Mwaandaaji wa onyesho la Mavazi la Lady in Red kutoka Fabak Fashions Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsi (kati) akizungumza na wanahabari leo asubuhi ndani ya hoteli ya Regency Park, kuhusiana na onesho hilo ambalo limepangwa kufanyika siku ya jumamosi Februari 6 kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempiski Hotel. Kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 20,000/= kwa kila kichwa. Kulia ni Mmoja wa wabunifu mahiri hapa bongo Ally Rhemtullah,Muwakilishi wa kampuni ya Darling Julius Ngatunga na shoto ni Muwakilishi kutoka New Habari House Peter Mwendapole.
Asia amesema kuwa katika onesho hilo kutakuwepo na burudani kabambe kutoka bendi ya Machozi Band ikiongowa na Lady Jay D pamoja na kikundi cha ngoma za asili Simba Traditional Dance.
Amesema wabunifu 16 mahiri wataonyesha ubunifu wao wa mavazi ambao ni Faruk Abdella, Manju Msita, Khadija Mwanamboka, Ally Rhemtullah, Mustafa Hassanali,Zamda George,Jamila Swai,Gymkana,Farha Sultan,Baraka, Fransisca, Bianca, Hiari, Joice, Salim Ali na Martin Kadinda.
Aidha Mwaandaji huyo ameongeza kuwa katika mchakato huo pia kutakuwepo na tuzo ta mbunifu bora wa mwaka 2010,tuzo ya Miss Beauty with purpose.Kama vile haitoshi kutakuwepo na mnada kwa ajili ya kusaidia/changia watoto yatima wa Mitindo House pamoja.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Darling Hair,Redd's,Utrack Total Control,Valye Spring,BenchMark Production,Sofia Produtcions,Michuzi Blog,Kitangoma Magazine,Zizzou Fashions,Jiachie Blog,8020 Blog,Kitangoma Magazine,Clouds Fm na wengineo kibao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...