Marehemu Imran Mtui
UONGOZI WA TASABA CHINI YA RAIS FIDELIS MSOMEKELA KWA MASIKITIKO MAKUBWA UNATANGAZA MSIBA WA KAKA YETU IMRAN MTUI ULIOTOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 31 JANUARI.

UONGOZI WA TASABA UKISHIRIKIANA NA MJUMBE WA UBALOZI WA TANZANIA INDIA WANAFUATILIA TARATIBU ZOTE ZA MSIBA.

KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA VIONGOZI WA TASABA NAMBA ZAO A SIMU ZIPO KWENYE KICHWA CHA UKURASA HUU (BOFYA HAPA).
MHESHIMIWA RAIS FIDELIS AMEWAOMBA WATANZANIA KUWA WATULIVU MUDA HUU WA MSIBA NA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KUHAKIKISHA TUNAMALIZA MSIBA HUU SALAMA.MSIBA HUPO KWA DADA HAKIKA

ADDRESS
3RD FLOOR
1ST MAIN
GOPALA REDDY LAYOUT
BANASWADI
BANGALORE-78
INDIA

MUNGU AILAZE ROHOYA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.
----------------------------------------
Mwanafunzi Mtanzania,
Imran Mtui auawa India

Habari zilizopo katika blogu ya Watanzania waishio Bangalore (TASABA), pia katika mtandao wa Twitter zinathibitisha kuwa, mwanafunzi wa Kitanzania, Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo kishiriki Cha Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa hauna kichwa.
Taarifa zinasema kuwa mwili huo ulikutwa kando kando ya reli katika eneo la Shivajinagar katika mji wa Bangalore ukiwa hauna kichwa huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya. Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Mimi nilipata taarifa hizo juzi jioni ambapo jana tulifanya kikao na wenzangu na kumtuma Ofisa wetu Mzee Amon Mwamanenge na mwanasheria wetu wamekwenda huko kupata undani wa tukio hilo," alisema Balozi Kijazi.

Alisema kuwa kwa sasa hawezi kutoa picha kamili lakini mwili wa kijana huyo umekutwa ukiwa hauna kichwa na mguu umebondeka. Kijana huyo aliyefariki alikuwa amemaliza Shahada ya Usimamizi wa Biashara (BBM) na alitambulika kwa jina la Imran Mtui. Aliwahi kuwa Mtunza Fedha wa Chama Cha Wanafunzi wa Kitanzania Waishio Bangalore (TASABA).

Habari hizi zimedhibitishwa na mdogo wa marehemu, Issa Mtui, kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Marangu, Moshi. Alieleza kuwa mwili wa marehemu unategemewa kuwasili nchini Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya taratibu za mazishi ambayo yatafanyikia Marangu.
Imrani ni wa pili kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia hiyo. Inadaiwa kuwa kabla mauti haijamkuta alitarajiwa jana angekuwa amerejea nchini baada ya kuwa amechukua vyeti vyake vya masomo ambavyo alikuwa akivisubiri baada ya kuhitimu masomo yake.

Polisi nchini India wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
------------------------------------------------
Kwa niaba ya wadau wote, Globu ya Jamii inatoa pole kwa wafiwa na kuwaombea wawe na subira wakati huu mgumu. Mola ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi - AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. Mungu ailaze roho ya merehemu Imran mahali pema peponi. Amen.

    ReplyDelete
  2. died so young men! i remember the boy back in the days at old moshi, i would like to extend my prayers to the family and friends ,i know what they go through right now, may god give them courage and strength .we love him but god love him most,u will always be rembered ,R.I.P MEN
    nyoni,mi,usa

