
Pichani kutoka kushoto, Juma Omary(Drums/uimbaji),Mohammed Mrisho (Gitaa/uimbaji), Mabrouk Omary 'Babu Njenje'( Mwimbaji), Waziri Ally (Keyboards/ uimbaji), Marehemu Chuky, Keppy Kiombile(Bass /Uimbaji).
Hii ni lebo ya santuri mojawapo ya zamani.
Katika miaka hii kulikuwa hakuna wizi wa kazi za sanaa kama ilivyo sasa. Teknolijia ilikuwa haiwezeshi mtu kukaa chumbani kwake na kunakili kazi za watu. Haya na mengine mengi yanapatikana katika libeneke jipya la mwanamuziki mkongwe John kitime liitwalo Wanamuziki Tanzania.
BOFYA HAPA

Katika miaka hii kulikuwa hakuna wizi wa kazi za sanaa kama ilivyo sasa. Teknolijia ilikuwa haiwezeshi mtu kukaa chumbani kwake na kunakili kazi za watu. Haya na mengine mengi yanapatikana katika libeneke jipya la mwanamuziki mkongwe John kitime liitwalo Wanamuziki Tanzania.
BOFYA HAPA
JAMHURI JAZZ BAND WALIKUWA WANAIMBA NYIMBO NA UNAJUWA WANAMAANISHA NINI. SIO NYIMBO ZA SASA HUJUI ZINA LENGO GANI. NAKUMBUKA BENDI YA JAMHURI ILIVYOKIWA IKITIKISA TANZANIA NZIMA NA AFRIKA YA MASHARIKI. YUSUF NA RAJABU, SIWALE , HALFANI NA WENGINE. BILA YA KUWASAHAU ATOMIC JAZZ BAND AMBAO PIA WALIKUWA WAKICHUANA SANA NA JAMHURI PALE TANGA. NAKUMBUKA ATOMIC WALIKWA WAKITIA ZOEZI BARABARA YA 3 NA JAMHURI BARABARA YA 16. JEE KUNA HABARI ZAO WOTE HAO? AKINA JOHN KIJIKO NA WENGINE.
ReplyDeleteJAMANI TUSIPENDE KUANDIKA TUSIYOYAJUA, SIKWELI KUWA ZAMANI WAKATIWA MATUMIZI YA SANTURI HAIKUWEZEKANA KUKOPI WAPO WENGI TU WALIOKUWA NA TEPU REKODA WALIWEZA KUFANYA HIVY NA HATA REDIO TANZANIA ILIKUWA MOJA WAPO YA WALIOKUWA WIKOPI PIA MULNGA REKODING'I STUDIO YA KAKOBE ILIKUWA MOJA WAPO KATI YA STUDIO NYINGI ZILIZOZAGAA MITAANI. INAWEZEKANA MWENZETU ULKUWA BADO UKO SHAMBA HATA HIVYO JOGOO LA SHAMBA HALIWIKI MJINI LIKIWIKA LAZIMA LITAUMBUKA UMEONA SASA.
ReplyDeleteSasa wewe Anon:09:17:AM
ReplyDeleteManeno yako ni kweli,zamani kazi za wasanii zilibiwa sana,na watu waliokuwa wanajihita Recording Studio,Pia kazi za wanamziki wengi zilitepiwa kutoka katika santuri LP na kuweka katika kanda za kaseti na kuuzwa mitaani bila ya idhini ya wanamziki wenyewe,Pia baadhi ya watnagazaji wa RTD nao walishiriki kwa kiasi kikubwa kuziuza nyimbo za wanamziki wa Tanzania ktk nchi kama vile kenya,na kenya nao wakaziuza kwa Lebo kukubwa ulaya na kungineko.
Mfano ni hai ni wimbo maarufu "Malaika" uliibiwa kenya na mwinzi alikuwa Fadhili William na kauza na kijipatia Royality zaidi ya Dola 100,000= aliyetunga wimbo huo na familia yake pale Moshi hadi leo hakuna walicholipwa.
Bendi ya Safari na binamu zao The Mushroom ya Kenya akina Teddy Karanda,ndio walikuwa wanaongoza kwa kuiba nyimbo na kuzichanganya ktk CD zao mfano wimbo wa "Ujinga wa Roho umekwisha" .
Lakini we Anon:mbona umeandika kuwa
"JOGOO LA SHAMBA HALIWIKI MJINI?
sasa nani?Jogoo la shamba?unamaana
John Kitime ni Jogoo la shamba au?
Taratibu ya kukopi nyimbo na kuanza kuuza ilianza mwishoni mwa miaka ya sabini baada ya teknolojia ya kanda za kaset kuingia nchini, Redio Tanzania walikuwa wanaweza kukopi nyimbo hata kabla ya hapo kwa teknolojia ya kand za spool, ila wao hawakuwa wanashughuluka na piracy kwa wakati huo
ReplyDeleteKITIME, RTD WALIKUWA WAKIUZA KASETI ZA NYIMBO MBALIMBALI KWENYE OFISI YAO KATIKATI YA JIJI NA KWENYE UWANJA WA MAONESHO YA KIMATAIFA, HUU NI UKWELI NA HII PIA NI PIRACY ILA TU WATU WALIONA NI SAWA TU KWA KUWA NI YA SERIKALI. JARIBU KURUDISHA KUMBUKUMBU ZAKO AU ULIZA WATU. JOGOO LA SHAMBA NI HUYO ALIYEJIFANYA ANAZIJUA ENZI HIZO KUMBE ALIKUWA BADO YUKO SHAMBA.
ReplyDelete