Ankal thenk yuu veri machi kwa kutupa nafasi wadau kukutana na kuyaaanika mamabo yetu mengi. Nimekutana na hilitukio juzi nikitoka kazini. kwenye picha nilizo attach utaona kuna kijana amelala barabarani, usidhani kagongnwa na gari au kaanguka bahati mbaya noo.
Huyo ni mmoja wa vijana wanaoitwa wa mitaani huku wamezoeleka kama Chokoraa. Hapo alijilaza makusudi na baada ya uchunguzi wangu nikagundua hataki kuamka mpaka apewe chapaa ya msosi. Eti anadai njaa imezidi. mambo ya gudi ankal, si unajua tena?. Picha na habari na Mdau Munisi from R-Chugga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. This iz veri sirias. What kind of an adult will this guy be?

    ReplyDelete
  2. Omba Omba HALEI MTOTO ATAKAYE JITEGEMEA..KAMA TAIFA NI OMBA OMBA USITARAJI WANANCHI WAWEZE KUJITEGEMEA..

    ReplyDelete
  3. Tue Feb 09, 05:56:00 PM una akili sana wewe sema tofauti yake huyo dogo na wengine ni usafiri wake wa asili(miguu) na mavazi(jeans). Ameiga mfano bora
    ogopa sana kuja kuuliza hilo swali na kujibiwa kwani wewe huwa unafanya nini unapokwenda huko? na tuna tofauti gani na wewe?
    sasa sijui na wao mtoni wakianzisha ile oparesheni ya kuondoa omabaomba kwa nguvu sijui itakuwaje???

    ReplyDelete
  4. Ninakubaliana na mdau mmoja wa globu hii ya jamii aliyesema kuwa "nchi hii imeishauzwa, acha kila mbongo ajifanyie anachoona kinamfaa!!"

    ReplyDelete
  5. Anon wa pili (05:56:00), Wananchi wanaweza kujitegemea hata kama nchi yao inapewa misaada. Usikuze utamaduni wa uvivu na kutafuta visingizio visivyo na msingi. Mimi ninatoka Arumeru na ninaishi Arusha lakini nitakuwa wa kwanza kukuambia kuwa wengi wa "machokoraa" wa hapa wanatoka katika familia ambazo zimeathirika na ulevi na ukatili (mababa alcoholic wanaowapiga mama wachapakazi na watoto na kupeleka pesa kwenye pombe). Tukiendekeza uvivu, ulevi, wizi na uongo tutabaki kungoja riziki yetu itujie kimiujiza na isipokuja kimiujiza tutakuwa kama wewe: "Walaumu wengine". Naomba nijibu: MBONA MAJORITY YA WATU WA MKOA HUU NI WACHAPAKAZI SANA NA SI MACHOKORAA UNAOWATAFUTIA VISINGIZIO VISIVYO NA MSINGI. Ukishindwa ntajua wewe ni mmoja wao hao machokoraa. Ndokwaruu.

    ReplyDelete
  6. tunarudi pale pale mjomba michuzi mrefu wa mbilikimoe huwa mbilikimo je mrefu wa omba omba huwa nani????swali kwa mkulu pale feri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...