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha sana, Inaelekea India sio kuzuri kabisa kwa sasa. Naona watanzania wananyanasika sana India. Ni tukio la kutisha hilo serikali inabidi kuingilia kati inaonekana kuna aina fulani ya uhasama kati ya wageni na wenyeji! kuna ubaguzi wa rangi huko serikali inabidi kufuatilia kwa haraka sana kwa usalama wa wanafunzi wengine waliobaki.
    My condolence to Mtuis Family.
    Mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  4. Kaka hii sio kabisa kwnini cc wa-tz tunaeshimu sana wageni lakini wao sio kabisa.pole familia ya marehemu,kuanzia sasa ukiona hamna majibu mazuri ya serikali yao nasi Wahindi wa hapa ni kuua tu make hawana lolote la maana dharau,viburi na pamoja matusi wa-tz lazima tuamke upole huu sio.ingekuwa nchi kama USA au UK ungesikia vyombo vyote vya habari dunia nzima kelele tupu na kuandika India sio sehemu salama kwa wanafunzi wa nje,lakini bongo kawaida mpaka misoup atupe taharifa.

    ReplyDelete
  5. kwa kweli inasikitisha sana, na ukweli ni kwamba wahindi huku India ni wabaguzi zaidi ya sana na hii si kwa Watanzania tu ni kwa wageni wote wenye asili ya kiafrika (ama rangi nyeusi) wakikuona wanakushangaa mno km ww ni malaika maybe ilhali wao ni zaid i ya weusi. Serikali iingilie kati hapa maana tutakwisha huku ama ndo basi tena hatupo huko?

    My condolences to all who touched with this grief.
    Rest in peace men........
    INDIA

    ReplyDelete
  6. Very sad news!RIP Imran...My thoughts and prayers go to his family

    ReplyDelete
  7. poleni wafiwa

    jamani yani amemaliza degree yake na vyeti kachukua afu anakufa kinyama ivo?tena alitakiwa awe amerudi bongo aendeleze familia yake na ajiwezeshe na nchi pia?what a loss!!

    inavoonekana india si kwema/shwari kabisa kwa wageni weusi asa from afrika...jamani hizi taarifa za kuuawa mala kuvamiwa kukamatwa kwa wabongo mbona ivi?

    KULIKONI?

    ReplyDelete
  8. Imenigusa sana ingawa huyu jamaa nilikua simfahamu. Inasikitisha...I hope waliofanya hivyo watapatikana na kushughulikiwa kisheria.

    Watanzania India, angalianeni, kuweni makini. Ilimradi sababu ya tukio hili haijulikani basi hamjui nani anafuata au ndio yamekwisha.

    R.I.P Imran

    ReplyDelete
  9. Tunaomba Serikali yetu iingilie kati kulifuatilia swala hili. Kwa kweli hali hii inatisha sana. Watoto wetu wanasoma huko na kama kuna matukio kama haya, kwa kweli itatufanya tufikirie mara mbili kabla ya kupeleka watoto huko kwa ajili ya masomo. kama alivyosema Ginfizz ingekuwa kitendo hicho kimefanywa kwa mwanafunzi wa Marekani ama Uingereza au nchi yoyote iliyoendelea basi ungesikia magazeti na vyombo vya habari vyote vingecharuka kulaani na kusema kuwa India ni sehemu ya hatari. Lakini hapa kwetu hakuna kauli ya kiongozi yoyote zaidi ya kusoma na kupata habari kwenye Globu hii ya jamii. Viongozi mko wapi? Hatua gani zinachukuliwa na Serikali zaidi ya kusubiri ubalozi wetu India kufuatilia?

    ReplyDelete
  10. I am very sorry for this event! I know how painful is especially for the family.

    Let us first wait and see how our government i s going to react about the whole issue! If nothing is going to be done then we have the right to do something about it. I am sure we can afford to this!

    ReplyDelete
  11. mimi ni mwanafunzi wa india ni kweli wahindi wanaubaguzi wa rangi hiki kifo kimetusikitisha sana...kwakweli vifo ni vingi..juzi kati tena kulikuwa na kifo cha mwanafunzi huku hyderabad lakini police hawakuchunguza chochote wala kufuatilia ipasavyo..its not safe anymore..naomba serekali ingilie kati tafadhali..tunawaheshimu sana wahindi sasa wakitaka vurugu na sisi tanzania tunamaliza.....tunahishi huku tunawajua ni wabaya sana...

