Sura za Huzuni na Majonzi kwa wanafunzi wa India waliopo Bangalore na Wenzao wa Mysore baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Muwakilishi wa Ubalozi Mr. Amon Mwamunenge juu ya maendeleo ya uchunguzi na taratibu za kusafirisha mwili wa Marehemu Imran Mtui kurudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya amani.
Home
Unlabelled
majonzi,majonzi, majonzi bangalore
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Poleni sana ndungu zangu!
ReplyDeleteRIP Mtui
Huyu kijana (Marehemu) alikuwa kijana mkimya sana. Namkumbuka tukiwa naye pale Old Moshi Secondary miaka ya 92/93 darasa moja na baada ya hapo sikuwahi kuonana naye tena. Yeye alikuwa mtu wa kutabasamu tu na mtulivu. Mungu aupumzishe mwili wake pema peponi mpaka siku ya kiama na akipenda amjalie Neema ya ufufuo wa kwanza. RIP Imran Mtui.
ReplyDeleteMdau Canada.
Kila niangalia hizi sura inanisikitisha sana, saana! yaani we acha tu. Vijana wenzangu tupunguzeni basi kuzurura usiku mkubwa au kwenda masafa ya mbali bila ya taarifa although hatujajua haswa sababu ya kijana wetu kuuliwa ila kueni wapole na wastahamilivu. Ukweli ni kwamba MUNGU yu pamoja nasi.
ReplyDeleteREST IN LARGE PEACE IMRANI
INDIA.
Inna lillahi waina illahim rajiun, pole sana wafiwa rahma akupeni moyo wa subra Allah ma amin.
ReplyDeletena wahida wa u.k pole sana dear.
Habari hii imenigusa sana,na inatisha na kusikitisha.Kuongea daima hakuleti suluhisho la tatizo au kuelekea kwenye suluhisho,bila shaka watu wanaweza kuongea lakini lazima kuwe na vitendo.Mimi niko njema ya nchi(Tanzania) lakini nashauri watu waliogushwa na jambo hilo huko Tanzania,mnaweza kufanya yafuatayo:
ReplyDeleteMuandamane hadi Ubalozi wa India na kuwakilisha malalamiko yenu kiofisi kudai maelezo ya sababu ya kifo hicho na kuhoji serikali ya India inafanya nini kuhusu usalama wa Wanafunzi wa Tanzania walio huko.
2.Kuandamana hadi ikulu,au kuitisha maandamano na kuishinikisha na kuhoji kwa nini serikali ya Tanzania bado inapeleka wanafunzi kusoma nchi kama India na Russia,kuna siku kucha waafrika au watu wenye ngozi nyeusi wanauwawa sana kwa ubaguzi wa rangi.SIO SEHEMU SALAMA KUISHI HUKO KAMA NI MWEUSI!
3.Vyombo vya habari vinaweza kusaidia kuleta ufahamu/kujua kwa WaTanzania kuhusu hili jambo.
Wanafunzi wa India wamekuwa wakiuwawa pia Australia kwa sababu za kiubaguzi na Wahindi na serikali yao wamefanya juhudi za kidiplomasia kama kutishia kutopeleka wanafunzi huko na kukata uhusiano wa kidiplomasia.Magazeti ya India wamekuwa yakilaumu polisi wa Australia kwa kutofanya juhudi za dhati kuwapata wauaji.
Imekuwa kawaida kusikia watanzania wanauwawa nje na hamna tamko lolote la kiofisi linalotolewa na Serikali ya Tanzania,je hawajali kama Serikali haiwajali raia zake inamjali nani?
Wananchi wanaitumikia serikali na Serikali ni lazima kuwatumikia wananchi wake,daima inabidi kutoa na kupokea,iwe pande zote mbili.
POLENI SANA KWA MSIBA/WAFIWA....TUKUMBUKE TUNAPO KUWA NCHI NYINGINE NA PIA IKIWEPO "NCHI YETU" KWAMBA, SEHEMU ZA VIUNGO (ORGANS) VYA MWANADAMU ZINA "HITAJIKA/ZINAUZWA" KWA BEI YA JUU SANA, KWASABABU YA UHABA ULIOPO NA WATU WENGI "WANAHITAJI/WAHITAJI" WAKO KWENYE FOLENI (WANASUBIRI)..VIUNGO VYA WATU KUTOKA "NCHI MASIKINI" VINAFAA SANA KWASABABU "WENGI WAO/WETU" HAWATUMII/HAWANA UWEZO WAKUPATA MADAWA YA VIWANDANI (YENYE ATHARI/MADHARA MBALI MBALI) KWAHIYO HAWAJAADHIRIKA/WANAVIUNGO BORA (ORGANIC ORGANS) NA NI RAHISI KUSHAWISHIKA .....UNAWEZA "UKAOA/OLEWA" UKARUDI KWENYE SANDUKU/JENEZA VIPANDE VIPANDE (KAMA AJALI) AU HUNA "FIGO/INI".
ReplyDelete"HUMAN TRAF...NG"
Ninatoa pole kwa wafiwa wote. Pia ningeshauri kwa vijana tunaopata fursa ya kuja nje kuwa waangalifu na maisha yetu huku ugenini. Ni bora kuonekana Mshamba na kuwa salama badala ya kujihusisha na watu wa ajabu ajabu ambao wanaweza kukudhuru. Huku nje watu wanaweza kuonekana waungwana lakini si wema. Kwa wale wakristo kanisani na marafiki wanaompenda Mungu ni salama zaidi ya kujirusha!
ReplyDeletePoleni mliofiwa na tunaobaki busara itumike huku nje ya nchi tulipo wengi.Tumekuja kutengeneza future zetu na ndugu zetu huko nyumbani.
Ndoto YA mchana pole sana . una moyo wa uzalendo. Lakini huku TANZANIA tunaishi kila mtu kivyake.Tunasahau kuwa linalomkuta mwenzetu na sie laweza kutukuta.
ReplyDeleteInasikitisha sana.sijui viongozi wamelala fofofo.!?
jamani inasikitisha sana kijana mdogo kama huyo kufa kifo kibaya namna hiyo.why?poleni sana familia ya marehemu mungu awaongoze katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.kwakuwa damu ya mtu haiendi bure basi na muuaji au wauaji watalipwa hapahapa duniani.kama sio leo basi hata kesho,haiwezekani kijana wa watu akauwawa kikatili hivyo.hata kama alikosa kosa kubwa kiasi gani hakupaswa kupewa adhabu kubwa ya kinyama namna hiyo.Why watanzania wengi wanauwawa nje ya nchi.serikali iko wapi jamani?kuhusu swala la kutembea usiku mbona wageni hapa kwetu wanatembea mpaka asubuhi?au na sisi tuwaanzishie?tumechoka sasa.(R.I.P MTUI
ReplyDelete