




Mtanzania aliyeuawa India azikwa bila kichwa
Na Charles Ndagulla na
Dixson Busagaga, Moshi
VILIO, simanzi na majonzi jana vilitawala mazishi ya Mtanzania Imran Mtui (31) aliyeuawa kikatili nchini India hivi karibuni, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Njoro Manispaa ya Moshi.
Mwili wa marehemu huo ulizikwa bila kichwa huku pia ukidaiwa kuwa na majeraha mengi mwilini kuanzia miguuni na kwenye paja lake karibu na kiuno huku kiwiko cha mkono wa kulia nacho kikidaiwa kunyofolewa.
Mwili huo uliwasili mjini moshi usiku wa kuamkia jana baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam, ukitokea nchini India huku gharama zote za kuusafirisha zikibebwa na serikali ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya mazishi, kaka wa marehemu, Maliki Mtui, alisema kuwa wameshtushwa na kifo cha ndugu yao hasa kutokana na marehemu kutokuwa na historia ya ugomvi.
Kwa mujibu wa kaka huyo, mwili huo pia umeonekana kuwa na alama za kamba kwenye mikono yake hali ambayo inaonyesha marehemu kabla ya kuuawa alifungwa kamba ili asiweze kujitetea.
Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kutokea katika mji wa Bangalore nchini India ambako marehemu alikuwa tayari amehitimu masomo yake ya biashara na utawala (Business Administration) na tayari alikuwa akijiandaa kurejea nyumbani.
Kaka huyo wa marehemu aliwaambia waandishi wa habari kuwa mdogo wake huyo alipatwa na mkasa huo akiwa njiani kuelekea mjini ambako rafiki yake wa kike ambaye pia ni Mtanzania aishie visiwani Zanzibar alikuwa akisoma.
“Niliwasiliana naye siku ya tukio kabla hajapatwa na mauti haya nikamuuliza anatarajia kurudi lini nyumbani akanijibu angerudi mapema na rafiki yake alikuwa akimsubiri lakini hakuweza kutokea” alisema.
Pamoja na kuishukuru serikali ya Tanzania kugharamia kuusafirisha mwili wa marehemu mdogo wake, Mtui ameitaka pia serikali kuwathamini raia wake walioko nje ya nchi kwa kufuatilia taarifa zao pindi wanapokumbwa na matukio kama hayo ya kuuawa kwa mdogo wake.
Naye msemaji wa familia ya marehemu Mtui ambaye pia ni shekhe wa msikiti wa Majengo, Shekhe Said Khatibu, alisema kuwa serikali haiwathamini raia wake walioko nje na ndiyo maana serikali haijatoa tamko rasmi kulaani mauaji hayo.
Shekhe huyo pia alisema katika kile kinachoonyesha kuwa idara za serikali zimelala, serikali imeshindwa kutuma hata mwakilishi kwenye mazishi hayo ambayo tukio lake lina utata.
Aidha, alipinga taarifa zote zilizotolewa na madaktari nchini India kwamba marehemu alifariki dunia kwa ajali ya treni na kusisitiza kuwa taarifa hizo sio za kweli.
Chanzo cha habari
BOFYA HAPA
poleni sanaa wafiwa mungu awape moyo mwenye uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.roho yake ilazwe mahala pema peponi ameen.
ReplyDeletemdau boksini
INNA LILAH WAINAILAH RAJIHUN.
ReplyDeleteMIMI KILIO CHANGU KIKO PALE PALE,TUACHE KUSEMA TENA INAUMA KILA NAPOSOMA HABARI KM HII.JAMANI TUKUTANE MPAKA BALOZI ZOTE ZENYE HIZI TABIA.BRO MICHUZI ORGANIZE HILI JAMBO KWA NIABA YA SISI TUSIO NA SAUTI KNY JAMII,HATUTAVUNJA SHERIA WALA NINI SOTE NI WASTAARABU LENGO LETU NI KULAANI TU HUU UNYAMA.BRO MICHUZI LEO KWA MTUI KESHO ITAKUWA HATA WEWE UMEENDA KIKAZI YAWEZA KUKUSIBU HILO JAMBO,ANGALIA SERIKALI YA INDIA ILIVYO NA UMOJA HATA KNY UPUUZI WAO. MTU KAUWAWA WANASEMA KAGONGWA NA TRENI,VIPI KUHUSU SISI?? KM KAWAIDA YETU TUTASEMA WATANZANIA SISI NI WAPOLE NA WAKARIMU,UKARIMU. TUNAKARIMU MPK VIFO?? WATU WA AINA GANI SIE. pls wana-bloggs msikazanie kupromote mambo ya kujirusha tuu hakuna jambo litakulipa na hutasahauliwa na jamii na kulaani mauaji ya aina yoyote. Naomba usibanie maoni yangu.
PLEASE BRO MISUPU PROMOTE IWE HATA ALHAMISI IJAYO naona watanzania tushasahau km kawaida yetu kelele za siku 2 kwisha.