    ReplyDelete
  12. ebu na sisi tuanzae kuwatoa hao wahindi mbiyo huku bongo.pumbafu zao

    ReplyDelete
  13. jamaaaaaani mtoto wa wifi yangu Imrani llllloh...ulikuwa ndio tegemeo la mama yako hasa baada ya baba yako kufariki, aliegemea soon utagraduate umsaidie leo wamekuondoa kikatili namna hii mwanangu? Mungu akulaze mahali pema peponi Imran. Wamekuchukia wakakuua, lakini sisi familia yako tunakupenda na Mungu anakupenda zaidi atakupumzisha.Amen

    ReplyDelete
  14. Mie naanza na bosi wangu hapa ambae ni muhindi nitamyofoa nywele hizo pambavu sana.... nina hasira kweli! jinsi tunavowaheshimu hapa kwetu nyumbani wao inakuwaje wanatunyanyasa kiasi hichi jamani> LOOO!! EH MOLAAAAAAAAAA!!!!! May he R.I.P

    ReplyDelete
  15. huku kwetu ndio tunawapa kichwa, maduka makubwa wao,wanaokaa magorofani tena town wao, wameifanya tanzania kama yao, wanaipenda tanzania lakini sisi wenye nchi hawatupendi kabisa! VERY BAD....

    ReplyDelete
  16. TUSEME NINI BASI? HASA KWA SISI WAZAZI JAMANI IMENIUMA KWELI, TENA NA WEWE DADA HAPO JUU UNAYESEMA NI MTOTO WA WIFI YAKO TENA ALIKUWA TEGEMEO NA KUWA BABA YAKE ALISHAFARIKI UMENITIA MAJONZI SANA JAMANI.

    SIJUWI CHA KUSEMA ILA NAWAOMBEA TU FAMILY YA MALEHEMU MWENYEZI MUNGU AWATIE NGUVU NA UVUMILIVU POLENI SANA.


    VIONGOZI MSIPENDE KURA KUTOKA KWA WANANCHI INABIDI MJITUME KUISAIDIA JAMII KAMA UKIJIONA DHAIFU ACHA UCHU WA MADARAKA MARA MOJA.

    ReplyDelete
  17. poleni wandugu kwa msiba wa kijana wetu, mwenyeezi munguu awape subira wahusika,pamoja na raisi wa tasaba[ambaye mwenyewe anajiita muheshimiwa!]

    ReplyDelete
  18. Kwanza poleni sana wafiwa, ndugu na marafiki. Pia wanafunzi Wakitanzania huko India mtulie wakati serikali na ubalozi wa Tanzania unafuatilia kisheria suala hili.

    Acheni comments za kibaguzi, makabila ya watanzania ni pamoja na Baniani, Wamanga, Wadigo, Bamakonde, Wagogo,Wagoa n.k

    Hao Wahindi wa India hawana uhusiano na Baniani wa Kitanzania. Vifo vya kutisha kwa Watanzania vinatokea pande zote kuanzia USA, UK, Italy, Ugiriki, India, South Africa, Brazil n.k

    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  19. Inasikitisha sana. Inauma mno. Imran nilimfahamu tukiwa pamoja miaka mingi Moshi. Alikuwa mwingi wa ucheshi, rafiki kwa wengi, kijana aliyejituma sana katika maisha...tutamkosa sana! Pole sana kwa familia. Tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu.

    Inna lillahi wainna illahi raajiuun. Kullu nafsin dhaikatul maut.

    ReplyDelete
  20. India,Malaysia,Russia,China siyo sehemu nzuri kwa wageni esp toka africa,wabaguzi na hapa malaysia african wengi washauliwa,china na Russia pia apafai kabisa

    ReplyDelete
  21. Nimesikitishwa sana na kifo cha rafiki yetu Imran. Natoa mkono wa pole kwa familia hapo Moshi. Tuko pamoja nanyi wapendwa.

