bad card
Nabii wa Reggae hayati Robert Nesta Marley aka Bob Marley alizaliwa 6 Feb 1945 kule kijijini St.Ann, kisiwani Jamaika aka jah make yah!
Hakuna asiye jua kuwa Bob ndie super star wa kwanza ktuoka ktk nchi masiki kama zinavyiitwa nchi za dunia ya tatu! super star huyu ambaye jina lake aliwezi kusaulika kwa kazi yake iliyozaa matunda ya kueneza mziki wa reggae dunia,njia ambazo alizotumia ni gitaa, na kanda za kaseti aina C90 ambazo limepenyeza mziki huo katika mipaka ya kila nchi. mziki wake huo wa Reggae ulifika mpaka katika nchi za kiafrika kwa kupitia kanda za kaseti C 90 au C60.

Bob Marley kama leo angekuwa hai basi angesherekea siku ya kuzaliwa.
Je? leo hii tunateknolojia nyingi mbona wanamziki wengi wamekuwa wavivu kutangaza kazi zao? je tujifunze nini kutoka kwa marehemu Bob Marley?(RIP)

Mdau Jah Pipo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hayati Robert Nesta alijitofautisha na wanamuziki wengi kwa kutoa nyimbo nyingi za kile alichokiamini. Ukiamini kitu ukakiimba wengine wanaweza kukiamini kwa urahisi kuliko ukiimba wimbo wa unachodhani watu wanaamini. Alitoa nyimbo nyingi lakini tofauti na wanamuziki wengi, nyimbo zake hazifanani na ukisikia nyimbo zake kadhaa basi hata ukisikia wimbo usioufahamu unaweza kuhisi ni Bobu. Aliamini katika dunia isiyo na ubaguzi (War), kujitegemea (so jah seh, get up stand up), umoja wa Afrika(Africa unite, Zimbabwe), kuhalalisha jani (easy skanking). Pia alipenda mapenzi (stir it up, she's gone).
    Utafanya marketing kadri uwezavyo lakini kama unauza bidhaa feki za China kuna ukomo wa kuuza bidhaa zako. Lakini kama unauza bidhaa za kueleweka ni kiasi cha kuwaonyesha tu watu bidhaa zako nao wataichangamkia. Chema chajiuza.

    ReplyDelete
  2. Tunaruhusiwa kuvuta bangi siku hiyo???

    ReplyDelete
  3. bila kusahau mjani

    ReplyDelete
  4. Hands down, Bob is a true Legend.

    Mpambika

    "Destruction of the poor is in their poverty. Destruction of the soul is vanity." Bob Marley

    ReplyDelete
  5. Kabla ya Bob Marley alikuwepo Jimmy Cliff ndie star wa mwanzo aliyeendeleza Reggae duniani.

    Bob Marley alipata umaarufu baada ya kufariki.

    Na May 11 ina uhusiano gani na Bob Marley?

    ReplyDelete
  6. Kuna tofauti kubwa kati ya Jimmy Cliff na Bob Marley.Bob Marley anapendwa kwa sababu yeye alikuwa "true revolutionary rasta",freedom fighter(musically).Sikiliza lyrical contents za Jimmy Cliff halafu usikilize za Mzee mzima Bob...acha wee!."No more internal power struggle,We come together to overcome the little trouble,And soon we'll find out who is the real Revolutionaries(wewe unafikiri nani aliwakomboa wazimbabwe!).Halafu ipate hii,"until the color of a man's skin,Is of no more significance than the color of his eyes(WAR).Nampenda Jimmy lakini Bob's shoes are too big for him.

    ReplyDelete
  7. Hakika Bob-Marley was the highest priest of reggae, ni kwamba hakuwa mwanamziki peke yake bali alikuwa mwanasiasa na alipeleka ujumbe wake kupitia muziki.
    Tofauti na watu wengi ambao Baba ni mzungu Mama mwesi wengi hujiita wazungu lakini Bob alisimama kwa mtu mweusi na ndio maana tutaendelea kumkumbuka daima.
    (RIP).

    ReplyDelete
  8. Mzee Kifimbo ChezaFebruary 05, 2010

    wewe Jah People,jifunze vizuri kuandika kiswahili,au na wewe unatumia mmea kama hayati Bob Marley?Mziki ndio nini?hua wanaita Muziki,usirudie tena kutuandikia vitu halafu una post,soma kwanza kabla ya ku post, urekebishe makosa ktk uandishi wako.

    ReplyDelete
  9. true leggae legends to have lived under the sun
    1. Hayati BoB Nesta Marle
    2. Lucky Dube
    baaasi, finish. hakuna mwengine ni hao tu na ni hayo tu.

    ReplyDelete
  10. HE WAS LIKE A MESIYAH WHAT HE SAID IS REAL AND WITH 5 YRS U WILL SEE ALL THOSE RIPING US EPECIAL MPS ANT ALL THOSE INTERNAL HAVE BAD INTETION TO THE SUCSSES OF OPPRESED PERISH WITH NATUAL MYSTICS

    TZFORCHANGE

    ReplyDelete
  11. Yaani wee unaejiita "Mzee Kifimbo Cheza" badala ya kuandika kuhusu topiki ya Bob unaandika ujinga wa kukosoa kiswahili cha mtu.Wewe unasoma comments za watu kutafuta ugomvi!hide your foolishness acha ujinga na roho yako mbaya!.Bob Marley we love my brother!

    ReplyDelete
  12. "We know you are a big tree and we are a small axe we gonna chop you down"!

    "We need another version and not another session" (Mix Up Mix Up)!

    "In the eyes of the wise, the fool is size"!

    "Until the philosophy which holds one race superior and another one inferior is finally distracted and abondened...and we know we shall win as we are confident in the victory of evil"

    Mwanangu Robert Nesta Marley you were taken from us at such a young age (36). RIP

    ReplyDelete
  13. anon unayeuliza "May 11 ina uhusiano gani na Bob?" hiyo ni tarehe na mwezi Hayati Bob alipotutoka.

    hakika alikuwa Godfather of Reggae.

    ReplyDelete
  14. Anonymous no 6 labda ulikuwa hujazaliwa lakini kwa sifa zote Bob Marley hakuhusika na kuikomboa Zimbabwe.

    Ile nyimbo yake ya "Africans liberate Zimbabwe" aliimba siku ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe ambapo alialikwa na ndio kwa mara ya kwanza (nadhani na ya mwisho kwani alifariki miezi michache baadae) alikanyaga Afrika.

    ReplyDelete
  15. Mzee Kifimbo Cheza amenifurahisha sana. Kweli nyani haoni ku***le. Amekosoa maandishi ya Jah People wakati naye lugha inampiga chenga. 'Hua' ni ndege wengine husema njiwa. Bila shaka alitaka kusema 'Huwa' wanaita muziki. Isitoshe ameandika kwa kuchanganya lugha. "kutuandikia vitu halafu una 'post'"? Kulikuwa hakuna hata umuhimu wa kutumia neno la kigeni. Ukisema anatuandikia vitu tayari ujumbe unafika maana tunaviona "globuni" :).

    ReplyDelete
  16. Hongera Jah Pipo kwa kutuletea kitu kisicho saulika!japokuwa mdau
    Kifimbo cheza,hana la kufanya zaidi ya kutia nuksi ktk heri.
    watu kama kifimbo cheza wamekosa mtazamo wa mawazo safi..baadala vichwa vyao vimejaa utumbo na pumba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...