Hao si wengine bali ni wanamuziki wa The Revolutions, ambayo sasa inajulikana kama The Kilimanjaro Band aka Wananjenje.
Pichani kutoka kushoto, Juma Omary(Drums/uimbaji),Mohammed Mrisho (Gitaa/uimbaji), Mabrouk Omary 'Babu Njenje'( Mwimbaji), Waziri Ally (Keyboards/ uimbaji), Marehemu Chuky, Keppy Kiombile(Bass /Uimbaji).

Hii ni lebo ya santuri mojawapo ya zamani.
Katika miaka hii kulikuwa hakuna wizi wa kazi za sanaa kama ilivyo sasa. Teknolijia ilikuwa haiwezeshi mtu kukaa chumbani kwake na kunakili kazi za watu. Haya na mengine mengi yanapatikana katika libeneke jipya la mwanamuziki mkongwe John kitime liitwalo Wanamuziki Tanzania.
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. JAMHURI JAZZ BAND WALIKUWA WANAIMBA NYIMBO NA UNAJUWA WANAMAANISHA NINI. SIO NYIMBO ZA SASA HUJUI ZINA LENGO GANI. NAKUMBUKA BENDI YA JAMHURI ILIVYOKIWA IKITIKISA TANZANIA NZIMA NA AFRIKA YA MASHARIKI. YUSUF NA RAJABU, SIWALE , HALFANI NA WENGINE. BILA YA KUWASAHAU ATOMIC JAZZ BAND AMBAO PIA WALIKUWA WAKICHUANA SANA NA JAMHURI PALE TANGA. NAKUMBUKA ATOMIC WALIKWA WAKITIA ZOEZI BARABARA YA 3 NA JAMHURI BARABARA YA 16. JEE KUNA HABARI ZAO WOTE HAO? AKINA JOHN KIJIKO NA WENGINE.

    ReplyDelete
  2. JAMANI TUSIPENDE KUANDIKA TUSIYOYAJUA, SIKWELI KUWA ZAMANI WAKATIWA MATUMIZI YA SANTURI HAIKUWEZEKANA KUKOPI WAPO WENGI TU WALIOKUWA NA TEPU REKODA WALIWEZA KUFANYA HIVY NA HATA REDIO TANZANIA ILIKUWA MOJA WAPO YA WALIOKUWA WIKOPI PIA MULNGA REKODING'I STUDIO YA KAKOBE ILIKUWA MOJA WAPO KATI YA STUDIO NYINGI ZILIZOZAGAA MITAANI. INAWEZEKANA MWENZETU ULKUWA BADO UKO SHAMBA HATA HIVYO JOGOO LA SHAMBA HALIWIKI MJINI LIKIWIKA LAZIMA LITAUMBUKA UMEONA SASA.

    ReplyDelete
  3. Sasa wewe Anon:09:17:AM
    Maneno yako ni kweli,zamani kazi za wasanii zilibiwa sana,na watu waliokuwa wanajihita Recording Studio,Pia kazi za wanamziki wengi zilitepiwa kutoka katika santuri LP na kuweka katika kanda za kaseti na kuuzwa mitaani bila ya idhini ya wanamziki wenyewe,Pia baadhi ya watnagazaji wa RTD nao walishiriki kwa kiasi kikubwa kuziuza nyimbo za wanamziki wa Tanzania ktk nchi kama vile kenya,na kenya nao wakaziuza kwa Lebo kukubwa ulaya na kungineko.
    Mfano ni hai ni wimbo maarufu "Malaika" uliibiwa kenya na mwinzi alikuwa Fadhili William na kauza na kijipatia Royality zaidi ya Dola 100,000= aliyetunga wimbo huo na familia yake pale Moshi hadi leo hakuna walicholipwa.
    Bendi ya Safari na binamu zao The Mushroom ya Kenya akina Teddy Karanda,ndio walikuwa wanaongoza kwa kuiba nyimbo na kuzichanganya ktk CD zao mfano wimbo wa "Ujinga wa Roho umekwisha" .
    Lakini we Anon:mbona umeandika kuwa
    "JOGOO LA SHAMBA HALIWIKI MJINI?
    sasa nani?Jogoo la shamba?unamaana
    John Kitime ni Jogoo la shamba au?

    ReplyDelete
  4. Taratibu ya kukopi nyimbo na kuanza kuuza ilianza mwishoni mwa miaka ya sabini baada ya teknolojia ya kanda za kaset kuingia nchini, Redio Tanzania walikuwa wanaweza kukopi nyimbo hata kabla ya hapo kwa teknolojia ya kand za spool, ila wao hawakuwa wanashughuluka na piracy kwa wakati huo

    ReplyDelete
  5. KITIME, RTD WALIKUWA WAKIUZA KASETI ZA NYIMBO MBALIMBALI KWENYE OFISI YAO KATIKATI YA JIJI NA KWENYE UWANJA WA MAONESHO YA KIMATAIFA, HUU NI UKWELI NA HII PIA NI PIRACY ILA TU WATU WALIONA NI SAWA TU KWA KUWA NI YA SERIKALI. JARIBU KURUDISHA KUMBUKUMBU ZAKO AU ULIZA WATU. JOGOO LA SHAMBA NI HUYO ALIYEJIFANYA ANAZIJUA ENZI HIZO KUMBE ALIKUWA BADO YUKO SHAMBA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...