    Imran ametangulia na sisi tuko nyuma njia hiyo kupita ni wajibu. Tulikupenda sana Imran na twamuomba Mola akuandalie mahali pema peponi. Amen!

    Kullu nafsin dhaikatul mawt.

    ReplyDelete
  22. Jamani, hao wahindi wanaoishi Tanzania, nao wawe wanatoa ushirikiano, pindi yanapotokea matatizo kama haya. sio wanakua wanajitenga kama sio watanzania. japo, wawe wanaguswa nao, kama watanzania mtanzania yoyote yule asilia,

    ReplyDelete
  23. Wadau wengine mnaonekana mna hasira sana msiwe hivyo lets wait and see how our Gvt will react as somebody said above. Maana mkisema muanze kuwapiga wahindi wa huko mumefikiria nasi tuliobakia huku si tutamalizika na kukosa haki zetu huku? Hamuwapigi wala kuwafukuza tunanyanyasika je mkifanya hivyo. we have to pressurise gvt to take its place.
    Mdau Osmania University
    India

    ReplyDelete
  24. Inasikitisha sana. M/Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
    Amin.

    ReplyDelete
  25. Hiyo comments hapo juu kuwa kijana alikuwa awe nguzo ya familia imenifanya niuzunike zaidi.

    Lazima Serikali ijue jinsi ya kuwakoromea hawa. China ilinyonga Mwingereza aliyekamatwa na Madawa ya kulevya ikakoromewa, sisi serikali iko Kimya kabisa. Lazima angalau nikarushe mawe mawili matatu pale ubalozi wa Hindi. Naomba kuelezwa upo wapi??? Hapa Dar!! *&+)£"!$%^&*((&*^& zao

    ReplyDelete
  26. JAMANI WATANZANI TUSIENDE INDIA KUSOMA WAHINDI NI WACHAWI WAKATILI NA NI WABAGUZI SANA,ANGALIENI SINEMA ZAO NIO MTAJUA WAHINDI WANATOBOA MACHO WATOTO ILI WAWE OMBA OMBA WAZURI ,WANAFANYA NDUGU ZAO VIWETE ILI WAPATE UTAJIRI NI WACHAFU PIA YAANI INDIA NI NCHI YA MWISHO MIMI KUWAI KUIWAZA KWAMBA NTAIVISITLICHA HIO KUSOMA.

    ReplyDelete
  27. Jamani inasikitisha sana kwa kifo chake.Alikuwa kijana mpole,mtaratibu asiyekuwa na makuu.Ninamkumbuka sana tumekuwa naye Moshi maeneo ya Majengo
    Mungu ailaze roho ya Imran mahali pema pepono Amen

    ReplyDelete
  28. Nimesikitishwa sana na Taarifa hii. Imeniuma sana,tena sana.Namuomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Imran pema peponi, AMIN.
    Ndugu wa marehemu wawe jasiri kupita kipindi hiki kigumu. Pole ziwafikie watanzania wote kwa kumpoteza kijana wetu.

    ReplyDelete
  29. Poleni wafiwa tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu, pia pole iende pale bangalore kwa Watanzania wote mnaoishi hapo lakini pia pole kwa wote tulioguswa na msiba huu. jamani wahindi ni zaid ya wachafu cha kushangaza ukitaka VISA yao pale ubalozini Zanzibar uone unavyonyanyaswa mara oooh! lete bank statement ya hela telee ilhali wao ni zaidi ya maskini tena huko wanaringa kwa kua na kiswahili na ukizubaa unaweza hta kutukanwa pale ubalozini zanzibar. kumbe wanatebgeneza mazingira ya kutumaliza huku.
    osmania university
    india

    ReplyDelete
  30. poleni wote mlioguswa na msiba huu kweli inauma sana Mungu wa rehema akuweke pepon Imran AMEN

