Hayati Mchungaji
Aaron B.C. Mabondo
Nimevipiga vita vilivyo vizuri,
Mwendo nimeumaliza, Imani
Nimeilinda. 2 Tim 4:7

Leo 04/02/10 ni mwaka mmoja toka Baba yetu mpendwa Mch. Aaron B.C. Mabondo wa Kibaha Picha ya ndege alipotutoka katika mwili. Mioyo yetu ina huzuni kumkosa lakini tunajua siku moja tutamuona Mbinguni.

Hatutamsahau baba yetu kwa malezi ya upendo
wa kiroho na kimwili aliyotupa, tumejifunza mengi kutoka kwake.

Kwa niaba ya familia ya Mabondo tunapenda kuwashukuru watu wote ambao wameendelea kuwa faraja kwetu na hasa kwa mama katika kumtia moyo kwa njia mbalimbali. Mungu awabariki na kuwazidishia upendo huo kwa wengine pia.
tangazo la msiba huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hayo ni maneno ya mtume paulo kwa mwanafunzi wake timotheo

    ReplyDelete
  2. Oh no, sikuju kuwa mzee Mabondo alifariki last year, he was such a great man aliyemtumikia Mungu kwa uaminifu. i remember jinsi alivyotutia moyo wakati marehemu baba yangu alipofariki; alitusalisha sala ya baba yetu uliye mbinguni, akatuambia kuwa tunaposema 'mapenzi yako baba yatimizwe', tunatakiwa tumaanishe hivyo. maana yake ni kuwa ni mapenzi ya Mungu kumchukua baba yetu, hivyo tuache mapenzi yake yatimizwe; sijawahi kumsahau mzee mabondo ever since, kila nikisali baba yetu huwa namkumbuka huyu mzee, na hii ilikuwa mwaka 1988! Mungu aendelee kuipumzisha roho ya mzee mabondo na mzee tarimu mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana. Kweli ninyi mmebarikiwa sana kuzaliwa na baba kama huyu. Nilihudhuria semina zake za mafundisho ya biblia pale arusha mwaka 1993. Hadi leo nakumbuka alisema, "Mungu hutusamehe makosa yatu kwa sababu zake Yeye mwenyewe" Siwezi kumsahau, He was great man of God!

    ReplyDelete
  4. heee alikufa mwaka sasa???siamini
    jamani huyu mzee nilikua sekondari o-level miaka ya 90 mwazo nilikua sikosi semina zake za mguso

    aisee Mungu azidi kuwatia nguvu na kuwaongoza wafiwa

    amen

    ReplyDelete
  5. Bwana Asifiwe kwa utumishi wa wazee kama huyu. Walimtumikia Mungu bila utata wala skendo za kumwaibisha Mungu mpaka mwisho wao. Sisi watumishi vijana tuige mfano huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...