Ni mimi mdau,
Bwatuka.
Huu ni UNYAMA.....Serikali itume wapelelezi wake wkafuatilie hii kesi...yaani mpaka tunazika mwenzetu bila kichwa? yaani inauma sana....
ReplyDeleteKWa kweli kitenda alichofanyiwa huyu kijana ni cha kinyama kupita kiasi. Serikali inapaswa kutoa tamko hata kama ni protest ya danganya toto tu. Watanzania wanawapelekea wahindi mapato mengi kwa wanafuzi wanaokwenda kusoma. Wagonjwa wetu wanakwenda huko kutibiwa na wanapeleka mapato makubwa. Kitendo hiki pamoja na maelezo ya dharau kimevuka mpaka. Lasivyo watanzania waanze kugomea kwenda vyuo vya india. Poleni sana ndugu wafiwa, jamaa na marafiki wote. Tunaomba Mungu aingilie kati na waliohusika Mungu mwenyewe ashughulike nao!
ReplyDeleteKweli jamani nani anataka kumzika mtoto wake bila kichwa.Inaniuma sana sijui kichwa cha mtoto wawatu kipo wapi.poleni sana wafiwa
ReplyDeletePole sana kwa wafiwa na wote walioguswa na Janga hili. Zaidi nasikitishwa sana na serikali yetu ya TZ.kwa kutoonyesha uzalendo kwa mtanzania aliye nje. Balozi nyingi hazipo kwa maslahi ya mtanzania. Watanzania tulio nje, wakati umefika kushinikiza serikali itutambue na kuuona mchango wetu, tuanzishe na kutunza jumuiya zetu popote tulipo duniani. tuwe na sauti moja kuhimiza maendeleo na kukosoa balozi zinazolegalega na zisizoonyesha uzalendo. Ni jukumu la serikali kushughulikia tatizo kama la Marehemu Imran, lakini zitahitajika jitihada kubwa na shinikizo kutoka kwetu kuibadilisha serikali yetu ya TZ, hasa kwa mtz aliye nje.
ReplyDeleteMdau, USA.
Napenda kutoa rambirambi zangu kwa wafiwa na kwa watanzania wote.Huu ni msiba wetu wote.Tunatakiwa tuondokane na ujinga tulionao kwamba watanzania ni wapole huku tunaumizwa,kwa nini serikali hajatoa tamko lolote?kama wengine walivyosema balozi zetu hazifanyi kazi kwani mimi mwenyewe nimefuatilia passport za wanangu huku ugenini wananizungusha tu na huku nimewalipa kila kitu kwa ajili ya passport hizo.Lini tutaamka na kuwa watu wenye misimamo?
ReplyDeleteSijui? Labda iwe ni siku hizi lakini nnachojua mimi ni kuwa wahindi wanadharau lakini si wakatili kiasi hicho bila sababu za msingi kama ilivyo kwa baadhi ya nchi nyingine za ulaya au afrika ya kusini.
ReplyDeleteNimeishi India kwa takribani miaka sita na matukio mengi yasiyo ya kibinadamu yaliyotokea yana sababu,tena sababu zinazoeleweka.Wahindi ni watu ambao hawana mda na mtu hasa wakishajua ni nini unafanya,yani kama ni mwanafunzi au vinginevyo,ikitokea ukawafanyia vurugu au kuwaingilia katika mambo yao,kuwadhulumu au kuwaonea basi hapo ndipo shida inapokuja kwani wanaweza kukufanyia kitu mbaya,wanaoifahamu India watakubaliana na mimi.
Kifo cha bwana Imran kinasikitisha kwa kweli lakini sitaki kuamini kuwa Imrani aliuawa bila sababu,yani swala laubaguzi,eti kwa sababu mtu ni mwafrika basi wahindi wananchukia kiasi cha kukuua kikatili kiasi hiko!! La hasha.Ubaguzi upo ila ni katika sehemu za kujipatia huduma na si vinginevyo.Kifo hiki kichunguzwe na taarifa zake zitolewe,kuna kitu hapo jamani si bure ohoooo.
Jambo usilolijua ni kama usiku wa...
Potz
omg!jamani! inauma mno kuzika mtoto bila kichwa oh MOLA eh MOLA! EH MOLA! Mlaze mahali pema peponi. AMINA!
ReplyDeleteHuyu Sheikh haitendei serikali haki hata kidogo. Ningedhani ile tu kugharamia gharama za usafiri wa mwili wa marehemu yaonesha kujali! Sasa hizo kauli zingine zimetoka wapi? Hivi jambo lolote lile jema hatuwezi kuliona? Ni watanzania wangapi wamepoteza maisha yao nje na ngugu na marafiki wanalazimika kuchanga gharama za kusafirisha maiti nyumbani na bado hawajailaumu serikali! Ama kwa vile tu hao wengine hawana undugu na huyu Sheikh?
ReplyDelete