    ReplyDelete
  31. MIMI KINACHONIKERA WABONGO NI KUONGEA SANA NO ACTION, NA KUJIDANGANYA KUWA WATU WA AMANI NA UTULIVU. SI KWELI SIE NI WAJINGA TU SIKU ZOTE WA KUILAMU SERIKALI BILA YA KU-TAKE ACTION. ISSUE KM HII VERY SENSITIVE(UHAI WA MTU). NILITEGEMEA HATA MMOJA KUSEMA TUKUTANE JUMATATU IJAYO WJANGWANI MPK UBALOZI WA INDIA ETC.
    MNABWABWAJA TU...
    UTAONA WATU WANAANDAMANA KWA KITU CHA KIFALA ETI CCM au CUF au CHADEMA wameiba kura,BUT HAMUANDAMANI KWA UHAI WA MTU.
    WABINAFSI TU WABONGO.
    KAMA VP ISONGE ACHENI KUCHONGA MUDA MREFU KNY BLOGG. JUMATATU ITANGAZWE KNY MABLOGS,MAGAZETI,TV,REDIO etc.
    NA SIO INDIA TU IWE HATA USA KM WANA HIYO TABIA AU SOUTHAFRICA.

    NI mimi mdau,
    BWATUKA.

    ReplyDelete
  32. ulichosema anoy Wed Feb 03, 05:12:00 PM bwatuka ni kweli kabisa watanzania tubadilike tuwe kwenye matendo zaidi na hata ofisi zetu za ubalozi nazo hazieleweki wao ni kulipisha viza tu,hawajali hata watu wao mbona mengine mnaiga kwa america kwa nini hamuigi na jinsi america anavyojali watu wake
    natangaza vita na wahindi

    ReplyDelete
  33. hii ni hali ya hatari kwa wanafunzi na watanzania waishio nchini india, ni suala ambalo serikari ya tanzania isilifumbie macho hata kidogo, maana watanzania wengi sana wapo huko. uchunguzi ufanyike kwa haraka na kijulikane chanzo. tukio kama hili lingetokea kwa nchi nyingine mtu wao kauwawa pangekuwa hapatoshi, tuangalie mfano wahindi wenyewe walivyokuwa wanauwawa na kupigwa kule Australia, ni jinsi gani walireact, mpaka waziri mkuu kule aliingilia kati. serikari ya tanzania kuwa serious na suala hili. watanzania india andamaneni kupinga hili kwa ajili ya usalama wenu.

    ReplyDelete
  34. Nchi zilizoendelea kama USA, Canada na UK hakuna ubaguzi wa kihivyo japo u can still feel it.

    Dawa ni kususia shule zao na watoto wapelekwe US, Canada na UK ambnapo wanaweza hata kufanya kazi kwa kanjanja.

    Its terrible guy kwa huo unyama. Sipeleki mtoto wangu kwenye hivyo vinchi

    So so so sad
    Poleni wafiwa na poleni wa tanzania wenzangu

    Take action na ikibidi funga ubalozi India.

    Tuwatimue nchini na kuacha kuwatukuza..

    Hakuna siasa wala ujamaa
    Wameua nguvu ya Taifa

    ReplyDelete
  35. jamani mnaenda india kufanya nini?? hawa watu ni wabaguzi sana!!!! Serikali ya tanzania iwarudishe wanafunzi wote wa kitanzania walioko huko tafazali! Pole kwa familia. RIP.

    ReplyDelete
  36. so pathetic yaani naona govt ya hawa watu(wahindi)hawaongei chochote hata kwenye newspaper hatuoni na sio huyo tu aliyeuawa siku hizi za karibuni kuna muivory cost amabye nayealichomwa kisu nasijui hata kesi iliishia wapi.kwahiyo kama wanafunzi waindia we really need support from home kwasababu kama govt yao inakuwa inapuuzia mambo kama hayo tunakuwa hatuna mtetezi.GOVT OF TANZANIA WAKE UP....

