewe hicho kiwanja kwani inelekea wewe ni chotara wa kigiriki.

    ReplyDelete
  7. Picha zinaonesha ufukwe lakini Kama utaangalia picha ya kati utaona ni kiwanja ambacho kimezungushwa ukuta na Kama nilivyoeleza kina hati zote za kisheria na pia kipo umbali WA Mita 60 kutoka ufukwe WA bahari pembeni ya kiwanja tayari ipo hoteli ya Palm beach, hii plot inawezq kuingia 3/4 banglaw na pia ni nafasi nzuri kwa uwekezaji. Yoyote aliye na masuali au anataka kujuwa zaidi anipigie kwenye simu zangu kwa mazungumzo ama ukaguzi

    ahsante
    Mdau bwejuu

    ReplyDelete
  8. Ukubwa wa kiwanja ni 1250 square meter

    Ahsante
    Mdau

    ReplyDelete
  9. Sehemu nimeipenda sana Beach front
    Hapa ndio nataka nizeekee

    ReplyDelete
  10. HAHAHAAH MBONA TUNAUZIANA MCHANGA WA PWANI SI PUBLIC PROPERTY? NIMEIPENDA HIYO HAHAHA TUNAUZIANA TUSNAMI NAONA. ILAK UMBUKENI SIKU HIZI SERIKALI NYUMBA ZA PWANI KAMA HAPO WANATAKAK UKATAZA KUJENGWA ZITAANZIA KULE KWENYE NYUMBA YA BATI JEKUNDU NDIO MWISHo. SEIF WA MALINDI.

    ReplyDelete
  11. wabeba box !kiwanja kinauzwa jamani,mtakuwa nafikia kwa ndugu zenu mpaka lini? mnatukela wezenu kwa vijitabia vya kufikia kwa ndugu

    ReplyDelete
  12. WEWE UNAKOSOWA BURE HIYO ENGLISH WEWE NDO MWENYE MAKOSA UKISEMA "IS THAT NOT A PUBLIC PROPERTY?" UNAMAANISHA UNAHUHAKIKKA KUWA HICHO KIWANJA NI MALI YA PUBLIC, YULE ALIYEULIZA "THAT IS NOT A PUBLIC PROPERTY?" YUKO SAWA HANA UHAKIKA N=KUWA HICHO KIWANJA NI MALI YA UMMA, KUNA TOFAUTI NA KUULIZA KWA MFANO "THAT IS NOT MINE" NA "IS THAT NOT MINE" WA KWANZA HANA UHAKIKA KAMA HICHO KITU NI CHAKE NA WA PILI ANA UHAKIKA KUWA HICHO KITU NI CHAKE. USIKOSOWE KABLA YA KUFIKIRI KIUNDANI KWANZA!!!!

    ReplyDelete
  13. Wote mkosea, ingawa wa mwanzo alikuwa sahihi zaidi. "Is that not public property? "That is not public property?" inatumika lakini siyo grammatically correct, kwa sababu ni statement ambayo inaishia na question mark. Msingi kueleweana kwa sababu hata wenye lugha wanafanya makosa hayo hayo na wanakereka ukiwarekebisha.

    ReplyDelete
  14. WATANZANIA YOU ARE AGUING SO MUCH FOR NOSENSE, I DON'T SEE THE KIWANJA HAPO KWA WALE WANAOPENDA KUBANAN MTAONA NI KIWANJA, HICHO KIJIENEO NI CHA KUTENGENEZA BARABARA HAPO MTAANI ILI WENYEJI WAWEZE KUPITISHA MAGARI, MTU AKIJENGA NA HAPO MAGARI MTAPITISHA WAPI AU NDIYO MKAO WA KUPAKI KWA MJUMBE? PLEASE!!!

    ReplyDelete
  15. hahahaa wee mdau unaekandia wabeba box kuzamia kwa watu waludipo home!!hahahahaaaa uwiii yani umenchekesha cjui umewaza nn?

    ila duh uwanja pembeni mwa bahari?afu tambarare ivo tsunami ikija apo kwishnei,,,bora kingekua mlimani ivi

    ila poa utapata mnunuzi

    ReplyDelete
  16. TUJITAHIDI KUJUA SHERIA ZA UUZAJI ARDHI NA ARDHI NI MALI YA NANI, ANGETANGAZA ANAUZA SHAMBA ISINGEKUWA SHIDA LAKINI ARDHI SIJUI! BONGO WOTE TUNAJUA KUSEMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...