    ReplyDelete
  37. Bwatuka...Umeongea point tupu.watu wanaandamana eti Israel kulipua mabomu Palestina,watu kuuwawa Afghanistan/Pakistan/Sudan wakati ndugu zao wakiuwawa kimya kazi kubwabwaja tu kwenye mablogs,angalia Swetu kauliwa na JWTZ watu kimya..tunapenda kuandamana kwa mambo ya kijinga sana ambayo hayatuhusu na wala hayatusaidii..UKARIMU HUANZIA NYUMBANI KWAKO.
    RIP-Imran.

    ReplyDelete
  38. MIMI PIA NA-SUPPORT MAANDAMANO KWENDA UBALOZI WA INDIA ILI KUITAKA SERIKALI IFUATILIE HIKI KIFO CHA MDOGO WETU
    NAJUA VIFO VINAVYOTOKANA NA MAUAJI NI VYINGI, LAKINI KUNA MWANZO

    WENYE KU-SUPPORT HII WAJITOKEZE

    MDAU MKEREKETWA

    ReplyDelete
  39. kwa kweli inasikitisha sana tena sana ...sisi tunaosoma buku india hatuna amani kabisa...ubaguzi ulikuwepo zamani tu,tunaitwa 'negros',tunachekwa,haturuhusiwa kuingia mahotelini'no negros allowed',tumepigwa,tumefungwa bila ya kosa,mapolisi wamebaka madada zetu etc tumestahamilia yote hayo kwa sababu tunataka tumlize elimu yetu tuondoke nchini kwa watu kwa salama lakini sasa naona hii nchi imekua ni ya hatari sana...TUNAULIWA JAMANI...hivi serikali yet mnafanya nini??? mnataka mpaka wangapi wafe ndo msikie kilio chetu?? australia wahindi wamepigwa tunaisikia mpaka kwenye bbc wanavolalamika na serikali yao kufatilia maisha ya watu wao huko....SERIKALI YA TANZANIA mnafanya nini??? WHEN WILL IT END?? tunaogopa na tunahofia maisha yetu....R.I.P Imra.we pyar that ur death was not in vain!!!!

    ReplyDelete
  40. Sikutaka kusema neno ila huyo anaedai Malaysia waafrika kibao wameuliwa ningependa kujua anakaa Malaysia ipi labda.. maana katika miaka mitatu niliopo hapa hakuna muafrika niliyesikia kauawa... aidha ni ajali au kapigana na waafrika wenzie. Sanasana wanaishia kutupiga tu ambapo mara nyingi tumeanza uchokozi sisi wenyewe. Other than that sijasikia hata tetesi. Hebu tuacheni kuongeza chumvi na kupalilia yasiyohitajika jamani.
    Na hizo comments za kibaguzi ndio mwanzo. Tukiziendeleza tutakua hatuna tofauti na hawa wanaoendekeza unyama. Unyama wa namna hii hauna rangi, nchi wala kabila. Kama roho yako ni chafu hata ungezaliwa mwekundu ukiwa Marekani utaishi kwa unyama huohuo. Basi tusikae hapa kupiga domo na kupiga vijembe wahindi ambao hata tukatae vipi ni ndugu zetu sawasawa na makabila yote yaliopo Tanzania, wengi wao wamezaliwa Tanzania kama mimi na wewe. Sasa ungeambiwa wewe kwamba nchi uliyozaliwa sio yako so 'nenda kwenu'? Hivi, kwani wasingekuwepo hayo maduka na hizo 'nyumba za magorofani' tungepewa sisi bure? Wamezifanyia kazi basi na sie makabila mengine tuhamasike!

    Imran, Mungu Ailaze Roho mahali pema peponi Aamin!

    Wakazi wa India poleni na msiba, Mwenyezi Mungu subhana wataala awape roho ya faraja nyote pamoja na ndugu jamaa na marafiki wa karibu.

    Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania...

    Embracing each and everyone with love from Malaysia!

    ReplyDelete
  41. Kama alivyosema Bwatuka tukutane tufanye maandamano kupinga hicho kitendo watanzania tunanyanyasika kwenye nchi za watu. Ushauri wa kutangaza kwenye mablog muhimu tuelekezwe tutatekeleza vipi maandamano. Hii ndio njia ya kutoa malalamiko yetu kama serikali aitekelezi wajibu wake kwa wakati unaotakiwa. Na walio nje ya nchi wafuate taratibu kufanikisha maandamano huko waliko, tuonyeshe upendo na mshikamano kwa marehemu IMRAN na family yake. RIP IMRAN

    ReplyDelete
  42. mdau Tarehe Wed Feb 03, 03:19:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous umenichekesha sana...neway poleni sana wafiwa na kama BWATUKA alivosema sie kubwabwaja tu ya swetu watu walichonga wee hakuna lilofanyika kama kawaida tutaandika comments hata 200 kesho kesho kutwa tushasahau na gavaa (govt) imesahau ngoma isambe kalale mbelee..inabidi action lets learn from wenzetu UK raia wao hata awe asili gani (kama yule muhindi asili ya brito alie uwawa CHina japo ni kweli alikwua na makosa ila walimsimamia kidete Brown mwenyewe alienda kuongea na prezda wa uchina yani raia wa uk/usa hawaguswi sehemu nyingine gavaa inaingialia kati.MH gava yetu eti jerry muro mpaka cctv wamemkamatia loh! jamani ngoja niache tu sina la kusema ila Mungu ibariki tu Tanzania na watu wake AMINA

    ReplyDelete
  43. Membe mwite balozi wa wahindi hapo bongo na mpe malalamiko ya Taifa zima la Tanzania kwamba tumechukizwa na mauwaji ya kijana wetu, na tunataka wote walihusika wakamatwe na hatua za kisheria ziwashughulikie.
    Tunataka vilevile usalama wa vijana wetu wanaondelea na masomo.

    M/Mungu akuweke mahali pema peponi ndugu yetu Imran Mtui. Amin. Na poleni sana ndugu zake wote wa karibu.

    ReplyDelete
  44. Oooh my God..!!

    This is my school mate at Old Moshi High School..!!(Mselle's days).How sad to such extremely untimely death of our national potential. Huyu mtu anayesema ubaguzi hupo kote wa kihivyo sio kweli. Mfano kataja USA kama nchi yenyewe ubaguzi wa namna hiyo, hi sio kweli ubaguzi uliopo hapa USA ni "Selfishness" kwa watu weupe (Majority) kupewa kipawa mbele kisicho halali kwa mambo ya kawaida ya maisha. Lakini sio ubaguzi wa jinsi hiyo wa kukatana vichwa jamani, that is beyond damage repair.

    R.I.P, my school mate, Imrani, God bless you as you are entering your permanet resident, we are all behind you just a matter of date, time, we will be with you soon dear.

    Mdau.
    MN.
    usa.

    ReplyDelete
  45. Poleni sana wafiwa. Nami naomba serikali yetu ikandamize serikali ya India wapate hao waliomwua. Maisha ya Kaka Mtui yameenda hivi hivi!!!! Lazima waliomwua wakamatwe la sivyo watauawa wengine. Jamani, ukienda India unasema bora kukaa Afrika. Mimi nilishakuwa huko, na nilishangaa umaskini wao kupindukia.

    Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  46. Poleni sana wafiwa. Nami naomba serikali yetu ikandamize serikali ya India wapate hao waliomwua. Maisha ya Kaka Mtui yameenda hivi hivi!!!! Lazima waliomwua wakamatwe la sivyo watauawa wengine. Jamani, ukienda India unasema bora kukaa Afrika. Mimi nilishakuwa huko, na nilishangaa umaskini wao kupindukia.

    Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  47. Jamani nimesikitika sana na huyu kijana mwenzetu kwa kukatishwa uhai wake. Familia imemgalamia sana tena sana mpaka kufikia kumaliza masomo yake na pia juhudi zake alizoziweka masomoni, hebu serikali yetu isimame na ikemee kitendo hiki ili iwasaidie na wanafunzi wengine waishio india. Serikali yetu ya Tanzania simama imara. Poleni sana familia ya Mtui.

    ReplyDelete
  48. WE WILL MISS U RIP, REMEMBERING THOSE DAYS IN MAWENZI SEC AND MOSHI TOWN , THIEOMO/ AKI. MACDONALD MRIANGA NO MORE TOO.

    TUMAINI GEOFREY TEMU

    ReplyDelete
  49. Ohhho! my God i dont have no word to tell or to say about this.its so hurts.Yaani nimeumia kiasi ambacho siwezi nikamweleza binadamu akanielewa.
    hii imenipeleka moja kwa moja mwaka 1994 dada yangu mpenzi alipoungulia katika secondary ya shauritanga baada ya kuachana naye siku ya jumamosi jioni na jumapili asubuhi akawa hayupo tena duniani na hata sura yake sikuweza kuiona.tunambiwa tushukuru kwa kila jambo lakini hili ni gumu ndugu zanguni linauma.yaani ninajaribu kujiweka kwenye nafasi ya mama yake na IMRAN nashindwa.pole sana mama faraja ya mungu ikufunike na mungu ailaze roho ya imran mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  50. R.I.P IMRAN.Kuhusu wabongo walioko india i think ni vyema kuwa waangalifu sana katika kila jambo na waepuka mazingira hatarishi au mida mibovu itakayopelekea kuwa katikaka hali hatarishi.Ubaguzi upo sehemu nyingi duniani u nid not to bother about it jus kip doin ur things.But 4 sure serikali ya tanzania haina budi kulisimamia kidete hili jambo ili wazazi wenye watoto wao india wawe na amani.India is a gud place to live but tatizo ni raia wake.wanafunzi walioko india nawasihi wasichukue hatua yoyote coz itawafanya wahindi wajue mnawachukia then issue itakuwa complicated.All we nid to do z to pressure our government into tekin a considerable measure about it.

    ReplyDelete
  51. mama HelenasraFebruary 05, 2010

    R.I.P Imran.
    Hivi wadau naomba kuuliza,kuna somebody Mazura na mchumba wake waliuawa marekani kama miaka mi4 iliyopita,ishu yao iliishia wapi?
    wauaji walijulikana na kisa ni nini?

    ReplyDelete
  52. Nasikitika sana ndg zangu kwa vitendo ambavyo vinafanywa na hawa wahindi,halafu tunawvumilia sio kwamba tusiwapeleke watoto wetu huko.tuvunje uhusiano nao na kila muhindi aliyeko huku nchini kwetu afe kama sio kufukuzwa nchini kwetu,kwani juzi tu tumemzika mtoto wa joseph lema kauwawa hukohuko india.sasa msipochukua hatua mwambieni huyo rais wao tumechoka. tutaanzana na watu wao kuwamaliza.Mungu awalaani kabisa wauaji wakubwa

    ReplyDelete
  53. I didnt know Imran, though I do know his cousin Abu, and even if I didnt I would like to apologise on behalf of India for the senseless murder of this young man, who I am sure had and has countless family and friends who will mourn his brutal loss, which is also a loss for Tanzania.
    I dont know the details of the tragedy but if it was racially motivated as the indications seem to be, my sense of shame and outrage is only that much greater. All the more so because India is rightfully outraged over attacks against its citizens in Australia...but then India also has to look at its treatment of its own citizens, those who come from the perennially underprivileged - those who have lived in India know what I am talking about. But as someone born in India and who above all cherishes its diversity and who is appalled by this latest outrage, unfortunately just one more amongst so many others - deepest condolences to Imran's family and friends. I am sure countless other Indians would join me in this...if they were told the facts of this case.
    Poleni
    Sputnik Kilambi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...